Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
- Thread starter
- #81
Kiongozi hujaelewa mantiki. Vyote viwili vinatubana. Ramani ndio iliyopelekea mkataba ambao inaondoa ziwa nyasa lote kwenye miliki ya Tanganyika. Wote mfahamu pia kuwa huyo huyo Mwingereza ambae ni chanzo cha ramani au mkataba (as the case may be) ndie aliyetawala nchi hizi mbili (South Rhodesia -Malawi) na Tanganyika (TZ). Ndie ambae sasa anahusika na exploration kwenye ziwa Nyasa au Malawi. Tunachopaswa kuangalia ni msingi wa hoja zetu! Kwani mipaka na nchi nyingine tumenaithibitisha kwa kutumia nini kati ya Ramani au Mikataba? Kama tukienda kwa staili hii eti mipaka iliwekwa na wakoloni hatuwezi kushinda hoja kwani bila hiyo mipaka ya wakoloni hata leo sisi tusingejiita nchi huru Tanzanian na hata ile kesi yetu na wakenya kuhusu mlima kilimanjaro au ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa pale Taveta tutakosa hoja za msingi kwa nini hilo eneo lisiwe la Kenya (nini kinatulinda)?!. Kwa hili hata tukienda kidiplomasia tutaingia kwenye chaka la kutengeneza mkataba mpya kama sio kuambiwa tumilikishwe sehemu ndogo ya ziwa nyasa kwa kuwa kisheria hatuna haki ya moja kwa moja. Kuwapiga stop Malawi wasifanye utafiti kwny ziwa lote hatuwezi, wao wanatueleza wamenza kwa eneo wanalotumia sasa na wanaweza kuendelea au kuacha pindi mgogoro wa umiliki wa ziwa ukiisha. Umakini unahitajika kwa hili, wabongo siku zote tunaishi kwa kutumaini huruma za wenzetu.
Nakubaliana na hoja zako ila kuna marekebisho kidogo na ninadhani umeteleza kwa bahati mbaya na unahitaji kuelimishwa. Mipaka yote haitawaliwi na ramani iliyochorwa bali inalindwa na mkataba uliopo hata kama ilikuwa ni ile tuliyoita bogus-treaties kama ule aliosaini Sultani kuuza kisiwa cha Mafia kwa kitambaa kinachoweza kuizunguka Mafia yote.