Waziri Nape Nnauye awasimamisha kazi vigogo wa TBC kutokana na utendaji usioridhisha

Just in:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Ndg Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.


Hongera sana Mhe waziri kwa kuona uozo uliopo hapo TBC, ni chombo cha umma na chenye vyombo vya kisasa lkn hakuna ufanisi wowote ukilinganisha na vyombo vingine binafsi! Angalau kipindi alicho kuwepo ndugu Muhando tbc ilianza kubadilika lkn ghafla mambo yakarudi yaleyale ya zamani. Tusioneane aibu ktk kipindi hichi cha mabadiliko ya kweli.
 
HEKIMA KWANZA umesema vizuri sana. Lakini kama Mh. Nape anasababu za kum'bypass' Mkurugenzi aweke wazi hilo kama Mh. Rais anavyoweka wazi mambo mengi anayoyatolea maamuzi.
 
Just in:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Ndg Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
mbona amemuacha clement mshana ? huwezi kuleta mabadiliko yoyote Tbc bila kumuondosha huyu , ni kazi bure , halafu mbona sababu za kuwaondoa zina ukungu mwingi ?
 
Hakuna televisheni isiyo na mvuto kama TBC.Hata Wana CCM hawaangalii TBC bali wanaangalia ITV.
Nape mwenyewe naye ni JIPU.
 
Nafikiri si kwamba amempita bali mwenye mamlaka ya kumtoa ni Mheshimiwa Rais
Mkuu Huyo Mpare Hagusiki Kwani Kaaga Kwao. Si Unaona Hata Nape Kampita Kama Siyo Kumsahau Na Sasa Anamalizana Na Hawa Wa Chini? Wewe Kama Mtu Tu Kule Kijijini Kwao UPARENI Usangi Anapandisha Kile KILIMA Chote Na Baiskeli Lakini HANYONGI Na Anafika Baada Ya Robo Saa Leo Utaanza Anza Vipi Kumgusa? Chezea Wapare Wewe!
 
Labda Kwakuwa Kapunguza Kwenda Mlingotini Na Kwa Msisi. Kwa Historia Na Mambo Yanayofanyika TBC Kama Kwenu Hujaaga Vizuri au Hufanyi UTALII WA NDANI Mara Kwa Mara ( Kwenda Kwa Waganga ) Basi Hapo Hukai Na Utaishia Kutokwa Na Mishipa Tu Kila Kukicha. Mtu Anatangaza Kipindi au Taarifa Ya Habari Huku Hirizi Nayo Ina Vibrate Tu Mfukoni. Chezea TBC Wewe!
Duuuh! hii kufuru sasa
 
Hii fukuza fukuza watajikuta wanafukuzana hadi kwenye familia zao
Hawana ubunifu wowote waheshimiwa wetu, kufukuza ni hatua ya mwisho sana ktk uongoz.
Tungeanza na kupeana mikakat na kuwezeshwa then mtu akishindwa hatua zaidi zichukuliwe.
Kwa mwendo huu hata watumishi nao pia hawatakua wabunifuwa.
Watakuwa wanasubir kufukuzwa tu.
 
Hii serikali ya Magu inabidi watengeneze maroboti ya kuyafanyisha kazi maana kwa mtu mwenye ubongo wake timilifu kukubali teuzi kirahisi rahisi sio issue tena bali kuchafuliana CV!
 
Back
Top Bottom