Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa

Nikupateje umeshaamka lkn kwa taarifa yako wajumbe 10 kutoka Malawi wapo hapa Bungeni wakijadiliana na spika kuhusu sakata hilo la mpaka, na wao ndio watakaotudhibitishia ni nani hasa ana wasiwasi au hofu kuhusu hayo maji ya ziwa katika nyuzi 33 E na huo mpaka ulionyooshwa kupita katikati ya Ziwa TUVUTE subira mchana haufiki
 
Ukiangalia current google map ziwa Nyasa liko Malawi! Sina lengo la kuibua mjadala upya ila ni jambo ambalo nimeliona sasa hivi. Mpaka wa Msumbiji na Malawi ziwani uko wazi unapita katikati lakini wa Tanzania unapita nje ya Ziwa.
Google Maps
 
Ujuha ulioonyesha kwamba kama mkataba wa wajerumani ulipitwa na wakati hayo makubaliano na wenyeji ambayo yamo akilini mwako yalifanyika lini wakati wenye mawazo kama wewe humu wametetea kwamba hata Nyerere hakuwahi kukaa meza moja na Banda kuhusu hili katika uhai wao.

Ujuha wako upo katika kuuacha ukweli unaoonekana na kuanza kuutafuta ukweli kwenye makaratasi,nasema makubaliano ya wenyeji yangekuwa na nguvu kuliko hayo ya wadhungu unaowaabudu, kwa kuwa wenyeji hawana makubaliano katika maandishi,makubaliano ya ASILI yanatawala,kila aishie kando ya ziwa anayo haki ya kutumia maji ya ziwa. HAPA PANAHITAJI HEKIMA YA KAWAIDA KABISA,wala hakutakiwi hata kupoteza muda wa kutafuta ukweli kwenye maandishi ambayo hayapo,ni muda mwafaka sasa kama nchi mbili zenye haki na maji ya ziwa Nyasa zikae pamoja kuweka mpaka ili kugawa hayo maji ya ziwa baina ya nchi hizo,kinyume na hapo ni upuuzi mtupu.
Hizo latitude na longtude zako zipeleke kwa wahusika ili watengeneze mpaka mwafaka.
Swala la Nyerere kukaa na Banda au kutokukaa haliondoi haki ya binadam wanalolizunguka ziwa kutumia maji ya ziwa kwa UHURU,amka wewe...
 
Ukiangalia current google map ziwa Nyasa liko Malawi! Sina lengo la kuibua mjadala upya ila ni jambo ambalo nimeliona sasa hivi. Mpaka wa Msumbiji na Malawi ziwani uko wazi unapita katikati lakini wa Tanzania unapita nje ya Ziwa.
Google Maps
bishoke umeshawahi kujiuliza kwanini mpaka kati ya Tanzania na Malawi umewekwa dotted lines tofauti na Malawi na Msumbiji ama Tanzania na Msumbiji ambako umechorwa kwa thick line??
 
Last edited by a moderator:
labda anataka kusema nini juu ya hili suala liende malawi ? bila shaka atoe solushen yake juu ya hili liende wapi tz au
 
Nikupateje kwanza niseme tu kwamba sihitaji kukupata kama jina lako lilivyo.
Pili nikuulize unachohangaikia ni kitu gani? Ile thread yako nyingine ulipewa hoja za kutosha kukujibu hoja zako. Sasa umekuja kuanzisha nyingine yenye hoja zile zile.
Hii bidii unayofanya kujaribu kuhadaa watu na vilatitudes hapa wala haikusaidii wewe mnyasa na makuwadi wenzako wa kinyasa mliojazana hapa nchini.
Malawi hawawezi kumiliki ziwa lote, watake wasitake lazima kuna kipande chetu ndani ya ziwa nyasa.

Thats the reality....in common sense mpaka hauwezi kuwa kwenye fukwe za Tanzania.....inamaana ukigusa maji tu uko Malawi....haiwezekani, huu utakua ni uchizi.
 
Mkubwa,

Nimesoma hotuba yote ya Membe mle Bungeni. Sijui kama wewe umeisoma. Sijaeleza mengine kwa sababu context ya thread hii ni kuonyesha jinsi Tanzania ni kama tumekurupushwa kulitetea jambo hili.

Tuje kwenye suala la Malawi kukatazwa kufanya utafiti. Usipoisoma vizuri ile context unaweza kuamini kwamba wamekatazwa. Lakini ukisoma hotuba ya Membe anasema kwamba kuna ndege za utafiti zilikuja zikatua January na February kwenye east coast of Lake Malawi.

Kama ndivyo ilivyo basi hapo ni kweli wanastahili kukatazwa maana ndege inatua nje ya mpaka ambao ni shoreline. Lakini kwa sababu waziri anajua huwa hatusomi na tunakurupuka, anajua kwamba hatutajiuliza hivyo.

Hivyo, kilichokatazwa na Malawi walichokubali ni kitendo cha ndege zao kutotoa kwenye eneokama Mbamba Bay.

Lakini Serikali suala la kwamba wasitumie ile nusu ya maji kuelekea kwetu membe anasema waliwashawishi wamalawi mkutanoni wasiitumie pia. Hapa Membe anasema inaelekea wenzetu walituelewa.

Sasa utasemaje kuwa inaelekea walituelewa kana kwamba mliwatumia barua na mnategemea baada ya kuisoma wanaweza kuwaelewa. Si hivyo. Walitoa rai hiyo mkutanoni na Membe alitakiwa kutuambia jibu la Wamalawi mle mkutanoni, je walikubali au walikataa.

Kulinagana na magazeti ya Malawi hata ya leo (NyasaTimes) wamesema hakuna cha kuwakataza kufanya research kwenye maji yao.

Hebu tafakari hapa. kwa nini membe hasemi resolution ya hizo meetings walizofikia na anaishi kuzitaja tarehe zake tu.

Sasa kama tulipitwa na sisi, binafsi nimeweka kwenye kalenda yangu kwamba kuna meeting nyingine siku 12 zijazo yaani August 20, 2012 itafanyikia mji uitwao Mzuzu huko Malawi. Tuwe watchfully tujue ni nini kiliendelea huko.

Kama unatumia hotuba ya Membe kujenga hoja basi muda wote utajikuta huna HOJA. Dokezo: mara nyingi Membe hasomi hutuba anapohutubia hata ukiona mezani kwake kumejaa karatasi. Mambo mengi aliyoyasema Membe bungeni juu ya Malawi ni ya ki intelijensia na hivyo angekuwa mjinga wa mwisho kuyaweka kimaandishi katika mistari minyofu.

Wizara yake ni nyeti na inayotumia habari za intelijensi (zilizokamili na zisizo kamili), ukitegemea usome hotuba iliyoandikwa unaweza usiambulie picha yeyote. So you either read his lips or between lines.
 
Nasema ivi, hilo ziwa wacha wajitia hashuo lao, TZ lazima ipate ilo ziwa, kama wanataka lote liwe lao basi waingie katika mipaka ya tanzania nawasema vijiji ama mikoa pia yao ili wasiwaathiri wale waliokuwa pembezoni mwa hilo ziwa! Ramani zote africa zimechorwa na mabeberu na mbona zinaheshimiwa? Kama ramani inavoonesha kuwa lake nyasa limegawiwa basi ndivo lilivo!! Wasituzingue, wakileta useng.... JWTZ wafanye kazi! Whats the point of having an army if you aint gona protect your stolen borders?
 
Kama unatumia hotuba ya Membe kujenga hoja basi muda wote utajikuta huna HOJA. Dokezo: mara nyingi Membe hasomi hutuba anapohutubia hata ukiona mezani kwake kumejaa karatasi. Mambo mengi aliyoyasema Membe bungeni juu ya Malawi ni ya ki intelijensia na hivyo angekuwa mjinga wa mwisho kuyaweka kimaandishi katika mistari minyofu.

