Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 63,599
- 112,654
- Thread starter
- #261
mimi waliniita mahali fulani kwa ajili ya semina nauliza semina ya nini naambiwa ni semina ya motivation & inspiration kufika bhana nikaona kuna tickets zimeandaliwa ambazo hazikutaja chochote kuhusu forever living zaidi ya picha za watu wamevaa suti nikajua yeeeess ndo penyewe hapa
akatokea jamaa mmoja akaongea takriban dakika 90 na wala hakuongea kitu chochote kuhusu forever living na kwa kweli aliongea vizuri sana kitu kimoja kilichonifanya nihisi kuna ulaghai ni kabla ya yeye kuanza kuongea aliweka speech ya nani sijui ambayo ilisaidia ku-brainwash watu na kuwaandaa kwa ajili ya kuikubali hiyo forever living
baada ya hizo dk 90 ndo akaanza kuleta masuala ya unene sijui na kuonyesha picha za sehemu za mwili wa binadamu zilizoathiriwa na magonjwa kama tezi dume nk halafu huyooo akafunua koba lake akatoa dawa za forever living aisee nilishikwa na hasira kali nikanyanyuka na kusepa muda huo huo