Watoto wa kariakoo mpo jf?

Wa Zanaki Primary nao walikua kikariakookariakoo....
haha Da Pretty wa zanaki unaweza kuwa sawa au si sawa wazee wengi wa kariakoo walipenda kuwasomesha watoto wao Shule ya Zanaki lakini kwa utundu wao hawakuweza kuendana na mazingira so wazazi wao waliwapeleka katika shule za mnazi mmoja lumumba na baadhi jamhuri..

Mie Sababu nimeishi Upanga na City Centre so nawafahamu kwa Sana... Tabia Za Watoto wa Karikakoo ni Wanakimbia Sana hata Sijui kwanini hakuna Wanariadha kutoka Kariakoo! Wanaongea Sana Tabia ya Udokozi ikiwemo kupapasa papasa macho hapa na pale kama kuku atafutaye chakula. Ukigombana nao cha kwanza wanakupiga mtama na walikuwa hawakosi wembe mfukoni. so unaweza kuchaniwa begi na ukifika home hakuna mkebe.

Pia Tabia zao hazikupishana na za watoto wa Magomeni na Ilala.. Watoto wa Kariakoo nilikuwa nawapenda kwene soccer tu japo walikuwa wanacheza sana rafu na mpira wanaujua
 
kaka hutupendi...unatuchukia sana mpaka unashindwa kuficha..
 
Pole The Romantic naona umekwazika...
Ila kwa kweli watoto wa Kariakoo mlikua wakorofi sana shuleni halafu mnapenda vikundi wakati kule kwetu hatukua na mambo ya vikundi. Sa nane ikifika mkitoka geti la shule kila mtu kivyake, kama atakuja, baba, mama, dereva au utaenda kwenu kwa mguu haya... Mimi nilisoma UPS kwa Marehemu mama Mahundi
 
haha Sio chuki Mkuu ni hali halisi nahadithia Jinsi ilivyokuwa kipindi hicho Sababu Muhimbili Mwalimu Ndosi alikuwa anawaita Manunda Na Zanaki pia Kulikuwa na Mwalimu Ndosi Mwingine naye alikuwa anawachapa Sana.. Mimi Siwezi Sahau Begi langu niliibiwa tulipokusanya Sehemu tukkkkkkkawa tunacheza Soccer japo nilipata madaftari yangu tu yametupwa... Wajua walivyokuwa Wanafanya!
 
Huyo Mama Hivi hakuwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Zanaki Pr? manake nakumbuka kama alishawahi hama zanaki akahamia ups kama sikosei na pia walimu wakuu walikuwa ni kina mama zanaki na upanga...

UPS nakumbuka zamani kulikuwa na fensi mbavu na kuna kinjia unapita mahakamani then unaenda tokezea Maktaba lol

Kuna Darasa Moja lilikuwa na Kinanda Kikubwa(Organ) ulishawahi kiona hicho Da Pretty!
 
Wa Kariakoo kumbusheni enzi zenu maana sie wengine sijui hata kama huku kwetu kulikua na vijimambo... Labda mix za jamatini
 
wewe utakuwa ulikuwa unaishi mitaa ya Maweni Longido kitonga alykhan au Mitaa ile yote midogo midogo karibu na Jamat ndio walikuwa hawakosi Jamatini mida ya jioni hadi saa mbili kula mix na vijimishikaki
 
haha Da Pretty wa zanaki unaweza kuwa sawa au si sawa wazee wengi wa kariakoo walipenda kuwasomesha watoto wao Shule ya Zanaki lakini kwa utundu wao hawakuweza kuendana na mazingira so wazazi wao waliwapeleka katika shule za mnazi mmoja lumumba na baadhi jamhuri..

Sababu ilitokana na ukubwa wa kariakoo kulinganisha na idadi ya shule kukidhi mahitaji, mfano kariakoo ilikuwa na shule nne, Mnazi Mmoja, kisarawe, Uhuru na Lumumba. Shule hizi hazikukidhi idadi ya wanafunzi kwahiyo ilibidi wengine waje city cente kusoma katika shule za Kisutu, Jamuhuri, Forodhani, Mtendeni na hata Bunge. Wengine ndo walikuja huko kwenu Upanga. Utaona kuwa City Center kutokana na idadi ndogo ya Waswahili (Kwasababu wahindi wengi walisoma shule zao) shule zao zilikidhi mahitaji ndiyo maana nafasi zilizobaki zilijaziwa na watoto wa K'koo na hata wale wa O'bey (bunge/forodhani).

Mie Sababu nimeishi Upanga na City Centre so nawafahamu kwa Sana... Tabia Za Watoto wa Karikakoo ni Wanakimbia Sana hata Sijui kwanini hakuna Wanariadha kutoka Kariakoo! Wanaongea Sana Tabia ya Udokozi ikiwemo kupapasa papasa macho hapa na pale kama kuku atafutaye chakula. Ukigombana nao cha kwanza wanakupiga mtama na walikuwa hawakosi wembe mfukoni. so unaweza kuchaniwa begi na ukifika home hakuna mkebe.

