Waziri kivuli CHADEMA aachia ngazi

I wish wa CCM nao wangejifunza haya ya kidemokrasia

kujiuzuru ndani ya muda mfupi namna hiyo kunazua maswali kwani hata yeye hajapata uzoefu wowote. ange present hata bajeti moja angalau

otherwise ni utaratibu mzuri hata Mbowe angeiga amwachie Zitto kidogo hata mwaka mmoja hivi
 
Letcia , anadhani ile nafasi ni yafamilia ya nyumbani kwake ! ile post ni ya umma, anapojiuzulu ni vyema akawajuza wananchi, iwe kwa maslahi ya chama, taifa au ya kwake binafsi.
19144_100229920007453_100000613353513_3411_1109588_n.jpg




Nilitaka nipite tu lakini kama kifaa chenyewe ni hiki,wacha tumjadili. Hongera Nguvumali kwa kunogesha ukumbi. Enhee wajumbe tuendelee. Sasa ana kosa gani kwa kuamuwa kujiuzulu iwapo keshajipima?
 
I salute Leticia! Lets be positive on her move. Kumbukeni ni waziri kivuli (waziri copy) siyo waziri mwenyewe hivyo impact siyo kihivyo kama mawaziri wa CCM wenye nguvu za kisheria!!!

Mbona walifika kutukanana kule mjengoni kwa huuhuu ukivuli?
 
Tatizo la watanzania wengi ni kuwa bado hatujaelewa vizuri maana ya kujiuzulu. Ni kuamua kuachia nafasi uliyonayo kwa sababu yo yote ikiwepo sababu nzuri - positive. Si lazima iwe negative always. Inaweza kuwa anataka kufanya mambo mengine ya Chadema na akaona apunguze majukumu ya uwaziri kivuli. Tusilazimishe kutatafuta tatizo ambalo hatujaelezwa.
ILa kwa vijana wa Nape ruksa kuzusha mambo.
Nakubaliana nawe kuwa Watanzania wana tatizo la kuelewa lakini kwa kawaida mambo yakizidi basi lazima wataanza kuelewa.

Nashangaa huelewi kwanini watanzania wanashangaa kwa hili ni mazingira na muda wa huo ujiuzulu wake ndio unaowapa watu mashaka.Tatizo zaidi ni kuwa sababu anazotowa hazikubaliki.
 
Kujiudhuru wadhifa ni jambo muhimu kama demokrasia inavyotaka, suala la kuweka wazi sababu za kujiudhuru wadhifa huo ni juu yake na Chama chake akipenda kusema ni sawa asiposema pia ni sawa. Tusubiri kiongozi wake wa kambi ya upinzani anaweza akatujuza hili. Ila nampa big up sana kwa uamuzi huo.


Kwanini atupe vitu nusunusu? Asitubanie kwani ikiwa Chama si kinataka kuja kutawala na ikiwa kama kiongozi si atakuwa mtawala sasa kwanini asiwajibike kwa wananchi?
 
Ana uhuru wa kutoa sababu au kutotoa, malengo yanabaki ni kuimarisha chama

Mambo haya yaliwafanya wenzao kujivuwa Gamba tunaogopa baadae ikatokea kujivua magwanda. Nyoka yuko msituni lakini hawa wanaoishi na wenzao wasije wakabaki bila nguo.
 
Mimi namuunga mkono. Heri ya lawama kuliko fedheha. Kama uwezo ni mdogo unaachia ngazi, sio unawasilisha hotuba kivuli ya wizara halafu unaonekana kituko. Kuwa waziri kivuli wa CDM ni lazima uwe makini, inahitaji upembuzi yakinifu katika masuala makubwa. Huyu mama niliwahi kumsikia kidogo akichangia bungeni, uwezo wake ni mdogo, tusimlaumu kwa hatua aliyoichukua wala tusiwe na hisia kuwa kafanyiwa lolote CDM.
Ingekuwa busara kwake kusema hivyo (uwezo wake mdogo) lakini kinachonishangaza mimim ni kuwa tumekuwa tukisema kuwa CDM ni chama makini na chenye uwezo sasa kutokea haya unayoyasema inawezekana sio kweli na kuwa ni sawa tu na vyama vyengine vinavyogombania ulaji?
 
Definetely huyu kaona viatu alivyo vivaa sio saizi yako. If you can't sustain the heat
it is better to quit the kitchen. Ameshindwa huyu kutengeneza budget mbadala ya
wizara yake.

Tofauti na JK Leticia ameona udhaifu wake na kuu-accept. JK naye tunaomba aige
mfano wa Leticia, hiyo ndiyo democracy


Pengine alifanya hivyo kwa kujuwa kuwa yeye kivuli tu, sasa JK naye ni kivuli.
 
micharuko ya ccm hii ..... soma habari kwa umakini wewe

mkurupuko

Unaita kukurupuka au wewe unakurupuka? Anatowa uzoefu kwa wengine yaani hcho kipindi cha miezi sita ndio ameshapata uzoefu? Na ni bajeti ya ngapi ameshawasilisha ili aitwe mzoefu? Wacha unazi wa kichaa, huyu bibi na atowe sababu halisi za maamuzi yake.
 
Yamemshinda, kaona uozo uliokuwepo, si uliona mawaziri vivuli kwenye ile report yao jinsi walivyoandika madudu, kuna mtu humu kaonesha hata tarakimu hawajui namna ya kuziandika. Kajionea, yanini taabu na raha zipo!
he! dada yetu umerudi? tulisikia umefungiwa! cdm walipumua
 
Utawaeleza nn watanzania?kuna siku utaukimbia uwakilishi wako,ndio tatizo la kuchagua sir name,babu hawezi kuwa mjukuu.
 
Kasoma alama za nyakati. Msimu wa kuwasilisha bajeti umefika na yeye yupo mazingira. Simply kaona hawezi zungumza. Cha msingi kachukua uamuzi mapema
 
Back
Top Bottom