Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Mradi wa umeme wa Julius Nyerere ni moja ya mradi unaotekelezeka kwa weledi mkubwa sana, sote tunajua mwezi wa sita mwaka huu ndiyo tulitegemea kuwasha mtambio namba 9 kwa mara ya kwanza lakini kwa jitihada za serikali na wakandarasi tuliweza kusogeza ratiba za kuwasha mtambo huu hadi mwezi wa pili, jana tumefanikiwa kufanya majaribio kwa ukamilifu kwenye mtambo namba 9 na tumeutembeza kwenye uwezo wake wa mwisho wa megawati 235," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati.
"Tuliahidi mwezi huu tuna ratiba ya kuzindua mtambo huu na ratiba hii iko palepale, tunawashukuru sana Watanzania kwa kuendelea kutuvumilia, matumizi ya umeme yanategemeana tukizalisha mwezi huu mgao utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunazalisha megawati 235 na mwezi wa tatu tutazalisha megawati 235 hivyo zitakuwa megawati 470 uhakika ni kwamba kufikia mwezi wa tatu mgao wa umeme utaisha nchini," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati.
Pia soma