ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Wana Jamvi habarini.
Jiji la Mwanza, ni jiji ambalo kwa sasa linaheshimika kwa harakati za kisiasa baada ya wabunge tena waliowahi kuwa mawaziri kubwagwa na vijana wado EZEKIEL WENJE-Nyamagana na HIGHNESS KIWIA-Ilemela. Wabunge hawa vijana, walichaguliwa kwa imani kubwa na Mwanza tuliamini wataonesha usimamizi wa rasilimali za umaa kwa manufaa ya umma.
Hali imekuwa tofauti kwa uchunguzi wangu, kwani wakati mvua zikinyesha, barabara za mitaani zile za vumbi zimekuwa kero hali inayopelekea watu kuhoji, HAWA NDO WABUNGE TULIOWACHAGUA?
Barabara ya kutoka kona ya BWIRU mpaka Nyasaka, madereva wa daladala wengi wanaikimbia kwa kuwa na mashimo. Magari yanaharibika kwa ubovu wa barabara hiyo. Na road hii ina wapiga kura, na tayari wameanza kulalama.
Barabara ya NUNDU-NYAKATO MECCO, nayo hali kadhalika. Hofu yangu ni kwamba, iwapo suluhisho halitatafutwa, basi wabunge hawa watakuwa wanawapa nafasi CCM kulitwaa tena JIJI la Mwanza.
Kulinusuru ni wao japo kuwa karibu na wananchi, kuwaelimisha kwa nini barabara hazitengenezwi na kama jamii ya eneo husika tufanyeje kuepuka hatari ya kukosa huduma ya usafiri inayotokana na uwepo wa barabara isiyopitika.
Kuendlea kujificha kwa wabunge hawa bila hata kutoa matamko kwa uzembe huu, inaonesha kwamba hawajali kwani kwa habari ya HIGHNESS alishahama na mtaa. Wakati akifanya kampeni alikuwa akilala nyumba moja iliyopo kwa Lema-Munazi, siku hizi hatumuoni pande hizo thus ametutelekeza na barabara yetu inayotutesa.
Watch out kijana, kwa ustawi wa chama.