Watu wanatumia changamoto ya stendi Manispaa ya Bukoba kupiga hela na Serikali ipo imetulia tu

The Great Haya

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,731
1,642
Baraza la madiwani lililopita kabla ya hili la sasa lilianzisha mchakato wa kujenga stendi katika manispaa ya Bukoba eneo la Kyakailabwa, na kabla ya kuimaliza muda wao ukaisha na hawakubahatika kurudi tena.

Hili baraza la madiwani la sasa limekuwa na mwitikio mdogo kuendeleza stendi hiyo huenda ni sababu za kisiasa kwa hiyo kuna hela za walipa kodi pale Kyakailabwa zimeota nyasi na badala yake wakaamua kuanzisha mradi wa kwao wa ujenzi wa stendi ya malori eneo la Ijuganyondo. Stendi ya malori mpaka sasa nayo ina kama mwaka imekamilika lakini haifanyi kazi kwa hiyo na hizo hela za walipa kodi ziko pale zinaanza kuota nyasi.

Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoa wa Kagera (Bukoba manispaa) aliwaambia wananabukoba kuwa rais ataleta pesa bilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi ya mabasi, na mwaka huu 2023 tukapata taarifa hela tayari ipo kwenye akaunti ya halmashauri. Pamoja na mivutano yote mwishowe baraza la madiwani ikaamua kwenda kuendeleza stendi ya Kyakailabwa.

Cha kushangaza wakati mkandarasi ameshaanza kazi Kyakailabwa mkuu wa mkoa akaagiza ujenzi usitishwe na hiyo hela itumike kukarabati stendi ya zamani akidai stendi mpya isubiri miradi ya TACTIC wakati magari yakitumia stendi ya malori (ambayo haina kazi mpaka sasa) ila mpaka sasa kimya.

Sasa cha kujiuliza kwa nini stendi ya Bukoba imekuwa na sarakasi nyingi na serikali imekaa kimya. Je sio kwamba watu wanaitumia kujipatia mtaji wa kisiasa na kujipigia ela watakavyo?

Tafadhali Rais aingilie kati huenda hata bilioni yake haipo tena na Bukoba mvua zimeshaanza tumechoka kuchafuka kwenye stendi ya matope.
 
Kwan stendi ya kyakairabwa haijaishaga tu?

Si walisema mwezi wa tisa?

Bora hata nilipohama bukoba japo ni kwetu...kuna ujinga mwingi na serikali iko kimya
Nadhani mkuu nimeeleza vizur hapo juu, wakati mkandarasi ameanza kazi kyakailabwa mkuu wa mkoa aliagiza ujenzi usitishwe na ela zitumike kukarabati stendi ya sasa akidai eti kyakailabwa isubiri miradi ya TACTIC, wakati mwingine hawa viongozi tunaoletewa huku Kagera nadhani hawatupendi.
 
Ok sawa...vip imeanza kukarabatiwa au ni maneno tu? Maana hata kama wangejenga kyakairabwa bado hapo mjini kati wangengeneza stendi tu at least ya madaladala...

Huko Dar manispaa ya kinondoni wametengeza stendi nzr sana ya mwenge na wametumia billion 9 tu...manispaa nyingi huwa zinafeli wap? Wanashindwa nini hata kukopa...
Hiv ni watu gan hawapendi mabadiriko?

View: https://youtu.be/y7Ky6-IxJeQ?si=KVGG4q1kzPtYlj02

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Bado mkuu japo inasemekana magari yatahama wiki hii au wiki kesho. Kuna vitu vinachekesha bukoba kuna kipindi mkurugenzi alitoa amri malori yote yapaki kwenye stendi mpya ya malori lakini cha kushangaza hakuna lori hata moja lilienda pale mpaka sasa stendi inataka kuota nyasi ndo wakaamua mabasi yawe huko kwa muda.
 
Kwan hiyo stendi ya maroli imejengwa kwa kuwekewa zege? Au ni mavumbi wanayojenga huku mikoani kuyaita stendi ya maroli?
 
Hivi ni mimi tu huwa naona central government huwa inatumia nguvu nyingi kuhakikisha mkoa huo unadidimia. Lolote linaloanza kuonyesha litaleta tija linaingizwa siasa kufanya uharibifu.
Tuanze na serikali ya Nyerere kuharibu KCU, sema hiyo serikali iliharibu baadhi ya vitu mikoa mingine pia.
Tuje baada ya vita hakuna reparations zilitolewa wakati uharibifu uliofanywa uko.
Tuje kwenye miradi ya kilimo na ufugaji sijawahi sikia serikali imetoa ruzuku au pembejeo. Yani Tanzania kuna mikoa inajiendea tu hiyo Kigoma, Lindi, Kagera alafu kuna mikoa inabebwa kupitiliza kama Dodoma na Pwani.
 
Ni wahaya wenyeww wanjididimiza ..jnakuwaje mkuu wa Mkoa laikuwa muhaya..katibu tawala prof kamzora muaya bado wakashibdwa
 
Bado mkuu japo inasemekana magari yatahama wiki hii au wiki kesho. Kuna vitu vinachekesha bukoba kuna kipindi mkurugenzi alitoa amri malori yote yapaki kwenye stendi mpya ya malori lakini cha kushangaza hakuna lori hata moja lilienda pale mpaka sasa stendi inataka kuota nyasi ndo wakaamua mabasi yawe huko kwa muda.
Kwan hiyo stendi ya maroli imejengwa kwa kuwekewa zege? Au ni mavumbi wanayojenga huku mikoani kuyaita stendi ya maroli?
Hayo hayo ya mavumbi wanaweka uzio tu basi hapo ela inatembea rejea heading ya uzi wangu
Hakuna walichofanya kama ni hivyo...kwa nini viongozi wanapenda mavumbi mavumbi...mtu utatumiaje zaidi ya billion 1 kujenga kitu hakina pavements? Mbona majumbani mwetu tunajemga pavements kwa gharama ndogo tu...
Aisee hela za serikali zinapigwa sana
 
Ni wahaya wenyeww wanjididimiza ..jnakuwaje mkuu wa Mkoa laikuwa muhaya..katibu tawala prof kamzora muaya bado wakashibdwa
Wahaya na mambo ya makabila hayahusiki katika maendeleo ya mji

Huu ni uzembe wa serikali na viongozi wake maana wao wana mamlaka na uwezo wa kuwawajibisha watendaji wake. wahaya wala makabila hayana jeshi, mahakama wala polisi.
Acheni kutoa excuse za ethnicity katika masuala ya maendeleo ya mahali...
 
Kwan hiyo stendi ya maroli imejengwa kwa kuwekewa zege? Au ni mavumbi wanayojenga huku mikoani kuyaita stendi ya maroli?

Hakuna walichofanya kama ni hivyo...kwa nini viongozi wanapenda mavumbi mavumbi...mtu utatumiaje zaidi ya billion 1 kujenga kitu hakina pavements? Mbona majumbani mwetu tunajemga pavements kwa gharama ndogo tu...
Aisee hela za serikali zinapigwa sana
Ni kweli mkuu kwa mvua ya Kagera alafu lori lililobeba matani ya mizigo liende kupaki kwenye matope litatoka kweli.
 
Baraza la madiwani lililopita kabla ya hili la sasa lilianzisha mchakato wa kujenga stendi katika manispaa ya Bukoba eneo la Kyakailabwa, na kabla ya kuimaliza muda wao ukaisha na hawakubahatika kurudi tena.

Hili baraza la madiwani la sasa limekuwa na mwitikio mdogo kuendeleza stendi hiyo huenda ni sababu za kisiasa kwa hiyo kuna hela za walipa kodi pale Kyakailabwa zimeota nyasi na badala yake wakaamua kuanzisha mradi wa kwao wa ujenzi wa stendi ya malori eneo la Ijuganyondo. Stendi ya malori mpaka sasa nayo ina kama mwaka imekamilika lakini haifanyi kazi kwa hiyo na hizo hela za walipa kodi ziko pale zinaanza kuota nyasi.

Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoa wa Kagera (Bukoba manispaa) aliwaambia wananabukoba kuwa rais ataleta pesa bilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi ya mabasi, na mwaka huu 2023 tukapata taarifa hela tayari ipo kwenye akaunti ya halmashauri. Pamoja na mivutano yote mwishowe baraza la madiwani ikaamua kwenda kuendeleza stendi ya Kyakailabwa.

Cha kushangaza wakati mkandarasi ameshaanza kazi Kyakailabwa mkuu wa mkoa akaagiza ujenzi usitishwe na hiyo hela itumike kukarabati stendi ya zamani akidai stendi mpya isubiri miradi ya TACTIC wakati magari yakitumia stendi ya malori (ambayo haina kazi mpaka sasa) ila mpaka sasa kimya.

Sasa cha kujiuliza kwa nini stendi ya Bukoba imekuwa na sarakasi nyingi na serikali imekaa kimya. Je sio kwamba watu wanaitumia kujipatia mtaji wa kisiasa na kujipigia ela watakavyo?

Tafadhali Rais aingilie kati huenda hata bilioni yake haipo tena na Bukoba mvua zimeshaanza tumechoka kuchafuka kwenye stendi ya matope.

Mama Mwassu Mkuu wa Mkoa Kagera aligundua kuna wizi akaanza uchunguzi. Baada ya hapo akagundua million mia 9 washaanza kuzichapa. Msikilize hotuba yake hakumungunya maneno. Hapo kazi ipo takukuru

View: https://youtu.be/3Vd7WYBjgoc?si=uchTbSqf3FLtFWJB
 
Haya ndo niliyoandika kwenye uzi huu, yaani yule mbunge byabato anapiga kelele tu huku wahuni wanapiga ela na hawaachi lazima watafute njia nyingine kuhakikisha ela inapigwa. Yaani serikali inabidi kuweka jicho la ziada bukoba pesa zinaliwa sana hili la stendi ni mfano mdogo kuna miradi mingi mambo ni hayo hayo.
 
Back
Top Bottom