Ni kwamba nchi ilikuwa na barabara nzuri muda wote mvua za El Nino ndio zimekuja kuharibu?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Katika kipindi cha maswali na majibu, wakati maswali yakielekezwa kwa Naibu Waziri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ndg. Deogratius Ndejembi, wabunge wote wanauliza nini mpango wa serikali baada ya barabara kuharibiwa na mvua za El Nino.

Yaani ni kama huko nyuma tulikuwa na barabara nzuri nchini na mvua za El Nino ndio zimekuja kuharibu, ni kwamba huko nyuma walikuwa hawaoni? Na jinsi wanayouliza ni kama kama wamepewa script sawa, naona post za JF kuhusu ubovu wa barabara mbalimbali nchini zimefanya kazi.

Barabara hizi zinatakiwa kuchukuwa miaka 20 mpaka 25 kabla ya kufanyiwa marekebisho, lakini viwango huwa vinazingatiwa mpaka zidumu kwa muda uliopangwa? Hapana, barabara inajengwa leo wiki ijayo inaluta viraka, mara nyufa, yaani upuuzi mtupu! Barabara zote zinaharibika kwa wakati mmoja, inashangaza!

Na walivyokuwa wajanja majibu yamekuja kimkakati karibia na uchaguzi waseme walikarabati barabara utafikiri huko nyuma walikuwa hawaoni. Mfano barabara za kawe, toka Gwajima awe Mbunge ziliwahi kuwa nzuri hata mara moja? Si ni yeye alimlaumu mdee kutofanya kitu na yeye kaja katuliza fuvu tuliii, tunakaribia 2025 ndio anajitingisha;

====

Wabunge walioliza kuhusu barabara zao kuwa mbovu;
Profesa Ndakidemi: Barabara ya mabogini Kahe imeharibika sana kutokana na mvua za El Nino, serikali ina mpango gani wa kukarabati barabara hii?

Jibu la Naibu Waziri: Serikali kupitia TARURA imeshapekela Milioni 368 kwaajili ya Moshi vijijini kwaajili ya ukarabati wa barabara mbalimbali ikiwemo barabara iliyotajwa na Prof. Ndakidemi

Justine Nyamoga: Kata ya Igumu na Image hazina mawasiliano kutokana na barabara kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea hatua gani za dharura zinachukuliwa ili wananchi wapate mawasiliano

Jibu la Naibu Waziri: Serikali imeshaanza kukarabati barabara za vijijini ambazo zimeharibiwa na mvua za El Nino ambapo kiasi cha Tsh. Milioni 498 zimepelekwa TARURA mkoa wa Manyara kwaajili ya uharibifu unaoweza kurekebishika kwa sasa kama kutoa tope barabarani, kuchonga baadhi ya barabara, kuweka changarawe, kuchimba na kusafisha mifereji na kurekebisha mikondo ya mito. Serikali inaendelea na jitihada za kutafuta fedha za kurekebisha miundombinu ya barabara zilizoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha kote nchini.

Justine Nyamoga: Kata ya Igumu na Image hazina mawasiliano kutokana na barabara kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea hatua gani za dharura zinachukuliwa ili wananchi wapate mawasiliano

Jibu Naibu waziri: TARURA kote nchini wanafanya tathmini ya uharibu uliotokana na mvua na tahmini ya kwanza ilifanyika hadi kufikia mwisho wa mwezi huu Januari. Pia Mtendaji Mkuu wa TARURA ameshawaelekeza mameneja wote wa mkoa kwa maeneo ambayo mawasiliano yamekata atafutwe mkandarasi kuweza kuunga baraara kama ya Image wakati fedha zinatafutwa kwa kushirikiana na wizara ya fedha.

Grace Tendega: Barabara ya kutoka Iringa kwenda Pawaga jimbo la Isimani kijiji cha Igodikafu, barabara ya Darajani kuelekea Mbuyuni imeharibika sana kwasababu ya mvua hii. Ni nini mkakati wa dharura wa serikali kuhakikisha wananchi hawa wanapata huduma?

Francis Ndurare: TARURA katika wilaya ya Kilwa imeshafanya tathmini ya uharibu uliotokana na mvua za El Nino katika barabara zetu za vijijini, ni lini serikali italeta fedha za dharura wilayani Kilwa?

Kakoso: Wilaya ya Tanganyika ni miongoni mwa wilaya ambazo zimepata athari kubwa sana za barabara zilizoko vijijini chini ya TARURA, je, serikali ina mkakati gani wa kunusuru barabara hizo ili wananchi wajee kupata huduma?

Jafari Chege: Zaidi ya 80% ya barabara ya jimbo la Rorya hazipitiki kutokana na mvua kubwa inayonyesha na kwakuwa tumefanya tathmini tayari na tumeandika barua kwa Mkurugenzi wa TARURA tulitaka tupate kauli ya serikali, ni lini sasa fedha hii itakwenda kwaajili ya marekebisho ya barabara hizi?

Noan Lemburis Saputi: Jimbo la Arumeru Magharibi limeharibika na mafurikoambayo yameathiri jimbo hilo kwa sehemu kubwa kuharibu barabara na madaraja. Ningetaka kufahamu serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba jimbo ya Arumeru Magharibi linaangaliwa kwa jicho la huruma kutokana na jiografia yake ili kupata fedha za dharura zaidi kukarabati barabara na madaraja?

Hamisi Taletale: Barabara za Mororgoro Kusini Mashariki zote zimeharibika, je, ni lini serikali itakuja kutukuleta pesa za mfuko wa dharura?

Flatei Massay: Kutokana na mvua za El Nino jimbo la Mburu Vijijini kata ya Eshkesh, Yaeda Chini, Gidhim, Tumati, Haydarer na Yaeda Ampa zote hazina mawasiliano na TARURA wameshapelekewa maombi, je lini fedha zitaletwa ili jimbo hili likapata mawasiliano?

Gwajima: Barabara zote za jimbo la Kawe Dar, zimevunjika na kukatika vipande vipande kwa sababu ya wingi wa mvua zinazonyesha, nimefika TARURA Mkoa na Wilaya wote wamesema hawana fedha. Nini mpango wa dhararula wa serikali kuokoa barabara za jimbo la Kawe? Neno dharura lizingatiwe


Majibu ya Naibu Waziri
Majibu ya Naibu Waziri: Nikijibu maswali kwa ujumla wake, fedha ya dharura tayari imeanza kwenda kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini. Mfano kwa Askofu Gwajima tayari kuna milioni 598 ambayo imepelekwa katika eneo lake kwaajili ya kuhakikisha barabara zinaanza kufunguliwa na kuweza kuanza kupitika.

Katika maeneo mengine yaliyotajwa na wabunge mfano Iringa kwa Tendega tayari fedha ya dharura imepelekwa pia. TARURA kupitia makao makuu yake tayari imeanza kutoa fedha za kupeleka. Fedha nyingine tunasubiri wenzetu wa wizara ya fedha waweze kuleta fedha kwaajili ya kwenda kuendelea kufungua barabara katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Spika akaongeza: Vipaombele vitolewa katika maeneo ambayo hayana mawasiliano kabisa halafu yafuate yale ambayo yana mawasiliano lakini hayapitiki, baadaye ndio tuwafikie hawa ambao wako vizuri kidogo, kwahiyo tahmini ifanyike kwa nchi nzima.


 
Back
Top Bottom