Lead Generation 101: Muongozo Kwa Wafanyabiashara Wanao Promote Bidhaa Zao Kupitia Mitandao ya Kijamii

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
131
259
Kainetics Lead Generation 101.jpg

Hello JF, ni muda umepita toka niandike kitu chochote humu, na kwa leo, since I feel like writing, nimeona niandike kuhusu kitu kinachoitwa Lead Generation; Skillset muhimu ambayo itabidi uwe nayo kama unalenga kutangaza bidhaa au huduma zako kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram, nk. Hata WhatsApp Statuses.

Bila kupotezea muda, mambo nitakayozungumzia humu ni pamoja na;

🏌🏾‍♂️Lead Generation + Basics
🏌🏾‍♂️ Aina Za Leads
🏌🏾‍♂️Kutangaza Bidhaa/Huduma Zako Kwa Akili
🏌🏾‍♂️ Extra Tips/ Do-Nots

Lead Generation+ Basics

Well, kama ni neno/concept geni kwako, kuelewa lead generation na ni jinsi gani inavyoweza kukusaidia kwenye kuboost mauzo yako unapotangaza Bidhaa au Huduma zako mtandaoni, itabidi uanze uelewe maana ya neno Lead.

Lead ni nini/nani?

Lead ni mtu ambae anaonesha interest/kuvutiwa na au uhitaji wa bidhaa au huduma zako kwa namna moja au nyingine.

Nikisema namna moja au nyingine, namaanisha...

i) Yupo mtu atakua interested kufahamu zaidi kuhusu bidhaa/huduma zako hivyo atakua na maswali ambayo angependa ajibiwe kabla hajafanya maamuzi ya kuwa mteja.
Mfano; Umepost tangazo lako kwenye magroup kadhaa kuwa unauza na kukodisha vyombo vya mziki na umetoa mawasiliano yako. Mtu alite kwenye stage hii atakutafuta akiwa na madhumuni ya kufahamu mambo kama gharama, aina za vyombo, vinamfikiaje, na vipi ikitokea itilafu mna share vipi gharama za matengenezo, nk.

ii) Yupo ambae tayari anatumia bidhaa/huduma zako za bure au zilizo sawa na zako (zinazopatikana bure) , na anataka kuanza kulipia. Let's say una channel YouTube unako post tutorials za Mapishi, lakini umeanza compile vipindi vyako na kuviuza kwa mfumo wa DVD's na Soft Copies.
Mtu atake kutafuta kwa stage hii, atakua anataka fahamu mambo kama; namna ya kufanya malipo, CD husika zinamfikiaje, zinakua na recipes ngapi, nk.

iii) Yupo ambae hayuko experienced kwenye mada husika, hajawahi sikia bidhaa/huduma kama zako na hapo nyuma hakua na uhitaji ila baada ya kupitia tangazo lako, akawa interested kujua zaidi. Hawa huwa wako wengi, na ndilo kundi ambalo (kwa bahati mbaya) hulengwa na matapeli, mtandaoni.

Aina za hawa Leads sio hizo tu, ni nyingi. Inategemea na makundi ya aina ya watu unayovuta kutokana na matangazo yako. Point nzima ya kuanzisha hii thread, ni kuweza wasilisha ushauri wangu kwa wale wanaofanya hii kitu ya kutafuta mauzo ya bidhaa/huduma/kazi zao mitandaoni na ushauri wenyewe ni huu; "Acha kutafuta wateja mitandani, bali wekeza juhudi zako katika kutengeneza leads".

Kutengeneza Leads ndiyo Lead Generation. Ni wachache mno ambao wanafanya hii kitu. Matangazo mengi ambayo utayakutana Facebook, Instagram, Twitter na hata humu JamiiForums (ukiachana na Sponsored Ads) mengi huandaliwa kwa madhumuni ya kukufanya ushawishike na kuwa mteja, jambo ambalo sio rahisi kutokea.

Matangazo mengi ya biashara utayakuta kwenye magroup, au Comments katika Posts zinazo trend. Yanakua marefu, yameandikwa kijanja janja, na kama yameambatanisha picha, basi huwa nyingi nyingi, za quality ndogo. Na kama zime editiwa (mf. Kuonesha bei, nk) basi zitakua edits za kitoto.

Kama umekua ukitumia njia hiyo kujitangaza aidha wewe au brand yako, unaweza fanya marekebisho machache yatakayo kupatia matokeo endelevu baada ya muda.

Kwanini Ufanye Lead Generation?

Kama uliwahi fanya biashara yeyote mtandaoni, na mtanzania, bila shaka utakua huna haja ya kuuliza hilo swali. Kuna kila sababu ya kuweka mikakati ya kujipatia leads ambao wako kwenye stage unayoitaka wewe (mtu ambae hajawahi sikia kuhusu bidhaa zako, mtu aliowahi zisikia ila hazifahamu kiundani, mtu anae zitumia tayari lakini unataka achukue iliyo bora zaidi, nk) Sababu chache ni kama hizi;

🌱 Itakupunguzia Stress; Hakuna kitu kibaya kama kufanya biashara na mtu aliyekuja na matarajio yake, kisha mwisho wa siku, bidhaa au huduma zako zishindwe kuyafikia. Kujua matarajio ya potential customers itakusaidia namna ya kudeal nao ili uweze fanya sales bila usumbufu.

🌱 Itakuwia rahisi kufahamu lead wako anataka nini hivyo kukupa shortcut kwa baadhi ya watu watakao onesha interest. Mfano; Kama unauza Skin Care Products kwa mtu mzoefu kutakua hakuna haja ya kuingia deep into details maana utakua unafahamu already kua ni mzoefu.

🌱 Utakua na chance kubwa ya kuwageuza hata wale wasio na interest/wenye interest ndogo, kugeuka kua Potential Customers

🌱 Itakuboreshea Brand Image (If you are a Brand)

🌱 Kutakua hakuna haja ya kudanganya watu ilimradi wakutafute/waguse link yako/wakupigie nk.

🌱 Mauzo yatakayo mengi kwa effort ya kawaida.

Unafanyaje Lead Generation?

Lengo kubwa la Lead Generation ni kuwageuza watu ambao hamjuani kabisa kuwa wateja, na sehemu ya Brand yako. Ili uweze kulikamilisha hilo itabidi uwekee mkakati wenye stage nne ambazo itabidi uzitumie kwa wakati wote. Ila kabla sijaziongelea stage hizi; Jitahidi kabla ya kuanza nazo, Uwe umefanya yafuatayo;

✅ Jitahidi uwe na Page binafsi kwa ajili ya biashara yako kwenye mitandao yote ya kijamii utakayokua unatumia.

✅ Hakikisha Page yako ina Logo na Cover Image iliyotulia.

✅ Hakikisha Page yako ina Mawasiliano yako muhimu kama Namba ya Simu, Email, Anwani na CTA Button

✅ Post Bidhaa/Huduma zako mara kwa mara na hakikisha posts husika hazina maelezo kibao. Kama utaambatanisha picha, basi ziwe na Quality nzuri na ikiwezekana zisiwe na maandishi ya aina yeyote ile (maybe weka logo yako tu, if necessary)

✅ Lastly, jitahidi uache kabisa tabia ya kucomment (spam) kwenye posts za watu wengine na magroup. Kwa kufanya hivyo, unapunguza hadhi ya brand yako kwa asilimia kubwa.

Baada ya kuhakikisha umefanya hayo tajwa hapo juu. Unaweza anza Lead Generation kimkakati kwa Hatua Zifuatazo;

1. VUTA WATU

Kwanza, tafuta watu unao walenga waliko, na wapatie sababu za kukufuatilia kwa umakini. Mfano;
Kama unauza furniture, basi jiunge kwenye magroup ya Home Decor, Interior Designs, nk.

Share maujanja, humo, ikiwemo maswala kama namna ya kusafisha masofa, kwa usahihi, miti mizuri kwa ajili ya kutengeneza furniture imara, designs kari za meza ambazo sii ghali kutengeneza , nk. Kiufuoi toa mambo yanayo elimisha, na kuburudisha kuhusu mada husika.
Baada ya muda utaanza kuvuta watu ambao wako na interest na mambo ya furniture, na ukianza kunotice upward trend kwenye shares na likes, basi anza kuambatanisha link ya page yako mwisho wa hizo posts zako unazo weka kwenye groups.

Inaweza kua kitu kama hii: "Kusoma Zaidi, Kuhusu Utengenezaji, Utunzaji na [Blah Blah Blah] wa Furniture, Follow na U Like Page Yangu 👉 (Link ya Page Yako)"

2. WABADILI NA UPATE MAWASILIANO YAO

Kupitia hatua ya kwanza utakua umejitwalia leads wa aina zote. Kwa mfano wetu ule ule wa furniture; taratibu utaanza kusanya watu ambao walikua hawanan interest na furniture ila wameanza kua nayo, wale ambao wana interest na wanapenda soma mambo kama hayo, wale wanaotaka kununua, wale wanaotaka boresha furniture zao, nk.

Hawa watu wote utakua una waredirect waende kwenye page yako, ambako itakubidi uwe una post mara kwa mara kuliko unavyofanya kule kwenye magroup. Sasa wakisha geuka followers, (by their own will and not click-bait) kitakachifuata ni kuwageuza kuwa wateja na kupata mawasiliano yao.

Namna ziko nyingi;

a) Toa GiveAway : Toa ka shindano katakako wachangamsha , na mpatie mshindi zawadi. Unaweza uliza swali simple na kuandika namba yaki ya simu, kua watume huko majibu. Unawaambia mshindi atatangazwa kwenye Page muda fulani. So hata ungekua na Page ndogo yenye Followers 100. Kama wako Authentic, kupitia GiveAways za design hiyo utakua unapata walau replies Inbox kama 35 minimum.

Pia kama unatangaza bidhaa zako Kupitia Tsapp Status, unaweza weka namba ya vocha kila jioni muda fulani. Itakusaidia kua na Constant Views.

b) Toa Offer ya Aina Yeyote Ile : Linaweza kua punguzo la bei, inaweza kua 'nunua mbili pata [kitu fulani] bure, nk. Hapa ndo unaweza ona mambo kama " Kupata Offer hii nitumie text 'NatakaOfa2525' kwenda [Namba Yako]

c) Gawa Kitu Cha Bure : Kama Biashara yako inaruhusu. Inaweza kua picha, infographic, maybe ni banner au poster (kama we ni Graphics Designer) nk. Watu wengi wanapenda vitu vya bure, na hio ni namna mojawapo ya kuwapata.

Dhumuni kubwa la stage hii ni kuwageuza strangers kuwa watu wenye idea na kitu unachokifanya, ila most importantly ni kupata mawasiliano yao.

3. WAUZIE

Mara nyingi huwa rahisi kufanya biashara successfully na mtu aliekutafuta mwenyewe kuliko ulie mtafuta wewe. Hio ndio sababu zile text za "Hello, namba yako nimeitoa kwenye Group X na mimi ni X na nafanya 1 2 3" huwa zinaboa.

Kama mtu angekua anataka kukufahamu angekutafuta mwenyewe and it's not the other way around. Hivyo jitahidi leads zako wanakutafuta wao kutokana na offer utakazokua umetoa, na jitahidi kutunza uaminifu. Kama umesema kuna discount, basi iwepo kweli na Uwauzie. Kama ni Giveaway, isiwe Fake. Tangaza washindi na uwape zawadi zao.

In the meantime, ukipata contacts zao haswa namba za simu. Kama una post bidhaa/huduma zako status lazima 20% yao watanunua bidhaa every now and then na bila usumbufu wowote kuliko wale mnao juana siku hio hio na kutaka muuziane vitu.

4. TENGENEZA FAMILIA

Ukifanya biashara na mtu kwa uaminifu na wakati, chances ni kua atarudi na yeye bila hata ya kutumwa atakutangazia biashara yako kwa watu wake wa karibu (kama inaruhusu)

Hivyo jitahidi kwa kila sale unayopata, mambo yaende sawa ili uzidi kujiongezea credibility. Na ndani ya muda mfupi utajikuta na familia kubwa tu ya wateja, na marafiki zao, na marafiki za hao marafiki , na kadhalika.

Huku ukiweza yafanya hayo yote bila kutokwa jasho kihivyo, au kua spammer kwenye posts na jituhada za watu wengine.

Ukioana unauzia watu wengi wengi kidogo, walau hata unapata mauzo 50 kwa mwezi, jaribu kutengeneza Sponsored Ad hata kwa $5 mara moja moja kukuza reach na engagement ya Page yako. Matokeo hayatokua ya haraka, ila eventually it will be worth it.

Itimisho

Kwa kufinalize, naweza shauri uwe na Graphic Designer kama biashara au huduma unazo promote ziko Visual. Kwa sababu isiyojulikana, picha mbaya mbaya zenye quality duni, huusishwa na utapeli, and you don't want that happening to your brand.

Pia ukiweza, wekeza kwenye blog/website ya biashara yako. Itakurahisishia mambo mengi mno na utaweza wafikia watu wengi zaidi. Pia mauzo, offers na giveaways unaweza automate humo humo kwenye tovuti yako. Hivyo kuku okolea muda.

Screenshot_20230328-063744_1.jpg

Lastly, nishauri utumie WhatsApp Business. Feature ya Labels ni nzuri sana. Unaweza Mark Stage Leads Zako Watakazo Kuwa Wanapitia Kuanzia; Stranger (through Interested, Participating, Customer, Recurring Customer, Critic ) hadi Final Stage, Family.

Hizo Stages nne kuu nlizozungumzia , ni Stages za kitu kinaitwa Sales Funnel. Same Concept, though.
Natumai utakua umejifunza jambi moja au mawili.

Nawasilisha, Kainetics
 
[mention]Kainetics [/mention] Hizi ndondo nazisomaga kwa lugha ya malkia leo naina umeandika kwa lugha yetu. Ahsante kazi nzuri.

Hivi Tz email marketing inafanya kazi kweli, kwa wateja labda sales channel tuseme ni LinkedIn in?
 
Kama una target watanzania mbadala wa email unakua namba za simu(WhatsApp) coz mambo mengi ambayo ungeyafanya kwa email marketing, haya apply kwetu. Ila kwa ku-center strategy yako kwenye namba za simu. Unaweza pata results zile zile
 
Point nzuri
 
View attachment 2568261

View attachment 2568258

Lastly, nishauri utumie WhatsApp Business. Feature ya Labels ni nzuri sana. Unaweza Mark Stage Leads Zako Watakazo Kuwa Wanapitia Kuanzia; Stranger (through Interested, Participating, Customer, Recurring Customer, Critic ) hadi Final Stage, Family.

Hizo Stages nne kuu nlizozungumzia , ni Stages za kitu kinaitwa Sales Funnel. Same Concept, though.
Natumai utakua umejifunza jambi moja au mawili.

Nawasilisha, Kainetics
nitumie maarifa gani kupata maneno ya kutag.
Kam hizi tags.

Screenshot_20230503-114505_1.jpg
 
Back
Top Bottom