ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,128
- 49,863
Hongera sana Serikali Kupitia Manispaa ya Kinondoni Kwa kujenga Standi Mpya na nzuri kama Airport Terminal.
--
Stendi mpya ya Mwenge imekamilika kwa 100% na itaanza kufanya kazi rasmi baada ya taratibu nyingine zikiwemo za upangishaji wa fremu kukamilika.
Mwandishi wa @AyoTV, , Bakari Chijumba amefika kwenye stendi hiyo ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 2020 ambapo amepita kwenye maeneo mbalimbali ya stendi hiyo na kukuta hatua zote za ujenzi zikiwa zimekamilika.
Ujenzi umegharimu Tsh. bilioni 10.067 na fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Kinondoni na Mkandarasi aliyejenga ni Heinan International LTD kutoka China.
Kwa mujibu wa taarifa ya Viongozi wa Halmashauri ya Kinondoni, fremu zote za biashara katika stendi hii zimepangishwa kupitia mnada ambao ulifanyika kwa mfumo wa TAUSI TAMISEMI kuanzia October 18-26, 2023 kwa njia ya mtandao.
Stendi ina uwezo wa kuchukua mabasi 100, bajaji 20 na pikipiki 40 kwa mara moja na ina vibanda vya kupumzikia abiria 27.
Kazi iendelee