Kwa hii Chipukizi ya Watoto wa Viongozi CCM inajichimbia kaburi.

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,614
15,942
Nimefuatilia kwa umakini sana huo mkutano wa UVCCM taifa ambapo vijana kadhaa (chipukizi) wamepiga kampeni kitaifa kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Chupukizi ndani ya CCM siyo kitu kipya tangu tunasoma huko chipukizi ilikuwepo lakini naona kama mwaka huu imekuja kivingine kabisa. Watu wazima viongozi wakishiriki kuwapigia kampeni watoto wao ili wachaguliwe katika nafasi mbali mbalimbali za uongozi ndani ya chama.

Siyo jambo baya lakini naona mapungufu kadhaa ambayo kama Chama kitaacha yaendelee basi CCM huko mbeleni kitakua ni mali ya watu wenye uwezo na viongozi serikalini. Nasema hivyo kwa sababu gani?

1. Tumeona watoto wote waliokua wanawania hizo nafasi ni watoto aidha wa wafanyabiashara wakubwa au viongozi wakubwa serikalini utasikia majina kama Nchemba, mahiga , sheta n.k na kiuhalisia watakaowezs kuwa na ubavu wa kufanya kampeni ni wenye uwezo wa kifedha na ushawishi unadhani atatoka mtoto wa mvuvi kule ukerewe aje kuwania nafasi za kitaifa kama hizo uwezo huo anaupata wapi? Hapa CCM tumefeli na mwisho siyo mzuri.

2. Hawa watoto kuanza kuwaweka kwenye majukwaa ya kisiasa kwa umri wao si sahihi kabisa. Umri huo watoto tunawanyima haki zao za msingi kama watoto kuanza kuwafanya wafikirie mambo makubwa ambayo ni tofauti na umri walio nao. Chipukizi ibaki kama ilivyokua mashuleni lakini kuanza kuipa attention za kitaifa kiasi hiki naona kama ni ujinga uliopitiliza. CCM inaelekea kubaya.

3. Naendelea kusisitiza kuwa CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi labda kama hiyo slogan siku hizi haipo tuambiwe. Kuna dalili viongozi wanaanza kuwaingiza watoto wao kwenye chama mapema kama ndio sehemu ya kupatia maisha huko baadae. Chama siyo mali ya viongozi. CCM kama mtashindwa kulikemea hili huko mbele naona kabisa mkijichimbia kaburi.

Ukifuatilia maoni ya watanzania wengi hata baada ya huu uchaguzi utagundua wengi wanaona ni kama watoto wa viongozi wanaandaliwa kuja kurithi nafasi za wazazi wao. CCM mkiliendekeza hili hiki chama huko mbeleni kitakua na hali ngumu nawaambia ukweli kutakua na matabaka ambayo mmeyajenga wenyewe. Nakumbuka marehemu Magufuli katika hotuba yake moja alipinga hili suala na mimi nilimuunga mkono sasa yamerudi.

Nikuombe mama samia wewe ndio mwenyekiti wa CCM taifa unapoona madhaifu kama haya kemea na usiruhusu CCM ikawa ni mali ya watu wachache. Hili la chipukizi nategemea utalitolea maekelezo mapema iwezekanavyo.

Ni mimi mwanachama mwandamizi wa CCM .

Sir John Roberts.
 
Mnaangaika bure na watoto wa vigogo wa CCM, hata Khalfan Kikwete; alishawahi kuwa mwenyekiti wa chipukizi baba yake alipokuwa raisi; leo hii hata habari na siasa hana.

Kwa watoto wa vigogo hawahitaji hayo madaraja zaidi ya hobby tu kwa sababu ya ya wazazi wao.

Huko mbele kwa mfumo wetu ni nani yupo ndani ya system anajuana na baba yake ili apate nafasi kirahisi.

Vinginevyo makada wengine wasio watoto wa vigogo lazima uonyeshe uwezo wako wa kukilinda ndio utalelewa mpaka system ikubebe.

Kuangaika na hao watoto na kuwalaumu kwa ambitions za wazazi wao ni kuwakosea tu.
 
Mnaangaika bure na watoto wa vigogo wa CCM, hata Khalfan Kikwete; alishawahi kuwa mwenyekiti wa chipukizi baba yake alipokuwa raisi; leo hii hata habari na siasa hana.

Kwa watoto wa vigogo hawahitaji hayo madaraja zaidi ya hobby tu kwa sababu ya ya wazazi wao.

Huko mbele kwa mfumo wetu ni nani yupo ndani ya system anajuana na baba yake ili apate nafasi kirahisi.

Vinginevyo makada wengine wasio watoto wa vigogo lazima uonyeshe uwezo wako wa kukilinda ndio utalelewa mpaka system ikubebe.

Kuangaika na hao watoto na kuwalaumu kwa ambitions za wazazi wao ni kuwakosea tu.
Hivi wewe unajua plan za khalfani kikwete? Hakatazwi kuingia kwenye siasa lakini watoto wa viongozi wanajengewa historia ya uongozi kuanzia wakiwa wadogo ndani ya chama kwa ushawishi wa wazazi wao.ndio maana kesho kutwa huyo halfani unaemsema akija kugombea urais au ubunge atasema kuwa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa chipukizi. Hiyo ni sifa kuwa ana uzoefu na uongozi. Sasa nakuuliza unaona hii platform ipo sawa kwa watoto wa watanzania wengine kupata hizo nafasi za kitaifa za chipukizi?
 
Siasa sio utumishi tena, siasa ni Ajira Mkuu.

WANAWAANDALIA WATOTO WAO AJIRA ZA KUJICHOTEA MAHELA YA WANANCHI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom