Watoto wa kariakoo mpo jf?

Huyo Mkama sharp alifika Upanga? Miaka gani hiyo?
Da Pretty Huyu Marehemu Mkama Sharp hakufika Upanga ila kwa wale waliokuwa wanaenda Viwanjani haswa Taifa na Karume ndio waliofanikiwa kumfahamu kwani alikuwa ni kama Kituko tu Bastola Kiunoni Mfupi anavaa miwani ya macho yenye lens nzito akizuia watu wasiluke Ukuta kuingia viwanjani so aliuwa ni kama chale chale tu sijui walikuwa wanamuogopea nini Sijui ...
 
Duduwasha ulienda kufanya nini pale CHUMBA CHA KINANDA?
Wakati tupo std 5 nilisomea lile darasa,mwaka uliofatia ndio kikawa chumba cha kinanda.
Mama Mahundi mi nilimkuta UPS tangu std 1 hadi natoka,badae akahamia Muhimbili ndiko alikomalizia kazi hadi alipofariki.
R.IP Mwalimu Mahundi Wjua watoto wa Upanga tukikaa mitaani tuanhadithiana kila kitu cha shule na kusifiana sie tuna uwanja mzuri au nyie haman hichi au kile basi ndio hivyo tena au Tuition pia...

wewe utakuwa ulisoma kipindi cha kina Pau Kubwa au A. Ngdk Msichana alikuwa Mbabe yule du..
 
Hizi naona ni personal attacks zaidi ambazo zitaharibu hii mada, naona unawamaidi kinoma watoto wa k'koo, japokuwa baadhi walikuwa hivyo lakini si wote, mbona hukutaja watoto wa temeke?
Temeke kulikuwa na Mwarabu anaitwa Hassan Ilibidi apewe jinala Chizi Muhimbili so Hassan Chizi na Kulikuwa na Mbabe Sana Bonge la Jeba kubwa sana Liliitwa Bukaba. na Kulikuwa na kamsopi, Olympio kulikuwa na Mwarabu aliitwa Hashim Mafishi alizidisha uhuni hadi akatumia Drug akaishia kuwa Teja.Majanga yalikuwa kote lakini waliokuwa wanawafundisha ni wa kariakoo. Tatizo la wakariakoo walikuwa wanakuja upanga na kwa kazi ya Kuiba tu utadhania zile movi za ma cowboy so mmoja akishawaona tu watu tunaandaa matawi ya mipapai akibakia mmoja basi fimbo za mipapai zinamuishia mwilini. Pale Don Bosco Father akianzisha mashindano timu za kariakoo tukiwafunga wanaanzisha fujo kha! kuna siku hadi refa mmoja ambaye ni wa kariakoo kwa sasa ni Shehe pia walimchapa.ati ameshindwa kuwabeba.

Hii ni kweli kabisa na inathibitisha kuona K'koo ilikuwa na timu za Simba, Yanga na Nyota Nyekundu (Timu kubwa za ligi kuu ya mpira bara). Enzi hizo kama wewe ni Simba ni marufuku kuvaa njano, watu hata walikuwa hawajui ligi za Ulaya zikoje. Ijumaa (shuleni) kabla ya mechi za jumamosi watoto wa k'koo husimama ubaoni kushindana kuandika list ya wachezaji watakaocheza kesho yake, taifa.
Mpira nilimaanisha timu zetu tukicheza nao... Wao walikuwa wanazichezea timu zao za mitaani kama Dar fire, Manyema n.k na Pale Uwanja wa Vijana walicheza sana waarabu na Zanaki Wahindi Kila Jioni Wahindi walikuwa wanacheza vizuri sana Mpira. Pia Mnazi Mmoja kulikuwa na timu ya ajabu na mkali wao alikuwa anaitwa Dalla...
Kijuso hadi leo anacheza dah!
 
R.IP Mwalimu Mahundi Wjua watoto wa Upanga tukikaa mitaani tuanhadithiana kila kitu cha shule na kusifiana sie tuna uwanja mzuri au nyie haman hichi au kile basi ndio hivyo tena au Tuition pia...

wewe utakuwa ulisoma kipindi cha kina Pau Kubwa au A. Ngdk Msichana alikuwa Mbabe yule du..
A.Ngdk kaolewa juzijuzi.
Mkama sharp amewahi porwa bastola barabara ya livingstone kwa muuza bangi maarufu Kitonsa,kirakoo kulikuwa na palestina,jambazi limeua sana mitaa ya upanga
 
Mpira nilimaanisha timu zetu tukicheza nao... Wao walikuwa wanazichezea timu zao za mitaani kama Dar fire, Manyema n.k na Pale Uwanja wa Vijana walicheza sana waarabu na Zanaki Wahindi Kila Jioni Wahindi walikuwa wanacheza vizuri sana Mpira. Pia Mnazi Mmoja kulikuwa na timu ya ajabu na mkali wao alikuwa anaitwa Dalla...
Kijuso hadi leo anacheza dah!

Pamoja mkuu, hata mimi nilimaanisha kihistoria upenzi wao wa kucheza soka la mchangani ndiko kulikozaa timu za Simba na Yanga. Hata ukisoma maeleza ya Mohamed Said utaona anavyosimulia jinsi walivyocheza mpira pale kidongo chekundu wakiwa wadogo.
 
mnazimoja shuleni kulikuwa na jamaa linaitwa mungu na wanadamu,lilikuwa lina mohican hair cut,lilikuwa linaishi kwenye shimo underground katika maeneo hayo
 
Kumbe watoto wa kariakoo jf hamtoshi,tatizo nini?access ya mtandao au?tukiweka watoto wa arusha hapa watafunika mbaya kama kwenye ule uzi wa makalio bar kwa mnaokumbuka si mliona wenyewe watoto wa ki R CHUGA walivyofunguka,kariakoo doro!kwaherini

watoto wa K'Koo wengi tulianzia mig33 na baadae facebook.
JF na mitandao mingine kwa uchache sana,
nitawapa stori ya msele wa kuitwa Manjilinji na mkasa wake jela la Ukonga.
 
R.IP Mwalimu Mahundi Wjua watoto wa Upanga tukikaa mitaani tuanhadithiana kila kitu cha shule na kusifiana sie tuna uwanja mzuri au nyie haman hichi au kile basi ndio hivyo tena au Tuition pia...

wewe utakuwa ulisoma kipindi cha kina Pau Kubwa au A. Ngdk Msichana alikuwa Mbabe yule du..

A. Ngdk sijasoma nae,
alikua anakaa mitaa gani?
Kamsopi kama wa Mangengesa Mdimi namfahamu hadi kesho,si walikua wanakaa sea view kwenye lile jengo lilikua refu kuliko yote miaka ile? Mule ndio tumejifunzia kupanda lift..
Pia watoto wa Upanga tulikua tunakutana sana Don Bosco na wengine mafundisho St. IMACULATE kwa Fr. Amadori.
Mi nilikaa mitaa hiyohiyo uliyoitaja ila umesahau Lugalo st. Kwa kina Ephraim Kibonde,Manase Zablon,Mtinangi.
Malik Rd kwa kina Telesphory Ndunguru,Undali kina Togani Ngota, Maria Goyayi, Ray Kasonga...
Alykhan kwa kina Koku yule alipata ajali akiwa na Kenedy Seusi akapoteza macho yote.. Unaikumbuka hiyo?
 
Nimejifunza kitu toka thread hii ya kudumu ianze,kitu chenyewe ni kwamba kutokana na mtiriri wa majina mbalimbali ya wakazi wa huko upanga inaonesha wazi upanga sio sehemu ya wazawa bali wahamiaji au wakuja kama wenyeji wenyewe wa kkoo wanapenda kuwatambulisha na wangependa mtambulike hivyo,hata kama umezaliwa ocean road lakini bado kiasili ni wakuja kwa kuwa ni mtoto ama mjukuu wa wahamiaji sio haramu bali wahamiaji tu
 
Kulikuwa na Mwizi Maarufu alikuwa anaitwa Ali Gulu.. Cha kushangaza alikuwa ana mguu mbovu anachechemea lakini ni mwizi tena yule wa kukaba na anaondoka pole pole hakimbiii alikuwa anakuja hadi mitaa a kwetu kuba na wenzake mitaa tote ya Upanga kawaliza sana wahindi na waswahili...

ukisiikia mtu anataka kwenda kariakoo unamshangaa na kumuuliza wewe humuogopi Ali Gulu

Huyu atakuwa kundi la kina Chite Spy nini?
 
mnazimoja shuleni kulikuwa na jamaa linaitwa mungu na wanadamu,lilikuwa lina mohican hair cut,lilikuwa linaishi kwenye shimo underground katika maeneo hayo
Dah Huyo Jamaa kama nilisikia Story ila ilikuwa ni kama mtu anatania tu kwani Upande wa pili opp na Shule ya Mnazi Mmoja kulikuwa na Mahandaki ya Miaka Mingi sikuelewa yalijengwa for iddi amin au world war 1 au 2, tatizo pale walikuwa wanaishi vibaka tena umenikumbusha nchi hii ndio imeshasahau kuwa na mahandaki endapo vita itatokea dah! na kile kiwanja sijui kama kishauzwa au lah! nitajaribu kupita nione ni jengo gani na la nani limejengwa pale....

Mnazi Mmoja Kulikuwa na Mlinzi Mmoja Bonge la Mtu jina limenitoka alishawahi muua Mwizi aliyekuwa anakimbizwa na wezi akaingia kwenye timing zake akamfyatulia Gobore so akafungwa kama Mwaka hivi. then akarejeshewa kazi yake bila silaha...

Pale karibu na kituo cha polisi kuna jamaa alikuwa anauza Mihogo na juice ya ukwaju poa sana sijui kama bado wapo! alijenga banda fresh karibu na mti wa ajabu ajabu mti una mizizi iliyotokeza ardhini na kuutambalia mti wenyewe hadi juu ulikuwa unatisha na ulikuwa una kivuri kizuri ajabu walikuwa wanadai kuna majini jamaa kila akipiga floor plasta baada ya siku mbili au tatu morning anakuta ishabomolewa na usiku hasikii sauti ya mtu kuvunja na kuna siku walikesha huku wakipiga ganja lakini wapi!

