Mapenzi ya shule: Nilipata mtoto nikiwa Sekondari

Natakakutulia

Member
Jan 20, 2020
56
385
Habari waungwana,

Nawasimulia kwa ufupi kisa changu cha mapenzi ya utotoni ila naanzia nyuma kidogo.

Nilipokuwa kidato cha pili nilikuwa naendela vyema tu na masomo japo sikuwa nafaulu sana, nilikuwa mpole sana na mkimya mno. Siku moja Mwalimu wa kiswahili akasema wanataka kuanzisha kikundi cha ngoma shuleni kwa ajili ya kupokea Mwenge maana ulikuwa unalala shuleni kwetu. Basi moja ya watu waliochaguliwa na mimi nilichaguliwa kujiunga na kikundi hicho ila sikutaka maana kwakweli nilikuwa na aibu mno na sikuwa najua kucheza ngoma.

Basi nikamwambia mwalimu hapana mimi siwezi, mwalimu akawa analazimisha kwa kusema nitafundishwa nitaweza. Nikajisemea kwa sauti ya chini acheze mwanae mimi siwezi, wanafunzi wakasema mwalimu kasema ucheze mwenyewe basi mwalimu akaniita mbele akanichapa sana kusema nimemvunjia heshima ila nilisema acheze mwanaye maana tulikuwa tunasoma na mwanaye na hakumchagua.

Kichapo kilizidi mpaka ofisini kwa mkuu wa shule akaenda sema nimemtukana na kumdhalilisha mbele ya darasa. Nikasimamishwa shule kwa muda wa mwezi mmoja nirudi na mzazi. Nyumbani mzazi ambaye ni mama alikuwa kasafiri kumuuguza bibi Muhimbili hospital na ilimchukua miezi mi3 na nusu kurudi ndio tukaenda shule. Nafika shule bado wiki moja mtihani wa kidato cha pili wa taifa ufanyike.

Nilifanya mtihani kwa kweli nilifeli, nilikosa wastani wa alama moja kuingia kidato cha tatu. Nikalazimika kurudia kidato cha pili. Wakati wote huo nilikuwa simjui kabisa mwanaume. Wakati nipo nyumbani kusubiri mzazi twende shule kuna mtu mmoja alikuwa anakuja kunisalimia kila mara ambaye ndiye aliyekuwa kaka mkuu wa shule(headboy).

Na hata nilipofeli alijitahidi sana kunishauri na kunitia moyo maana nilimwambia mimi sikumtukana mwalimu ila sikupenda tu kucheza ngoma nk. Basi kaka mkuu akasema kama unaweza kuwa unabaki shule jioni nitajitolea kubaki ili nikufundishe ufaulu mtihani wako wa marudio. Nikaona ni jambo jema nikawa nabaki na yeye anabaki tunasoma (ni wengi walikuwa wanabaki shule mpaka saa 12 sio jambo geni hivyo sikuogopa)

Twende kwenye kisa kamili

Wiki ya kwanza tukasoma vizuri sana na kwa kuwa yeye ndie aliyekuwa kinara wa darasa lao kwa kipindi hicho yeye alikuwa kidato cha 3 ila alikuwa na akili sana kiasi kwamba walimu walikuwa wanamwambia atusaidie wengine. Basi hata tulivyokuwa tunasoma wote hakuna aliyeona ajabu na tulikuwa tunatoa dawati nje tunasoma hapo nje hivyo hakukuwa na shida yoyote ile.

Wiki ya pili akaniuliza hivi huwa unapewa hela ya kula shule maana sijawahi kukuona ukila chochote? Nikamjibu mama yangu hana uwezo wa kunipa hela hivyo nashinda njaa mpaka nirudi, ada tu ya kurudia kagoma kunipa hata sijui nitaitoa wapi. Basi akasema usijali mimi mwenyewe wazazi wangu masikini sana ila napambana mwenyewe weekend nagonga kokoto nauza na pia huwa nawachotea watu maji au kuwabebea mizigo hivyo napata hela nanunua nguo, madaftari, ada nk.

Akasema sasa hela ya kula nitakuwa nakupa na ada nitakulipia nikafurahi balaa (Ada ya shule ilikuwa 40,000 kwa mwaka day school) ada ya mtihani wa Taifa sikumbuki vizuri ila kama ilikuwa 20,000. Akasema aliuza kokoto akapata laki moja hivyo atanipa kesho yake ada na ya mtihani nikaona kama Mungu kaniletea malaika, kunifundisha bure, ada na ada ya mtihani jumlisha hela ya kula kila siku.

Basi nikaendela kusoma kila asubuhi ananiletea mtihani nafanya muda wa mapumziko nampelekea anasahihisha na kunifundisha nilipokosea past papers kibao napewa mpaka wanafunzi wenzangu tuliorudia wote wakaanza kuona wivu.

Ikifika saa nne naletewa 1,000 nikale mapumziko yaani nilijiona kama nimebadili maisha hivi. Ilipofika ijumaa ya wiki hiyo Akanikabidhi hela ya ada kamili kabisa nikalipa. Nikaenda kumwambia mama nimelipiwa ada; mama akanifokea sana na kuniambia nimrudishie hela zake na nikatishe mawasiliano na huyo kaka sio mtu mzuri kwangu, mama akaniuliza kama kashaniambia chochote nikasema hapana.

Basi sikumsikiliza mama wala nini nikakaa kimya maisha yakaendelea, nikaanza kufaulu na kushika nafasi ya KWANZA darasani, waalimu mpaka wakaanza kunitolea mfano wa kuigwa kuwa mtu ukiamua kusoma unafaulu kama mimi. Siku moja Kaka Nkuu akanambia anataka weekend moja twende kwao nikapafahamu yeye kwetu anapajua. Basi nikadanganya nyumbani kuwa naenda Kanisani maana kutoka nyumbani ni kama unatoka gerezani ni ngumu mno.

Tukakubaliana nikitoka niende shule nyuma ya vyoo vya walimu tutakutana hapo saa 3 asubuhi. Basi nikaenda Kanisani kweli ili kuweka ushahidi kuwa kweli nilikwenda na kumuomba ruhusa sister kuwa naumwa narudi nyumbani nikasepa kwa kwenda kwa kaka mkuu. Nikamkuta kakaa ananisubiri, basi akanibeba kwenye baiskeli tukaenda hadi kwao nikawakuta wazazi wake na ndugu zake akanitambulisha kwao kuwa mimi ni mwanafunzi mwenzie nk huwa ananifundisha nk. Basi tukanywa chai kisha akawaaga ananirudisha nyumbani.

Wakati tuko njiani akasema nataka twende kwa yule rafiki yangu anaesoma shule fulani twende kwao tukachukue notes angalau uone mji wewe kwenu tu siku zote nikamwambia nikichelewa nitapigwa sana akasema huchelewi basi tukaenda...... Kumbe kashampanga mwenzie aondoke aache mlango wazi yeye atakwenda. Basi tukafika huyo mwezie alikuwa kapangiwa chumba na wazazi wake wanakaa kijijini yeye anasoma mjini hivyo lilikuwa ni geto.

Basi tukafika piga hodi kimya, akauliza kwa majirani akaambiwa kaenda sijui wapi alikuwa hapa hapa naona hata mlango hajafunga ingieni tu atawakuta, basi tukaingia ndani, kuna kitanda na kiti na meza na jiko la mchina (la mafuta) tulipofika mle ndani akaanza kunitania yaani hapa mimi ndio baba mwenye nyumba na wewe mama mwenye nyumba hebu pika ugali faster tule basi, yeye kakaa kitandani mimi kwenye kiti. Basi tunacheka mara akatoa karatasi akasema njoo uone hii hesabu ukiiweza kui-solve nakupa 1,000.

Basi nilipofika pale badala ya kunionesha swali akanikumbatia, nikataka kujitoa akakaza mikono akaniuliza ina maana bado hujaelewa kuwa nakupenda? Nikashangaa akasema nakupenda tafadhali nipe nafasi sitakuumiza. Basi nikaanza kupambana kutoka. Kiumbo nilikuwa mdogo kama ambavyo umri nilikuwa mdogo pia, alinibembeleza sana sana kwa machozi huku kanishika mwisho akasema anafanya kidogo wala haitanidhuru chochote, mbona amesaidia sana mpaka nafaulu nk mimi nakuwa sina huruma kiasi cha kushindwa kumsaidia yeye mimi binadamu gani.

Nikakubali kwa sharti la kufanya kidogo tu, ndio ukawa mwanzo wa penzi. Siku hiyo nikatolewa bikra yangu kizembe kabisaaaaaaaa na kisha kubembelezwa kwa vizawadi zawadi na kurudishwa nyumbani kufika nyumbani nikachezea kichapo heavy kutoka kwa mama sitasahau kichapo kile. Kumbe wakati napigwa nalia Kaka Mkuu (naomba nimuite R) hakuwa mbali na nyumbani alibaki kusikiliza nini kitatokea, baada ya kichapo kukamilika mama akasema rudi ulipotoka ni saa 2 usiku.

