Maishamapya
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,279
- 375
Haya ndio mambo ya Misri kudai kuwa ni marufuku kwa Tanzania kutumia maji ya ziwa Victoria huko Shinyanga na Mwanza - Sababu, mikataba ya wakoloni!
Aliyekomaa nalo ni huyu Membe na sijui kwa nini amelichukua so public kiasi hiki. Hakuwa na sababu za kulipeleka Bungeni kiasi kile halafu unafika huko kwa sababu hukujiandaa majibu yenyewe yanakuwa paragraph mbili na hizi zenye makosa wakati huohuo kuna mazungmzo yanaendelea. Wenzake wote tangu Nyerere walijua kuwa hili si rahisi kiasi hiki na kulipa public interest kama linavyomtokea puani sasa.
Yeye angefanya diplomacy ya kimyakimya kama anavyofanya kimyakimya kwenye suala la OIC na husikii kelele zinamsakama.
Lakini hata leo Membe akitaka kulikoroga la OIC basi nalo alipe publicity kama alivyofanya hili la Malawi. Nadhani hili ilmempa a sounding class.
Nikupateje Wacha kumung'unya maneno wewe.Aliyekomaa nalo ni huyu Membe na sijui kwa nini amelichukua so public kiasi hiki. Hakuwa na sababu za kulipeleka Bungeni kiasi kile halafu unafika huko kwa sababu hukujiandaa majibu yenyewe yanakuwa paragraph mbili na hizi zenye makosa wakati huohuo kuna mazungmzo yanaendelea. Wenzake wote tangu Nyerere walijua kuwa hili si rahisi kiasi hiki na kulipa public interest kama linavyomtokea puani sasa.
Yeye angefanya diplomacy ya kimyakimya kama anavyofanya kimyakimya kwenye suala la OIC na husikii kelele zinamsakama.
Lakini hata leo Membe akitaka kulikoroga la OIC basi nalo alipe publicity kama alivyofanya hili la Malawi. Nadhani hili ilmempa a sounding class.
Nikupateje Wacha kumung'unya maneno wewe.
Umemjibu Yericko Nyerere kwamba ampelekee Membe hizo taarifa sahihi alizokuwa nazo ili apatiwe tuzo. Nami nikakushauri kwamba kwanini usimpelekee wewe hizo latitudes sahihi ili nawe upate tuzo? wala usitafute kuhamisha goal post kuelekea kwa membe kwamba ndiye anakomaa, yes hata akikomaa ni wajibu wake kama waziri wa mambo ya nje.
Ambacho wengi wetu tunajiuliza hapa wewe unakomaa kwa maslahi ya nani? tukisema una dalili za umalawi unang'aka. Kama kweli wewe ni mzalendo wa kweli na una nia thabiti ya kuisaidia nchi yako, kwanini usimpelekee waziri membe latitudes sahihi ili aweze kuwa na hoja ya msingi katika meza ya mazungumzo? na unatambua kikao kingine ni tarehe 20/08/2012 kwahiyo bado hujachelewa kupeleka findings zako ili kuisaidia Tanzania kama kweli wewe ni mtanzania.
Mkuu Mwita,
Tasi hana gamba; mimi ni mzalendo halisi niashi kwa kipato halali sitegemei ajira kutoka serikali ya JMT; CCM wala sifanyi biashara na vyombo hivyo, mimi ni clean ila nina wasiwasi sana na watu wa kaliba yako wanaopiga kelele gamba la kobe ilhali wao wenyewe wamevaa magamba ya kasa; hapa nilimpongeza Yericko Nyerere kwa kuongea ukweli na kuonyesha uzalendo na utaifa, pitia posti za vijana wako wa Chadema kina matola, precise pangolin na wengine tu; badala ya kuwakemea vijana wako umekimbilia kunishutumu, mimi nilipitia JKT najua nini maana ya utaifa na unazi wa kichama, kwangu taifa mbele period!!! I trust you don`t be simple just because you want to side with some stupid and simple minded makamanda
Chama
Gongo la mboto DSM
Siku mpya imeanza, ngoja sasa nizane kujibu hoja zenu ambazo ni rahisi sana kama ifuatavyo.Ngoja nilale tutakutana asubuhi.
Wewe Mmalawi usitake kutufanya sisi wabongo hatujuwi haya mambo, kukufahamisha ziwa Nyasa kwa juu liko latitude ya 9 degree na dakika 40 kwa longitude ya 34 degree na dakika 15 (kwenye lamani ya QDS 273/2) ambayo inaitwa Lupila.
Kusini ziwa liko kwenye longitude ya 34 degree na dakika 40 ambalo ni eneo la Lundu kwa wenyeji wa huko watakuwa wanapafaham na latitude yake ni 10 degree na dakika 45 (QDS 297-1 Lituhi).
Naomba nikukumbushe kitu kimoja unapotaja hizi point huwezi kutaja latitude pake yake bila kutaja longitude yake na kwa UTM Ssystem huwezi kutaje X- cordinate bila Y - cordinate na ARC1960 kwa WGS84 ni conversion tu ndugu yangu 300m kwa X na 200m kwa Y.
Asante kwa ufafanuzi mkuu! Huyo mmalawi wakuogopwa!
Ujuha wa wamalawi na wanaowaunga mkono umelala kwenye imani ya kile wakiitacho makubaliano ya wajerumani na waingereza,wala si makubaliano wenyeji wa mwambao wa ziwa hilo,hata kama akili yako haijakomaa ni mahakama ya nguruwe pekee inayoweza toa haki kwa Malawi kumiliki ziwa lote wakati hilo ziwa linagusa ardhi ya nchi nyingine inayokaliwa na watu ambao wanayo haki ya asili kutumia maji ya ziwa hilo. Iwe Membe kakosea malatitude na malongitude au kapatia ukweli unabaki kama ulivyo kuwa ziwa ni mali ya wale wanaoapakana nalo nusu kwa nusu
Temporary treaty aimed at resolving the boundaries between British sphere of influence and German sphere of influence.
Only lake victoria was marched upon the delimiting line between them.
The rest of interterritorial waters were not, simply because there were no lands (habitable) between Tanganyika and Nyasaland.
The Lake was being treated by both as international waters. There were German and British gunboats sailing freely in those waters prior to 1914.... why do you think Britain allowed German vessels in their waters? Or vice versa?
Mwacheni aendelee kupepeta uongo wake hapa!
Siku mpya imeanza, ngoja sasa nizane kujibu hoja zenu ambazo ni rahisi sana kama ifuatavyo.
aliyesema watanzania ni wavivu wa kusoma au kutafiti hakukosea tena ni Rais wenu wa thrid phase (Mkapa).
Mimi naweza kuamini kitendo cha kuona ziwa liko shared kule Mozambique kimewachanganya na kuwafanya muige.
Nikupateje Wacha kumung'unya maneno wewe.
Umemjibu Yericko Nyerere kwamba ampelekee Membe hizo taarifa sahihi alizokuwa nazo ili apatiwe tuzo. Nami nikakushauri kwamba kwanini usimpelekee wewe hizo latitudes sahihi ili nawe upate tuzo? wala usitafute kuhamisha goal post kuelekea kwa membe kwamba ndiye anakomaa, yes hata akikomaa ni wajibu wake kama waziri wa mambo ya nje.
Ambacho wengi wetu tunajiuliza hapa wewe unakomaa kwa maslahi ya nani? tukisema una dalili za umalawi unang'aka. Kama kweli wewe ni mzalendo wa kweli na una nia thabiti ya kuisaidia nchi yako, kwanini usimpelekee waziri membe latitudes sahihi ili aweze kuwa na hoja ya msingi katika meza ya mazungumzo? na unatambua kikao kingine ni tarehe 20/08/2012 kwahiyo bado hujachelewa kupeleka findings zako ili kuisaidia Tanzania kama kweli wewe ni mtanzania.
Mkuu chama unapozungumzia masuala ya kitaifa halafu unaanza kuchomekea vijembe hapo itakuwa vigumu kusalimika na mashambulizi ya ku-counter.
Kwahiyo ni muhimu kujiepusha na lugha yoyote yenye kuudhi ama kejeli kwa wenye itikadi tofauti na wewe tunapozungumzia masuala ya nchi yetu, mipaka ya nchi yetu. Otherwise nimekusoma, washauri na wenzako wajitahidi kujitegemea kama wewe, hii ya kutegemea huruma ya chama ndio inawafanya wageuke kuwa manamba.
Nimeamua kuiweka hii kwenye separate thread kwa sababu nimeona ina extra concept kulingana na ile ya jana.
Wakati nanunua gazeti nilitumaini kabisa Membe atakuwa na hoja ya ku-convice kwani humu JF mnaongea tu kama mimi. Kwa wale waliosoma RAIA MWEMA wafungua attached paper kwenye ukurasa wa iv. Ndipo anaeleza msimamo wa Serikali kuhusu mpaka wa Ziwa Malawi.
Nakiri kwamba hata wakati naleta thread ile ya kwanza, nilitumaini Bernard Membe atakuwa ameongelea findings ambazo zingetushawishi na mimi nisingesita kuungana kwenye nia ya kukidhi madai haya ya Lake Malawi.
Lakini baada ya kusoma speech ya Membe basi matumaini yote ya kulipata Lake Malawi yamenitoka. Narudia sipingi Tanzania kupata sehemu ndogo ya Lake Malawi kama baadhi mnavyoropoka. Na hata mnavyoropoa wengine hainipi matumani ya kulipata hilo Ziwa. Lakini aliyenisikitisha zaidi ni Waziri Membe na sasa kwangu ni dhahiri kwamba tusahau kabisa kulipata Ziwa hili.
Siku moja nilifanya hesabu ubaoni nikapata jibu na baadaye nikaongeza madoido mwalimu akanikata maksi akasema "Kujitawaza kwingi mwisho unashika kinyesi". Naona ndugu yetu Waziri Membe kaingia katika mtego huu. Kwa nini nasema hivi? Ninanukuu majibu yake kama ifuatavyo:
****
Mheshimiwa Spika,
Lipo tatizo la muda mrefu kati yetu na nchi jirani ya Malawi linalohusiana na mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Tatizo lenyewe ni kwamba Malawi wanadai kwamba ziwa lote kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa mwaka 1890.
Mheshimiwa Spika,
Tanzania kwa upande wetu tunasema kuw ampaka wa kweli kati yetu na malawi unapita katikati ya ziwa hivyo kufanya eneo lote la Kaskazini Mashariki ya Ziwa kati Latitude digrii 9 na digrii 11 kuwa mali ya Tanzania kwa mujibu wa mkata huouo wa Heligoland wa mwaka 1890 ambao ulikubali kuwa kwa vile kuna maeneo ya mpaka ambayo hayana mantiki, pande zinazohusiana zikutane na kurekebisha. Aidha tunazo ramani ambazo waingereza wenyewe walipitisha mpaka katikati kama ulivyo mpaka kati ya Msumbiji na Malawi.
****
Nimemalizia hapa kwa sababu mengine yanayofuata ni diplomatic process. Sasa hapa tuchambue hotuba hii ya Membe. Binafsi nimeusoma mkataba wote wa Heligoland na wala si alichokisema Membe. Kama membe anataka kuikomboa Tanzania walau tupate sehemu ya Ziwa basi washauri wake wamempotosha kutumia mkataba ule ambao hautetei hoja yake hata kidogo.
Lakini pia Membe ni mmoja wa wanaodhani watanzania wa sasa hawajui kufukua mambo na ndiyo maana kwenye thread yangu nimesema tutumie usomi wetu. Membe ametaja kwamba sehemu ya ziwa kati ya Latitude digrii 9 na digrii 11 ni mali ya Tanzania.
Hapa ndipo Membe ameumbuka umbuko ambalo hatalisahau. Kwa nini nasema kaumbuka. Kaumbuka kwa sababu geography ya Tanzania wote tunaijua. Ncha ya juu kabisa ya Lake Malawi iko kwenye coordinate { S9.49214 E34.03563} ambapo ni only 7.0km kutoka kijiji kiitwcho Matema kilichopo kwenye coordinate { S9.49601 E33.97215}.
Ukiangalia coordinate hizi maana yake ni kwamba Ziwa Malawi linaishia kwenye Latitude 9.49214. Sasa hapa Membe anasema eti ni kuanzia Latitude 9. Kwa maana hii ya Membe kama Ziwa ni letu kuanzia latitude 9 maana yake ni kwambaMmembe kafanya makosa kwa kulirefusha ziwa hili kwa umbali wa 54.4km kuelekea kaskazini!
Watu mnaotoka kusini hasa Mbeya mnafahamu sehemu iitwayo Matamba. Hapa coordinate zake ni { S9.01171 E34.09959}. Kwa mujibu wa Membe, hii Matamba ingekuwa imeguswa na Ziwa hili!
Hakika waliomletea Membe hizi data wamemvuruga kuliko kulietengeneza suala hili. Ziwa Malawi au Nyasa linaishia kwenye Latitude 9.49214 kama nilivyosema hapo juu. Hapa membe kadanganya Bunge na kadanganya watanzania kasi kwamba sijui sasa ni nani mwenye nguvu ya kulitetea hili.
Tuje sasa kwa upade wa kusini yaani unaotambuliwa na membe kama sehemu yaetu ya Ziwa. Membe anasema sisi mali yetu ni mpaka kwenye latitude 11. Sijui wangapi mmeona kosa hili la mwaka. Unaposema kwamba unaishia hapa kwenye Latitude 11, je mnaotetea hoja hii mnaelewa madhara yake? Kama hamyajui basi mimi nayasema hapa.
Kama Membe kasema Bungeni kwamba tunaishia kwenye Latitude 11 basi maana yake pale ni kaskazini ya sehemu iitwayo Liuli ambayo iko { S11.05023 E34.63908}. Kumbe, Mwanakijiji wa Liuli haruhusiwi kuvua samaki kwenye ziwa lile kwa sababu ni sehemu ya Malawi, kwa mujibu wa Waziri Bernard Membe!
Yaani mwanakijiji huyu wa Liuli, anakuwa amekiuka mpaka kwa kilomita 6.6 kwa mujibu wa Serikali anayoshiriki membe wala si kwa mujibu wa Serikali ya Malawi!
Nimeanza na mfano huo wa Liuli ambao najua wengine hampaju ahapo. Sasa tuje kwenye mfano ambao wengi mnaujua na mmeutumia kunipinga humu na kuniita mimi ni mmalawi.
Mfano wenyewe ni wa Mbamba Bay. Ndiyo maana nimesema kajipangeni hii kesi tutajikuta tunasambaratika tukidhani tunatetea huku tunajiangamiza. Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.
Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Mbamba Bay haiko katika eneo linalotambuliwa na Waziri Membe kwa latitude degree 0.30519!
Uki-convert hizi latitude kwenda kwenye kilomita basi maana yake Membe haitambui Mbamba Bay kwani iko 33.7km nje ya eneo ambalo Tanzania tunamiliki ziwa!
Waziri membe pia inaelekea kuwa hajui mpaka unavyopita pale Msumbiji. yeye anasema kule ni nunu kwa nusu lakini wote fungueni ramani muone kama hilo nalo lina ukweli. Mpaka wa Msumbiji ni nusu kwa nusu kuanzia kwenye latitude 11 had 13 lakini kuanzia hapo kueleka kule chini kusini ziwa lote liko sehemu ya Malawi na linaishia kwenye coordinate {S14.44635 E35.23539} ambako ni latitude 14.44635.
Hivyo, tujenge hoja zinazojikita kwenye ukweli na tusishabikie mambo kama vile Simba na Yanga. Hapa hatufanyi ushabiki. Hapa tunasaidia kujenga na kupima hoja kama kweli tunaweza kuisaidia nchi yetu kupata sehemu ya ziwa hili.
Ninasubiri kwa hamu kuona mtakuja na hoja gani kuhusu hizi findings zinazochambua hotuba ya Membe na matokeo yake niliyoeleza humu.
Hata Misri walikuja na hoja kuwa Tanzania haturusiwi kutumia maji ya ziwa victoria kwa matumizi zaidi ya kunywa.Lakini leo kule shinyanga ninayo bustani kubwa kishenzi inatumia maji ya ziwa victoria.Kwa taarifa yenu aliyeukataa huo mkataba wa kishenzi ni Mh.Ngoyai Lowassa EDUARDO wakati akiwa waziri wa maji.Chezea LOWASSA WEYEEEEE MALAWIEEEH!!! Utatoka manundu