Wizara yake ni nyeti na inayotumia habari za intelijensi (zilizokamili na zisizo kamili), ukitegemea usome hotuba iliyoandikwa unaweza usiambulie picha yeyote. So you either read his lips or between lines.

hii kitu imo katik hotuba ya membe...kama huna hotuba hiyo soma hata gazeti la raia mwema la jana lina hotuba nzima na kuna hicho kipengere cha latitude 9 hadi 11.....
 
hii kitu imo katik hotuba ya membe...kama huna hotuba hiyo soma hata gazeti la raia mwema la jana lina hotuba nzima na kuna hicho kipengere cha latitude 9 hadi 11.....

Edson, mosi mimi sikuwa najibu juu ya latitude bali alichokisema Membe juu ya Malawi na vifaa vya utafiti wanavyovileta upande wa ziwa wa Tz. Nilichotaka kusema ni kwamba Membe na Serikali wanajuwa fika juu ya uchokozi wa Malawi na jinsi Malawi walivyokiuka makubaliano ya hatua za mwanzo za mazungumzo. Uchokozi au kutokubaliana kati yao kusingeweza kuandikwa kwa undani katika hotuba ya Membe, vile vile ikumbukwe viongozi wa Bunge la Malawi walikuwapo bungeni hivyo basi Membe akawa anatumia nafasi ile kuwapa "salamu". Membe hakuwa na jukwaa la kuanika kila kinachojiri juu ya mazungumzo ya nchi hizi mbili kwasababu anajuwa bado mazungumzo yanaendelea.

Pili, mleta mada nazani anachuki binafsi. Kosa la kiufundi la latitute alilofanya Membe halistaihili kichwa cha habari ya thread hii. Mleta maada anaongea kana kwamba lugha ya latitute na longtude kwa wananchi wa Tz ni sawa na lugha ya maisha magumu, ufisadi, wizi wa rada, EPA, ubovu na rushwa TANESCO, nk. Ebu, mleta mada ajaribu kuwauliza wabunge nini maana ya latitude na longitude aone wangapi watajibu. Mods, mada nyingine zinatufanya JF tuwe kama mazezeta fulani wakati ni tegemeo la viongozi na tz kwa ujumla.
 
hii kitu imo katik hotuba ya membe...kama huna hotuba hiyo soma hata gazeti la raia mwema la jana lina hotuba nzima na kuna hicho kipengere cha latitude 9 hadi 11.....

Edson,

Asante kwa kunisaidia kuwaelimisha hawa jamaa. Lakini hata hapa tulipowafikisha naona tumefanya kazi kubwa. Kwa nini nasema hivi?

nasema hivi kwa sababu wewe pitia thread nzima tangu jana nilipoianzisha. Jana yote hawa mabwana wametumia kuniponda bila mafanikio na bila data. Utakumbuka walileta data hawakujua wanapambana na mtu wa iana gani kwani nilikuwa sichkui dakika kuzipangua data zao, tena zingine mbovu kuliko za Membe mle Bungeni.

Leo hali ya hao wachangiaji naona inabadilika. Inabadilika kwamba taratibu wameanza kukubali kwamba Membe alikosea na akalidanganya Bunge na akatudanganya watanzania. Lakini kwa ujanja hawataki Membe afike hatua ya ku-apologise bali sasa wanaleta hoja nyingi kutetea makosa yake.

Mmoja kasema tusitegemee ushahidi wa Membe uliomo kwenye kumbukumbu za Bunge yaani Hansard. Huyu anasahau kwamba wiki nane zilizopita hansard za Bunge za htouba ya Jakaya Kikwete zilitumika kwenye ushahidi wa kesi ya Profesa Mahalu inayoweza kuhukumiwa leo ambapo kwa mujibu wa Rais wa sasa ni kwamba Profesa Mahalu hakufanya makosa kule Italy. Hivyo, bado ku-water down hotuba ya Bungeni haiwasaidii hawa mabwana.

Haya mwingine hapo juu kwenye post iliyopita kaja na dhana kwamba makosa ya membe mle bungeni ni kutokana na kwamba kwanza huwa hasomi na anafanya kazi ki-inteligensia. huyu pia ni yaleyale kwamba kelele zote za jana wameshindwa na wamefika mahala wote sasa tunajadili makosa ya Membe isipokuwa sasa tunatunga sababu ama kumhukumu ama kumtetea.

