Waziri Mulugo: Tanzania ilitokana na muungano wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe

JAMAA KILAZA WA UKWELI!! presentation imeandikwa zanzibar, ila kwakuwa yeye ni kilaza anajua ni zimbabwe!! sio siri, jamaa kachemka, hata usomaji wake hajiamini, mcheki presentation gani anasoma macho muda wote kwenye paper, si anatakiwa kuwaangalia wasikilizaji wake!

Masikini mbavu zangu............ Haaaaaa siwezi.... Hivi hii kitu ilikua kweli au watu manamtania! kweli tumefikia hapa? Sasa mtu kama huyu unategemea ataleta miundombinu gani kwenye elimu? mtu kama huyu kweli anaweza kua na habari hata na hiyo kazi zaidi ya kusubiri mshahara! Inawezekana ukaingia kazini hujui baadhi ya mambo, basi fanya bidii ili ufikie kiwango. Apelekwe akasome lakin tusitegemee maendeleo yoyote ya elimu kwa mtu kama huyu. Aaaaaaaaaaaaaaaaa this is too much! nimewahi kukutana na watu wazugaji lakin kama yakifanywa mashindano huyu wakimnyima ushindi watakua wamemuonea au wamechakachua
 
Hapo kwenye RED, naona umejidondosha mwenyewe. Mie niliandika hivi:

Huu UPUUZI huwezi ukasema umepitia Seminary..... AIBU
Sikonge hapa umeniangusha ndugu yangu! Hivi uwezo wa mtu unaangaliwa kutokana na dini yake? Angalia CV yake hii hapa uone kama aliwahi kusoma seminary huyu!

First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name: Mulugo
Member Type: Constituency Member
Constituent: Songwe


EDUCATION
Rukwa Primary School, Chunga Primary Education 1982 1989 PRIMARY
Mbeya Secondary School O-Level Education 1990 1993 SECONDARY
Songea Boys' High School A-Level Education 1994 1996 HIGH SCHOOL
Open University of Tanzania BA (Economics Education ) 2002 2008 GRADUATE CERTIFICATIONS
 
Nimesikiliza halafu nikajiuliza hivi ingekua enzi za Mwalimu Nyerere halafu waziri wake anakwenda nje ya inchi kufanya madudu kama haya ingekuaje? Zimbabwe!!!! wapi na wapi halafu hata kusoma kiingereza hajui ile 1964, katamka "wani naintini sikte foo"badala ya naintini sikte foo.
 
Kulaaleki!. MIMI siamini kama alijitambua kuwa yeye ni waziri na si memba wa original comedy!.. Lazima niende chunya nikatafute cv yake na kuchunguza kiwango cha elimu (hata ya uraia) ya wapiga kura wake!.
 
Makosa mawili kwa naibu waziri wa elimu, kwanza muungano sio kati ya tanganyika, pemba na zanzibar. Zanzibar ni mkusanyiko wa visiwa vya pemba na unguja, hakuna muungano wa pemba na unguja, vime-exist kwa miaka na dahari kama nchi moja, FACT !. Lakini baya la kosa la pili zaidi ni kiusema tanzania ni musanyiko wa tanganyika, pemba na zimbwabwe. Aibu kwa taifa..na inawezekana ndio hali halisi ya mikutano hata ya mawziri wetu katika baraza lao...
 
First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name: Mulugo
Member Type: Constituency Member
Constituent: Songwe


EDUCATION
Rukwa Primary School, Chunga Primary Education 1982 1989 PRIMARY
Mbeya Secondary School O-Level Education 1990 1993 SECONDARY
Songea Boys' High School A-Level Education 1994 1996 HIGH SCHOOL
Open University of Tanzania BA (Economics Education ) 2002 2008 GRADUATE CERTIFICATIONS

mmmm!
.......
 
Duh! kimsingi jamaa anahutubia kwa kiswahili akitumia maneno ya kiingereza; tena hapa anasoma yaliyoandikwa. Je ingekuwa ni swali la papo kwa pao angesema nini?
 
Sikonge hapa umeniangusha ndugu yangu! Hivi uwezo wa mtu unaangaliwa kutokana na dini yake? Angalia CV yake hii hapa uone kama aliwahi kusoma seminary huyu!

First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name: Mulugo
Member Type: Constituency Member
Constituent: Songwe


EDUCATION
Rukwa Primary School, Chunga Primary Education 1982 1989 PRIMARY
Mbeya Secondary School O-Level Education 1990 1993 SECONDARY
Songea Boys' High School A-Level Education 1994 1996 HIGH SCHOOL
Open University of Tanzania BA (Economics Education ) 2002 2008 GRADUATE
CERTIFICATIONS

EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
The Parliament of Tanzania Member - Songwe Constituency 2010 2015
Southern Highland Secondary School School Managing Director 2008 2010
Southern Highland Secondary School Administrative & Personnel Officer 2005 2010
Southern Highland Secondary School Teacher 2000 2004
POLITICAL
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - National Executive Committee 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Secretary General - Mbeya Region (Parents) 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - Chunya District Political Committee 2007

Ningekuwa na mamlaka; nadhani digrii hizi za online na zile za correspondence kutoka OTU ningezipa kiwango fulani chini ya zile digrii zinazotokana na on campus kama vile UDSM, Mzumumbe, SUA na SAUT kutokana na ukweli wa academic drills zinazofanyika on campus ni ngumu sana kuliko zhizi za online. Ndiyo maana hata China na Marekani wanathamini sana elimu kwa kuhakikisha kuwa watoto wengi wanakwenda college.
 
Kwa nchi kali kama Ujerumani, China na Japan; huwezi kupata madaraka ya kiwango cha uwaziri kama una elimu ya kubabaisha hata siku moja!
 
Mkuu kajitahidi kwani hajazaliwa nacho hicho kimombo
Sidhani kama hilo tatizo limetokana na kukijua au kutokijua kimombo. Je na habari ya NACTE inaoffer master had PhD? Au hata maana ya NACTE haijui?
 
dooh hi ni kali ya mwaka! Inonyesha mtoa mada alikuwa na woga kwani ilikuwa ulazima wa yeye kuongea Kiingereza?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hawezi kuwa kilaza kwa ulimi kuteleza tu.Huku ni kumkosea adabu waziri wetu.Hata ninyi huwa mnakosea tena mambo makubwa na bado mnajiita wasomi.Tafuteni vitu strong vya kujadili sio errors za kuokoteza ili muonekane jamvini.
 
Hivi huyu Waziri ni MUISLAMU au vipi Maana Waislamu ndio hua wanaishia Elimu za Madrasa tu; hawasomi sana!!! Teh!

Kwa hivyo umeona sasa Mpemba Mbishi, suala la ukilaza halina dini. Kuna Waislamu smart sana kama ilivyo Wakristo na Wajadi. Vile vile kuna Waislamu mbumbumbu kama ilivyo kwa Wakristo na Wajadi. Ushahidi kwamba Mwl Nyerere haukuwapendelea Wakristo.
 
"...Presentation consist of seven parts. Education system in Tanzania and I will explain in education for development, achivements in skills developments, challenges in skills development, a way forward and I will end with conclusion.

Introduction.

Ladies and Gentlemen, the United Republic of Tanzania is geagraphically located in East Africa. Tanzania was formed in one nineteen sixty four by unifying the indian ocean islands of zimbabwe and pemba".

Mimi nadhani, huyu bwana wampe ofisi nyingine (kama wanamhitaji sana kwenye cabinet) lakini sio kusimamia elimu. Taifa litapotea!

Hii video inapaswa iwekwe kwenye mtandao wa Magogoni kuonyesha udhaifu wa aliyemteua. Ni bora angepewa wizara ya Sophia Simba kama jamaa ana umuhimu wowote wa kuwa kwenye cabinet. Kweli hii ni aibu kwa WIZARA, DHAIFU, NA TAIFA
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom