Naomba Ushauri: Napoteza pesa mno nahisi kuchezewa

antanarivo

JF-Expert Member
Jan 9, 2018
448
870
Kwanza kabisa napenda kuweka waZi kuwa kila kitu katika huu Uzi ni ukweli mtupu na ndo Hali nayopitia katika maisha yangu

Pia Kuna Mambo utaona nilikuwa nafanya au naendelea kuyafanya kama mjinga lakini ndo najikuta nafanya hivyo so naomba mtu anayeweza kunishauri Basi azingatie yote haya

Back 2015:
Nilivotoka chuo tu nikarudi home nikakaa Kama wiki hivi ikabidi niondoke home kulingana na kuwa nimelelewa tu pale Ila sio wazazi wangu wa kunizaa ni walezi maana hakuna mzazi wangu hata mmoja ninayemfamu ,( Mungu awarehemu). Nilivotoka home nilienda kujitolea shule moja hivi kufundisha ambako nilipiga kazi almost miezi 6 hivi kwa makubaliano ya kulipwa 60k kwa mwezi lakini nililiowa mwezi mmoja tu mingine yote kwa lugha rahisi niite nilidhurumiwa,

2016 January nikatafuta kampuni moja Ivi ya kijasiriamali ya kuuza bidhaa kwenye mitaa na kwenye magari Kama umewahi waona jamaa wanaoongea Sana kwenye gari wakiwa wanauza bidhaa Basi ndo mfano wa hio kazi ambayo nimepiga kwa muda wa mieZi 6 kampuni ikafa. So Kuna vihera vichache ambavyo nilikuwa navitunza kama 150k Ivi ambayo kwangu ilikuwa kubwa kipindi hicho so nikapanga room 20k kwa miezi mitatu na iliyobaki nikanunua godoro malaika na shuka ,maana Kule kwenye kampuni tulikuwa tunahudumiwa kila kitu isipokuwa msosi , so nikaendeleza kazi yangu ya kuuza bidhaa kwa muda huu nikawa nanunua madukani na kwenda kuuza mtaani, nakumbuka nilianza na 16k Kama mtaji ambapo nilijumua sabuni za kuogea dazan mbili na mafuta ya kupakaa

Nilikimbiza miezi kadhaa mtaji ukakua kiasi chake ,ikabidi niachane na kuuza bidhaa nijiingize kwenye kufundisha masomo ya utengenezaji bidhaa kadhaa za ujasiriamali ambazo nilikulaga course ya wiki moja kipindi Niko chuo ,so nikawa naandaa semina for free lakini baada ya semina nauza vitabu ambapo ndo faida ikawa inapatikana hapo nilipiga kazi hio kwa miezi Kama mitatu hivi nikapata total kama milioni 8 hivi huku miezi imesogeasogea,katika pitapita zangu humu jf nikakutana na uzi wa jamaa anaitwa Ontario uloenda kwa heading ya biashara ambayo hakuna benki itataka uijue,baada ya kusoma ule Uzi nikavutiwa kwa kuwa fedha nilikuwa nayo Basi nikatenga milioni moja kwa ajiri ya nauli malazi na ada ya mafunzo kwa siku 5 za mafunzo pale jangid plaza

Nilifanikiwa kuhudhuria darasa siku Zote tano huku nikiwa nalala gesti maana ndo ilikuwa Mara yangu ya kwanza kuja dar.

Baada ya kumaliza mafunzo sikufanikiwa kufungua Acc yoyote ya kutrade sababu nilikuwa Sina I'd yoyote wakati huo ko nikaamua kupotezea ,nilivorudi mkoa ikabidi nifanye semina kadhaa ili nirudishe ile milioni niliyoitumia kwenye hio semina na nikafanikiwa kama nilivopnga na mahesabu yangu yakarudi Kama mwanzo ambapo nilikuwa na million 8+
Mwanzoni mwa 2018 nikatafuta mkoa utakaonifaa kwa biashara ya mtaji huo nikaona ni dar ambapo nilipanga kuanza na biashara ya miamala mpesa na tigopesa na huduma zingine ndogo ndogo baadae wakatangaza maombi ya kutuma ajira Mimi sikutuma coz nilikuwa tayari Nina plan ya kufungua biashara, kweli nikafanikiwa kusafiri mpaka dar na ilinichukua siku 4 kutafuta eneo laini za wakala na nyumba ya kuishi na kazi ikaanza

Nimeenda nayo ile kazi na kweli nilibarikiwa kazi ikawa inanilipa nikaongeza na huduma zingine za stationary na nikawa nazidiwa na wateja so nimeenda na hio kazi huku mtaji ukikua Hadi kufikia 12+milioni

Ilivoingia 2019 siku moja baba mwenye nyumba jioni kanitumia text kuwa nimuwekee 700k kwa namba yake jioni nikifika atanipatia so nikaona sio mbaya nikamtumia hio pesa aliyohitaji lakini ilivofika jioni kanambia hio hela alitegemea kuwa mtu angemletea lakini hakuleta so nimsubirie kidogo, kweli nikaona sio mbaya nikaendelea na mambo yangu lakini ile hela mpaka siku ya tatu jamaa bado hajanipa nikawa nafikiria namna ya kuirudisha ile pesa ili nisione pengo maana niliongeza huduma Za benk wakala pia

Njia rahisi nikaona kubeti licha ya kuwa sikuwahi kubeti hata siku moja huko nyuma

Nakumbuka siku hio asubuhi navojisajiri na app ya betting nikaona Kuna Liverpool na Barca wanacheza usiku so sikuchelewesha ikabidi ni deposit 500k kwenye ile acc ya betting na nikampa Liverpool kuwa ashinde

Lakini ilipofika huo usiku bahati haikuwa kwangu nikajikuta nimeloose yaani Liverpool kapigwa 3-0 nakumbuka ilikuwa mwezi wa tano 2019 ,hapo nikazidi kuchanganyikiwa na nikaanza kubeti ovyoovyo ili mradi pesa irudi na viwango nilivyokuwa naweka ni kuanzia 100000 Hadi 500000 na hakuna mechi nilizokuwa nawin baadae nilivoona mtaji imepungua nikapanga kuuza fremu na vifaa vyote vya kazi niingie mkoa nikatuli nianZe kufanya forex niliyojifunzaga kwa wasouth walioletwa na Ontario pale jangid plaza.

Nilikuwa kila nikijaribu kuuza haviuziki huku naendelea kubeti mpaka nikajikuta nimebaki na 2milion pekee ikabidi nistop kubet nihangaikie kuuza vitu vya ofisi na gethon

Nilipambana bila mafanikio wateja hawaonekani baadae nikahisi Nina mikosi nikaingia humu nikaseach mganga wa kienyeji ambaye angetoa mikosi nikaona Kuna mtu amewahi kucomment kwenye Uzi wa jamaa aliyekuwa anauliza naye mganga na alielekeza yupo huko bagamoyo ikabidi na Mimi nichukue ile adress nimfuate yule mganga nilifika usiku Kama wa saa nne hivi nikaenda kulala kwa jamaa aliyenipeleka na bodaboda ili asubuhi niamkie kilingeni

Asubuhi ilipofika nikaamkia pale nikawakuta wanamajengo Hadi ya kulaza wagonjwa nikawaona wale vijana na nikawaambia direct kuwa na nahisi mambo yangu hayako sawa naomba mnisaidie ili mambo yakae sawa wakanitajia vitu vinavyotakiwa pale kuwa ni kuku,Nazi na sanda nyeupe

Nikatoa ile hela ili vitu vikatafutwe Kama 45000 hivi Basi wakaanza kusoma vitabu vyao vya kiarabu huku waloniambia Mimi niwe nachoma udi na kusema shida zangu pamoja na kuziweka zile Nazi kwenye Moto Kama nazikausha fulani hivi