Huwezi kukubaliana na dhana ya huyu eti kwamba Membe hasemi sababu za ki-intelegensia kuhusu suala la mpaka wa Malawi. Kuna inteligensia gani hapo? Kwani mpaka unaweza kuuficha watu wasiujue? Mpaka na mkataba ule ni suala la wazi. Hii si biashara kiasi kwamba tunaficha mkakati tusizidiwe na wapinzani.

Kama anaficha uwezo wa jeshi letu basi ni haki na hakuna aliyemuuliza. Mbona Lowasa kuhusu maji ya ziwa Victoria hakuwa na cha kuficha bali yeye tangu mwanzo alisema hatambui mkataba wa mwaka 1920 na tukamuelewa.

lakini Lowasa naye wakati ule angejifanya kama Membe kwamba mkataba ule wa Misri wa mwaka 1920 na sisi tuna haki, na hiyo haki ingetupa uhalali wa kuvuta maji kuja Shinyanga, basi tungempiga Lowasa kama tunavyompiga Waziri Membe sasa hivi.

Hivyo, binafsi ninafurahi hapa tulipofikia kwenye thread kwamba kweli Membe kakosea na alichotakiwa ni kurekebisha hansard tuendelee na mengine japo kwa hilo tu inaleta dalili kuwa sijui hali imekuwaje ya mazungumzo ambayo mengine hatutaambiwa.

Kumbuka ni hawahawa viongozi wetu waliowahi kusema wanaenda kumtetea Mugabe kwenye Commonwealth. Walipofika kule na Commonwealth ikakataa kwamba Mugabe na Zimbabwe yake wataendelea kupata economic sanctions hadi wa-comform na standard za Commonwealth.

Si Kikwete au Thabo Mbeki waliotaka kuzungumza tena habari ya Mugabe, walitoka mkutani Kikwete hataki hata kusalimiana na waandishi wa habari kuhusu msimamo wao wa kuitetea Zimbabwe.

Najua hapa nikikaa kimya wanazi wataniuliza ilikuwaje Kikwete akahudhuria CHOGM wakati ilikuwa bado ni utawala wa Mkapa. Hiki kilikuwa ni kipindi kile Mkapa amelazwa Uingereza akiumwa mguu na ikabidi Kikwete apite Londo kumsalimia na kisha akaenda kwenye Mkutano ule.
 
Edson, mosi mimi sikuwa najibu juu ya latitude bali alichokisema Membe juu ya Malawi na vifaa vya utafiti wanavyovileta upande wa ziwa wa Tz. Nilichotaka kusema ni kwamba Membe na Serikali wanajuwa fika juu ya uchokozi wa Malawi na jinsi Malawi walivyokiuka makubaliano ya hatua za mwanzo za mazungumzo. Uchokozi au kutokubaliana kati yao kusingeweza kuandikwa kwa undani katika hotuba ya Membe, vile vile ikumbukwe viongozi wa Bunge la Malawi walikuwapo bungeni hivyo basi Membe akawa anatumia nafasi ile kuwapa "salamu". Membe hakuwa na jukwaa la kuanika kila kinachojiri juu ya mazungumzo ya nchi hizi mbili kwasababu anajuwa bado mazungumzo yanaendelea.

Pili, mleta mada nazani anachuki binafsi. Kosa la kiufundi la latitute alilofanya Membe halistaihili kichwa cha habari ya thread hii. Mleta maada anaongea kana kwamba lugha ya latitute na longtude kwa wananchi wa Tz ni sawa na lugha ya maisha magumu, ufisadi, wizi wa rada, EPA, ubovu na rushwa TANESCO, nk. Ebu, mleta mada ajaribu kuwauliza wabunge nini maana ya latitude na longitude aone wangapi watajibu. Mods, mada nyingine zinatufanya JF tuwe kama mazezeta fulani wakati ni tegemeo la viongozi na tz kwa ujumla.

Mleta mada hajalazimisha hata mmoja wenu kuiona hii ni subject ya maana. Ni nyinyi wenyewe mnajigonga kumjibu na hadi thread imekuwa ndefu yaani page saba sasa na post 132 na LIKES saba na PM tele ambazo hana sababu ya kuwaonyesha humu.
 
Nikupateje umeshaamka lkn kwa taarifa yako wajumbe 10 kutoka Malawi wapo hapa Bungeni wakijadiliana na spika kuhusu sakata hilo la mpaka, na wao ndio watakaotudhibitishia ni nani hasa ana wasiwasi au hofu kuhusu hayo maji ya ziwa katika latitude 33 na huo mpaka ulionyooshwa kwenda nyuzi 230 SSW TUVUTE subira mchana haufiki

Watanzania ndugu zangu.

kwa ushauri wangu naomba kama hamjui basi acheni kabisa kutaja haya mambo ya latitude kama hayakuwanata kichwani tangu darasa la sita.

Sijui kimekuingia nini kichwani hadi ushindwe kujua hata kwa kuangalia tu kwamba latitude 33 ni chini kabisa umeshaivuka hata Tropic of Capricon na unakaribia kuimaliza Republic Of South Africa!!!!! Mji wa Portville wa South Africa uko kwenye latitude hii!!!!

Ndiyo utetezi wenu huu na tunasema tuna haki ya kutoa maoni!!!!!
 
Edson, mosi mimi sikuwa najibu juu ya latitude bali alichokisema Membe juu ya Malawi na vifaa vya utafiti wanavyovileta upande wa ziwa wa Tz.

kuna mahali hii topic ambapo imejikita kwenye vifaa vilivyoletwa na mawawi upande wa tanzania??!!...
 
Mleta mada hajalazimisha hata mmoja wenu kuiona hii ni subject ya maana. Ni nyinyi wenyewe mnajigonga kumjibu na hadi thread imekuwa ndefu yaani page saba sasa na post 132 na LIKES saba na PM tele ambazo hana sababu ya kuwaonyesha humu.

Sipati unacho ongea hapa in relation to the subject!
 
kuna mahali hii topic ambapo imejikita kwenye vifaa vilivyoletwa na mawawi upande wa tanzania??!!...

Edson,

Waache wadanganyane. Wanabeza suala la coordinates yaani longitude na latitude wakati ndilo hilo tu litakalimaliza mgogoro huu.

Wanadhani ni enzi za mipaka kuweka mawe wakati technology hiyo ilishapitwa na wachina karne nyingi walipojenga The Great Wall of China.

Kama hujui latitude na longitude za mpaka wako wowote basi acha kabisa kujiingiza kwenye kesi ya mipaka maana ni kuliabisha taifa na porojo zitakazotoka mdomoni mwako.

Membe alilijua hili la latitude na ndiyo maana akalipeleka na kulitamka Bungeni. Tatizo ni kwamba data alizopeleka zinawapa matumaini wajinga wanaomuamini wakati tunaoelewa na ambao mmeamua kuhakikisha mnajua kabisa tuna haki y akuwa na wasiwasi na mbinu za utetezi anazotumia Membe na washabiki wake
 
Nyie mnaongea habari za vita wakati kuna wadogo zetu wameingia jeshini juzi juzi masharobaro wanategemea kwamba Tanzania ilishapita kwenye zama za mapigano , wanategemea kula shushu tu hapo JWTZ. Habari hizi zinawastua sana.:evil:
 
Sipati unacho ongea hapa in relation to the subject!

Usimsumbue Edson,

Mgogoro wa mpaka wa Malawi na Tanzania haujajikita kwenye ndege mbili zilizotua January na February mwaka huu. Mgogoro huu ni wa zaidi ya miaka 50 sasa na tumeshalisema hilo mara kadhaa.
 
Mleta mada hajalazimisha hata mmoja wenu kuiona hii ni subject ya maana. Ni nyinyi wenyewe mnajigonga kumjibu na hadi thread imekuwa ndefu yaani page saba sasa na post 132 na LIKES saba na PM tele ambazo hana sababu ya kuwaonyesha humu.
dah! mkuu umekimbia mita nyingi mno. naanza kuwa na mashaka kama wewe ni mtanzania au mmalawi.
 
Back
Top Bottom