Pia kulikuwa na Mzee kinyozi ... Zamani Nywele zinanyolewa na wazee tu ambao ndio walikuwa vinyozi vijana hawakuipenda hiyo kazi.
 
A. Ngdk sijasoma nae,
alikua anakaa mitaa gani?
Kamsopi kama wa Mangengesa Mdimi namfahamu hadi kesho,si walikua wanakaa sea view kwenye lile jengo lilikua refu kuliko yote miaka ile? Mule ndio tumejifunzia kupanda lift..
Pia watoto wa Upanga tulikua tunakutana sana Don Bosco na wengine mafundisho St. IMACULATE kwa Fr. Amadori.
Mi nilikaa mitaa hiyohiyo uliyoitaja ila umesahau Lugalo st. Kwa kina Ephraim Kibonde,Manase Zablon,Mtinangi.
Malik Rd kwa kina Telesphory Ndunguru,Undali kina Togani Ngota, Maria Goyayi, Ray Kasonga...
Alykhan kwa kina Koku yule alipata ajali akiwa na Kenedy Seusi akapoteza macho yote.. Unaikumbuka hiyo?
Name Calling noma nimekumbuka manake unaweza tokea ukataja na langu pia lol... Nawajua hao na wengine siwajui Kbnde kwa Don alikuwa hakosekani lol Wanaona huwajui jui... lol huyo kwenye red ndiye.. Ila Mh!~ Manake Jamaa alikuwa Ni Mkali wa Kufuatilia Totoz Sana.. Nadhani ile kazi yake keshaacha ya ukonda wa Basi lao nadhani kama nilimuona siku kwenye gari Nissan Patrol...

hapo kwenye bluu dah sikumfahamu ila ni sad news japo zamani...Manase Sikuwahi jua alipokuwa anakaa lol zaidi ya kuwa namuona kuja mtaani kwetu na huko DON Pamoja na Uwanja wa Zanaki kwenye Basketball walikuwa wakubwa hao lol hadi Marehemu Justine Kalikawe R.I.P. naye alikuwa anaishi Lugalo St. Mitaa ile Siwezi Isahau Olympio,Urambo,Mtitu,Ruvu, isimani ulikuwa uanpitika jeshi wakaufunga kwa muda then ikawa ndio nitolee hadi leo hawajaufungua ule mtaa lol kulikuwa na Duka la Ushirika Mule na lingine lilikuwa ndani ya Eneo la Scout.. Sisahau kula Ugali wa Njano.. Da Pretty nikikuona Sura yako haitokuwa Ngeni lol
 
Huyu atakuwa kundi la kina Chite Spy nini?
Dah hayo makundi duh pindi hicho sikuweza fahamu.. ila baadae Yalikuja makundi Mengi na yalikuwa yanapigana na Kuchanjana mapanga kwenye Minanda wanapokutana Kuna kundi Moja lilikuwa linaongozwa na Jms mtoto wa Mama kwao Mambo fresh ila anajua sana Fujo alikuwa anakaa kwenye lile gholofa la Wakimbizi Lumumba.. kuna time wakaibuka wahuni wakijiita mapanga Shaa! aibu wanatembe kundi kubwa la zaidi ya watu 20 hadi 30 kwa mwendo wa kasi wakikukuta ujue hali yako ni mbaya...
 
Nyie watoto wa Upanga kuna mtu anakumbuka haya maneno...
Huo Wimbo vipi mbona haujakaa kiupanga upanga? Michezo ya Watoto karibu mingi inafanana ,, Ukuti ukuti wa meme wa meme, Komborela, Tampo, Baba na Mama,Yai Bovu,Maji ya Ndimu,Ana ana ana Do, Gololi Sachi, Kidali Po, Tikbar Tik, Soccer, Karata n.k..

Nina Ndoo yangu eeeh! yakuteka Maji eeh!
Maji ya Barafu eeh! Watoto msitizame Nyuma..
Yai bovu linanuka..

Maji ya Ndimu Maji Ndimu!.. Saga! saga! saga! huku kichwa kikiwa Chini
Funika Funua.... Hapo Unapigwa Konzi kabla ujanyanyua Kichwa Juu
 
Hata mi wimbo wake sijaujua.
Umesahau Upanga tumecheza sago pia(ule mchezo wa kurusha betri)
Ila we ulikua mtundu sana,unayajua hadi ya lumumba,mnazi mmoja,mkama sharp!
Pale jeshini mtaa wa Magore kulikua na mibuyu,basi tukitoka kanisani au mafundisho tulikua tunapita kuwaomba mabuyu yale ambayo hayajapasuliwa,wanajeshi wa miaka ile walikua wapole maana yakianguka tunawekewa,yasipoanguka wanatuambia..lol.
Sahivi mjeshi gani aokote ubuyu eti awawekee watoto watapita.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom