blea
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 379
- 114
vipeperushi dar wachaga warudi kilimanjaro!
kitafuata nini baada ya kurudi
vipeperushi dar wachaga warudi kilimanjaro!
Hicho kipeperushi mbona kama kimeandikwa na mtu ambaye shule ilikua kituo cha polisi, halafu imejaa gadhabu mno!
Ndugu yangu hiyo chuki inayoenezwa na hao wapemba wa uamsho ndiyo hivyo, hao wabara wanavyosemwa huko zanzibar utafikiri huku bara hakuna wazanzibari. Mi nashangaa sana, kariakoo imejaa wapemba, temeke imejaa wapemba, namanga wapemba, kinondoni wapemba, ilala wapemba, morogoro wapemba, wapemba wako maeneo yote huku. Nenda tegeta maduka ya mbao, cement n.k. wapemba au wanafikiri muungano ukivunjika tutawaachia waendelee kukaa huku halafu wao watutimue kwao?safi sana maana haiingiii akilini wabara wafukuzwe pembe ili hali wapemba wapo kibao huku bara
Nimepita!
Nyerere alisema jeuri ya wazanzibar kujiita wazanzibari, inatokana na muungano. Pasipo muungano hakutakuwa na Zanzibar, badala yake kutakuwa na Unguja na Pemba. Hizi ni dalili tosha kwamba baada ya muungano kuvunjika, watabaguana tena. Kama nia yao ni kuikataa bara, kwanini wasiungane pamoja bila kujali uunguja na upemba kuikabili Tanganyika?
Vipeperushi hivi vimesambazwa kwa kasi jana katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar vikiwa na ujumbe unaowataka Wapemba waondoke Unguja na kurudi kwao Pemba wakajipange huko kuukataa Muungano. Sehemu ya waraka huo - angalia kiambatanisho....