Waziri Nchimbi hakuvamia kwa bahati mbaya maandamano ya waandishi wa habari leo Jangwani

Hata mimi nimeshangaa sana coverage aliyopewa kwani inaonekana alikuja kuwakejeli wanahabari pamoja na chadema kuwa mkiandamana kwa kuomba kibari na kuruhusiwa hamtauawa.Na aliyeuawa huko Iringa ilikuwa ni halali kwake sababu ya kukaidi amri halali.Rai kwa waandishi wa habari msipokuwa na umoja mtakwisha kweni wenzenu wametangaza kutoshirikiana na polisi nyie mnampa coverage kubwa namna hiyo(itv hapa na pale) na kumruhusu kuongea maneno ya kejeli ati anawapongeza kwa kuwa mmeomba kibali na kuruhusiwa,Je Mwangosi alitakiwa aombe kibali cha kuandika habari au kumtetea mwandishi mwenzake ili asiuawe.Unganeni la sivyo bahasha na kutochukuliwa kwenye ziara za viongozi kutawafanya muendelee kuwa watumwa.Story sasa imebadilika sio kulaani mauaji ya mwandishi ila ni kufukuzwa waziri huku ujumbe akiwa amewapa.
 
Masikini police, shule zao ndogo, mishahara migodo kazi ngumu, wanaua mpaka watu wanaopigania haki zao
 
Mi niko against na mleta mada it seems like anamlinda Nchimbi asichanwe live kesho!! Vichwa vya habari napendekeza viwe WAZIRI ATIMULIWA, AZOMEWA..ect. content ya habari iwe yote yaliyo tokea na matamko!!
 
Bushman,

Well noted, Nchimbi hana uwezo wa kuongoza wizara...kwanza aliiba kura na kupata ubunge...

Hivi CCM wanajipenda kweli?? Madaktari...Waalimu...Waandishi wa habari....Wananchi maisha magumu...kazi wanayo 2015

Karibu kunapamabazuka, hawana pa kushikia na wala hawajui wafanye nini,mabadiliko ni lazima,ni mpango wa mungu.
 
Nchimbi is CCM Presidential aspirant in 2015.
Why is he doing such stupidity?

Very very poor man!

mzee kama hata EMMANUEL NCHIMBI ATAKUWA RAIS BASI TANZANIA NI ZAIDI YA SHAMBA LA BIBI,YEYE MWENYEWE VYETI MAGUMASHI UNATEGEMEA NINI HAPO KWENYE SEKTA YA ELIMU HASA KWA WAPAMBE WAKE SI ATAGAWA VYETI BANDIA KAMA NJUGU KWA MAKADA WA CCM.HE CAN'T BE SIO TANZANIA HII YA SASA SONGEA KWENYEWE UCHAGUZI ALICHAKACHUA KUANZIA UBUNGE MPAKA UMEYA,HAUKUMBUKI HUYU NDIYE ALITOROKA NA SANDUKU LA KURA?????
 
haina haja hata yakukaa na polisi meza moja maana walifanya haya wakijua nini kinafanyika picha zinajionyesha kwa kila jambo
 
kweli ukiwa mjinga huwezi kujitambua kama nawewe uko kwenye kundi la wajinga huyu jamaa anfikiria nchi yetu bado iko kwenye miaka 1960s' kazi kweli kweli yaani hawa ndio tunao hamu kweli yaani ni kichapo kwenda mbele asitegemee ataishi milele kwenye system ipo siku ndio atajua nini tunaongelea
 
Mh. Waziri wangu soma hapa.

1. Waziri wangu uzalendo uko wapi
Mwangosi auawa bure dola iko macho
Ona hawa wa kalamu katu hawakutaki
U wapi u hodari nawewe umewekwa kando

2. Nasema yangu Nchimbi kaza moyo twende
Sioni uhalali roho kuzitutumua
Jua leo ni ya Devi kesho kalamu butu
U wapi uhodari nawewe umewekwa kando.

3. Mwatofauti maneno nazo hisia
Mara ncha kali mara chadema ni chanzo
Washika kalamu nao wasema ni jeshi letu
U wapi uhodari na wewe umewekwa kando.

4. Twatazamia taifa lenye ukungu
Ulipo ni zao lao wenye kukutubi
Sioni uwepo wako sasa wakataliwa
U wapi uhodari nawewe umewekwa kando

5. Tanzania ya leo haipo bila ya wewe
U bora kuliko wao ndivyo ulivyojinadi
Ubora wako u wapi kijiwe wakutakia
U wapi uhodari na wewe wakataliwa

6. Dola yetu adhimu haisimikwi na Nchimbi
Uwepo wako hauko sioni chang'aa
Ona aibu yako wote wakuzomea
U wapi uhodari na wewe umewekwa kando

7. Hatamu thabiti haiuzwi kwa maneno
Wana habari sasa wataka kiwingu king'oke
Nipe jipya Kassanga sambamba tuelekee
U wapi uhodari na wewe unakataliwa

8. Asubuhi yafika habari zimejizika
Nani atakayesikia umahiri wako
Kigoma nayo Kiteto yataka wanahabari
U wapi uhodari na wewe umekataliwa.

9. Kassanga pole kwako naikomea
Wote wacheka ungunge ulojitambia
Waseme wote kwako waandishi weka shime
U wapi uhodari na wewe umekataliwa

10. Serikali yaenda vema nchini
Kwani waandishi waipa mkazo bwete
Zuia Nchimbi nione wapi wasikilizwa
U wapi uhodari na wewe umekataliwa.

G Kassanga
Tabora.
 
mi niko against na mleta mada it seems like anamlinda nchimbi asichanwe live kesho!! Vichwa vya habari napendekeza viwe waziri atimuliwa, azomewa..ect. Content ya habari iwe yote yaliyo tokea na matamko!!

mimi huyu nchimbi si mpendi mpaka basi!!!!!!!!!!kumtetea huyu ni sawa na kumtetea muharifu,huyu alikwenda pale jangwani kuchakachua taarifa ndio maana nikasema alikwenda pale kuwatoa kwenye jambo la msingi alikwenda kama nani??na kwa mwaliko wa nani????
 
"I can not teach you violence, as I do not myself believe in it. I can only teach you not to bow your heads before any one even at the cost of your life" Gandhi

Mederators please help me to give this fela a Big Like cause ama using Mobile i cant do it ma self.
Bro u gave me the masage of the day From father Gandhi.
 
Back
Top Bottom