Waziri Tizeba aamua kuondoka hotelini baada ya bili ya 100milioni

Hii kwa UKAWA ni faraja kwasababu wakati wa campaign itabidi Dr. Magufuli atoe majibu ya kina kuhusu matumizi Tshs 100 million za Naibu Waziri Tizeba kama malazi pale New Africa Hotel.
 
Kama umejiandikisha,kadi itunze kabatini na onyesha hasira zako "October 25"

Mimi mpaka sasa sijajiandikisha, imeniuma kukosa chance ya kujiandikisha kutokana na muda na mazingira, anyway Mungu atanipigania in the next few years kupata haki yangu!!
 
Waziri Dr. Charles Tizeba makamu wa Mwakyembe ambaye amekuwa akiishi katika hoteli ya nyota 4 ya New Africa aondoka baada ya bili kufikia milioni 100.

Hiyo ni bili ya malazi na mlo wa asubuhi tuu achana na buffet na vinywaji!

Jamani huyu waziri ni mzalendo kweli wa kuishi hotelini hadi kufikia kiasi hicho cha pesa? Sina hamu jamani sijui wadau mnalipi la kusema.

Source ni The Guardian on Sunday habari na Floriani Kaijage!
Lipi la kusema? subiri 25th oct utaona "mneno" wangu!
 
Jamani japo hatumpendi Kagame walau tuige mazuri yake basi mawaziri na maafisa wa ngazi za juu serikalini wanawezeshwa kujenga nyumba yake na kutumia gari lake (anapewa allowance ya mafuta & matengenezo) sisi huku wandugu tunavurunda tu. Waziri anateuliwa anaenda kufanya sherehe (kuchinja ng'ombe kadhaa) maana anajua huo ni ulaji tu zaidi anaishi hotelini mpaka bill inafika 100m??? binafsi ni mwanachama wa CCM lakini kwa hili mtanisamehe
 
Na sasa muuzaji anataka mumchague awe raisi wenu,haki ya mungu hoteli zote zitajaa mawaziri
Hii yote ni matokeo ya sera za serikali iliyopo madarakani, yaani walijimilikisha nyumba za serikali zilizotokana na jasho/kodi ya kila mtanzania na kuwafanya wakoloni na nyerere wajinga. Serikali si ili ahidi kujenga nyingine?
 
Waziri Dr. Charles Tizeba makamu wa Mwakyembe ambaye amekuwa akiishi katika hoteli ya nyota 4 ya New Africa aondoka baada ya bili kufikia milioni 100.

Hiyo ni bili ya malazi na mlo wa asubuhi tuu achana na buffet na vinywaji!

Jamani huyu waziri ni mzalendo kweli wa kuishi hotelini hadi kufikia kiasi hicho cha pesa? Sina hamu jamani sijui wadau mnalipi la kusema.

Source ni The Guardian on Sunday habari na Floriani Kaijage!

Tizeba hana makosa, asingefanya kazi wakati akiishi kibarazani, mwenye kusajili kuulizwa na kulipa bill hiyo ni kijana wa site, Nyapara John Pombe Magufuli, atao majibu ya kina na hiyo ni trella tu ya madudu ya Nyapara atakayokumbana nayo huku SITE wakati wa kampeni! Hakuna kulala mpaka kieleweke!
 
Sio yeye ni serikali ya sisimu inayotudanganya kweny majukwaa,ww km mkuu wa kaya alienda matibabu ya takriban mwez mzima hawa watashindwa nn
 
Tatizo si talakimu,tatizo ni nani mlipaji?
Kulala hotel ya bei kubwa Kwa mwafrika isiwe sababu ya sisi wafrika wengine kushangaa.
Tutashangaa iwapo mlipaji ni Sisi wenyewe tuliompa dhamana ya kututumikia alafu akashindwa kututumikia kwa uadilifu.
 
kazi ipo,naona karudi mzigoni.


magufuli kuwarudisha watendaji wa kikwete tafsiri yake kikwete alikuwa mzuri.
 
  • Thanks
Reactions: cmp
Waziri Dr. Charles Tizeba makamu wa Mwakyembe ambaye amekuwa akiishi katika hoteli ya nyota 4 ya New Africa aondoka baada ya bili kufikia milioni 100
halafu wanataka tulipe kodi kumbe niwakalipie bili za kukaa mahotelini kwani huyo naye hakuchukua zile nyumba za serikali jamani mie kodi basi uuuuuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Wakubwa zetu hawana tofauti na fisi tena mwenye roho mbaya. Fisi ni mroho lakini akishiba hana ubaya na mtu. Hawa mafisi wetu ni waroho na wana roho mbaya. Huoni bosi wao anavyokesha kiguu na njia wakati waliomchagua wanakufa kwa kukosa asprin. Wetu si viongozi bali matapeli wa kawaida wanaopaswa kutupiwa mawe kila wapitapo.
 
Aisee bill ya 100M mlipakodi analipia baada ya kukatwa kodi ya mzalendo ama?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom