Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Una maana kati ya watu milioni 40 hakuna angalau watu 4,000 wenye uwezo wa kuongoza? Au wapo lakini hawapati nafasi? Na kama hawapati nafasi ni kwa nini hawapati nafasi?
Mkuu NN, Kati ya watu 40ml. wapo wazee, watoto, wasio na uwezo wa kufanya kazi kwa sababu nyingine zozote na pia wapo wenye uwezo. Kinacho sababisha wenye uwezo kutopewa nafasi za kushika madaraka makubwa zipo nyingi. Chache ni kama zifuatazo;
1. Kutokujulikana uwepo wao (kwa wateuzi)
2. Kutokuaminika kwa wateuzi (maslahi ya taifa na binafsi)
3. Kutofautiana kiitikadi
4. Kutokuwa na sifa za kushika madaraka yanayohusika (sio wabunge, sio wasomi wa fani husika, sio wenzao n.k.).
5. Kutokujali kwa wanaoteua.
Kwahiyo Mkuu, sababu hizo na nyingine nyingi, ndizo zinazosababisha kila mara watu wale wale kurudi kwenye safu za uongozi, kuendelea kwa utendaji usioridhisha, kujiamini kunakopita kiasi kwa walioteuliwa (wakidhani kuwa wao ndio pekee wanaofaa).