William Malecela: Watoto wa viongozi na uongozi wa taifa letu!

- Well, sijui tatizo la Januari lipo wapi maana amepitia sehemu nyingi sana za kusoma bongo na hata amefanya kazi kwenye sehemu za ajabu sana kama kwenye kambi za wakimbizi, baada ya kuhangaika sana bongo akaweza kupata nafasi ya kwenda kusoma nje, akarudi bongo na kuwa msaidiziw a Rais, na sasa ni mmoja wa viongozi makini sana bungeni, mimi nafikiri anatakwia kwua mfano wa kuigwa maana ameonyesha kwamba ni competent, hasa ishus za umeme na nishati ninamuheshimu sana huko!

- Kwenye ukweli tukubali tu, badala ya kulalamika bila facts!, Tanzania sasa hatuko tena kwenye siasa za Ujama, sasa tumekwua mabepari ambao huongozwa na ubinafsi, na ndio unaongoza duniani so naona wengi mnachanganya sana mawazo ya kijamaa jamaa na siasa tulizonazo sasa za kibepari, badilikeni wandugu, sisi sio wajamaa tena!

William @ NYC, USA.

Hata wamarekani ni mabepari lakini wameliona hilo ndio maana Jebb Bush alifikiria kugombea uraisi 2012 lakini ame-back off kotokana na jina la familia hasa kwa hiyo mess alioisababisha kaka yake GW Bush aka Dubya!!
Watanzania nao wanaliona hilo kwa akina Riz1, January, Nnauye etc
Tumechoka na remixes
 
Siku moja nilikuwa nafuatilia mama Maria Nyerere anaojiwa wakati wa kumbukumbu ya baba wa taifa. Alisema kwamba kila siku Mwalimu alikuwa analalamika mshahara hautoshi?? Mfano hai Makongoro mwanae alisema kwa mara ya kwanza kwenda EUROPE aliletwa na rafiki wa baba yake... na hata yeye alikuwa ana shangaa ni jinsi gani watoto wa mawaziri wana soma nje na wao watoto wa raisi wanashindwa kwenda huko?
Jamani ni ufisadi tuuu ndo umewawezesha kufika huko mliko na kama baba zenu wangekuwa na machungu hakika elimu ingekuwa bora na tungekuwa kama SCANDINAVIAN country ambako elimu ni bure tangu chekechea mpaka PHD. Wiliam napata shida sana kukuamini kwani baba yako amekuwa waziri tena mpaka waziri mkuu lakini leo hii hakuna hata lami MVUMI? wakulima wa zabibu hawana soko? nenda Ngome, Dabalo na kwingineko wagogo bado wanaishi kwenye TEMBE wewe upo NEW YORK na ndoto za kuwa kiongozi?? Tembelea Bihawana secondari shule iliyo kuwa inasifika kwa ubora,leo hii chini ya uongozi wa baba yako zabibu zote zimekufa shule hawana hata test tube... tujiulize enzi za mwalimu ilikuwaje? mbona aliweza? Wewe mzee wako anakaa uzunguni na analindwa kwa posho zetu!!!
Nina machungu sana sana nafikiri muda si muda wakati utafika na you will pay back!! Ni ayo tu nitachangia baadae... Hasira sana.
 
mkuu unajua mishahara ya hao watu wanaofanya na wakimbizi? hacha kabisa kwanza hizo ni nafsi hadimu sana,
kwa kifupi Historia ya huyo bwana ni mfano tosha,
kazi kidogo mara masomo USA,
kamaliza shule anakuwa BOSI IKULU, maana sio kusema tu akapata kazi ikulu alikuwa bosi pale,
ina maana watu wote pale ikulu hakuna aliyekuwa na experience na qualification kuliko za JANUARY?
hata huko kwenye ubunge ilikuwa na mahali pa kupitia tu kushika wizara sema bahati mbaya GAMBA yakazidi (offside) kwa mzee
na MKULU wa kaya isitoshe watu walii - spot hiyo movement

- Hapana alipomaliza shule, alienda na kujiunga na foreign ministry, kule akakutana na Waziri aliyekwua kwenye kampeni ya urais akamuona anaamfaa akamchukua na amsaidie kwenye kampeni, zilipoisha ndio kawa msaidizi wa Rais, sasa kosa lek nini hapo mkuu?

William @ NYC, USA.
 
Hata wamarekani ni mabepari lakini wameliona hilo ndio maana Jebb Bush alifikiria kugombea uraisi 2012 lakini ame-back off kotokana na jina la familia hasa kwa hiyo mess alioisababisha kaka yake GW Bush aka Dubya!!
Watanzania nao wanaliona hilo kwa akina Riz1, January, Nnauye etc
Tumechoka na remixes

- Tatizo ni kuiweka isomeke kikatiba ya Jamhuri!

William @ New York, USA.
 
Like I said hawajakatazwa kugombea lakini wajue tu perception ya majority ya wananchi waliokuwa nayo towards baba zao itawaathiri na wao. Mtoto wa Magufuli leo hii akigombea wadhifa atapata support toka kwa walio wengi. Jiulize ni kwanini?
 
Siku moja nilikuwa nafuatilia mama Maria Nyerere anaojiwa wakati wa kumbukumbu ya baba wa taifa. Alisema kwamba kila siku Mwalimu alikuwa analalamika mshahara hautoshi?? Mfano hai Makongoro mwanae alisema kwa mara ya kwanza kwenda EUROPE aliletwa na rafiki wa baba yake... na hata yeye alikuwa ana shangaa ni jinsi gani watoto wa mawaziri wana soma nje na wao watoto wa raisi wanashindwa kwenda huko?
Jamani ni ufisadi tuuu ndo umewawezesha kufika huko mliko na kama baba zenu wangekuwa na machungu hakika elimu ingekuwa bora na tungekuwa kama SCANDINAVIAN country ambako elimu ni bure tangu chekechea mpaka PHD. Wiliam napata shida sana kukuamini kwani baba yako amekuwa waziri tena mpaka waziri mkuu lakini leo hii hakuna hata lami MVUMI? wakulima wa zabibu hawana soko? nenda Ngome, Dabalo na kwingineko wagogo bado wanaishi kwenye TEMBE wewe upo NEW YORK na ndoto za kuwa kiongozi?? Tembelea Bihawana secondari shule iliyo kuwa inasifika kwa ubora,leo hii chini ya uongozi wa baba yako zabibu zote zimekufa shule hawana hata test tube... tujiulize enzi za mwalimu ilikuwaje? mbona aliweza? Wewe mzee wako anakaa uzunguni na analindwa kwa posho zetu!!!
Nina machungu sana sana nafikiri muda si muda wakati utafika na you will pay back!! Ni ayo tu nitachangia baadae... Hasira sana.

- Yale yale, kwanza huku niliko sikuletwa na anybody ila nilijileta mwenyewe kwa nauli yangu, halafu sasa hivi sigombei anything lakini nikiamua ni haki yangu ya kikatiba, mengine naona sio topic yake hapa, huwezi kulima zabibu kama hamna mahali pa kuziuza maana sasa tuna wine toka South Africa, bara bara ya lami inawekwa kwenye sehemu ambayo itaweza kupita malori yatakayoilipia ile bara bara Mvumi kuna niini cha kuepeleka malori ya kujilipia hiypo bara bara ya lami, mengine mbona ni common sense japo kidogo tu kabla hujaandika na kujivua nguo hapa mbele ya public!

William @ NYC, USA.
 
- It is just perception, it has nothing to do na the law of our land!

William @ NYC, USA.
perception is reality!!
Hata uwapake mafuta ya mgongo hatukubali kudanganywa na magamba mapya v/s ya zamani. DNA ni ile ile tuu, mkuu Malecela.
Karibu Bronx
 
Kwa bahati nilipata kusoma ngambo! ila kitu ambacho ninajiuliza na nitazidi kujiuliza ni kwamba hivi? hawa baba zenu wanapokuja huko kwani nini basi tusijaribu ku implement hata vinavyo wezekana? Kila siku nilikuwa naona aibu nikifikiria home.. I mean Tanzania. Tutafika? Leo hii watu bado wanakufa na kipindu pindu karibu kabisa na Ikulu (Jangwani na Mwananyala) wakati kuna maeneo tangu uhuru there is no even a single episode of cholera?(Masaki, Osterbay)
Nani wa kumlaumu? Njoo leo kigogo angalia watu wanavyo ishi kwenye slums? jamani leo unataka tuendelee na wale wale tuuu. Toka New York njoo nyumbani ujionee mwenyewe! Hakika inatia uchugu... Ni kweli kuna mambo ambayo ni magumu kwetu lakini je? hata maji tuna uziana? wakati maji ni kitu cha bureeeeee kabisa? Swala la usafi si kiivo sana we need political will tu. Ni kutokana na sera za baba zenu ndo zimetufikisha hapa. Ndo maana this philosopy ya kujivua gamba bado haina mashiko kabisa. Njoo home tufanye kazi hapa njoo nikupeleke Orkasmet (Simanjiro), Terati. Emborate, Loboisireti, Kambi ya chokaa, Mewadani, Barigishi na kwingineko ndo utajua ninacho kuambia.
 
- Mkuu fungua topic ya haya maana hapa sio mahali pake, hapa ninazungumzia haki ya watoto wa viongozi kikatiba, kugombea nafasi za uongozi wa taifa letu!

- Acha kuivuruga topic, tafadhali sana!

William @ NYC, USA.
 
by William Malecela on Saturday, May 14, 2011 at 1:56pm

@ NEW YORK CITY: Ni lazima tukubaliane kwanza kwamba watoto wa viongozi wa Tanzania ambao wengi wameanza kuingia kwenye siasa na kushika nafasi mbalimbali wana haki kabisa ya kushika nafasi yoyote ya uongozi wa taifa kama Watanzania wengine. Haki yao ya Kikatiba kuchaguliwa au kushiriki nafasi yoyote ya kisiasa kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo haifutwi au kuondolewa kwa sababu ya nafasi za baba zao kwa taifa letu, sasa au huko nyuma.

-Tatizo kubwa ambalo lipo au niseme mawili ni kwamba kuna hisia kuwa watoto hao wanapewa nafasi hizo si kwa sababu ya kustahili wao wenyewe bali kwa sababu ya kubebwa au kutengenezewa mazingira ya kushika nafasi mbali mbali kwa sababu ya wazazi wao. Hili tumejionea likitokea kwa vyama vyote vya siasa nchini, yaani watoto na ndugu wa viongozi wakishiriki kwenye uongozi pia!

- Na pili, endapo wanashika nafasi ambazo zinahusiana na masuala ya utawala na sheria itakuwa vigumu sana kwa watoto hao kutengua au kuchukua hatu ambazo zitawaonesha kuwa wanafumua mambo yaliyoyofanywa na wazazi wao au hata kushindwa kuchukua hatua mbalimbali kwa sababu ya wazazi wao.

- Hivyo, hisia za haya mawili zinawafanya wananchi wengi kuona kuwa katika nafasi kadha wa kadha hasa za kisiasa ni vigumu sana kwa watoto kuwawajibisha wazazi wao - aidha kwa kusahihisha makosa yao au kuwachukulia hatua kama inapasa. Jambo la msingi ni kuweka msingi na utaratibu kuwa kila Mtanzania anapata nafasi ya kulitumikia taifa lake kwa kustahili kwake yeye mwenyewe na si upendeleo (uwe wa kidugu, kidini, kikabila, rangi au ushawishi).

- Na pale inapotokea kuwepo ushahidi wa upendeleo kutokana na nafasi za baba zao basi wananchi tujitokeze na kusema wazi palipopindishwa sheria, lakini sio kulalama tu bila sababu za msingi na hasa wivu, maana ni haki yao pia kushiriki taifa bila kuvunja sheria.

Ahsanteni.

William Malecela.

Haya tena, William naona unapenda sana kuizungumzia hii issue ya watoto wa mafisadi. Kwa upande wa wengi tafadhari watanzania sio wajinga au hawana akili kuona tunayoyaona. Taifa lolote lile likiwa kwenye hali ya kukandamizwa na kunyimwa haki kwa wananchi kutumia hiyo hiyo Katiba inayowapa watoto wa mafisadi kuandaliwa itakuwa vigumu kuwaona hii ni "wivu" kama unavyotumia maneno yako. Ndivyo wengi mafisadi wanafikiria kwamba wananchi wengi wanawaonea wivu kwa sababu kila kitu mlichokuwa nacho hata mkiibia Taifa vinaitwa wivu sio. Hakuna atakae kataa kwamba katika jitihada za kubadilisha nchi yetu kutakuwa na asilimia ndogo wasio na mwelekeo na kuwa na interest zingine mfano unaofanana ni mabadiliko ya magamba ndani ya ccm.
Daily News | CCM yet to be seen to ‘walk the talk’ on corruption fight

Jambo jingine tunaona unaumia sana na kutokukubadilika kwa hawa watoto wa kifisadi nchini. Watanzania wanajua kwa uwazi kwamba ufisadi na taratibu za hii Katiba ya ccm ndizo zimechangia kuingiza huu mtandao wa hawa watoto madarakani. Katiba ya ccm inaonyesha wazi sio demokrasia wala haki ndio inahitajika kufanya uchaguzi bali ni Tume ya NEC peke yake wananchi waiamini kama hii miaka yote 50 tuliwaamini Taifa lingefika katika umaskini wa namna hii. Maswali unatakiwa ujiulize wewe mwenyewe kabla hujaandika hizi hoja ni kwanini ccm na watoto wao hawataki kuandika Katiba ya Wananchi? Kwanini Tume ya uchaguzi, NEC inaendeshwa na chama kilichopo madarakani bila kushirikiana na vyama vingine? Au wananchama wa vyama vingine hawana haki kama ccm au sio Watanzania? Ukitafakari haya maswali utapata jibu kwanini wananchi asilimia kubwa wanaona njama za kuendeleza utawala kwa watoto wao chini ya hii Katiba ya sasa. Unajuaje election ingekuwa "True free election Tanzania", kikwete, January, Nape wangechaguliwa?

Watanzania wote wanahaki ya kugombea na kuwa viongozi, tusiendelea kubadisha maneno na kupigania haki ya watoto wachache wa kifisadi na kudai kwamba wao ndio wana haki sana kuliko wengine. Mbona sioni ukiandika na kupigania haki ya watoto huko mikoani? Haki ya maisha bora, elimu bora, huduma bora mahospitalini? Haki ya wazazi kuwa na kazi ili kujenga familia zao ipo wapi?

Kinachoonekana wazi hapa either William unajua ukweli unachoongea au unataka ku-twist the truth uonekane victim ukitaka kuingia katika siasa za ccm. Mtanzania yeyote aliepata exposure hasa Marekani sitegemei atapata ideas kama hizi, Marekani kuna kila inform na education just on your finger tips. Do your researches na kuwa mkweli acheni kutaka sympathy zisizo na maana katika jamiii ya watanzania. Taifa letu linahitaji wananchi waje na ideas za kujenga Taifa na kuna issues nyingi sana zinahitaji solutions and I don't think this is one of them. William kama mkweli pigania "Constitution for Tanzania" tubadilishe mwelekeo wa Taifa, this is critical na ndicho kinakwamisha maendeleo yetu Tanzania. I am confident una-hidden agenda na wewe sio truthful na hautakuwa kiongozi mzuri katika jamii yetu, sad to see this.

Separation of powers political doctrine originating from the United States Constitution, according to which the legislative, executive, and judicial branches of the United States government are kept distinct in order to prevent abuse of power. This U.S. form of separation of powers is associated with a system of checks and balances
Separation of powers under the United States Constitution - Wikipedia, the free encyclopedia

William, soma hii article na utuleze kama ccm na watoto wake kama hamfuati njia za Mugabe Tanzania. Mnashikilia NEC na mkidai Tanzania una free election wakati tukiuliza January, Nape, Kikwete wamechaguliwa vipi hamtaki kujibu, tutawaamini kitu gani watoto wa viongozi. Safisheni ndani kwanza kabla ya kwenda public....
BBC News | AFRICA | Mugabe bans election challenge
 
- Yale yale, kwanza huku niliko sikuletwa na anybody ila nilijileta mwenyewe kwa nauli yangu, halafu sasa hivi sigombei anything lakini nikiamua ni haki yangu ya kikatiba, mengine naona sio topic yake hapa, huwezi kulima zabibu kama hamna mahali pa kuziuza maana sasa tuna wine toka South Africa, bara bara ya lami inawekwa kwenye sehemu ambayo itaweza kupita malori yatakayoilipia ile bara bara Mvumi kuna niini cha kuepeleka malori ya kujilipia hiypo bara bara ya lami, mengine mbona ni common sense japo kidogo tu kabla hujaandika na kujivua nguo hapa mbele ya public!

William @ NYC, USA.

Nikweli South Afrika wanaproduce wine na kila shamba kuna winery industry, hatuna sababu ya kusema kwamba sasa hivi hatuna haja ya kulima zabibu? Kwa taharifa yako kama wakulima wakiwezeshwa basi everything itakuwa ok. Kwa taharifa yako Dodoma ina advantage ya kuwa na 2 seasons tofauti na south ambako wanategemea msimu mmoja tu. We can create internal demand na ikifika wakati tunaweza ku export. Hongera kama ulikwenda huko mwenyewe!!! ishu ni kwamba tukiangalia ni nini wazazi wenu walifanya inakuwa ngumu kuamini kama mnataka kuleta mageuzi. Na sikubaliani na hoja yako kwamba lami inawekwa kwenye njia ya maroli ...mhhhh kitu cha kwanza ni kutengeneza miundo mbinu alafu maroli yatapita. Ni ajabu sana kumwambia investor aje awekeze wakati barabara ni kichomi?? Piga lami alafu uone maroli yatakavyo miminika hapo mvumi.
 
Haya tena, William naona unapenda sana kuizungumzia hii issue ya watoto wa mafisadi. Kwa upande wa wengi tafadhari watanzania sio wajinga au hawana akili kuona tunayoyaona. Taifa lolote lile likiwa kwenye hali ya kukandamizwa na kunyimwa haki kwa wananchi kutumia hiyo hiyo Katiba inayowapa watoto wa mafisadi kuandaliwa itakuwa vigumu kuwaona hii ni "wivu" kama unavyotumia maneno yako. Ndivyo wengi mafisadi wanafikiria kwamba wananchi wengi wanawaonea wivu kwa sababu kila kitu mlichokuwa nacho hata mkiibia Taifa vinaitwa wivu sio. Hakuna atakae kataa kwamba katika jitihada za kubadilisha nchi yetu kutakuwa na asilimia ndogo wasio na mwelekeo na kuwa na interest zingine mfano unaofanana ni mabadiliko ya magamba ndani ya ccm.
Daily News | CCM yet to be seen to ‘walk the talk' on corruption fight

Jambo jingine tunaona unaumia sana na kutokukubadilika kwa hawa watoto wa kifisadi nchini. Watanzania wanajua kwa uwazi kwamba ufisadi na taratibu za hii Katiba ya ccm ndizo zimechangia kuingiza huu mtandao wa hawa watoto madarakani. Katiba ya ccm inaonyesha wazi sio demokrasia wala haki ndio inahitajika kufanya uchaguzi bali ni Tume ya NEC peke yake wananchi waiamini kama hii miaka yote 50 tuliwaamini Taifa lingefika katika umaskini wa namna hii. Maswali unatakiwa ujiulize wewe mwenyewe kabla hujaandika hizi hoja ni kwanini ccm na watoto wao hawataki kuandika Katiba ya Wananchi? Kwanini Tume ya uchaguzi, NEC inaendeshwa na chama kilichopo madarakani bila kushirikiana na vyama vingine? Au wananchama wa vyama vingine hawana haki kama ccm au sio Watanzania? Ukitafakari haya maswali utapata jibu kwanini wananchi asilimia kubwa wanaona njama za kuendeleza utawala kwa watoto wao chini ya hii Katiba ya sasa. Unajuaje election ingekuwa "True free election Tanzania", kikwete, January, Nape wangechaguliwa?

Watanzania wote wanahaki ya kugombea na kuwa viongozi, tusiendelea kubadisha maneno na kupigania haki ya watoto wachache wa kifisadi na kudai kwamba wao ndio wana haki sana kuliko wengine. Mbona sioni ukiandika na kupigania haki ya watoto huko mikoani? Haki ya maisha bora, elimu bora, huduma bora mahospitalini? Haki ya wazazi kuwa na kazi ili kujenga familia zao ipo wapi?

Kinachoonekana wazi hapa either William unajua ukweli unachoongea au unataka ku-twist the truth uonekane victim ukitaka kuingia katika siasa za ccm. Mtanzania yeyote aliepata exposure hasa Marekani sitegemei atapata ideas kama hizi, Marekani kuna kila inform na education just on your finger tips. Do your researches na kuwa mkweli acheni kutaka sympathy zisizo na maana katika jamiii ya watanzania. Taifa letu linahitaji wananchi waje na ideas za kujenga Taifa na kuna issues nyingi sana zinahitaji solutions and I don't think this is one of them. William kama mkweli pigania "Constitution for Tanzania" tubadilishe mwelekeo wa Taifa, this is critical na ndicho kinakwamisha maendeleo yetu Tanzania. I am confident una-hidden agenda na wewe sio truthful na hautakuwa kiongozi mzuri katika jamii yetu, sad to see this.

Separation of powers political doctrine originating from the United States Constitution, according to which the legislative, executive, and judicial branches of the United States government are kept distinct in order to prevent abuse of power. This U.S. form of separation of powers is associated with a system of checks and balances
Separation of powers under the United States Constitution - Wikipedia, the free encyclopedia

William, soma hii article na utuleze kama ccm na watoto wake kama hamfuati njia za Mugabe Tanzania. Mnashikilia NEC na mkidai Tanzania una free election wakati tukiuliza January, Nape, Kikwete wamechaguliwa vipi hamtaki kujibu, tutawaamini kitu gani watoto wa viongozi. Safisheni ndani kwanza kabla ya kwenda public....
BBC News | AFRICA | Mugabe bans election challenge

- All over the map mkuu yaani nimeshindwa kusoma mpaka mwisho labda uikarabati tena maana haieleweki kabisaa!

William @ NYC, USA.
 
- It is just perception, it has nothing to do na the law of our land!

William @ NYC, USA.

Nfikiri William kweli nimefikia kusema kwamba either umechanganyikiwa au close to lose your mind. Unachopigania humu sikioni kama unataka kuonyesha wewe umebalika tofauti na Baba yako alivyokuwa utawalani na kuharibu Taifa letu au unataka kuendelea kupigania legacy ya Malecela, you are losing the battle...

I think you are crazy and close to be in insane if keep up like this...
 
Kubebwa kwa watoto wa viongozi na vigogo kupo tena sanaaa

Mfano

  • Niikuuliza wewe Williama hiyo kazi unayofanya ulifanya interview wapi na wenzako maliofanya nao interview wako balozi gani ?
  • Nenda pale BOT utakuta ingawa wengi wa watoto wa vigogo wana elimu wana sifa but. kupata kwao kazi kuna force behind iliyoendana na vimemo.
Watoto Wengine ni kweli wana akili wana uwezo lakini wanabbewa kwa kutafutiwa maeneo yenye "milo" au sheemu zenye milo. Mfano Wizara kama ya Nje na fedha hata mwanafuzi kufanya internship ni kazi kama huna mjomba wala shangazi pale.

Mwandishi yeyote achunguze wanafuzni wa chuo wanaokubaliwa internship yao pale MOFA alafu utaelewa.......

Wahasibu wa wanapofaya interview serikalini waatupwa Wilayan lakini haijawai kukosewa mtoto wa kigogo akapelekwa wilayani. Unabai unajiuliza kinachofutwa kupangwa shemu ni alphabet au ukiwa mtoto wa mkubwa basi inakuwa kama ushafanyiwa VETTING na hivyo kupelekwa MOFA sio kazi kubw kama ukiwa mtoto wa "masanja"

Siku CAG akianza kufanya Aduting ya Human reouce recruting na allaoction za wafanyakazi wa serikali hasa kwenye wizara na vyombo nyeti anaweza kuibua mengi.

willy rudi bongo uone watu wa ngara n.k wanavyoishi! Nafikiri utajua kwanini tuna machungu na watu wanaofanya mizaha na shida zetu kwa maslahi yao

Kaka hana sababu ya kwend Ngara aende kwao Dodoma au Mtera aone hali ikoje na natamani akifika apande yale mabasi ya kwao Urafiki and there likes!
 
- Mkuu fungua topic ya haya maana hapa sio mahali pake, hapa ninazungumzia haki ya watoto wa viongozi kikatiba, kugombea nafasi za uongozi wa taifa letu!

- Acha kuivuruga topic, tafadhali sana!

William @ NYC, USA.

Mkuu una haki zote za kuwa kiongozi mie sikatai kabisa....ila najaribu kukuambia kwa nini watu wanapiga kelele. Ni haki yako kuwa kiongozi lakini ujue kwamba u need to prove beyond the basics kwamba hutakuwa tofauti. Samahani kama nimekuudhi ila ukweli ndo huu. Nafikiri ngoja niwaachie wengine pengine waongee unayopenda kuyasikia.. nilikuwa napita mkuuuu samahani sana.
 
- All over the map mkuu yaani nimeshindwa kusoma mpaka mwisho labda uikarabati tena maana haieleweki kabisaa!

William @ NYC, USA.

Thats why I think you need to stay true to yourself na tutaona unaelekea wapi kimaisha na kijamii.... Pole Sana!
 
Wananchi lets move on kwenye topics zingine beneficial kwa Taifa letu. We tried na kama tunavyoona hapa, bado mwenzetu anataka kuishi kama watoto wa Mubarak. Hataki kusikia kitu ila wale wanaokubaliana na sera za ccm. Why waste our time in this thread, myself I think William you should have called someone and discuss all these pain he his going through and end there, its not for public interest. People already spoke on this matter long time ago...
 
Back
Top Bottom