William Malecela: Watoto wa viongozi na uongozi wa taifa letu!

- Mkuu sijawahi hata mara moja kutetea uozo iwe wa CCM chama changu, au Chadema msimamo wangu uko wazi sana kuanzia hapa na blogs zote ninazoshiriki, ukweli ni ukweli na uongo ni uongo, CCM wakifanya vyema ninasema na wakiharibu ninasema na kule Facebook ninasema wazi bila kuficha on ishus,

- HOWEVER: nisichotaka ni kuwa bendera fuata upepo, hapana shule nimejisomesha sana huku majuu kwa hela zangu mwenyewe, ili nisiwe mjinga wa kufikiriwa na wengine, I like CCM ambako mimi ni member sikatai kwamba kuna mambo mengi ndani ya CCM hayakubaliki, ndio maana ninataka mabadiliko kutokea from within na wengine muyalete form outside, waamuzi ni wananchi. I like Chadema as chama, lakini siwaamini sana baadhi ya viongozi wake! Otherwise wote tupo pamoja na TAIFA KWANZA!

William @ NYC, USA.
Mkuu kutetea ni pamoja na kusema kauli tata ya katibu wa ccm sio issue bali mkulu! Hizi ni propaganda mkuu,ulipaswa kushangaa na kuuliza hilo gamba basi ni nini? Lakini hujakosoa huo mkanganyiko wazi bali ukaamua kuwaaminisha watu pale unapoamini! Je chama ni mwenyekiti? Kama sio what is going on there? Wewe ni kizazi tena damu yetu usifungwe na mbinu hizi zinazoshindwa za ccm.ukitaka ueleweke kuwa muwazi na mkweli tu.werevu wengi wanapita humu usipindishe mambo kwa personal benefit mkuu.
 
Tatizo ni matayarisho extra wanayopewa kusomeshwa vyuo vya nje vyenye sifa za kimataifa, huku sisi wenzenu tukipata mafunzo kwenye shule za kata zilinazozoofishwa na ufisadi wa baba zenu!

Halafu hizi nafasi za wakuu wa wilaya wanazozawadiwa kuwajengea CV na kuwatajirisha ni matumizi mabaya ya madaraka. Katiba tunayoitaka ni kuondoa ubaguzi huu, itupe haki sawa na fursa sawa. Sio wengine walipiwe mabilioni kusoma Oxford na sisi hata madawati hakuna na tunasoma Eckenford! Hatuna ugomvi na mwl. JK Nyerere kwa kuwa watoto wake walipewa fursa sawa!

Je yupi mtoto wa hawa mafisadi waliosomeshwa kwa fedha za mafisadi anaweza kujiunga CDM na kupinga ufisadi kwa nguvu zote! Angalau Makongoro alifanya hivyo kwa kuwa alijua hakula cha kifisadi! Mpaka baba yake alipofariki mafisadi wakamrubuni!

Nadhani Nyerere angelikua hai Makongoro asingelirubuniwa na Mkapa!

- Zed mambo mengine ni facts of life kwamba hata wewe ukiwa waziri siamini kwamba utataka watoto wako wasome bongo, wakati unao uwezo wa kuwasomesha nje kwenye elimu bora zaidi. Kosa kubwa Tanzania tunashindwa kuelewa ni kwamba majuu wana system ambazo zinampa kila mwanandamu ku-explore potential zake kielimu, hakuna binadam ameumbwa bila talent hata moja, kwa hiyo mtoto ambaye baba yake ni kiongozi anafanya vibaya shule za chini hapa bongo, akienda majuu kule anatihaniwa na kuangaliwa wapi anafaaa na kuepelkwa huko, sasa talent yake ikiwa full explored automatically anaanza ku-perform kuliko hata his imaginations, sasa akirudi bongo tunashangaa aaghhh huyu darasani alikuwa zero, hapana ndio tofauti yetu bongo na majuu!

- Kuhusu Makongoro wengi inaelekea hamumjui vizuri, mimi ninakumbuka Marehemu baba yake akimcheka kwamba he would never raise to anything in politics na yeye akimjibu kwamba ni kwa sababu ya kuwa mtoto wake ndio maana atakapata sana shida ku-raise above his name, lakini aliposhinda ubunge wa upinzani, Mwalimu was the first one kumpa pongezi tena nakumbuka sana akumuita "Mheshimiwa Mbunge", na Makongoro kwenye kampeni alimshambulia sana Mwalimu kwamba amemrithisha urais mkapa, kwa hiyo kampeni za uchaguzi zilikuwa ni waste of time and money za taifa.

- Lakini then came the political charges kwamba wapinzani wanamtumia tu Makongoro, soon watamtupa which they did, sasa unaona matatizo ya mtoto wa kiongozi anapoamua kuwa kiongozi upinzani, sasa amerudi CCM he seems to make a lot of sense, lakini bado kuna mtoto wa baba wa taifa kutoka mostly wapinzani, let the man be himself as he is badala ya hizi title zisizo na faida kwake as a man na mwananchi,

- Watoto wa viongozi waruhusiwe kuwa wananchi, wanapofanya mazuri na wanapofanya mabaya pia!


William @ NYC, USA.
 
Kwamba wana haki ya kushiriki hilo ni kweli.Lakini hilo haliondoi ukweli kwamba kuna upendendeleo.Haki ni haki lakini haipatikani bure mara pengi hupiganiwa.Ninaamini kwenye process ya watoto hao na viongozi kuipigania ama kuipreserve haki hiyo,basi nepotism hutokea.
 
Watoto wa viongozi hawawezi kuleta mabadiliko yenye tija kwa Taifa.Sidhani kama watawachukulia hatua wazazi wao walioshiriki kwenye ufisadi.Sana sana wataendeleza ufisadi kwa kutumia mbinu mpya.Shida si kutawala,bali kutaka kuendelea kuwa madarakani by any means neccessary.

- Mkuu Mushi iweke hii kikatiba ya Jamhuri yetu, itasomeka vipi mkuu wangu?

William @ NYC, USA.
 
- Mkuu sijawahi hata mara moja kutetea uozo iwe wa CCM chama changu, au Chadema msimamo wangu uko wazi sana kuanzia hapa na blogs zote ninazoshiriki, ukweli ni ukweli na uongo ni uongo, CCM wakifanya vyema ninasema na wakiharibu ninasema na kule Facebook ninasema wazi bila kuficha on ishus,

- HOWEVER: nisichotaka ni kuwa bendera fuata upepo, hapana shule nimejisomesha sana huku majuu kwa hela zangu mwenyewe, ili nisiwe mjinga wa kufikiriwa na wengine, I like CCM ambako mimi ni member sikatai kwamba kuna mambo mengi ndani ya CCM hayakubaliki, ndio maana ninataka mabadiliko kutokea from within na wengine muyalete form outside, waamuzi ni wananchi. I like Chadema as chama, lakini siwaamini sana baadhi ya viongozi wake! Otherwise wote tupo pamoja na TAIFA KWANZA!

William @ NYC, USA.

Nakuunga mkono kwenye red if you mean what you mean....nimesoma baadhi ya post wako wanaokuzungumzia vizuri kama fighter, no more to add kwa kuwa sikufahamu.....hatuna uwezo wa kupima nia ila utakuwa kapu moja na wengine kama utakuwa uko-driven na factors zinazowa-drive watoto wengine wa vigogo "kushiriki keki tuliyoizoea"

By the way, what is your opinion in a more general term kwa kuwaangalia watoto wenzako wa viongozi wengine? Are they like you? Maana hapa hatuzungumzii Willy tu, ila general as a system kwa watoto wa vigogo
 
Kwa mtizamo wangu tatizo ni kubwa zaidi kuliko maelezo; katika miaka ya hivi karibu uongozi wa juu umechukuliwa na watu ambao maisha yao yote ya utumishi wa umma yamekua kwenye siasa.

Inavyoelekea watu aina hiyo wanachukulia siasa kuwa ni ulaghai, kwa maana kwamba wanachukulia siasa kuwa ni tathmilia inayolenga kuchota akili za umma bila ya kuwa na mahudhui yeyote. Na hivyo unaweza ukaanzisha mjadala wa chama kujivua gamba, ukawaacha wananchi waogelea, kila mtu anajaribu kuwa bigwa wa kutoa tafsiri ya nini hasa maana halisi ya kujivua gamba.

Kwa kuwa hawa watoto wa wakubwa wamekulia kwenye utamaduni huo, itakuwa ni balaa kwa nchi yetu kuendelkeza mfumo wa kuridhishana madaraka.
 
- Mkuu sijawahi hata mara moja kutetea uozo iwe wa CCM chama changu, au Chadema msimamo wangu uko wazi sana kuanzia hapa na blogs zote ninazoshiriki, ukweli ni ukweli na uongo ni uongo, CCM wakifanya vyema ninasema na wakiharibu ninasema na kule Facebook ninasema wazi bila kuficha on ishus,

- HOWEVER: nisichotaka ni kuwa bendera fuata upepo, hapana shule nimejisomesha sana huku majuu kwa hela zangu mwenyewe, ili nisiwe mjinga wa kufikiriwa na wengine, I like CCM ambako mimi ni member sikatai kwamba kuna mambo mengi ndani ya CCM hayakubaliki, ndio maana ninataka mabadiliko kutokea from within na wengine muyalete form outside, waamuzi ni wananchi. I like Chadema as chama, lakini siwaamini sana baadhi ya viongozi wake! Otherwise wote tupo pamoja na TAIFA KWANZA!

William @ NYC, USA.

William hongera sana kwa kujisomesha mwenyewe angalau umeweza kuokoa pesa za wakulima, lakini hilo pekee halikufanyi wewe uwe tofauti na watoto wa viongozi wengine wanaofuja mali za Taifa. Nitakubaliana na wewe iwapo utasema hadharani kukana matendo machafu ya viongozi wa CCM akiwamo Raisi, kukana maovu aliyoyafanya Mzee Malecele (hatuna haja ya kuyadili). Siku zote unaleta pointi lakini unakwepa ukweli.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Ni mara chache sana watu waliokuwa na priveledge kama hizo i.e kuwa watoto wa viongozi, kuwa na uelewa wa matatizo halisi ya mtanzania.Kama baba zao wenyewe hawajui kwanini sisi ni masikini,unategemea watoto waje na jibu gani?Sana sana ni kujijenga na kujiimarisha kuyalinda madaraka na hizo priveledges by any means neccessary.Vibaraka wenye kunufaika wanao kibao pia.
 
Kaka Willium Salaam,

Kwanza nitangulize kutoa tongotongo lifuatalo....hakuna mtu anaeona WIVU kwa watoto wa viongozi wa Tanzania kisiasa na wao kufuata nyayo za baba zao....wala kusema mtu hastahilio kuwa mwanasiasa kwa kuwa mzazi wake alikuwa mwanasias sio sahihi kwa kuwa unamkosea haki yake ya kikatiba....hivyo binafsi sioni tatizo wewe na watoto wengine wa vigogo nao kuwemo kwenye siasa

But wait here, let's face reality, hebu tuambie ukweli, ungekuwa unetumia "Matonya" mbele ya jina lako ungekuwa hapo? labda ndio lakini sidhani mtu kama Ridhiwani angefika hapo. Vipi yule mtoto wa Ghadaffi, can you tell me angekuwa na uwezo? Je angesikika hata kwenye TV akibwabwaja kumtetea mzazi wake kama angekuwa ni mtoto wa kawaida?

Nasema hivi kwa sababu wengi wa watoto wa wakubwa hawaingii kwenye siasa kwa sababu wanajua kuna jukumu la kufanya bali kwa sababu wanajua kuna "keki ya kula" ambayo wamezoea kuila siku zote na wangependa waendelee kuila....Ni kweli wapo wenye uwezo na nia njema, hawa nafasi wanaistahili ila sio kama yule mtoto wa mkuu wa wilaya fulani niliesoma nae bonge la kilaza lakini alienda nje na leo ni mfanyakazi jiwizara moja eti na yeye anatupangia sera na mipango ya maendeleo...................what a shit...

Kweli mkuuu umetusaidia kupanua huu mjadala...Yaani hali hii inazidisha simanzi tukiwaona wale watoto wa wakubwa waliokuwa vilaza, wakiambulia makarai (C), make ups, supplimentary exams na vitu kama hivyo kwamba leo ndio watunga sera wa nchi hii au wale wanaosimamia uchumi wa nchi yetu pale BOT.


Inakera sana!
 
nyie mnaojiita watoto wa viongozi mna dhambi ya dhuluma, mmelelewa na hela za dhuluma, mmebeba dhambi ya dhuluma!!

Baba zenu waliiba hela zetu kuwasomesha,tatizo letu tunaogopa mtaileta ile dhambi kwenye utawala ambao tunataka kuusimamia!
 
by William Malecela on Saturday, May 14, 2011 at 1:56pm


@ NEW YORK CITY: Ni lazima tukubaliane kwanza kwamba watoto wa viongozi wa Tanzania ambao wengi wameanza kuingia kwenye siasa na kushika nafasi mbalimbali wana haki kabisa ya kushika nafasi yoyote ya uongozi wa taifa kama Watanzania wengine. Haki yao ya Kikatiba kuchaguliwa au kushiriki nafasi yoyote ya kisiasa kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo haifutwi au kuondolewa kwa sababu ya nafasi za baba zao kwa taifa letu, sasa au huko nyuma.

-Tatizo kubwa ambalo lipo au niseme mawili ni kwamba kuna hisia kuwa watoto hao wanapewa nafasi hizo si kwa sababu ya kustahili wao wenyewe bali kwa sababu ya kubebwa au kutengenezewa mazingira ya kushika nafasi mbali mbali kwa sababu ya wazazi wao. Hili tumejionea likitokea kwa vyama vyote vya siasa nchini, yaani watoto na ndugu wa viongozi wakishiriki kwenye uongozi pia!

- Na pili, endapo wanashika nafasi ambazo zinahusiana na masuala ya utawala na sheria itakuwa vigumu sana kwa watoto hao kutengua au kuchukua hatu ambazo zitawaonesha kuwa wanafumua mambo yaliyoyofanywa na wazazi wao au hata kushindwa kuchukua hatua mbalimbali kwa sababu ya wazazi wao.

- Hivyo, hisia za haya mawili zinawafanya wananchi wengi kuona kuwa katika nafasi kadha wa kadha hasa za kisiasa ni vigumu sana kwa watoto kuwawajibisha wazazi wao - aidha kwa kusahihisha makosa yao au kuwachukulia hatua kama inapasa. Jambo la msingi ni kuweka msingi na utaratibu kuwa kila Mtanzania anapata nafasi ya kulitumikia taifa lake kwa kustahili kwake yeye mwenyewe na si upendeleo (uwe wa kidugu, kidini, kikabila, rangi au ushawishi).

- Na pale inapotokea kuwepo ushahidi wa upendeleo kutokana na nafasi za baba zao basi wananchi tujitokeze na kusema wazi palipopindishwa sheria, lakini sio kulalama tu bila sababu za msingi na hasa wivu, maana ni haki yao pia kushiriki taifa bila kuvunja sheria.

Ahsanteni.

William Malecela.


Kaka mimi hawa waupinzani naweza kuwasamehe kwa kuwa siasa za upinzani ningumu sana na zinaitaji muamko na kujitolea kwa nguvu zoite, tumeshuhudia watu wengi wakiogopa kuingia upinzani kwa kuwa wanaogopa CCM itawafanya mbaya kwenye biashara zao na maisha yao ya kila siku,
Ila ukweli ni kwamba ni rahisi kwa watu waliojitolea na kujenga majinakwenye upinzani kushawishi ndugu zao na watu wakaribu kuliko watu wasio wajua, Atleat sikuhizi kuna muamko!

kwahiyo kuwalaumu UPINZANI kwa hili ni kuwaonea kwani mazingira ndio yansababisha haya yote!

Ila kwa CCM hilo halisameheki tunaona watu wasio na uwezo wanavyobebwa na kuachwa vijana wenye huwezo mkubwa sana tena kupita hata WAZAZI hao wano wabeba watoto wao!

Ni kwa nini nyerere hakufanya hivi?
Ni kwanini Sokoine hakufanay hivi?
Ni kwa nini .......... hakufanay hivi? Hope tunamkumbuka alifariki hukokusini kwa ajali ya helikopter!
 
willy rudi bongo uone watu wa ngara n.k wanavyoishi! Nafikiri utajua kwanini tuna machungu na watu wanaofanya mizaha na shida zetu kwa maslahi yao
 
Hili ni jambo tata sana na si rahisi tu kusema kuna upendeleo au hakuna, tutumie busara tu kujadiliana bila kutoa hukumu.
Mkuu William kuna mambo ambayo ni magumu kuyatolea ushahidi wa moja kwa moja lakini ushahidi wa kumazingira unaonyoshe ingawa haujitoshelezi kama ushahidi kamili. Nakubaliana nawe kuwa watoto wa viongozi wana haki sawa kama wengine, na wanstahili fursa sawa.

Nafasi hasa za kisiasa zinatia shaka kwani wazazi viongozi huwa na 'influency na network nzuri' kwahiyo ni rahisi kwao ku- manipulate system in favor of their interest. Mtoto wa kiongozi akiwa mbunge wa kuchaguliwa haina shida, lakini kama kwa mfano wapo watoto 10 au 15 wa nafasi za kuteuliwa inatia shaka.

Mkuu hivi inakuwaaje kwa mfano mahali kama BoT kuwe na watoto wa viongozi tupu!
Inawezekana kabisa watoto hao wana sifa nzuri sana kutokana na ubora wa elimu na maarifa yao. Wasi wasi unaletwa na baba zao (viongozi) ambao wamekuwa si wa wazi. Kelele za BoT ziliposikika wakatafutwa watoto wawili watatu na kutolewa kafara. Gavana akaunda tume kuchunguza hao waliobaki, jambo la kushangaza ni kuwa hakuna taarifa yoyote ya kuwatuhumu au kuwasafisha iliyotolewa. Hapa ndipo watu wanabaki wakijuiuliza kuna nini kinafichwa? na ni kwa sababu hizo wanaendelea kuamini kuwa ipo namna.

Kwa vile utaratibu wa kupata viongozi wa nyanja zote si wa wazi, inakuwa ngumu sana kwa baadhi ya watu kuamini haki inatendeka.
Mfano mzuri upo ndani ya Chama chako cha CCM, mara tunaambiwa Bashe si raia anaenguliwa kugombea ubunge, waziri anajitokeza na kusema ni raia baada ya mchujo,je huu si ushahidi wa kimazingira kuwa hila zilitumika? Ukiangalia issue nzima unaona ina influency ya viongozi, sasa katika mazingira haya utawezaje kukataa kuwa ushawishi wa viongozi wazazi au walezi si sehemu muhimu kwa mafanikio ya watoto wao?

Nasema haki itendeke lakini si tu itendeke bali ionekane inatendeka kwa watoto wa viongozi na watoto wengine, kwa mfumo wetu usio na uwazi na uliojaa rushwa dhana hii itabaki vichwani mwa watu, na wala asidhani mtu kuwa ni suala la wivu na husuda.
 
Ridhiwani wakati wa kampeni 2010 alipita Jimboni kwangu! Alimwahidi kijana mmoja ukuu wa Wilaya......nilicheka sana nilipoipata hiyo. Yule dogo alikuwa anapewa Hadi ripoti za maendeleo ya Wilaya as if naye ni kiongozi wa nchi.....sababu ya Jina Kikwete....
 
Hivi hizo ndiyo nini? Manake nimekuwa nikizisoma soma tu humu bila hata kuelewa ni vitu gani.

Pole mkuu na pia hongera..Inaonekana hukuwahi kukutana na vitisho vya Ma-Prof wa bongo..

Hiyo ni mitihani ambayo wanapewa watu walioshindwa mtihani wa kwanza (first sitting) katika vyuo vikuu vya hapa Bongo. Pia inaweza kuchukuliwa kama special exam endapo mtu huyo atakuwa hakuwahi kufanya mtihani wa kwanza kwa sababu za msingi zilizomfanya auhairishe. Mara nyingi watu wanaoenda kwa kuchechemea (vilaza) walikuwa wanaokoka kwa kufanya hiyo mitihani ingawa kama ni Sup exam huwezi kupewa pass mark zaidi ya C!!!

Karibu Bongo Dar mkuu!!
 
Ridhiwani wakati wa kampeni 2010 alipita Jimboni kwangu! Alimwahidi kijana mmoja ukuu wa Wilaya......nilicheka sana nilipoipata hiyo. Yule dogo alikuwa anapewa Hadi ripoti za maendeleo ya Wilaya as if naye ni kiongozi wa nchi.....sababu ya Jina Kikwete....

Ndiye Rais wenu huyo baada ya Hussein Mwinyi
 
Mbona kwenye awamu ya kwanza watoto wa wakubwa hawakuwa wengi kwenye siasa kama sasa?. Inakera sana...ial yana mwisho!!
Dark City, Enzi za Mwalimu, uongozi ulikuwa ni kwa vito tena kwa kujitolea. Sasa uongozi wa kisiasa ni professional ambayo ni ajira rasmi tena ndio the top most paying job motive ikiwa not to lead but to gain, reap and sometimes rob!.
 

Similar Discussions

16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom