Website ya UTT haipo hewani na nimeweka zaidi ya milioni 100 nimepanic. Vipi hatujapigwa huko?

Mimi naishi ughaibuni (Diaspora) ila nimekuwa mwekezaji mzuri kupitia taasisi ya uwekezaji inaitwa UTT ipo hapo kwetu bongo na nimejiunga na mfumo wa kupokea gawio la faida kila mwezi uitwao BOND fund na sasa nimeshaweka zaidi ya milini 100 sasa mpaka muda huu nataka kwenda kulala akili inagoma kabisa toka juzi nimejaribu kuingia kwenye app ya UTT mara kadhaa kuangalia maokoto inani-logout automatically nikaona nipoe kidogo ila presha iko juu sijui kwanini muda huu nikaona nijaribu kuingia kwenye website yao naona pia site haipo hewani aisee sasa hapa nahisi kupagawa sijui sijui shida nini au ndio yale mambo ya deci yanataka kuhamia huku UTT.

Ambao mpo huko Tanzania naomba mfuatilie hili suala natamani kufahamu kama tatizo lipo upande wangu au lipo upande wao kiufundi hapa naona damu inakwenda mbio kweli hata kula nimeshindwa. Asanteni

View attachment 2765950
...Kumbe Diaspora mmeishafahamu Neno 'Maokoto' ?? ...ama uko Bongo, Mkuu ?
 
Back
Top Bottom