Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838
Serikali iliwahi kusema inatumia Bil.550 Kwa mwaka Kuagiza magari, vipuri, mafuta na matengenezo Kila mwaka.

--
Akijibu swali la Mbunge Asia Abdulkarim Halamga aliyehoji sababu za Serikali kutumia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) ambaye ananunua Magari kwa gharama kubwa kuliko bei ya Soko la Dunia, Waziri wa Fedha, Dkt, Mwigulu Nchemba amesema Serikali inatazamia kuanza kuwakopesha Watumishi wenye sifa ili kuondoa mzigo wa Mafuta na Matengenezo Serikalini.

Kuhusu utaratibu wa kuagiza Magari moja kwa moja Viwandani badala ya kutumia Mawakala, Dkt. Mwigulu amesema "Kuna baadhi ya mazingira yanaruhusu Serikali kununua kwa mawakala, pia, baadhi ya Viwanda havipendi wanunuzi waende moja kwa moja Viwandani".

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na Wizara ya Fedha Bungeni mwaka 2022, Serikali ilikuwa na Magari 15,742, Pikipiki 14,047 na Mitambo 373 huku ikitumia zaidi ya Tsh. Bilioni 500 kila mwaka kwaajili ya Ununuzi wa Magari mapya, Mafuta, Vipuri na Matengenezo.



My Take
Naona Kuna kigugumizi Cha kuchukua maamuzi.

Toka mwaka juzi mnaongelea hili jambo na hamfiki Muafaka.

Semeni kama Serikali kwamba deadline itakuwa lini? Na Je Madereva mtaajiri wa Umma au Kila boss na dereva wake?
 
Sasa gari ya milioni mia tatu huyo DED au DC atamaliza lini kulilipa?? AU atakuwa kwenye ajira only kununua gari?
Ukisoma btn the lines.

V8 zitabaki Kwa Rais na Pm bas, wengine watarudi kwenye Land cruiser mkonga.

Na kinachosikitisha, wanachukua hatua hizo Leo, Si kwamba wanasikiza wananchi no, ni kwamba madeni yamewaelemea.
 
Back
Top Bottom