Why wasomi na waelewa hawapendi chama tawala?

kifupi ni kwamba ccm wame kaa madarakani miaka 40 nahakuna maendeleo yoyote yale wame fanya na wao wana jua kila siku waziri mkuu anasema kwamba tuna chekwa tuna shindwa na rwanda nchi ndogo wana taka maendelea kwa uchungu wa maendeleo, tatizo la watanzania wengi wana njaa na ukiwa nanjaa ni rahisi sana ku iuza haki yako ili watoto wapate kula na n.k lakini jinsi miaka inavyo kwenda watu wana elimika kama jirani zetu wa kenya ccm mwisho wao uko karibuni siku watu watasema hii nchi siyo ya wachache or ya kifalme watu wana rithi shana na hawa jali machungu yetu wanacho jali ni bank acount zao zime jaaa vipi?inauma sana.
 
Tanzania iliyoelimika ni big threat kwa uhai wa CCM. Ndiyo maana CCM haioni umuhimu wa watanzania kuelimika especially mpaka kwenye level ya university.

Si kweli kwamba wasomi hawaipendi CCM la hasha, bali CCM ndiyo haiwapendi wasomi kwa kuendekeza mfumo wa kuziba midomo watu wenye mtazamo chanya na nchi. CCM kama kingekuwa chama cha kanuni basi huu ni wakati muafaka wa kuhakikisha kinaingiza wasomi wengi kwenye chama kwa kuweka wazi kuwa level fulani ya nafasi za uongozi ni lazima zishikwe na watu wenye level ya elimu ya chuo kikuu.

Tatizo lao kubwa ni kukumbati watu wenye elimu ya darasa la saba ambao uwezo wao wa ufahamu wa dunia ni finyu sana zaidi ya kujikomba na kuwasifia wakubwa ili watupiwe makombo. Matokeo yake tunapata viongozi mbumbumbu wanaotaka kuiendesha nchi kwa mitazamo yao finyu ambayo ndicho chanzo cha watu wenye uelewa kukichukia chama hichi.
 
1-Je ni wana jelous?
2-Wana uelewa wa jinsi ambavyo haki haitendeki?
3-Wanafahamu zaidi ya wizi unaofanyika?
4-Wanaufahamu wa mambo yanayofanyika nchi nyingine?
5-Wanafahamu jinsi rasilimali ambavyo haziwasaidii watanzania ipasavyo?
6-Hawaridhiki na utendaji kwa ujumla?
7-Wanajua walivyotakiwa kupata na kufanyiwa na serikali lakini havifanyiki?

Ninahitaji mchango wako mdau wa JF.......

Asante kwa kutoa jibu mwenyewd!
 
hakuna kitu kizuri kama kutambua kusoma mana yake kuelewa unapo elewa unaweza kuchuja zuri na baya ndio mana walio enda shule wana kuwa wepesi wakuelewa japo mimi sijaenda shule nime ishi nje nazani ime kuwa sababu ya mimi kuelewa,viongozi wetu wame tembea lakini hawa taki kuiga wala hawana wivu ,wana masikio lakini hawa taki kusikia angalia nchi kama botswana dimond pekee ndio wanayo tegemea lakini sabababu wana uchungu na maendeleo wana endelea vibaya sana nasisi tanzania tuna kilakitu maratatu zaidiyao lakini tuna funga mkia nchi ya watu wasio kua na uchungu wa maendeleo.angalia nchi zote za Asia miaka30 iliyopita zili kuwa kama tz lakini kwa sababu wali amua wizi hauna ma leo hii wako mbali sana kama nchi za ulaya angalia nchi kama maleysia wame amua kuja africa kujifunza kulima mawese leo hii ndio wana ongoza duniani kutoa mawese na sisi mawese kigoma hayana kazi wala baz.angalia nchi kama sngapole wao wana tegemea bandari tu lakini leo hii ni nchi tajiri kushinda nchi nyingi za ulaya,na bandali bongo zime jaa kila mkoa nani mwenye kufaidi mtoto wa kingunge park zote za dar yeye ndio mmiliki na pesa ana tia mfukoni.lakini iko siku wana nchi watanzania tuta amka kwa pamoja mana umoja ni nguvu muda huu tupe leke watoto shule kwa bidii ili waje wa ikomboe inchi yetu ambayo sasa hivi ime tekwa na watu wa chache.
 
Nchi hii ina utajiri mwingi sana!madini ya kila aina,mengine hayapatikani popote duniani na bado mengine yanagundulika mfano uranium imelala pale namtumbo bado kuliwa tu na wajanja!utalii upo juu sana tz,kilimanjaro na wanyama wa kila aina bt still unaambiwa nchi ni maskini hata kujitgemea budget yetu wenyewe hatuwezi!!Hili lipo wazi sana kwamba tumeibiwa uwezo wetu wa kufikiri na kuchambua mambo!!Rushwa imetawala,ubinafsi,ten % za mikataba fake ndio inayotucost!!Wizi mtupu wa chama tawala watu wasiopenda maendeleo ya taifa!Ni wazi hakuna msomi mwaminifu asiyeliona hili na ambaye haoni ni pretender tu..ni mnafiki,mwoga asiye na dira na anayetaka kujipendekeza!Lets be realistic mapinduzi yanahitajika!!Tufike mahali tukubaliane nchi hii isiongozwe kwa mazoea
 
Back
Top Bottom