Waziri Mwigulu: Serikali itakopa Tsh. Trilioni 8.69 kwaajili ya Bajeti ya mwaka 2024/25

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema serikali inatarajia kukusanya na kutumia TZS trilioni 47.4 katika bajeti ijayo. Mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa TZS trilioni 34.4, washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia TZS trilioni 4.29 na mikopo ni TZS trilioni 8.3.

Mwigulu amesema hayo bungeni akiwasilisha mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya mwaka 2024/25.
 
Bila chuki wala hiyana, huyu Mh. anayeitwa Mwigulu Nchemba sijawahi kumkubali.

Ukitazama kikao kilichofanyika baina ya serikali na wafanyabiashara wa Karia Koo huyu jamaa ana uelewa mdogo sana!

Yaani ni mtupu kabisaaaaa! Ni kiburi tu cha chama Tawala ndicho kinachomlinda.
 
Hao washirika wa maendeleo waliwaambia watatoa hicho kiasi, au ni wishful thinking ya Mwigulu na Samia?

Kama wasipotoa tunarudi kule kwenye nakisi ya bajeti, matokeo yake pesa hazitafika mawizarani kama ambavyo wizara husika ziliomba..

Baada ya hapo ni mkwamo, miradi kadhaa haitasogea, licha ya serikali hiyo hiyo kuwa tayari ilishakopa trilioni kadhaa kwa ajili ya kuongezea kwenye bajeti hiyo hiyo..

Umaskini ni mbaya asikwambie mtu, unaweza kuwa na shida ya kiasi fulani cha pesa, ukaomba ukaomba lakini bado usipate kile ulichohitaji, bado ukaamua na kukopa kabisa, lakini bado kuna baadhi ya mambo yako hayatasogea!.

Lakini ajabu ya karne sasa, utakuta viongozi hao hao wanaoshuhudia huo mkwamo, bado wanatoa pesa nyingi kwaajili ya kununua v8 zenye viyoyozi ili ziwape raha wakiwa safarini, hapa ndipo utatambua kama taifa tu maskini wa akili pia.
 
Tuzidi kuliombea taifa la Israel
Waambie wapunguze ubaguzi kwa wayahudi wenye asili ya afrika kwa maana ya waethiopia. Waliwakuta pale wakati wanaingia Israel wakiwa miguu peku wanatia huruma.

Wakumbushe wayahudi wasisahau kuwa waethiopia wamekuwa wakiishi pale tangu miaka ya Yesu, na inakisiwa kuwa Nabii Issa ni mtu mwenye asili ya Ethiopia, wapunguze hizo sera za kizayuni ambazo zinapeleka ubaguzi mpaka kwenye vikao vya UN.
 
Wayahudi wa Ethiopia ndio hawa Akina Tundu Lisu na Kagame
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema serikali inatarajia kukusanya na kutumia TZS trilioni 47.4 katika bajeti ijayo. Mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa TZS trilioni 34.4, washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia TZS trilioni 4.29 na mikopo ni TZS trilioni 8.3.

Mwigulu amesema hayo bungeni akiwasilisha mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya mwaka 2024/25.
we ulitakaje?
 
Waambie wapunguze ubaguzi kwa wayahudi wenye asili ya afrika kwa maana ya waethiopia. Waliwakuta pale wakati wanaingia Israel wakiwa miguu peku wanatia huruma.

Wakumbushe wayahudi wasisahau kuwa waethiopia wamekuwa wakiishi pale tangu miaka ya Yesu, na inakisiwa kuwa Nabii Issa ni mtu mwenye asili ya Ethiopia, wapunguze hizo sera za kizayuni ambazo zinapeleka ubaguzi mpaka kwenye vikao vya UN.

Unadanganya Sana. Hao waethiopia ni uzao kwa Malkia wa Sheba na mfalme Suleiman. Na uzo wao ulikuwa Ethiopia baada ya Malkia wa Sheba kubeba ujauzito wa mfalme Suleiman. Na Kuna kipindi walienda kuchukuliwa Ethiopia kupelekwa Israel. Wale origin yao ni Ethiopia sio Israel.
 
Kwa mtazamo wangu ,ipo haja kubwa sana Kwa serikali kibuni njia mbadala wa kupata fedha ambazo zitaweza kujitosheleza kwenye budget ya Taifa na si kukopa kila mara. Kwa sasa ianze kulipa deni la Taifa kwani limekuwa kubwa sana ili kuepusha ongezeko la kila mwaka.
Mbona tunvyo vyanzo vingi tu hapa kwetu ,mbuga za wanyama,maziwa,migodi,gesi,makaa ya mawe nk.
 
Back
Top Bottom