Kwanini Pemba iko nyuma sana kimaendeleo kulinganisha na Unguja?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Najiuliza je sababu ya Pemba kuwa nyuma kimaendeleo ni kwamba ni mbali sana na kisiwa cha Unguja ambacho ndiyo makao makuu ya serikali ya visiwa hivyo viwili. Pemba ipo zaidi ya km 130 na ipo karibu na Tanga kuliko Unguja.

Je, kwa kuleta maendeleo Pemba ni sababu gani hasa inayozuia mpaka leo Pemba wasiwe na kiongozi wao na unguja iwe na kiongozi wake ili kuleta maendeleo badala ya sasa watu kuendelea ni mpaka waende Tanga, Unguja au Dar?

Mfano kwasasa wazanzibar wanataka mafuta yakipatikana yasaidie Zanzibar na yasiwe ya muungano swali Je mafuta yakipatikana Pemba karibu na Tanga halafu mapato ya mafuta yakaishia Unguja🤔!

Kwa hili kutakuwa na sababu gani ya msingi ya serikali ya Tanzania kwa ujumla wake kukubali hili? Tusije tukawa na nchi ambayo ina mabwanyeye ambao wao tu ndiyo wanataka maendeleo wakati ndugu zetu wa Pemba pamoja na rasilimali zao wanabaki na umasikini.

Isije ikawa watu wa unguja wanadai haki ambazo wenzao wa Pemba hawana. Sisi kama Watanzania tusikubali kuwaacha wenzetu wa Pemba wakiwa wanabaguliwa na Unguja halafu tukasema haituhusu sio sawa.

Kama kuna mtu ana mawazo tofauti anielimishe!
 
Mkuu,

Kwanza, unapaswa kufahamu kuwa mipaka karibia yote imerithiwa kutoka kwa Wakoloni. Visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa himaya ya Sultani.

Baada ya nchi zote kupata uhuru, zimeendelea kuheshimu mipaka hiyo.

Pili, umbali usikubabaishe. Kagera ipo karibu zaidi na Uganda na Rwanda kuliko kulivyo karibu na Dodoma yalipo makao makuu ya nchi yetu. Kigoma ni mdomoni kabisa mwa Burundi.

Je, sehemu tajwa zitambuliwe kama mikoa ya nchi jirani kwa sababu zipo karibu kijiographia? La hasha!.

Swala la ugawanaji wa rasilimali mafuta, itategemea utashi wa mamlaka husika.
 
Hizi choko choko za kitoto sana za kujaribu kujenga mazingira kuwa pemba imetengwa na wapemba wawe na chuki za aina hii ya kutengwa, wapemba hawana akili za kitoto za aina hii, wapemba ndio waliohakikisha kuwa mstari wa Mbele miaka yote 80 kudai uhuru wa zanzibar tangu enzi za utawala wa uingereza mpaka sasa, wala hawajawahipo kutamka kuwa wanataka kujitenga hata siku moja na wanajua kuwa maendeleo ya Pemba yapo nyuma.

Miaka yote hio wanapigania Zanzibar kama nchi na hawajawahipo kupigania Pemba peke yake,hii haijawahi kutokea kwenye historia ya zanzibar.

Maendeleo ya Pemba yapo nyuma kulinganisha na Unguja tangu utawala wa sultan, miaka yote ndio ipo hivo hivo na enzi hizo hakukuwa na siasa za uunguja na uPemba kama ilivyooandikizwa sasa.

Ni hivi unguja na pemba ni nchi moja ndio inayoleta Zanzibar, kama ilivyo Mtwara na Dar es Salam yote ni Tanganyika, na dar kuna maendeleo makubwa kuliko mtwara, au sehemu nyengine yeyote zinakotoka tanzanite, gesi,dhahabu na mazao yote yanayoitajirisha dar. Hii haimaanishi kuwa hizo sehemu nyengine zimenyimwa.
 
Wenyewe wanasema kwa sababu ya Upinzani na maanisha cuf na ccm pemba ni ngome ya cuf kwa sasa act
 
Hizi choko choko za kitoto sana za kujaribu kujenga mazingira kuwa pemba imetengwa na wapemba wawe .
Kuifananisha Jiji na vijiji. Ni sawa na kuifananisha Afrika na Ulaya. Ni sawa na kufananisha uchumi wa waarabu n wahindi nchini pamoja na watu weusi.

Fikiria upya, historia inaonyesha mijini kuwavutia zaidi vijana, wawekezaji na wadau mbalimbali.

Hata huku ulaya Kuna utofauti kati ya vijijini na mijini. Huwez kufananisha maendeleo ya NW na Lowa ukapata majib ya harakaharaka.

Historical matters
 
Pemba ipo zaidi ya km 130 na ipo karibu na Tanga kuliko Unguja. Je, kwa kuleta maendeleo Pemba ni sababu gani hasa inayozuia mpaka leo Pemba wasiwe na kiongozi wao na unguja iwe na kiongozi wake ili kuleta maendeleo badala ya sasa watu kuendelea ni mpaka waende Tanga, Unguja au Dar?
Ulianza vizuri, hapa ukaharibu. Pamoja na kwamba Pemba haiangaluwi ipasavyo na serikali, haihalalishi Pemba hiyo kuwa na kiongozi wake mbali na yule wa Zanzibar yote. Nisingependa tugawanywe.
Mfano kwasasa wazanzibar wanataka mafuta yakipatikana yasaidie Zanzibar na yasiwe ya muungano swali Je mafuta yakipatikana Pemba karibu na Tanga halafu mapato ya mafuta yakaishia Unguja🤔! Kwa hili kutakuwa na sababu gani ya msingi ya serikali ya Tanzania kwa ujumla wake kukubali hili?
Ni hakika kwamba mafuta yakipatikana Pemba lkn haihalalshi na wala sio kosa kwa suala la mafuta kubakia Zanzibar.

Haya ni matakwa ya makubaliano ya muungano ya 1964. Mafuta kuingizwa ktk mambo ya muungano ni uhuni tu na tamaa za wakubwa lkn ni batili kisheria.

Isije ikawa watu wa unguja wanadai haki ambazo wenzao wa Pemba hawana.
Hivyo ndivyo ilivyo. Wao, kwa jeuri, husema Wapemba hawakupindua.
 
Unajifariji,nje ya muungano hakuna uzanzibari bali kuna uunguja na upemba weusi na waarabu koko. Kinacho waunganisha sasa ni muungano tu.
Jambo usilolijua ni usiku wa kiza. Muungano una miaka 59 lkn Zanzibar ipo tangu kuumbwa hii dunia ikiwa na visiwa vya Unguja na Pemba. Huu muungano uwepo au usiwepo, Zanzibar itaendelea kuwepo.
 
Mkuu,

Kwanza, unapaswa kufahamu kuwa mipaka karibia yote imerithiwa kutoka kwa Wakoloni. Visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa himaya ya Sultani.
Baada ya nchi zote kupata uhuru, zimeendelea kuheshimu mipaka hiyo..

Pili, umbali usikubabaishe. Kagera ipo karibu zaidi na Uganda na Rwanda kuliko kulivyo karibu na Dodoma yalipo makao makuu ya nchi yetu. Kigoma ni mdomoni kabisa mwa Burundi.

Je, sehemu tajwa zitambuliwe kama mikoa ya nchi jirani kwa sababu zipo karibu kijiographia? La hasha!.

Swala la ugawanaji wa rasilimali mafuta, itategemea utashi wa mamlaka husika.
Jibu Mujarabu🙏🙏
 
matajiri wakubwa wanatoka Pemba kama wanashindana kuendeleza kwao na kukaa huku Tanganyika na kupingwa Muungano hiyo ni shauri yao
 
Mkuu,

Kwanza, unapaswa kufahamu kuwa mipaka karibia yote imerithiwa kutoka kwa Wakoloni. Visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa himaya ya Sultani.

Baada ya nchi zote kupata uhuru, zimeendelea kuheshimu mipaka hiyo.

Pili, umbali usikubabaishe. Kagera ipo karibu zaidi na Uganda na Rwanda kuliko kulivyo karibu na Dodoma yalipo makao makuu ya nchi yetu. Kigoma ni mdomoni kabisa mwa Burundi.

Je, sehemu tajwa zitambuliwe kama mikoa ya nchi jirani kwa sababu zipo karibu kijiographia? La hasha!.

Swala la ugawanaji wa rasilimali mafuta, itategemea utashi wa mamlaka husika.

Kagera sio kisiwa na hapo ndiyo nimetofautisha
 
Najiuliza je sababu ya Pemba kuwa nyuma kimaendeleo ni kwamba ni mbali sana na kisiwa cha Unguja ambacho ndiyo makao makuu ya serikali ya visiwa hivyo viwili. Pemba ipo zaidi ya km 130 na ipo karibu na Tanga kuliko Unguja.

Je, kwa kuleta maendeleo Pemba ni sababu gani hasa inayozuia mpaka leo Pemba wasiwe na kiongozi wao na unguja iwe na kiongozi wake ili kuleta maendeleo badala ya sasa watu kuendelea ni mpaka waende Tanga, Unguja au Dar?

Mfano kwasasa wazanzibar wanataka mafuta yakipatikana yasaidie Zanzibar na yasiwe ya muungano swali Je mafuta yakipatikana Pemba karibu na Tanga halafu mapato ya mafuta yakaishia Unguja🤔!

Kwa hili kutakuwa na sababu gani ya msingi ya serikali ya Tanzania kwa ujumla wake kukubali hili? Tusije tukawa na nchi ambayo ina mabwanyeye ambao wao tu ndiyo wanataka maendeleo wakati ndugu zetu wa Pemba pamoja na rasilimali zao wanabaki na umasikini.

Isije ikawa watu wa unguja wanadai haki ambazo wenzao wa Pemba hawana. Sisi kama Watanzania tusikubali kuwaacha wenzetu wa Pemba wakiwa wanabaguliwa na Unguja halafu tukasema haituhusu sio sawa.

Kama kuna mtu ana mawazo tofauti anielimishe!
Uchawi na ushirikina unawatesa sana
 
Jambo usilolijua ni usiku wa kiza. Muungano una miaka 59 lkn Zanzibar ipo tangu kuumbwa hii dunia ikiwa na visiwa vya Unguja na Pemba. Huu muungano uwepo au usiwepo, Zanzibar itaendelea kuwepo.

Sio kweli visiwa vilikuwa tofauti lakini sultan kwasababu alikuwa mtawala mmoja ndiyo maana ikaunganiswa lakini zamani visiwa hili vilikuwa sehemu za biashara na baadae kuwa sehemu za biashara za utumwa kutoka Bara na nchi za afrika ya kati kama Kongo.
 
Back
Top Bottom