Nikatoka ndani nikazunguka nyuma ya nyumba huku nalia nawaza nifanye nini namlaumu R kaniletea balaa, kidogo nasikia jiwe limetupwa karibu yangu naangalia alietupa naona mtu kajificha kwenye mti ananioneshea ishara njoo, namuona kupitia mwanga wa taa za nje za jirani kwambaliii maana kwetu hakukuwa na umeme. Nikatoka hapo kwa kunyata mpka pale alipo akanambia tukimbie na mimi nikajikuta nafata maelekezo yake tukakimbia kuelekea kwenye giza zaidi.

Tulipoona tuko salama tukaanza kuongea akasema nimesikia umefukuzwa usijali turudi kule tukalale tukaondoka mpaka kule jamaa yake akatupisha akaenda kulala kwa mwenzake sisi tukalala mle ndani ila hakunigusa mpaka asubuhi. Asubuhi saa 12 akanambia turudi kwenu nitakwambia cha kufanya, tukarudi mpaka karibu na nyumbani kulikuwa na jengo moja halijaisha kujengwa akasema ingia humo lala jigalagaze uwe vumbi tu kisha tulia humo humo anza kulia yeye akasema atakuwa maeneo ya karibu kuona kinachotokea.

Kumbe akaondoka kwenda kwa mtoto mmoja tulikuwa tunasoma shule moja akamtuma aje nyumbani kunitafuta yule mtoto alipofika akakuta mama yupo na majirani anajilaumu kunifukuza kumbe yeye alikuwa ananipiga bit halafu mimi nikasepa mazima, alipofika akaambiwa hebu jaribu kumtafuta kwa wenzenu sisi tunaenda Polisi wakati anarudi akampa taarifa akamwambia rudi kawaambie yupo mle kwenye jengo anaogopa kurudi atachapwa, wakaja wakanikuta mle jengoni wakaniuliza nililala wapi nikawaambia humu nishachuma majani ya mti kuweka kama mtu alilala wakaamini watu wakamsema mama nikarudi home.

Basi tukawa tunabaki kusoma na mapenzi yakaanza; mara tushikane mara hiki mwisho nikawa natamani kumuona tu nashinda darasani kwao mpaka nafukuzwa na waalimu. Mtihani wa mwisho matokeo yalitoka mazuri sanaaaaa. Nikaingia kidato cha 3 hapo sasa ndio kasheshe lilianza.

Mapenzi yakanoga kweli kweli yaani ukisikia mapenzi ya kihindi ndio yale. Tulishindwa kuficha ikawa shule nzima wakajua kuwa natoka na Headboy na walimu pia ila wakawa wanashindwa kutufukuza maana yeye kidato cha nne ndio anategemewa kuleta one ya kutokea Sayansi na mimi kidato cha tatu ndio nishakuwa nyota wa darasa. Waalimu walishatuchapa, tushauri ila wapi tulijitahidi tu kupunguza ukaribu tukiwa shule na tukatengeneza njia za kuwasiliana yaani herufi tulizipa namba, mfano A tuliipa alama ya 00, B ilikuwa 2 kwa hiyo nikiandika 200200 ni baba hivyo tulikuwa tunatumiana vi memo vya hivyo kupitia kwa marafiki ambao walikuwa wanajua uhusiano wetu.

Tukitoka shule hatubaki tena kusoma tunaondoka kwenda kutembea ananibeba kwenye baiskeli hao kutembea, alininunulia nguo ambazo alikuwa anakaa nazo yeye anakuja nazo nabadili kwenye vichaka tusepe. Siku moja tuko matembezini uso kwa macho na mama hata sijui alifata nini maana tulikuwa tunaenda kutembea mbali na mazingira ya kawaida kila siku yaani tulikuwa wajinga. Ila hatukuwa tunafeli yaani nilijikuta nafaulu tu japo nguvu ya kusoma nilipunguza ila nilikuwa nakuwa wa kwanza.

Tukamkimbia mama tukidhani hajatuona na niliporudi nyumbani mama wala hakuniuliza kitu nikajua hakutuona nikapata amani tukalala asubuhi mimi yule shule. Saa 3 kengele ikagongwa iliyoashiria shule nzima tukusanyike tukajiuliza kuna nini mbona kengele imegongwa tukatoka kuelekea mstarini mara namuona mama kasimama na walimu nikataka kukimbia, R akanioneshea ishara tulia nikatulia.

Basi mwalimu wa nidhamu akasimama akasema kuna mwanafunzi anaitwa Gladnes (sio jina langu halisi) anasoma kidato cha tatu mchepuo wa sayansi aje hapa. Nikageuka nikamtazama R akanioneshea ishara nenda. Nikatoka mbele ile kufika tu mama akavuta fimbo iliyokuwa mkononi kwa mwalimu nikala za ovyo ovyo kama 10 hivi bila kujua kosa. Kisha akaanza kuongea kwa hasira kuwa alituona niko na kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi wa hapa anavyohisi na tulikuwa tunatembea huku tunafanya mambo ya ajabu ajabu ya kiutu uzima, KIJANA njoo mbele mama huyo walimu wanajua anayetafutwa nani na wanafunzi pia wanajua ila wote walikaa kimya. Mama akanizaba kibao yuko wapi huyo mjinga mwenzio mimi nalia tu huku nimeinama chini. Mwalimu mmoja akasema “huyo kijana ni yupi?” Nikajibu hasomi hapa, anasoma shule fulani.

Nikamtetea walimu wakanichapa karibu walimu wote mbele ya shule kwa kweli nilikula kichapo heavy na kupewa adhabu ya kuchimba kisiki. Mama akaondoka wanafunzi wakarudi darasani, waalimu wakamwita R wakamwambia unaona huyu binti alivyo mshenzi ana wanaume mpaka shule nyingine na leo alikuwa anafukuzwa shule sema mzazi wake kamuomba sana asamehewe. Basi R akaomba radhi na kusema kashaachana na mimi muda tu na wala hayuko nami ndio maana hata kunifundisha kaacha. Kumbe huwa swali likinishinda namuuliza tukiwa kule geto maana kila weekend natoroka naenda kwake(Alimshawishi kaka yake mmoja ampangie chumba eti ili awe anajisomea kwenye umeme maana kwao pia kulikuwa hakuna umeme) so hapo tukawa kama tumeanza maisha maana nami nina funguo na nguo zangu kule.

Basi baada ya tukio lile sikwenda shule kama siku 5 yaani wiki nzima naona aibu japo nyumbani nilikuwa natoka napitiliza geto kwa R nakaa napika akirudi anakuja na madaftari ya watu wa form 3 naandika na yeye ananiandikia na kunisahihishia nikirudi home nimeandika kumbe shule sijaenda wala nini. Wiki iliyofuata nikaenda shule nachechemea nikasema nilipigwa sana tena nyumbani mpaka nikaumia mguu nikashindwa kwenda shule kumbe hola nilitafuta gia tu ya kutokea.

Maisha yakaendelea, tukatafuta eneo la kukutania porini kabisa yaani sijui tulikuwa tunawaza nini( Nilipita huko mwaka juzi sasa watu ndio wamenza kujenga na nilikuwa na mama nikatamani kusema maana nilijikuta nacheka tu ila nikashindwa kumwambia) Kule tuliapaita WAPI? Ni eneo ambalo liko nje ya mji watu walikuwa wanaenda huko kuokota kuni na kuchunga kifupi ni porini kuna miti mingi sana hata mtu akisema akuue anakuua na huwezi pata msaada maana watu hawapiti mara kwa mara huko.

Nilikuwa natoka shule saa 8 na nusu, nakimbia mbio sana nyumbani nikifika nakuta hakuna aliyepo nyumbani wapo kwenye mihangaiko, naingia naweka begi natoka mbio nawahi sehemu ambayo ni njia ya kwenda huko namkuta ananisubiri ananibeba kwenye baiskeli hao porini tutakaa huko tutacheza wakati mwingine tunakulana hukohuko kisha ananirudisha mpaka karibu na home saa 12 niko home(najaribu kufupisha visa) watu walisema mpaka wakanyoosha mikono juu wakaniacha wakabaki kusema madam anafaulu basi.

Kufupisha story,

Siku moja tukiwa porini tulienda weekend na kwa kipindi chote hicho nyumbani nilikuwa nakula usiku tu! Mchana ananilisha na gharama baadhi ananigharamia, alikuta kanunua kamera anapiga picha wanafunzi na hivyo nilikuwa na picha kama zote. Sasa tukiwa kule porini alikuja na chakula wali na nyama, ile kafungua hotpot mimi nikahisi harufu kali sanaaaaa nikashikwa kichefuchefu tapika sanaaaaaaa.

Hata hamu ya wali sitaki kuona akaniuliza una shida gani? mwezi huu umeingia mwezini nikajibu niliona kama damu ila haikuendela mpaka leo, Akasema au una mimba? Kidogo akatania mimba zangu hazipo hivyo ungekuwa na mimba wewe ungekuwa umelazwa maana zinasumbua balaa tukacheka akasema twende ukapime.

Tukaondoka hadi maabara akaenda ongea na nesi nikaitwa majibu yanatoka nina ujauzito tena nesi anasema mimba yenyewe itakuwa na zaidi ya mwezi hii. Akaongea na nesi atusaidie tuitoe nesi akasema sawa njoo na 50000, tukaondoka nimepoa kama mawazo kibao ila yeye ananitia moyo kuwa itatoka na mambo yatakuwa mazuri. Akanambia hatakuja shule siku 3 anaenda kufanya kazi apate hiyo hela basi tukaagana nikaenda home. Nikaanza kujificha nisikutane na mama uso kwa uso maana alinambia asije akaniona akajua kuwa nina mimba.

Basi alipoenda kwao usiku uleule baba ake mzazi akapata ajali mbaya akalazimika kwenda kukaa nae hospital zoezi la kutafuta hela likafa tena bila mawasiliano maana simu hatukua nazo ndio zilikuwa zimeanza anza miaka ya 2000. Huku mimi nikaa siku tatu nikajua ya nne atakuja shule kunipa kinachoendelea ila sikumuona hadi wiki ikakata nikasema au kanikimbia nikajawa na huzuni na wasiwasi nikaanza kujuta.

Nikaondoka hadi kwa mama yangu mdogo nikamweleza ukweli kuwa nina mimba naomba msaada wa kutoa, mamdogo akanifokea ila akamwambia mama ananiomba nimsaidie shughuli kwake kwa wiki moja mama akakubali nikawa natokea kwake naenda shule. Ma dogo hakuwa na hela ila alikua anajua dawa za kienyeji za kutoa mimba. Akachemsha ya kwanza kunywa ikagoma nikaumwa tumbo tu, alibadili dawa moaka ambazo alisema hizi mtu mwenye mimba ya miezi 9 akinywa anapata uchungu anazaa hivyo nataka upate uchungu uzae tuila wapiiiii. Mara ya mwisho aliniletea moja aliyotoa kwa wasukuma nilipokunywa na kuweka ukeni niliona kizunguzungu mpaka nikapoteza fahamu ila mimba haikutoka.

Wiki ya tatu ndio R anakuja shule ananiambia kilichojiri akasema amepata sh. 70 kesho nisije shule nipitilize kwa nesi, yeye nitamkuta huko. Kweli tulikutana huko, Nesi akamuita dokta dokta kunishika tumbo akasema hiyo mimba ina miezi 3 hawezi kuitoa kwa 50000 labda kwa kutusaidia kama tuna 100000 sawa, R akamwambia amuongezee 20000 akagoma kabisaaaaaa, ikabidi R aombe siku 3 ili akatafute 30000.

Basi tukaondoka Rhakuja shule siku 3 ya nne akaja akasema kapata na ana 10000 ya ziada atanipa ya kununulia matunda wakati najiuguza kesho yake tukaenda kwa dk. Akachukua ile laki, nikapandisha kitandani akaanza mara akasema aisee hii mimba nikiichokonoa huyu binti anakufa siwezi imekaa vibaya sanaaaaa. Niliishiwa nguvu nikabaki kulia tu. Akarudisha hela.

Tukatoka na R pale nje akanambia mimi wiki ijayo nafanya mtihani wa mwisho usiogope Nakupenda sana nikimaliza shule nakuoa utajifungua ukiwa kwangu nina uwezo wa kukulea hata usijali. Basi nikaenda nyumbani huku najipa moyo.Kumbe mama ameshaona nina mabadiliko na alikuwa ananisubiri nirudi ili twende hospital yeye hata kwenye biashara zake hakwenda ananisubiri mimi.

Nimefika akasema vua nguo za shule mguu kwa mguuu zahanati nataka kujua mabadiliko yako yana nini kimejificha, Nikakumbuka nesi aliponipima aliomba mkojo tu nikasema sasa mama leo nakuchezea akili utanisamehe. Nikamuita mdogo wangu wa kiume tunayefatana nikamwambia naomba kakojoe mkojo wako weka kwenye chupa niletee mama asione na usimwambie mtu ntakuleta ubuyu nikitoka shule, akakubali akafanya kama nilivyomwagoza, mimi ndani nikauchukua mkojo nikaweka kwenye mfuko wa plastiki kisha nikaudumbukiza kwenye mfuko wa chupi, kuna chupi zilikua na mfuko kwa mbele.

Nikatoka ndani kwa kujiamini kabisa tukaenda hospital, wakaomba mkojo nikaenda chooni nikamimina mkojo nikapeleka, kupima sina mimba japo nina dalili zote za mimba basi tukaondoka kurudi nyumbani huku mama haamini kile kipimo kama kilitoa majibu ya kweli. Akaniacha siku 1 siku inayofuata akanifata shule akanambia kuna dk nataka twende akakuone unaumwa nini maana wewe sio mzima utakuwa unaumwa sio kwa kulala huko na kutapika kila muda nikataka kukimbia akanidaka mkono akanishika vyema alinikokota moaka kwa dk. Yule daktari jama alisema tu mama sina haja ya kumpima mkojo kwa kumuona tu huyu ni mjamzito labda apande nimshike tuone ina umri gani, akanivuta kwa nguvu akanilaza kitandani akashika tumbo akasema mimba kubwa kabisa hii inaelekea miezi mi4 .

Mama akakaa chini akaniuliza mimba ya nani nikakaa kimya daktari akasema nenda nyumbani kazungumze naye taratibu atakwambia , mama akaanza kulia baba yako kufariki ndio unanisumbua hivi hivi angekua hai ungeleta momba nyumbani kweli. Alilia mpka nikajiona mjinga mara mia nikajutia ila sina jinsi ya kuitoa tumbini mwangu. Kwa kweli niliomba msamaha na kusema kuanzia siku hiyo naachana na R iwapo mama atanisamehe ila sikusema kwa sauti. Maana kimsingi nilishajiapiza sitamtaja hata waniue.

Tukarudi nyumbani wala sikuulizwa wala nini ila mama akawa hanisemeshi yaani hata nikimuita haitiki kifupi kaninunua. Baada ya wiki mbili kupita mama akaanza kuongea na mimi na kuniuliza shule itakuwaje nikamwambia mama nikizaa, nitasoma tu hata elimu ya watu wazima. Mama aliishia kunitukana tu kuwa nimeharibu maisha yangu nikakoma nitahangaika mpaka nikome.

Mawazo na majuto juu yametawala usku kucha nakosa usingizi nalia mpaka mama akaanza kuona huruma na kusema utaharibu mtoto, hebu kaa tulia ndio ushayavulia nguo yaoge unalia nini wewe si umeona bora mtoto kuliko elimu msubiri acha kumliza humo tumboni. Mama akanipeleka Kliniki na kuninunulia ngua za kuvaa wakati wa ujauzito nk. Akapiga moyo konde akaanza kunifariji kuwa nikizaa ataona jinsi gani nitasoma hata kama kunipeleka kwa mjomba alienda shule walimu wakamwambia aandike barua kuwa naumwa ugonjwa ambao siwezi hudhuria shule ili mwaka unaofuata nipewe uhamisho nikasome shule nyingine. Asante sana mama yangu ulisimama hasa kipindi hiki.

Siku moja mama akasema ngoja twende tukatafute mchicha mana nilikuwa nakula mchicha na ugali mboga zingine siwezi, mara ghafla tunaona piki[iki inapanda upande wetu kuangalia vizuri namuona R anashuka na mizigo nikastuka nikamuoneshea ishara aondoke ila wapi ndio akaniita kabisa nusu mkojo utoke. Basi mama akasema turudi kwanza kwani nani huyo nikasema alikuwa anasoma shuleni kwetu ila kamaliza hivi juzi juzi.

Basi akasalimi vizuri akapewa kiti akakaa, akaanza kujieleza yeye nani na kusema kuwa yeye ndio mwenye huu ujauzito wangu na anaomba radhi kwa utovu wa nidhamu ila anaomba achukue jukumu la kulea ujauzito na mtoto iwe kwa kunichukua wakati huu au kwa kulea nikiwa nyumbani na kama kuna adhabu basi yupo tayari kuikabili aliongea kwa hekima sana na unyenyekevu kiasi kwamba mama akainama akasema kijana ndio nimeambiwa umemaliza kidato cha nne unaweza kulea mimba? Akajibu ni ngumu ila sina jinsi inabidi nijitahidi. Mama akasema hata nikikufunga sina bnitakachopata la msingi nenda ukipata chochote mletee mwenzio ili mimba ikue mtoto azaliwe.

Akatoa sh. 100000 akanipa mama akamuuliza umetoa wapi akasema anafanya kazi za vibarua pamoja na kupiga picha. Mama akasema angalau una akili ya kutafuta hela. Akaruhusiwa kuwa anakuja kuniona na wakati mwingine ananichukua ananitembeza yaani ikawa full amani kata yake na mama. Akanipeleka kwao ndugu zake na wazazi wake wakanipokea, wakaanza hadi kuja nyumbani kuniona.

Matokeo yakatoka R ana division one ya 12 akapangiwa shule uzuri hakupangiwa mbali na mimi miezi ikatimia nikajifungua mtoto wa kiume mwenye kilozake za kutosha kopi ya baba yake. Baada ya hapo nikanyonyesha miezi mitatu R akaomba anichukue nikaishi nae. Alipangiwa beni ila akaomba asome day akaanza day anatoka anenda shule akirudi ananikuta nyumba maisha yalienda mpaka mtoto alipofikisha miezi 6.

Siku moja R akaja nyumbani na fomu ya shule ya private akasema nimekutafutia nafasi shule hii nishapata nimeongea na kaka kakubali kukulipia ada nataka usome ili mama afurahi. Dogo utamuacha na mama nisaongea nae kakubali utakuwa unamnyonyesha ukirudi. Basi kwenda kumapa mama yangu taarifa hiyo kwa kweli alifurahi moaka akaruka akasema sasa mwanangu soma na mimi nitawasaidia chakula nitakuwa nawaletea unga na mchele na mboga nikipata.

Mama alienda ile shule ya mwanzo akachukua uhamisho nikkaenda kuendelea kidato cha nne, nilisoma huku nanyonyesha mwanangu mpaka nikamaliza kidato cha nne na huku nikiwa nimeolewa. Yeye naye aliingia kidato cha sita na mimi matokea yakatoka nikiwa nimepata divion 2. Nikapangiwa kwenda kidato cha tano mkoa tofauti na nilipkuwa nikiishi. R alisikitika sana nikiwemo na mimi tusema tutafute nafasi ya kuhama ila ikashidikana mwisho tukakubaliana atakuwa anakuja kila baada ya wiki mbili.

Mtoto akachukuliwa na mama yangu maana bibi yake upande wa baba alikuwa hawezi lala na mtoto usiku maana alikuwa anauza biashara stesheni usiku. Baba wa mtoto yaani R Akasema atakuwa anapeleka matumizi na kwenda kumuona mtoto kila baada ya siku mbili. Nilimuachisha kunyonya huku nilipopona kifua nikaenda shule.

Nilianza kusoma kidato cha tano bila shida na R kama alivyoahidi alikuwa anakuja na kipindi hicho kashanunua simu na mimi kaninunulia nilikuwa naificha tunachat usiku akija jumamosi ilikuwa siku ya kutoka tunakutana mjini tunaenda gest tunakulana anarudi mkoa. Na mtoto alikuwa anaendelea vyema anaenda kumuona na kupeleka matumizi kifupi alikuwa anatimiza majukumu yake bila shida yoyote mpka mama alikuwa anasifia anasema mwanangu umepata mme mwema japo bado wadogo.

Nirudi nyuma kidogo, yeye alipomaliza kidato cha sita alifaulu kwa kupata division one tena akawa anasubiri kwenda chuo, japo yeye hakuwa anataka kwenda chuo alitaka aende ualimu ili apatewazazi wakamkatalia ajira fasta anioe kabira rasmi, wakamwambia aende chuo, wakati huo alikuwa kafungua kituo anafundisha tution anapata hela kifupi alikuwa mpambanaji sana.

Nilipofunga shule ile likizo ya kidato cha tano kwenda sita nilifikia kwake nyumbani nilienda kusalimia tu kifupi nilikuwa nishahama nyumbani japo dogo alikuwa kashanisahau hanitaki nikawa naona huzuni ila basi tu sina jinsi yeye na bibi tu na alishatembea na kukimbia tayari.

Nikaondoka kurudi kidato cha sita na R alikuwa kajiunga chuo kikuu cha Dar es Salaam. Tukawa karibu zaidi kiasi kwamba naweza kwenda Dar na kurudi shule kwa siku moja bila shida kabisa. Siku moja nimeenda kumtembelea nikamkuta kalala ananambia anaumwa nikamsindikiza hospital akapimwa akakutwa na malaria akapewa dawa. Nikapanda gari kurudi shule, jioni yake akazidiwa sana kiasi kwamba akakimbizwa muhimbili akiwa hajitambui kabisaaaaa, wazazi wakapewa taarifa kuwa R kazidiwa mama yake akapanda gari kwenda Hospital.

Akawa anapatiwa matibabu ila hawakugundua shida zaidi , akaweza kuongea akasema naomba mpigieni simu Gladnes niongee nae usku nikapigiwa simu nikaongea nae akasema anaumwa sana na hajui anachooumwa Nijue tu ananipenda sana na anaomba nijitunze kwani kwa kuumwa kwake anaweza chukua muda hatujaonana maana atashindwa nitumia nauli ya kwenda na yeye hataweza kuja mpaka apone.

Kwa huzuni kubwa Usiku huo alifariki dunia😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭 Nilipigiwa simu usiku wa saa tisa kuwa R hatuko naye tena tenaaaaaaaa Nilihisi maumivu makali moyoni nililiaaa mpaka matron akastuka akaja akanikuta na simu na akaniuliza unalia nini nikasema mme wangu kafaaaaaaaaa! Mtron akauliza ina maana umeolewa mimi hapana rafiki yangu akanisaidia ni babu yake ila alikuwa anamuita mke wake maana kafanana jina na bibi yake kidogo matroni akaelewa na kunituliza kisha akachukua simu maana haturuhusiwi ila baadae akasema kama utaenda msibani nenda nayo ila isirudi na nitakukagua.

Kesho nikapewa ruhusa kwenda msibani nikasafiri hadi nyumbani tukaondoka na mama na mwanangu kwenda msibani, tukalala kesho yake maiti ikaja sikuamini kama kweli nilihisi naota ila ndio ukweli akazikwa nilikosa raha nilikonda kama uzi niliona kama dunia hainitaki nilitamani hata na mimi niumwe nife ila mwanagu nikimfikiria najipa tumaini jipya na vile alivyo kopi ya baba.

Nikaa wiki nikalazimishwa na mama kurudi shule yaani nilirudi huku moyo hautaki. nikasoma nikamaliza kidato cha sita. Nikaenda chuo nikasoma miaka mitatu nikamaliza, kipindi chote hicho nilikuwa single yaani sikuwa nataka mwanaume kifupi nilikuwa naona kama kuwa na mwanaume ni kumsaliti R.

Basi nipomaliza tu nikapata kazi hata sikupata shida ile kuomba tu nikapata kazi nzuri na hapo nikasema ngoja niwe na mwenza wakati huo nilisha mchukua mwanangu namsomesha. Kifupi mwanangu alikopi sura mpaka akili kwa baba ana akili sana sana Mungu anikuzie na kumtunza yaani.

Nikaingia kwenye mahusiano yaliyozaa ndoa, najuta kufunga ndoa jamani najuta mwenzenu, nilizoea kudekezwa na kubembelezwa huku nilkuja kukutana na mtu aliye fata mshahara maana hakuwa na kazi kama yangu kipato nilikuwa namzidi. Hela ikitoka anataka nitoe bank nimakabidhi nikimpa ananipa nauli tu na ananunua kila kitu kupitia hela yangu na kuacha 5000 ndani ya dharura mtu asiiguse mpaka kuwe na dharura yaani ukikataa kipigo kinafata niliteseka mpaka. Kibaya hela iliyobaki yake na yangu anaenda honga wanawake mpaka anawaleta ndani nyie acha tulikaa vikao mpaka ndoa ikavunjika.

Nikaa mwisho nimekuja pata Mwanaume mwingine anaenijali na kunitunza angalau ameufanya moyo wangu utlie na kuona nafuu. Nimeamua kuandika kifupi hapa mwisho maana nimechoka kutype.

Asanteni acha nifupishe hivyo, Sijutii kumpata mtoto yule maana ananipa raha kwa tabia na maendeleo yake ya masomo yupo fit Mungu anilele na kunitunzia.

R.I.P. Baba wa mwanangu.
 
Hata sijui nisemeje. Kwanza nikupongeze kwa njia ulizopitia na wewe akili unayo Mana kufeli kwako inaonekana Kuna tatizo lilikuwepo.
Ulivyopambana mpaka ukamaliza chuo. U mwanamke jembe kwa kweli.

Pia kwanza pole kufiwa na mme wako wa kweli wa dhati kabisa ambaye kiagano na kidini anajulikana kuwa ndiye aliyekufungua macho ya dunia.

Pole na unajitambua pigania furaha yako na maisha yako unayo mkononi jamani. Usijali kulea ndoa huku unateseka. Usione aibu kuachana na mwanaume ambaye hakupi hitaji lako.
 
Hata sijui nisemeje. Kwanza nikupongeze kwa njia ulizopitia na wewe akili unayo Mana kufeli kwako inaonekana Kuna tatizo lilikuwepo.
Ulivyopambana mpaka ukamaliza chuo. U mwanamke jembe kwa kweli.
Pia kwanza pole kufiwa na mme wako wa kweli wa dhati kabisa ambaye kiagano na kidini anajulikana kuwa ndiye aliyekufungua macho ya dunia.

Pole na unajitambua pigania furaha yako na maisha yako unayo mkononi jamani.
Usijali kulea ndoa huku unateseka. Usione aibu kuachana na mwanaume ambaye hakupi hitaji lako
Asante, huyu mwanaume wa ndoa nilishaachana nae nipo na mwanaume mwingine ambaye mwakani tunafunga ndoa
 
Pole, sana mkuu kwa hayo yote, R.I P R hakika jamaa alikuwa na mapenzi ya kweli sana kwako. Wanaume wachache sana Wa Sikh hizi wenye mapenzi ya kweli namna hiyo. Kweli kizuri hakidumu.

Lakin badae ulikuja kujua R alifariki kwa ugonjwa gan, malaria tu? Au. Mungu ambariki mwanao azidi kuwa na akili nzuri
 
Back
Top Bottom