Shughuli ikaendelea baadae walivomaliza kusoma na mm kunuia ikabidi nikazipasue zile Nazi na nikavishwa ile sanda nyeupe nikaogeshwa na dawa Fulani hivi baada ya hapo wakasema tayar Mambo yako yatakuwa super wakanambia kuwa nirudi baada ya wiki mbili na wakagurantee kuwa hivo vitu ambavyo haviuziki Basi nitaenda kuuza

Nikachukua boda mpaka lami na hapo nikapanda Basi mpaka tegeta nikatafuta gari la kwenda gethon ,nilivofika nikaanza kupigiwa simu na watu wakiulizia vile vitu nilivyokuwa nimetangaza Sasa sikujua ni ile tiba au tu watu walipanga kunitafuta yaani kwamba hata nisingeenda labda wangenitafuta tu ilikuwa suala la muda so sikujua exactly hasa baada ya wiki nikawa nimefanikiwa kuuza kila kitu nikapata Kama 4 milion na ile milioni 2 iliyobaki nikawa kama na 6milion+

Nikarudi mkoa Nikatumia Kama 2.2milion kupanga na kununua vitu vyote vya msingi gethon tayari kwa kuanza forex

Wakati huo nikawa nimepata I'd so nikafungua acc kwa templer nadhani ambao ni trader wanamjua nikaanza kudeposit na kutrade na nilikuwa sijawahi kutrade hata demo nikaanza moja kwa moja real account huku nikawa nasambaza affiliate link za brokers tofauti tofauti so niliendelea na shughuli hizi mbili huku forex ikinibariki maana mwanzoni nilikuwa naprofit Sana na nikawa nawaza utajiri muda wote baada ya Kama wiki hivi nikaanza kuchoma acc kila nikideposit nachoma, nilichoma pesa zote nikabaki Sina kitu, baadae wakati napita YouTube nikaona habari moja ya kuwa Kuna mzee huko sumbawanga anatengeneza radi ambapo kwangu ikawa kigezo kuwa angeweza kunitoa mikosi na kung'arisha nyota yangu so nikachukua namba nikampigia akadai anaweza kunitatulia ile shida niandae 100k sikuchukua round nikaondoka asubuhi kupitia mbeya nikafika sumbawanga saa tatu usiku nikalala gest na asubuhi nikamtafuta yule doctor , akanipa tiba nikarudi lakini sikuona mabadiliko bado na Kuna dawa za kuoga alinipa kiukweli sikuona mabadiliko labda Kama yalitokea indirect

So nilivofika home ikabidi nianze kuuza kimojakimoja huku naweka forex nachoma baadae nikauza kila kitu nikadeposit na kuanza kutrade huku nalala gesti nawithdraw dola 20 nakula na kulipa gesti mtaji wote upo kwenye acc, nimeenda Kama wiki hivi hela ikaungua ikabidi nitoke gest niingie mtaani kutafuta vibarua yaani hapo hata Mia moja Sina na hakuna wa kumuazima hela katika kipindi niliona Cha mtemakuni Basi ni kuanzia October Hadi December 2019 ambapo nilikuwa nalala nje na kazi Sina mpka nikawa naomba watu njiani wanipe hata jero ya kula maana vibarua vikawa hamna kabisa Yani kila nikitafuta naambulia patupu, nikaja nikauza simu kwa hasara ilimradi nipate hela ya kujikimu , nikaanza kuingia migodini lakini ile kazi sikuiweza kwa maana hata abc zake nilikuwa sijui

Ikabidi niache nikakumbuka Kuna siku nilikuwa nasambaza affiliate link ikabidi nitoke huko migodini nije mjini kwenye internet cafe nicheki Kama kweli wanalipa, nikalog in broker wa kwanza ni zero ,wa pili naye ikawa zero huyu watatu ile nalog in tu nakutana na commission ya dola 240$ ambayo ni Kama 600k kasoro chap nikanunua simu na zilizobaki nikadeposit na kuanza kutrade ambayo nayo nikaichoma so mpaka leo hapa kati nimepitia mengi Ila huyu broker ananilipa commission nzuri ambayo kwa mwezi ni kati ya Dolla 200$ na 500$ na analipa kila siku lakini nachoshindwa kujizuia ni kuwa hii hela Nikilipwa naanza kuitrade na nachoma Hadi mwezi unaisha nakuwa Sina kitu yaani nimekuwa Kama addicted Fulani hivi maana naweza trade nikaprofit Hadi $1000 na muda mwingine naweza withdraw nikanunua vitu vya ndani lakini siku nikichoma najikuta nauza Tena vile vitu na kudeposit Tena ambapo naweza choma na kurudi sifuri Tena ko maisha yangu yanazunguka tu hapo hakuna Cha maana nafanya na hii Hali naichukia vibaya mno lakini kuacha siwezi kabisa ,

Mfano hapa nilikuwa naishi chumba Cha pango la 130000 na vitu vya ndani vya kupendeza baada ya Kodi kuisha nimeshindwa kulipa maana hela niliyoweka ya Kodi nimechoma so nilichofanya nikauza kila kitu nimaepanga room la 40000 na nimebaki na godoro tu na shuka na wakati getho lilikuwa full .

Yaani nashindwa kujua Nina shida gani nimeogea chumvi ya mawe wapi nimeenda kwa madoctor wa asili bado mambo magumu

Hatari niliyonayo saivi nikuwa Sina kazi nategemea commission wakinilipa ndo nakula na kutrade ambapo daily nachoma

Nifanye nini niweze kunyoosha mambo yangu jamani maana najikuta nazunguka palepale hakuna nachofanya

Mimi nahitaji niwe na mchongo mwingine nje na hii commission na nimekaa muda mrefu almost miaka miwili nazunguka palepale na hakuna Cha kufanya na vipi ukishakuwa addicted na jambo Fulani unaweza liacha kwa namna gani maana huwa nafutaga account lakini najikuta naZirudisha Tena

Sorry kwa Uzi mrefu

MFANO HII NI COMMISSION YA MWEZI WA 12 HUU YAANI TOKA TAREHE MOJA HADI LEOView attachment 2063570
View attachment 2063617View attachment 2063618
 
Angalau umetoa ushuhuda kuwa waganga wa kienyeji hawana msaada. Itawasaidia wengine kuepuka kuwatumia.

Hata hivyo maisha yako si mabaya ukiepuka tamaa unapotrade. Shida ni kuwa hujifunzi kutokana na makosa. Jiepushe kutrade ukiwa tayari una demand ya jambo kubwa linalohitaji pesa mfano kodi ya pango. Inashauriwa katika betting na forex utumie pesa ambayo hupo tayari kuipoteza.

Wakati mwingine ukipata pesa ingia ubia na mtu mwingine kwenye uzalishaji kuondoa uhuru kujiamlia kuuza vitu vyako mara kwa Mara.
 
Mkuu nimesoma uzi wako mpaka mwisho nikupe pole lakini pia nitoe pongezi kwa jamiiforums kwa kufanya platfom hii iwe msaada kwa wadau wengi sana kama ambavyo umeelezea ushauri uliopata kupitia chanzo hiki.

Jambo la kwanza ambalo binafsi naliona ndio tatizo kwako na pengine kwa watu wengi ni ile tabia ya kuuza uza vitu pindi uchumi ukiyumba. Uchumi ukiyumba haujiimarishi kwa kuuza products zako, kwasababu hivyo vitu ili vikuletee faida unapaswa kuviuza kwa bei ya juu zaidi ya uliyo nunulia, hapo ndio utanufaika.

Lakini ni swala ambalo haliwezekani TV ulionunua 700k ukaitumia miezi 3 afu leo ukataka kuiza ukaiuza zaidi ya 700k. Mara nyingi kwasababu una shida unajikuta hata bei unapangiwa utajikuta umeuza 300k na utaiona nyingi kwasababu moment unayopitia huna hata senti mfukoni.

Kingine maswala ya betting mzee hiyo attempt siji kumshauri mtu, mimi ni muhanga wa hilo. Kuna siku nilikua nimesanda mfukoni nina kama 30k hivi nikafungua JF nikakuta kwenye newsfeed uzi wa wazee wa kubet uko on top

Nikaufungua hapo nikakutana na comments za miamba na magwiji wa kubet, nakumbuka siku ile kulikua na mechi kati ya real madrid na ajax halafu ndio mechi ya kwanza kwa kocha zidane.

Niliposoma comments nikakuta kila mdau kampa real madrid na tena ukizingatia yupo nyumbani, wadau walikua wameweka list ya timu nyingi wanazozibetia na mimi hapo nikawa motivated, nikajisemea kwasababu mimi mgeni kwa hii tasnia ngoja nibet mechi moja hii hii ambayo kila mtu kamtabiria real madrid ushindi.

Nikaweka mkeka wangu wa 12k, mechi ikachezwa usiku mi nikalala. Asubuhi nacheki kuangalia meseji ya muamala hola, ingia live score nakuta madrid kachapika.

Kesho yake jamaa yangu wa kitaa akanishawishi tena nikawa inspired nikatia 5k mechi ya barcelona na real betis, nikam'betia barca ashinde naye aka draw, nikasema sheenzi 17k imepotea kindezi na ndio ukawa mwishio wa kubeti kuanzia saizi hata barcelona niiskie inacheze na mbeya kwanza kwa odds za nyingi siweki hela yangu.

Kwa hiyo mkuu unachokipitia wewe, ni wengi tumekipitia/tunakipitia ila tume sizi tu hatujaamua kushare na wadau changamoto zetu.

Ila mawazo ya kufikiria ushirikina hapo ndio umebugi man, sijajua ni kupagawa kulikokuja baada ya wewe kupoteza pesa au niaje

Kuna mwana aliibiwa pesa zake magetoni jamaa alikua very frustrated nikamshauri akapumzike atulize akili aakanielewa akaniachia simu yake akaondoka.

Kumbe jamaa alikua amefanya harakati nyingi za kumbaini mwizi na kurudisha hela zake

Wakati nipo na simu yake niliona namba ngeni ina piga kwenye simu yake na kwasababu ni mchizi wangu mwenye hiyo simu ikabidi niipokee.

Kumbe mchizi alifikia hatua ya kumpigia simu mganga na hakupokea na mimi nililoipokea ndio akawa ananielekeza kua yeye ni mganga na amekuta missed call pamoja na message

Basi namimi sikutaka nimuoneshe kama mimi sio mlengwa na kwasababu najua situation yote nikamchana nikasema ndio nimeibiwa nataka unirudishie pesa zangu

Mganga akasema sasa unatakiwa utoe 70k kwa ajili ya kununua material ya kuagulia, nikamuuliza "mzee si hiyo hela unaweza kuirudisha" akajibu ndiyo nikamwambia mimi hapa mpaka nimekupigia simu unirudishie hizo pesa ni kwamba sina akiba yeyote kwa hiyo kama inawezekana we ungekata huko huko kwenye zile hela nilizoibiwa hiyo 70k. Mganga akacheka halafu akakata simu.

Kwa hiyo mkuu utagundua wazo la kwenda kwa mganga ni kutengeneza mfereji mwingine wa kuzidi kupoteza hela tena.

Na hata hiyo ya kusema baada ya kutoka kwa mganga vitu vyako vikauzika mimi nakuambia haikusababishwa na mganga, ni juhudi zako mwenyewe. Ingekuwa ni mganga na ili kuthibitisha kua ni nguvu za kiganga zimetumika ungemwambia fanya uchawi nataka kuuza TV nilionua 700k kwa shilingi 2M

Nguvu yako ya kutangaza ndio iliyoleta wateja, siku zote biashara ni matangazo hata huyo mganga kwanini kaweka mabango mitaani yenye namba za simu mpaka jf? Kwanini asitumie madawa yake kuvuta wateja wakaenda bila kuweka matangazo, halafu ukifika kambini anakudanganya kua anayo dawa ya kuvuta wateja wakati kashindwa kukuvuta wewe uje kwake bila mabango aliyoweka mtaani

Na kwenye swala la forex ina maana hukuangalia malalamiko mengi ya wadau wakimtuhumu huyo mentor wako kwa ulaghai na utapeli wa kuwafanya watu waunguze accounts tena kwenye biashara ambayo una invest kiwango kikubwa cha pesa??

Wabongo wana kauli yao wanasema ukiitwa kwenye fursa ujue wewe ndio fursa, na nature ya wa africa inanifanya nikubaliane na kauli hiyo.

Kwamba sehemu yeyote yenye maslahi ya kweli muafrika hawezi kutumia nguvu kubwa hiyo kujitolea kuwapa maarifa wengine wanufaike na huo mchongo

Hiyo ni sawa na wale matapeli wa online global ambao wanakuambia wanakuuzia package ya dawa kwa 500k halafu unatengeneza pair ambayo kila mtu ukim invite utakua unajiingizia 50k kwenye account yako plus zile package unaweza ukaziuza ukapata double profit.

Ni wezi tu sema kwasababu wanalipa kodi inewaongezea ujasiri na watu imekua ngumu kuwabaini kwasababu wanafikiri ingekua sio scam wasingeruhusiwa na serikali
 
Kijana acha tamaa, wew hauna mikosi wala huhitaji matibabu ya kusafisha nyota, ni vile tu unatafuta pakutorokea matatizo uliyoyasababisha kwa tamaa zako.

Hawa waganga wa mijini mamission town watakuliza sana maana hawanaga lolote zaid ya utapeli, just imagine mtu umetapeliwa pesa ndefu, alafu mganga unamwambia akusaidie kurudisha pesa then madai yake atayakata kwenye ile pesa ikipatikana, mganga anagoma unajuwa kwanin? Kwasababu hana imani wala uwakika wa tiba zake kuwa zinafanya kazi zaid ya utapeli.

Acha papala kukurupukia mambo usiyoyajua, na ukiendelea na hiyo tabia basi juwa kabisa maendeleo utazidi kuyasikia kwa wenzako.

Unaonekana wew una jitihada za kaz lkn upumbavu wako wa kuamin kila mtu unakucost, pia matumiz mabaya yaan haujar kile upatacho, you spend more than what you invest, then unategemea nini kama sio kufirisika.

Kama kweli hii stori imekutokea basi rudi kwenu kijijin kajipange upya, mjin hapakufai maana utazid kupapalikia na mengine ambayo huyajui, mfano uyo mwana jf alichotolea uzi umu wew ukajiingiza kichwa kichwa bila hata kuhoji ukitegemea nini kama sio kuangukia pua..

Kwisha habari yako
 
Mkuu nimesoma uzi wako mpaka mwisho nikupe pole lakini pia nitoe pongezi kwa jamiiforums kwa kufanya platfom hii iwe msaada kwa wadau wengi sana kama ambavyo umeelezea ushauri uliopata kupitia chanzo hiki.

Jambo la kwanza ambalo binafsi naliona ndio tatizo kwako na pengine kwa watu wengi ni ile tabia ya kuuza uza vitu pindi uchumi ukiyumba. Uchumi ukiyumba haujiimarishi kwa kuuza products zako, kwasababu hivyo vitu ili vikuletee faida unapaswa kuviuza kwa bei ya juu zaidi ya uliyo nunulia, hapo ndio utanufaika.

Lakini ni swala ambalo haliwezekani TV ulionunua 700k ukaitumia miezi 3 afu leo ukataka kuiza ukaiuza zaidi ya 700k. Mara nyingi kwasababu una shida unajikuta hata bei unapangiwa utajikuta umeuza 300k na utaiona nyingi kwasababu moment unayopitia huna hata senti mfukoni.

Kingine maswala ya betting mzee hiyo attempt siji kumshauri mtu, mimi ni muhanga wa hilo. Kuna siku nilikua nimesanda mfukoni nina kama 30k hivi nikafungua JF nikakuta kwenye newsfeed uzi wa wazee wa kubet uko on top

Nikaufungua hapo nikakutana na comments za miamba na magwiji wa kubet, nakumbuka siku ile kulikua na mechi kati ya real madrid na ajax halafu ndio mechi ya kwanza kwa kocha zidane.

Niliposoma comments nikakuta kila mdau kampa real madrid na tena ukizingatia yupo nyumbani, wadau walikua wameweka list ya timu nyingi wanazozibetia na mimi hapo nikawa motivated, nikajisemea kwasababu mimi mgeni kwa hii tasnia ngoja nibet mechi moja hii hii ambayo kila mtu kamtabiria real madrid ushindi.

Nikaweka mkeka wangu wa 12k, mechi ikachezwa usiku mi nikalala. Asubuhi nacheki kuangalia meseji ya muamala hola, ingia live score nakuta madrid kachapika.

Kesho yake jamaa yangu wa kitaa akanishawishi tena nikawa inspired nikatia 5k mechi ya barcelona na real betis, nikam'betia barca ashinde naye aka draw, nikasema sheenzi 17k imepotea kindezi na ndio ukawa mwishio wa kubeti kuanzia saizi hata barcelona niiskie inacheze na mbeya kwanza kwa odds za nyingi siweki hela yangu.

Kwa hiyo mkuu unachokipitia wewe, ni wengi tumekipitia/tunakipitia ila tume sizi tu hatujaamua kushare na wadau changamoto zetu.

Ila mawazo ya kufikiria ushirikina hapo ndio umebugi man, sijajua ni kupagawa kulikokuja baada ya wewe kupoteza pesa au niaje

Kuna mwana aliibiwa pesa zake magetoni jamaa alikua very frustrated nikamshauri akapumzike atulize akili aakanielewa akaniachia simu yake akaondoka.

Kumbe jamaa alikua amefanya harakati nyingi za kumbaini mwizi na kurudisha hela zake

Wakati nipo na simu yake niliona namba ngeni ina piga kwenye simu yake na kwasababu ni mchizi wangu mwenye hiyo simu ikabidi niipokee.

Kumbe mchizi alifikia hatua ya kumpigia simu mganga na hakupokea na mimi nililoipokea ndio akawa ananielekeza kua yeye ni mganga na amekuta missed call pamoja na message

Basi namimi sikutaka nimuoneshe kama mimi sio mlengwa na kwasababu najua situation yote nikamchana nikasema ndio nimeibiwa nataka unirudishie pesa zangu

Mganga akasema sasa unatakiwa utoe 70k kwa ajili ya kununua material ya kuagulia, nikamuuliza "mzee si hiyo hela unaweza kuirudisha" akajibu ndiyo nikamwambia mimi hapa mpaka nimekupigia simu unirudishie hizo pesa ni kwamba sina akiba yeyote kwa hiyo kama inawezekana we ungekata huko huko kwenye zile hela nilizoibiwa hiyo 70k. Mganga akacheka halafu akakata simu.

Kwa hiyo mkuu utagundua wazo la kwenda kwa mganga ni kutengeneza mfereji mwingine wa kuzidi kupoteza hela tena.

Na hata hiyo ya kusema baada ya kutoka kwa mganga vitu vyako vikauzika mimi nakuambia haikusababishwa na mganga, ni juhudi zako mwenyewe. Ingekuwa ni mganga na ili kuthibitisha kua ni nguvu za kiganga zimetumika ungemwambia fanya uchawi nataka kuuza TV nilionua 700k kwa shilingi 2M

Nguvu yako ya kutangaza ndio iliyoleta wateja, siku zote biashara ni matangazo hata huyo mganga kwanini kaweka mabango mitaani yenye namba za simu mpaka jf? Kwanini asitumie madawa yake kuvuta wateja wakaenda bila kuweka matangazo, halafu ukifika kambini anakudanganya kua anayo dawa ya kuvuta wateja wakati kashindwa kukuvuta wewe uje kwake bila mabango aliyoweka mtaani

Na kwenye swala la forex ina maana hukuangalia malalamiko mengi ya wadau wakimtuhumu huyo mentor wako kwa ulaghai na utapeli wa kuwafanya watu waunguze accounts tena kwenye biashara ambayo una invest kiwango kikubwa cha pesa??

Wabongo wana kauli yao wanasema ukiitwa kwenye fursa ujue wewe ndio fursa, na nature ya wa africa inanifanya nikubaliane na kauli hiyo.

Kwamba sehemu yeyote yenye maslahi ya kweli muafrika hawezi kutumia nguvu kubwa hiyo kujitolea kuwapa maarifa wengine wanufaike na huo mchongo

Hiyo ni sawa na wale matapeli wa online global ambao wanakuambia wanakuuzia package ya dawa kwa 500k halafu unatengeneza pair ambayo kila mtu ukim invite utakua unajiingizia 50k kwenye account yako plus zile package unaweza ukaziuza ukapata double profit.

Ni wezi tu sema kwasababu wanalipa kodi inewaongezea ujasiri na watu imekua ngumu kuwabaini kwasababu wanafikiri ingekua sio scam wasingeruhusiwa na serikali
Umeongea vingi kwa mapana zaidi hongera sana, kuna kitabu niliwah kusoma think and grow rich, kile kitabu kimeelezea nguvu ya fikra (mawazo yetu), ukiwaza na kupanga vibaya unapata matokeo mabaya, ukiwaza na kupanga vzr matokeo mazuri ni yako.
Jamaa ana mkono wa hela, mishe mishe zake anazopotia unaona amewah kupata hela vizuri tu ila changamoto zake ni kama ifuatavyo:-
1. Ana akili ya kijadi (asili) kuamini amini ulozi katika maisha yake, ukisha waza upuuzi wa aina hii kwango changamoto ya aina yoyote ile unaiona mikosi, hata ukatoa hela bank ikatoka risti bila hela na hela ikakatwa moja kwa moja utawazia mikosi jambo ambalo la kawaida tu na ukifatilia hela inarejeshwa

2. Akili zake kuhimili hela ndefu kidogo bado, yani akipata hela kidogo zaidi ya awali anapata wenge, anaanza kutafuta namna ya kuitumbua badala ya kutumia hiyo faida kupanua kile alichokuwa akifanya na kumpa hiyo faida.

3. Alishalidhika na maisha ya kati na mishe mishe za kati, angekuwa na ndoto kubwa asingekuwa anamake na kuuza na kurejea lifestyle ile ile.

Ushauri wangu:

Inaonekana jamaa ana moyo wa kuhusltle, kushawishi na kutafuta, kwa sasa kuna watu wanaagiza mizigo mikubwa ya vitu used but clean toka Ulaya, ingia kwao chukua bidhaa zao nadi mitandaoni na groups mbali mbali za whatsapp, weka faida yako kidogo tu ili upate mzunguko mkubwa, ukifanya hili litakupa faida na huku ukiendelea na mishe zako, pia unajijengea mbinu na kipato cha kuagiza mzigo wako kama wao
 
Angalau umetoa ushuhuda kuwa waganga wa kienyeji hawana msaada. Itawasaidia wengine kuepuka kuwatumia.

Hata hivyo maisha yako si mabaya ukiepuka tamaa unapotrade. Shida ni kuwa hujifunzi kutokana na makosa. Jiepushe kutrade ukiwa tayari una demand ya jambo kubwa linalohitaji pesa mfano kodi ya pango. Inashauriwa katika betting na forex utumie pesa ambayo hupo tayari kuipoteza.

Wakati mwingine ukipata pesa ingia ubia na mtu mwingine kwenye uzalishaji kuondoa uhuru kujiamlia kuuza vitu vyako mara kwa Mara.
Hili neno:.."hupo" ...ulimaanisha "upo" au "haupo"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom