Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
kama unaona elimu ni ghali, jaribu ujinga. na kama unaona chadema haifai, jaribu ccm.
Kabla hujaandika umejiuliza vizuri kwamba kwa nini barabara hizo ni za vumbi toka tupate Uhuru? Kwa miaka mingapi barabara hizo hazikuangaliwa na haikuwa hoja isipokuwa walipoingia Chadema ndio zinatazamwa na kuwa sababu ya uwakilishi mbaya wa Wabunge hawa?.
Barabara zote hutegenezwa kutokana na mipango ya miji ama toka mfuko wa serikali za mitaa ama serikali kuu hatuna mfumo wa madaraka mikoanikusema kwamba mbunge anawajibika moja kwa moja. Kama barabara hizo zipo chini ya manispaa ya jiji nadhani hoja hii ungeipeleka kwa wahusika yawezekana kuwa uzembe uko huko ama serikali kuu.. Labda ungefuatilia hansard za bunge na kutazama uwakilishi wa wabunge hawa kuhusiana na barabara hizo kama wamewakilisha..
siyo rahisi kwa kila mwananchi kwenda council kusikiliza vikao vya madiwani, lakini ni wajibu wa mbunge kurudi kwa wananchi na kutoa ufafanuzi wa masuala yaliyozungumziwa council. Barabara ni mbovu, yeye katulia, si wananchi watajitafutia majibu?
Juzi maeneo ya Kiloreli kwa msuka, wananchi walikerwa na hali ya barabara, waendesha pikipiki wakaamua kuziba eneo lililokuwa korofi, walipofanikiwa, wakataka kila gari linalopita pale wachangie japo 500/=. Watu waovu wakapiga simu polisi-Ilemela, Polisi walikuja na kuwatimua wale wananzengo.
Mbunge yeye katulia tu. Ataikost CDM huyu, nasema haya kwa uchungu na kwa kuwa sina njia nyingine ya kumfikia
Ulikwishawahi kuhudhuria vikao vya halmashauri na hukuona wabunge hawa wakikemea?Au unadhani ni mpakawaende kwenye vyombo vya habari au bungeni!Fanya utafiti kwanza ndipo uje na kauli kama hizo,pia suala la mtu kuhama ni la mtu binafsi ili mradi anaishi jimboni kwake,au ulitaka akae unapopataka wewe?
mtamaholo,
nakubaliananawe kuwa kuna haja ya wabunge wa cdm kuwa tofauti na vilea vitambi vya ccm. Barabara unazoongelea ziko hasa jimbo la ilemela kwa mh. Hyness.
Kwa kifupi barabara ya kilimahewa nyasaka imeshapata fedha za ujenzi wa lami probably itaanza mwakani. Kuhusu kuharibika kwa barabara hizo na kutorekebishwa ni kwa sababu mvua zinanyesha kwa wingi sana mza na barabara za vumbi ukizitengeza kwenye mvua ni kama unatwanga maji kwenye kinu. Utaparua mvua itakuja kiharibu fasta. Hicho ni kizuizi kinachokwamisha uparuaji wa hizo barabara.
sasa wewe unataka aje afanye mkutano na wananchi bila kibali? Wakiomba kibali wananyimwa kisingizio al shabaab.ongea na polisiccm watoe vibali vwa political gatherings.
wenze alishahama mwanza,amemwamisha mke wake anasimamia duka la madawa dar ni kama masha tu,mi nashauri mkuu wa mkoa dar wafukuze dar wabunge wetu mkosamali,kafulila na wale wa ccn karibu wote wapo dar
ni vigumu kuwalaumu wabunge, lakini si busara pia kuwatetea. Kitu cha msingi hapa ni kujua pesa zinazokusanywa kutoka vyanzo vya ndani na zile zinazo top -up toka kwa wafadhili au serikali kuu ni kiasi gani na zinatumikaje. Ninavyojua mimi nchi hii yote si mza pekee inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo haziwezi kutatuliwa kwa bageti ya mwaka mmoja. Yamkini jiji linavipaumbele vingine nje ya barabara vilivyoelekezewa rasilimali chache zilizopo.