Waziri Nape Nnauye awasimamisha kazi vigogo wa TBC kutokana na utendaji usioridhisha

Mgonjwa anafukuza wagonjwa wenzake
Hapo sasa halafu tujiulize unafukuza watumishi leo ni lini uliwapangia majukumu mpaka uone mapungufu yao ukizingatia huo uwaziri wa NAPE hauna hata miezi miwili.SUGU alikuwa sahihi aliposema mawaziri wanaongozwa na MIZUKA .
 
Huyu yuko juu ya mamlaka yake, hawezi kumfukuza labda amesha muomba JPM acheze nae. yote hii ni kulazimisha TBC kuendeshwa kisiasa. Naiona TBC ikienda kuwa kama gazeti la Uhuru na mzalendo. Magazeti ya kufungia maandazi na vitumbua.
Mimi sikumbuki ni lini nimefungua station ya TBC.

I think there is a problem somewhere...Ninavyoelewa mimi Waziri hana mamlaka ya kuchukua hatua zilizochukuliwa. Hao waliosimamishwa mamlaka yao ni ya Bodi ya Wakurugenzi. Waziri anapaswa kutoa maelekezo kwa Bodi ya Wakurugenzi, na katika kusimamisha kazi kuna taratibu lazima zichukuliwe au kufuatwa ikiwa ni pamoja na wahusika kutoa maelezo yao kuhusu tuhuma zinazowakabili... Mimi nadhani lipo tatizo somewhere. Mimi naogopa jambo baya huenda likawapata hawa mawaziri...ni muhimu wapewe ulinzi, vinginevyo, you never know...
 
Just in:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Ndg Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
Duh ... yaani hapa ndio mie nachanganyikiwa kabisa kama sio kukanganyikiwa; hivi bosi wa TBS ni nani hasa kiutendaji na kuwajibikaji, ni waziri? Kwani ndiye aliyeteua hao watendaji? Vipi nafasi ya bodi ya TBC na management yake, yaani mtu yeyote anaweza kuja na kusema tu, "Hamna kazi ..." ili mradi yupo juu? Ni ipi nafasi na mgawanyo wa madaraka wa mihimili ya dola; serikali (executive arm), mahakama (judicial arm) na bunge (legislative arm)?
Au ndio basi kuitikia speed ya "Hapa Kazi Tu" pasipo kufuata utaratibu? Hivi ofisi ya waziri iko wapi (majukumu yake); sio wizarani?
Walio nguli wa kanuni na taratibu za utendaji serikalini na taasisi zake mtusaidie kutujuvya
 
Watendaji fanyeni kazi kwa umakini wenu tu, kama mtu ana lake ataaibika mwenyewe.......
Hapa ni kazi tu majungu si mtajiiii......
 
Kama hii habari ni ya kweli, basi Nape atakuwa amefanya makosa sana.

Waziri alitakiwa ku-deal na Mkurugenzi mkuu wa TBC na sio mfanyakazi mmoja mmoja ndani ya shirika.

Huku ni kuingilia utaratibu wa ndani, au aseme kabisa kuanzia sasA kila idara ndani ya TBC itakuwa inareport moja kwa moja Wizara na sio kwa Mkurugenzi Mkuu.
Naona ndio utaratibu wao siku hizi maana mie nilisangaa kumsikia waziri Muhongo ,pamoja na usomi wake, akitoa maelekezo kwa mameneja wa mikoa wa TANESCO ya kiutendaji!
 
Ni upuuzi mtupu na ukosefu Wa fadhila. Leo wamesahau walivyowasaidia kwenye Uchaguzi tena kwa kutumia Pesa za wananchi!? Ndio akili imewajia salsa!? Shenzy!
 
Kusimamishwa kazi kwa watumishi kumezidi sasa.
Wakuu wa wilaya walipoanza mechi hii watu na taasisi nyingi tu zilipiga kelele. Mechi imehamia kwa mawaziri tena kwa bao mbili mbli, watu na taasisi zile zile kimya.
 
NI WAKATI SASA KWA TBC KUJIENDESHA BILA RUZUKU.
IMEPATIWA KILA KITU, INA MATANGAZO LUKUKI / IJIENDESHE SASA YENYEWE SASA!,HAKUNA JINSI TENA.
 
Wakuu wa wilaya walipoanza mechi hii watu na taasisi nyingi tu zilipiga kelele. Mechi imehamia kwa mawaziri tena kwa bao mbili mbli, watu na taasisi zile zile kimya.
Hahahaa..... Serikali ya awamu hii inavunja rekodi ya kusimamisha watendaji wengi katika kipindi kifupi sana.
 
Nape anapenda sifa ametoka kwenye michexo kaingia kwenye tbc mwambie kwanza aonyeshe bunge live ndo 2mwelewe lasivyo 2naomba mwongoxo
 
Back
Top Bottom