Why watu wenye mafanikio wamesoma kayumba? Samatta, Diamond, Doctors, Engineers, President etc

Ukitaja tusiime ama english medium za kati.. huwezi taja IST.. naona kama umeweka mfano ambao hauna uhalisia wa uzi.. IST watoto hawabebi begi kubwa na kufatwa na school bus alfajiri na kurudishwa jioni... uwezo wa ist unajulikana.. na sizani kama kuna member humu ana mtoto ist.. maana mitaa niliyokulia sijawai kuona mtu anasoma.IST


Chuo nimesoma udsm sijawai kuona mwanafunzi kasoma IST then akaja udsm... weka mfano wenye uhalisia ndugu
Thank you
Ukisoma IST lazma uende nje ya nchi ili ufafanane mtaala na wao

ACSEE na IB(Baccalaureate)haviendani
 
Umaskini tu,
ILA kiukweli elimu Bora Inapatkana INTERNATIONAL SCHOOLS.

Tanzania tuna uhaba sana wa ajira,

Ila Ni ngumu sana kukutana na bahasha ya kijana alietoka TANGANYIKA INTERNATIONAL SCHOOL akiomba ajira mitaani.

Pia, Ni ngumu kuskia graduate wa TANGANYIKA kaajiliwa ktk utumishi wa Umma.
Hasa hizi kada za chini chini Kama ualimu,nursing, n.k

Jiulize wakimalizaga wanaenda wapi?

Na hizi shule Kila mwaka zipo, na zinatoa wanafunzi wengi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nursing ni kada ya chini ???
 
Mafanikio ni relative term...

Watoto wa International School huwezi kuwakuta serikalini wakiishi kwa majungu na kujikomba..wanaishi kwa taaluma na elimu zao.

Wapo huko private sectors wakifanya ya duniani kuliko ya tanzania..

Everyday is Saturday......................... :cool:
 
Mi ukiniambia umeelimika halafu huijui lugha ntakuona chenga kuna wabongo kibao wamesoma hizo shule za kulipia ila lugha yao kawaida bora nipeleke mtoto nchi jirani hata ikiwa aio international kuvile kwanza ataijua lugha pili atapata exposure, bongo michosho tu mtu kagraduate tusiime ila kingereza kibovu
 
Watoto wa English medium ndiyo think tanks,wao wanafanyakazi za kitaalamu na kutegemewa nyuma ya ofisi,siyo FRONT OFFICERS
 
Habari wadau..

Mbona watu wengi wenye mafanikio wamesoma kayumba?

Hizi shule za kizungu zinakosea nini kuandaa watoto ?

Nimepima sector zote.. kuanzia michezo, business, politics, music, engineering naona kayumba wanaongoza...

Nawaza tu hizi shule za mtoto kubeba begi kubwa na kuchukuliwa na school bus saa 12 asubuh na kurudi saa 10 jioni au saa 12 jioni. Zinaweza kweli kumuandaa samatta au mchezaji hata wa yanga na simba mbeleni

Nawaza diamond wa mbeleni anaweza toka hizi shule kweli

Nawaza magufuli wa mbeleni anaweza toka hizi shule kweli?

Nawaza mwanangu nimpeleke goverment school kisha niwape walimu hela za tution shuleni kwake.. na kisha ada ambayo ningelipa tusiime nijikaze na kujitahidi kumjengea kila mwaka chumba kimoja...

Target kila mwaka chumba kimoja... ili nikishindwa maisha wapate hata pa kupangisha kama nikiondoka duniani...kuliko kupeleka ada shule ambazo imetokea corona ya miezi miwili tu zinanyanyasa walimu. Shule haziruhusu talent zinakomaa na mtoto siku nzima anashinda darasani hapati hata muda wa kucheza
Mkuu nadhani wewe bado mdogo.naomba nikufahamishe kuwa hadi mwishoni mwa miaka ya 1990-99 shule za umma zilikuwa bora kuliko private schools na seminaries,wakati huo vilaza pekee ndo walikuwa wanasoma private school.Hivyo hawa uliowataja ambao mmoja au wawili ndo mafanikio yao ni matunda ya elimu walisoma before 2000.Kayumba zilizaliwa wakati wanaccm walipoanza kuona fursa kwenye elimu yetu,matokeo yake wakaamua kuua shule za umma ili wapige pesa
 
Jidanganye tu mkuu,siwezi kusomesha wanangu kayumba,hao uliowataja wanabebwa na vipaji(talanta ,usanii) vyao na sio shule!! Doctors,Engineer katika level ya chuo wote wanakutana MUHAS , CoET etc
Halafu hao hao wanaaokutana huko UD ndo baadae wakaajiliwe na watoto waliobebwa na vipaji.....unachekesha. talents ndo ndo wealth of all time. Ww pia umeaminishwa ktk kusoma na kuajiliwa.
 
Wenyewe hakuna waliposema kuwa wamefanikiwa,wewe unawasemea.

Wewe mtoa mada umejuaje kuwa wao wamefanikiwa ?

Mafanikio ni kufikia malengo ambayo mtu amejiwekea,wao hujui wamejiwekea malengo gani.

Kuwa na pesa sio mafanikio kwa kila mtu,ili ujue mafanikio ya mtu lazima ujue alikuwa na azma gani.
Acha siasa na wivu ....wote hao waliotajwa ktk context ya kitanzania wamefanikiwa
 
Ili kufanikiwa kwenye maisha ya Kitanzania lazma uwe Aggresive kwenye kuchangamkia fursa. Ni km jinsi mchimba madini anavyopambana kutafuta dhahabu.Tatizo shule za English Medium zinamfundisha mtoto kana kwamba life is very smooth and common with the same formular. Uzungu uzungu sana.

Lakini kiuhalisia ili kufanikiwa kimaisha lazima upitie hussle nyingi ikiwemo kufanya kazi za dhihaka,kulala chini,kuokota makopo, kushinda porini n.k Watoto wa English medium wanafundishwa aina fulani wa maisha ambayo hayapo kwenye jamii yetu kwa kiasi kikubwa. Ndio maana wakimaliza shule wanaishia kutembea na bahasha tu

Watoto wa Saint Kayumba wanasoma katika hali ya kumfanya mtoto apambane. Hakuna kudeka deka kule. Mtoto anaenda shule kabeba fagio,begi,jembe, na dumu la maji. Tayari anaanza kufeel machungu ya maisha mapema na kuanza kumjengea hasira ya kuwa mpambanaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ata kujifunza kula bagger ni maendeleo
 
Yawezekana ukawa sahihi kwa kiasi fulani lakini kuna utofauti kwa kiasi fulani kwamba mtoto wa S.Kayumba anaweza kujichanganya katika mazingira tofauti ili kujitafutia riziki. Hawa wa Eng. Medium huwa wako dormant na very sluggish kwenye kupambana. Mda wote wanaweza kazi maofisini tu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Usiforce mambo ..unachoandika ni mtazamo tu.
 
Tunasoma Elimu ya wazungu ili Tuajiriwe kwetu,Hao wanafanikiwa kwa sababu wamefaulu kutumia Elimu yao ya kuzaliwa kutawala mazingira yao...
 
Halafu hao hao wanaaokutana huko UD ndo baadae wakaajiliwe na watoto waliobebwa na vipaji.....unachekesha. talents ndo ndo wealth of all time. Ww pia umeaminishwa ktk kusoma na kuajiliwa.
Mkuu elewa comment kwanza na sio kukurupuka , simshomeshi mtoto kayumba kwasababu aje kuwa na pesa bali shule za efemu akademia mtoto anakua na upeo mkubwa kuliko kayumba hivyo itamsaidia sana mtaani katika kutafuta maisha iwe kwenye kipaji,biashara au kazi.
 
Back
Top Bottom