Waziri Nape Nnauye awasimamisha kazi vigogo wa TBC kutokana na utendaji usioridhisha

Just in:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Ndg Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
Si walimwondoa Tido muhando kwa hila kwanini wasiendelee na hao hao!
 
binafsi sioni kabisa TBC wanachofanya in comparison to other national TVs, wako so backward and narrow, they really need revamping, wanahitaji chachu katika management kwa ujumla
 
Sasa huko serikalini mbona kunakua kuchungu .....sijui twende wapi ...private wanapelekeshaaaaa....kilimo kwanza tu ndio suluhu:rolleyes:
 
Sasa hivi Mawaziri wanafikiri eti kufukuza watu kazi ndo utendaji bora,wasubiri na wao mambo yatakapowageukia.kumfukuza mtu kazi ni huwa ni adhabu ya juu sana katika sheria za kazi kwa mujibu wa ILO ambayo huchukuliwa baada ya jitihada zote za kumrekebisha huyo mfanyakazi kushindikana.Lakini akina Nape wao wanafanya kama vile kupiga gitaa tu!
 
Kuna mawaziri wataiangusha hii serikali kwa kutaka sifa hii ni kazi ya mshana na sio waziri mawaziri kasi ya rais mnaifanya ionekane maigizo wengine ndio hao wa kutuma sms wengine ndio hao wa kufunga mageti na wahandishi wa habari wamuone wengine timua timua tutaona mengi mwaka huu
 
Hata kama ni kweli kwa Nape ni chuki binafsi tu.

Sijui watu mantiki mnajifunza wapi? sasa mnataka viongozi wasichukue hatua kwa sababu watu watasema ni chuki? kweli tulizoeshwa vibaya; watu wanaogopa kuchukuliana hatua kwa sababu watu watasema ni chuki. Sasa, Nape ana chuki gani na hao watu wawili labda utueleweshe; walimfanyia nini hadi akawachukia na kuwasimamisha kazi?
 
dah,wandugu embu tuwe tunajipima kabla ya kuongea,wangekuwa wanapewa onyo mngesema hao viongozi ni wajinga,kwa kuwapa maonyo hao watu wanaoila nchi,wanatimuliwa mnataka wapewe muda na onyo,je hivi ndivyo mliokuwa mkitaka katika miaka ya nhuko nyuma?kipind kile kulikuwa na kelele sana mara hoo kwa nini rais au Serikali haiwachukulii hatua wabadhirifu na wazembe ,sasa wanachukuliwa mnakuja na mengine,hakika watanzania ni vema tukajitafakari na kujipima kabla ya kutoa kauli zetu kwani wakati mwingine zinatutukana wenyewe bila kujua
Kwa akili yako kuchukua hatua ni kumfukuza mtu kazi, kama ni hivyo tutegemee kesi nyingi sana na watu kulipwa mamilioni ya pesa.
 
Just in:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Ndg Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
Kila mtu anamtafutia ulaji mtu wake
 
hv hii habari kwenye taarifa ya habari ya leo ya TBC wataionyesha kwl? au kwnye breaking newz yao wataiweka, ingetakiwa isomeke hv kwenye taarifa yao ya habari "hatmae nasisi TBC twatumbuliwa jipu letu na wazir nape"
 
Back
Top Bottom