Watoto wa kariakoo mpo jf?

Kariakoo ilikua zamani,siku hizi wamevamia wageni na kuondoa radha yote ya kariakoo,sasa hivi wamejaa wachagga na wakinga na wapemba!bora wapemba walikuja siku nyingi kidogo

kwani kati ya wachaga na wakinga na wapemba wapi hasa ni watanganyika ni wepi hasa ni wageni zaidi lol Ukiamua kuwa mbaguzi kuwa mbaguzi hasa sio unachovya nusu nusu.

Na kukumbusha umesahau na wachina......... Na wahindi ofcousre lakini hao ni .............. wenyeji lol. Au wachaga ni wageni zaidi ya wachina na wapemba......
 
yeah Kim..
ilikuwa raha na huru.. Hawa wengine wanaongelea Kariakoo ya juzi naona.. Hawaijui ya zamani... Ambapo,mtaa wa Msimbazi ulikuwa na full functional street lights.. Senene wanajaaa magari si mengi,unaruhusu wanao wakakamate senene barabarani.. Kariakoo hiyo nani mwingine anaijua..

mradi usisifie Kkoo ya kipindi cha "wakuja" Nyerere kuna watu wa gerezani hawatakuelewa
 
umemshika pabaya,basi inatosha mzee!
kanishika pabaya wapi mpendwa...kama mtaa nimemwambia unataka nimpe namba ya nyumba ili iweje sihitaji ndugu wa hiari na uze huu,kwani kuzaliwa kkoo kunaongeza nini katika maisha yetu ya kila siku kama si juhudi binafsi za mtu
 
Watu wa upanga nao bwana kweli wahindi,yani mlikua mnamuogopa mlemavu eti anawabia then hakimbii anatembea tu,kweli nyie ni watu wa upanga.
Muhahaha Huyo ali Gulu alikuwa ni Noma hata wa kariakoo walikuwa wanamhofia nasikia kuna Saa flan zilitoka miaka yake zilikuwa zinaitwa Disco zilikuwa za betri jina la zamani kimweku mweku ukivaa hizo ukihisi kupishana nae unaivua na kuiweka ndani ya chupi kwani jamaa alikuwa ana sachi mifukoni na anachukua vyote.. Polisi wenyewe walikuwa wanamhofia kwani na wao wakizubaa anawapora jamaa alikuwa na ubavu wacha...

Upanga sie Hatukuitwa Wahindi Weusi tulikuwa ni Wengi Sana wahindi wa Kutafuta na hao wahindi walikuwa wanatuogopa Balaa
 
Shule zetu Upanga Zanaki na Muhimbili Watoto wa Kariakoo walikuwa Na Matusi Wezi Walituibia Sana Mabegi Mikebe na Pesa na Wanaongea kama Chiruku Na Walikuwa wanapenda Nyimbo za Mchiriku na Mnanda Sana Eti na Watot waliokuwa wanasoma Olympio walikuwa wanatuogopa na sisi Majirani zao kwani walikuwa wanajifanya na wao Wahindi
 
huyo hakukutana na sharp mkama huyo
 
kanishika pabaya wapi mpendwa...kama mtaa nimemwambia unataka nimpe namba ya nyumba ili iweje sihitaji ndugu wa hiari na uze huu,kwani kuzaliwa kkoo kunaongeza nini katika maisha yetu ya kila siku kama si juhudi binafsi za mtu

onyesha utoto wako wa mjini wewe
 
Enzi hizo mtaa wa Pemba ndo kulikuwa kunapatikana raba mtoni,mashati ya yekeyeke,bati (jeans).Sabuni na Colget toka nje.
Mwee bila kusahau watu walikuwa wanafungiwa matambara badili ya nguo (kupigwa kagari)
 
kwani kati ya wachaga na wakinga na wapemba wapi hasa ni watanganyika ni wepi hasa ni wageni zaidi lol Ukiamua kuwa mbaguzi kuwa mbaguzi hasa sio unachovya nusu nusu.

Na kukumbusha umesahau na wachina......... Na wahindi ofcousre lakini hao ni .............. wenyeji lol. Au wachaga ni wageni zaidi ya wachina na wapemba......

tatizo si wageni kuliko wapemba bali walikuja baadae sana...ila kuna mzee mmoja wa kichagga alikua na bar pale nyamwezi toka enzi,huyo ndio mchagga wa kwanza na tulikua tunamshangaa baadae tukamkubali kama mwenzetu..
 
Enzi hizo mtaa wa Pemba ndo kulikuwa kunapatikana raba mtoni,mashati ya yekeyeke,bati (jeans).Sabuni na Colget toka nje.
Mwee bila kusahau watu walikuwa wanafungiwa matambara badili ya nguo (kupigwa kagari)

mwanangu hiyo ilikua inaitwa kanyaboya,wameuziwa sana wakuja,anaonyeshwa raba mtoni kali(walikua wanakuja nazo mabaharia watu wanzikodi kwa ajili ya kupigia mafala)baadae anafungiwa akipanda uda ile afungue aangalie anakuta mawe au matambara!
 
Mchagga mungine maarufu ambae alikuja baadae baadae kidogo kariakoo ni Augustine Mrema ambae alinunua nyumba ya washakaji zangu pale sikukuuu jirani na BIG MAYAI pembeni ya SAIGON CLUB ilipokua zamani,sio hii saigon ya sasa!
 
Shule zetu Upanga Zanaki na Muhimbili Watoto wa Kariakoo walikuwa Na Matusi Wezi Walituibia Sana Mabegi Mikebe na Pesa na Wanaongea kama Chiruku Na Walikuwa wanapenda Nyimbo za Mchiriku na Mnanda Sana Eti na Watot waliokuwa wanasoma Olympio walikuwa wanatuogopa na sisi Majirani zao kwani walikuwa wanajifanya na wao Wahindi

Wa Zanaki Primary nao walikua kikariakookariakoo....
 
Mtaa wa pemba ulikuwa maarufu kwa mirungi (soda za kresti), pia kulikuwa na refa mmoja maarufu aliyechezechaga mpira kidongo Chekundu na Mnazi mmoja aliyeiitwa Mandemla. Pale karibu na hospitali ya Mnazi Mmoja kulikuwa na harufu nzuri ya mikate ya Bakresa wakati wa jioni.
 
yap! wewe kweli mzawa...........
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom