Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Una maana kati ya watu milioni 40 hakuna angalau watu 4,000 wenye uwezo wa kuongoza? Au wapo lakini hawapati nafasi? Na kama hawapati nafasi ni kwa nini hawapati nafasi?

Mkuu NN, Kati ya watu 40ml. wapo wazee, watoto, wasio na uwezo wa kufanya kazi kwa sababu nyingine zozote na pia wapo wenye uwezo. Kinacho sababisha wenye uwezo kutopewa nafasi za kushika madaraka makubwa zipo nyingi. Chache ni kama zifuatazo;

1. Kutokujulikana uwepo wao (kwa wateuzi)
2. Kutokuaminika kwa wateuzi (maslahi ya taifa na binafsi)
3. Kutofautiana kiitikadi
4. Kutokuwa na sifa za kushika madaraka yanayohusika (sio wabunge, sio wasomi wa fani husika, sio wenzao n.k.).
5. Kutokujali kwa wanaoteua.

Kwahiyo Mkuu, sababu hizo na nyingine nyingi, ndizo zinazosababisha kila mara watu wale wale kurudi kwenye safu za uongozi, kuendelea kwa utendaji usioridhisha, kujiamini kunakopita kiasi kwa walioteuliwa (wakidhani kuwa wao ndio pekee wanaofaa).
 
Kweli Hapa JF we dare talk openly... Hata kama ni off point au pumba! Vidole, meno na meno ndio vinampa mtu merits za kuwa kiongozi bora? La Haula Wa Laku'wata!!

Lets focus on qualitites, kama anazo au hana
MMMM twayib unajua humu ndani wapo wengine hawana tofauti na hao tunaowasema.sawa na nyani kucheka mkia wa mwenzane.
 
Kama JK yuko serious, basi watakuwa sio mawaziri watatu tu, lazima iwe zaidi ya hapo.
 
Wakuu,

Nifahamisheni Ngeleja ana matatizo gani? Najua Masha kweli kazi imemshinda lakini Ngeleja mbona kama anajitahidi japo wizara yenyewe imejaa mizengwe.

Inatakiwa waziri apewe madaraka yote ya kuja na vision mpya juu ya energy. Huo umeme wa mafuta na maji pekee hautatutosha huko tunakoenda na itakuwa gharama kubwa.

Kuna haja ya kuwa na miradi midogo midogo ya umeme ya kiwilaya badala ya miradi mikubwa mikubwa ambayo kukiwa na tatizo nchi nzima inatikisika.

Ngeleja wizara imemshinda hiyo. Mpaka hii leo hajafanya chochote kuandika mikataba mipya ya madini ili kuhakikisha Watanzania tunanufaika. Kiwira, mpaka leo anapiga kalenda tu badala ya kutwambia nini kilichojiri katika deal ya Mkapa kujiuzia mgodi huo kwa bei poa. Pia usisahau alishatoa ushauri wa kutaka TANESCO wanunue mitambo ya Richmond?Dowans kwa mabilioni, kama siyo wabunge kuja juu basi deal lingine la kifisadi lingepita bila matatizo.
 
Ngeleja wizara imemshinda hiyo. Mpaka hii leo hajafanya chochote kuandika mikataba mipya ya madini ili kuhakikisha Watanzania tunanufaika. Kiwira, mpaka leo anapiga kalenda tu badala ya kutwambia nini kilichojiri katika deal ya Mkapa kujiuzia mgodi huo kwa bei poa. Pia usisahau alishatoa ushauri wa kutaka TANESCO wanunue mitambo ya Richmond?Dowans kwa mabilioni, kama siyo wabunge kuja juu basi deal lingine la kifisadi lingepita bila matatizo.
Kuongezea tu, Ngeleja na Wasira ni watu wa Rostam Aziz.
 
na zaidi ya hapo tuseme tumsamehe haya mambo yenye contradiction, lakini kuna mengine mazuri tu, lakini ameshindwa kuyafanya eg kuja na mradi wa umeme wa muda mrefu, iwe stigler au mwingine wowote, halfu, katika ya muhula atatuambia nchi ina ukame, matumizi yameongezeka etc etc , hivyo richmond nyingine ije?
mimi ninge penda ange kuwa pro-active, ndio maana kuna wakati Raisi alimkemea kwamba alitegemea jambo fulani liwe limefanywa lakini lilikuwa halijafanywa.
Yaani angekuwa anafikiria mbali( to think ahead), sio mambo ya zima moto.
 
Tatizo la uongozi Tanzania haliko kwenye umri, elimu, sura, au kuvuta sigara. Liko kwenye uwezo.

Mkuu unaweza kuwa na watu wenye uwezo,Qualifications kwenye uongozi/organisation fulani but if those people are not MANAGED CORRECTLY they will end-up being Liabilities tu!!
 
Mkuu unaweza kuwa na watu wenye uwezo,Qualifications kwenye uongozi/organisation fulani but if those people are not MANAGED CORRECTLY they will end-up being Liabilities tu!!

Well said ndugu;

In addition to management styles, i think leadership yetu bado ina challenge kubwa ya kuwa na mikakati yenye timelines; mara nyingi namna yetu ya mipango ni kama ya hapa JF ambapo kila jambo linaishia hewani. Focus ya serikali yetu ya January 2008 si ya sasa kwa kiasi kikubwa... kuna-swing kama twanga pepeta!

Our government system needs radicle reform, bila kujali, naweza kusema kwamba mfumo wa sasa unamnyima "executive person" yeyote kufanya final decisions; kila jambo lina msonge na mpaka feedback ije... ni kasheshe.

Tumedectralise concept na context ya governance kinadharia lakini everything iko central with exception ya procurement and contract management katika local levels... Naamini yote haya yanaweza yakawa yanaathiri utendaji wa bwana Masha kwa namna fulani, hasa kwa sababu background yake haiko integrated sana na vijungu vyetu vya kila siku

No matter how good you are, if the system is mulfunctional... utaishia pua tu!!

Tunahitaji vitu vitatu muhimu; decisive government yenye results framework; true delegation; na mwisho ni competitive people kuongoza vitengo na sio mtu kufanya kazi sehemu muda mrefu au umri... hao watu wenye uwezo wapo na wanafanya maajabu private sector na katika anga za kimataifa.. unkiwarudisha tu ndani ya system kinakua kituko

TUJIULIZE.. WHY?
 
Una maana kati ya watu milioni 40 hakuna angalau watu 4,000 wenye uwezo wa kuongoza? Au wapo lakini hawapati nafasi? Na kama hawapati nafasi ni kwa nini hawapati nafasi?

hawana hela hawako kwenye system, watakutana wapi na kikwete wako huko olidonyo, na wengi wao sio sisiemu
 
hawana hela hawako kwenye system, watakutana wapi na kikwete wako huko olidonyo, na wengi wao sio sisiemu

Dawa yake rahisi tu;

Kujiunga na CCM, jipendekeze na ukifika juu unaonyesha true colours... Hivi kwanini pasiwe na mamluki wa upinzani ndani ya CCM, yaani wawe wa CCM ndani ya upinzani tu?
 
Information-starved society!

Mtu kaja na speculation lake "Mawaziri watatu wakalia kuti kavu" na sisi rrrrrrrrrrrrr tunajikita kujadili ma ghost watatu!

Shekhe Yahya civilization!
 
Muendelee kututonya.Ila L.Masha na Nchimbi hawamsaidii vilivyo Rais ni vizuri watemwe,
 
Sio rahisi L. Masha na Nchimbi kutemwa kama unavyodhani. Mkuu akifanya hivyo, atakuwa anadhoofisha zaidi nguvu zake mwenyewe mwaka 2010. Maana nionavyo hadi sasa ni kwamba, 2010 itakuwa ngumu kweli kweli.
 
Nimesikia kuwa sijui kama si kweli kuwa Slimu Ahmed atagombea Uraisi kwa tiketi ya Chadema ,naona Chadema kinakuwa Chama cha Waarabu.
 
Nimesikia kuwa sijui kama si kweli kuwa Slimu Ahmed atagombea Uraisi kwa tiketi ya Chadema ,naona Chadema kinakuwa Chama cha Waarabu.

Jamani hizi comments zingine hazina tija kwa taifa na maendeleo yetu. Wakati akiwa Waziri Mkuu mbona hukuwa na hoja kama hii?????
 
Baada ya Masha kushirikiana na kina Rostam Aziz na Lowassa kumhujumu Mengi, sasa mfanyabiashara huyo naye amefanikiwa kumnasa Masha. Habari za ndani toka kwenye kambi ya Masha zinadokeza kuwa Waziri huyo kijana anahaha baada ya nyaraka zinazoonyesha matumizi mabaya ya madaraka katika mradi wa vitambulisho vya taifa kutinga kwa Mengi. Wadadisi wa mambo wanachambua kuwa sakata hilo linaweza kabisa kumwondoa waziri huyo kijana katika nafasi yake ya kisiasa.

PM
 
Last edited by a moderator:
Awamu ile tuliambiwa kuwa mafahari wawili wakigombana.....Kisha yakaja maneno(kasa?)kuwa wamepatana na bla,bla nyiiingi...Bottom line ikawa wameyamaliza kiutu uzima!!
Haya ya kumnasa yanatokea wapi tena?Au ndo mambo ya visasi!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom