Waziri Nape Nnauye awasimamisha kazi vigogo wa TBC kutokana na utendaji usioridhisha

Just in:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Ndg Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
Hii ndiyo shida ya kuwaingiza serikalini watu wasio na kikomo na itikadi zao za kichama
 
Wafanyakazi waliobakia wajiongeze waangalie wenzio wa Uganda,Kenya,SA etc wanafanayeje kazi na wanavaaeje,waende kwy forum zao wapate maarifa mapya itawasaidia kubadilisha muonekano wao na utendaji wao kwa ujumla.
 
Just in:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Ndg Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
Nami ngoja nitafute wa kwangu nifukuze
 
Watu humu jamii forums wanafiki sana, kila siku ilikuwa kuitukana na kumkashifu Tbc sasa leo mambo yamebadilishwa kutokana na utendaji mbovu bado mnaponda, hivi nyie viumbe mnataka nini? Duh
 
Kama hii habari ni ya kweli, basi Nape atakuwa amefanya makosa sana.

Waziri alitakiwa ku-deal na Mkurugenzi mkuu wa TBC na sio mfanyakazi mmoja mmoja ndani ya shirika.

Huku ni kuingilia utaratibu wa ndani, au aseme kabisa kuanzia sasA kila idara ndani ya TBC itakuwa inareport moja kwa moja Wizara na sio kwa Mkurugenzi Mkuu.

maguful ni mkurupukaj hata hawa watendaj hali kadhalika! inashangaza sana
 
Back
Top Bottom