Hizi naona ni personal attacks zaidi ambazo zitaharibu hii mada, naona unawamaidi kinoma watoto wa k'koo, japokuwa baadhi walikuwa hivyo lakini si wote, mbona hukutaja watoto wa temeke?

Watoto wa Kariakoo nilikuwa nawapenda kwene soccer tu japo walikuwa wanacheza sana rafu na mpira wanaujua

Hii ni kweli kabisa na inathibitisha kuona K'koo ilikuwa na timu za Simba, Yanga na Nyota Nyekundu (Timu kubwa za ligi kuu ya mpira bara). Enzi hizo kama wewe ni Simba ni marufuku kuvaa njano, watu hata walikuwa hawajui ligi za Ulaya zikoje. Ijumaa (shuleni) kabla ya mechi za jumamosi watoto wa k'koo husimama ubaoni kushindana kuandika list ya wachezaji watakaocheza kesho yake, taifa.
 
Mkama Sharp alikuwa bado hajaanza makeke ipindi cha ali gulu... Mkama baadae akiwa na akina Koba..
mkama na koba wapi na wapi mzee,kipindi mkama sharp anatingisha kariakoo koba alikua anapigana ngumi na iraq hudu na stanley mabesi relwe gerezani enzi hizo,akiwa kijana mdogo!
 
haha Sio chuki Mkuu ni hali halisi nahadithia Jinsi ilivyokuwa kipindi hicho Sababu Muhimbili Mwalimu Ndosi alikuwa anawaita Manunda Na Zanaki pia Kulikuwa na Mwalimu Ndosi Mwingine naye alikuwa anawachapa Sana.. Mimi Siwezi Sahau Begi langu niliibiwa tulipokusanya Sehemu tukkkkkkkawa tunacheza Soccer japo nilipata madaftari yangu tu yametupwa... Wajua walivyokuwa Wanafanya!

Tatizo lenu na nyie mlikua mnajifanya wahindi weusi ndio mana,na si unajua hata kariakoo tulikua na wahindi lakini mhindi wa kariakoo na upanga tofauti,mhindi wa kariakoo sio mhindi wa dengu na cheuro!anapiga chips dume na samaki wa kukaanga kwa kwenda mbele!
 
Kariakoo kulikuwa nna Nyumba za Udongo Nyingi Kuna ambayo ilikuwa inanikera pale Mtaa wa Magira kwa Mafundi pikipiki ambayo ilivujwa kama sikosei 2010 sasa kuna gholofa kubwa... Kwa wakina Faiza bado kuna Nyumba Movu Mbovu pale Nyuma ya CCM Head office mtaa wa kariakoo
 
tulikua tunaziita nyumba za mbavu za mbwa!
 
Huyo Mama Hivi hakuwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Zanaki Pr? manake nakumbuka kama alishawahi hama zanaki akahamia ups kama sikosei na pia walimu wakuu walikuwa ni kina mama zanaki na upanga...

UPS nakumbuka zamani kulikuwa na fensi mbavu na kuna kinjia unapita mahakamani then unaenda tokezea Maktaba lol

Kuna Darasa Moja lilikuwa na Kinanda Kikubwa(Organ) ulishawahi kiona hicho Da Pretty!

Duduwasha ulienda kufanya nini pale CHUMBA CHA KINANDA?
Wakati tupo std 5 nilisomea lile darasa,mwaka uliofatia ndio kikawa chumba cha kinanda.
Mama Mahundi mi nilimkuta UPS tangu std 1 hadi natoka,badae akahamia Muhimbili ndiko alikomalizia kazi hadi alipofariki.
 
mkama na koba wapi na wapi mzee,kipindi mkama sharp anatingisha kariakoo koba alikua anapigana ngumi na iraq hudu na stanley mabesi relwe gerezani enzi hizo,akiwa kijana mdogo!
Wacha unataka kuniambia hawakufanya kazi pamoja?

Kuna kisa Kimoja kesi alikuwa anaifuatilia Koba sababu anawajua sana watoto wa kariakoo so aliwalea lea sana Sharp alikuwa anawapunguza manunda kwa Shaba tu, Karikaoo ilikuwa inatisha unakabwa nje nje na mwizi akikamatwa kesho unakutana nae tena uache Mambo ya Mapolisi...

Koba na kina mabesi ni Tofauti pia Koba aliibukia pindi zile na kina Matumla Nilishuhudia Game karibu zote pale Diamond Jubilee Tanzania walipotwaa Ubingwa, Zama zao kina Isangula, Rashid Matumla,Haji Matumla, Joseph Marwa walitwa Dhahabu Timoth Kingu ndio alituangusha baada ya kuchapwa na Mzambia Ngumi Jiwe Chini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom