Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

Yaani watanzania ndo wamewakata kwelikweli mbinu ya kwanza kutumia wasichana wakali pili kuonyesha mafanikio ya uongo si mnajua tena maskini kwa tamaa
 
mi kuna mmoja alinitoa boko hadi posta,nisijue ananiitia nini,duu nilipewa semina nakulazimisha nichukue mzigo muda huohuo nilikuwa na pay kidogo,nikakataaa maana nilikuwa natetemeka kwa hasira
Hahaha mi wakuniita kwa sasa nafwata nyayo halafu nawabadilikia
 
1477369162648.jpg
 
Ni kweli aisee, wanaboa sana.

Kuna siku wamenitoa Mbezi mpaka Makumbusho nikajua bonge la mchongo.

Mwisho wa siku nakuta ni ishu za forever Living, nili mind sana aisee, basi tu utu uzima nikaamua kupotezea.

Hawa jamaa wanaboa sana, usiombe wakapata namba yako ya simu, utakoma
ukaishia kula ubwabwa tu
 
Habari za weekend.....

Wauzaji wa bidhaa za forever living, kwanza hongereni kwa kufanya hiyo biashara inayohitaji kipaji cha hali ya juu kuweza kuongea sana na kumshawishi mteja, ni kipaji kwakweli.

Back to topic, mmekua mnatumia mbinu za uongo na kulazimisha sana mteja ili mtangaze biashara aaagrrrr hii mbinu yenu Inakera sana,inaboa sana

Mfano 1: siku za karibuni nikialikwa mahali, nikaambiwa ni semina nauliza semina ya nini nikaambiwa semina tu nihudhurie napigiwa simu za kusisitiza nikaona isiwe tabu ngoja niende nikaahirisha vitu vya muhimu kwenda semina, kumbe ni kwenda nyumbani kwa mtu kuoneshwa bidhaa za forever, wtf? Kwanini umdanganye mtu? Can you imagine nilikua nafeel vipi wakati naoneshwa hizo bidhaa? Mxyu nilikua nimekasirika sana

Mfano 2: dada mmoja kwenye group la whatsapp alitoa mwaliko, jaman karibuni kwangu sehemu flani kuna shughuli, msosi na bia vipo mtakula mtakunywa mtasaza, tunauliza ni nini ubarikio, engagement au nini mchango vipi anakomaa nyie njooni tu eeeh walaji na wanywaji wakaenda eneo la tukio wamevaa suti kumbe ni kuoneshwa bidhaa za forever, Wiki nzima group kimya hakuna anaeongea kumbe watu wamenuna

Mfano 3: Wauzaji wa online, mtu anasema una mtaji wa laki njoo whatsapp tufanye biashara ukiuliza biashara gani unaambiwa njoo whatsapp, unaenda whatsapp anakutumia video la mb 100 kutangaza forever.

Hii ni mifano michache, hivii hamuoni mnakwaza watu? Hakuna mbinu nyingine za kutangaza bidhaa zenu bila uongo??? Au bila kudanganya hamuuzi? Mnakera sanaaaaa
Ni hayo tu
Nakupta ila mie naona tatizo liko kwako hasa ukitaka kuwa mkweli na wa haki. Ulitamani maisha fulani simple ndo maana ukanaswa na mtego huu. Hebu tuwe watu objective and rely on our objectives hapo hatutayumbishwa.
 
Nakupta ila mie naona tatizo liko kwako hasa ukitaka kuwa mkweli na wa haki. Ulitamani maisha fulani simple ndo maana ukanaswa na mtego huu. Hebu tuwe watu objective and rely on our objectives hapo hatutayumbishwa.
Kwamba nilitamani kuuza forever au sijakuelewa
 
Kweli jamanii, mm kuna mama kaniganda mpaka natamani nibadili laini ya simu kila cku njoo kwa semina mara mavideos kibao Whatsup jamanii,... Aaaghhg kweli wanaboa bhana
Forever living wanajua kumganda MTU khaaa! Mi pia kuna MTU alikua ananiganda wee....kuona ananiganda sana ...nikataka kujua zaidi kuhusu forever longing coz nilikua naijua tuu kawaida...nikaingia Google nikawanasoma habari zake, katika kusoma nikakutana na mzungu mmoja, yeye yuko forever nae...tukaendelea kuchati kuhusu forever....hapo nikagundua kumbe kuingia forever kumbe mnaandikiana hadi mkataba....akanitumia mkataba ktk ambao watu hupaswa kusaini wakitaka kujiunga forever living....nikausomaa....katika kifungu cha Tisa au kumi if I'm not mistaken kinasema hivi ukijiunga forever living "HUWEZI KUJITOA FOREVER LIVING UNTILL THE EVENT OF DEATH" nikamuuliza kuhusu hichi kifungu akawa nae hana majibu ya kujitosheleza. Nikarudi kwa yule alokua ananiganda nikamuuliza kuhusu hicho kifungu mbongo mwenzangu ( c unajua wabongo tulivyo waongo) akasema hicho kifungu hakipo OK nikamwambia nitumie huo mkataba...akasema atanitumia...mpaka Leo....!! Kwa hiyo tuwaonee huruma wameingia ktk kampuni na kusaini mikataba wasoijua kiundani...mtu huwezi kulazimishwa kukaa mahali ambapo hamna maslah....km MTU ameingia kwa hiari atoke kwa hiari....kwa hyo wanatafuta watu wa kusaini mikataba ya ki- bogus.
 
Haa haaa hii mbinu iliwahi kuninasa miaka 3 iliyopita,niliambiwa kuna semina nilipodadisi zaidi nikaambiwa ni masuala ya biashara kufika ni mipasho ya managers jinsi walivyofanikiwa kimaisha na blah blah kibao.

Baada ya muda nikagundua waliofanikiwa ni waanzilishi ndio wanapiga mifedha kupitia wanachama wapya.Bahati nzuri sikuingia nilinunua bidhaa chache kwaajili ya majaribio lakini sikuona kitu cha tofauti zaidi kuvuta wanachama kwa nguvu na ushawishi mkubwa.

Hii biashara si mshauri mtu mwenye akili zake ajiingize hata kidogo.Kwanza itakuwafanya uonekane mwehu kiasi fulani,pili itakuchukulia muda wako,fedha zako na nk.
Yeah....unasema ukweli...waliofanikiwa ni wale waanzilishi...wageni wao ni kutuma video na picha za mafanikio za wale walowatangulia......
 
Kwa jinsi unavyoongea neno upumbafu inaonyesha ni nembo ya maisha yako
Sikiliza dini ni imani si kitu ambacho kina uhakika kwa asilimia zote kwahiyo ukiona mimi au yule anaamini kidogo ama hana imani na dini usimchukulie kama majinga unaamini tu....huna uhakika ni upumbafu sana kuabudu kanisa msikiti shehe shemasi mimi siamini
 
Back
Top Bottom