Watoto....best interest.....


Mwj1, ...hebu msome Aspirin hapa...;



Iweje binti mpaka amalize chuo kikuu ndio aje atambulishwe huyu sio baba'ko? Dhulma kiasi gani kwa mtoto hiyo?
kumjua Biological Dad wake?

...ilikuwaje ni ngumu kusema, ila wa baba wengi hutumia busara kwamba mtoto ni mdogo acha mama mtu aondoke nae.
Hayo mambo ya utaratibu nk yanapotokea maugomvi Mwj1 hakunaga na formula bana, yanalipukwa tu,...unajishtukia
mama na watoto wameshaondoka wewe umebakia na nyumba yako. Ngumu sana kuelezea, kwani kila mtu anakumbwa na
experiences zake, ila hakuna cha ajabu kuwa mama wengi huondoka na watoto wao.

Hapo kwenye sheria usimamizi na utekelezaji wake sahau.
Mheshimiwa moskwito..... kibaya zaidi baba naye alikuwa anajua kuwa yule ni binti yake.... aliuziwa mimba!...... Hili liliibuka baada ya baba kukorofishana na mama na bahati mbaya binti akawa upande wa baba yake.......... akashangazwa kuambiwa baadae kuwa yule anayemtetea wala si baba yake, na kama vipi wajipange ampeleke kwa baba yake halisi ili ahuhudie alivyo "gentleman" kuliko huyo aliyefikiri ndo baba yake...............kilichotokea, naogopa kukiweka hadharani hapa... waweza kulia aisee!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kuna swali langu Mbu kasema anagugo mabrasha yake...
Mama ana haki gani kwa mtoto wa chini ya miaka 7?

  • Kukaa na mtoto au
  • Hata kuamua mtoto akae wapi.....
Japo la muhimu sio content za sheria....la muhimu ni mtoto kupata kilicho bora toka kwa wazazi wote.

...Oooppss, nilidhani umeiona,...wataalamu wa sheria watakuja kuiweka sawa.
Niliandika Haki ya mtoto ni kupata malezi ya wazazi wake wote wawili (kama wapo hai)
na ni Wajibu wa wazazi kuhakikisha hilo linatekelezeka.

Kwa mama hapo anafungwa na wajibu wake kama mzazi kuhakikisha mtoto anapewa Haki yake kuonana na baba yake.

 
Raha kwa alie/atakaekuwa mzazi mwenzako...Una busara kupita maelezo!!

Nice thread mkuu iliyojaa michango yenye maana katika jamii mana hili suala lipo sana tu!!

BJ mzima?
RR got 2 kids to take care of....
Thanx for the compliment....ila not that wise....
Ila ikija maamuzi kuhusu watoto wangu nitawalinda kwa nguvu zote....hata ikimaanisha kupindisha misimamo yangu!
 
Kisaikolojia mtoto anaweza kuwa trained kuwa unavyotaka awe up to seven (7) years baada ya hapo hakunjiki. Labda wameangalia hilo. Brain ya mtoto inakuwa flexible up to seven years baada ya hapo anaanza naye ku argue and ask "why?".
Kwahiyo saikolojia hiyo ndo inaifanya sheria imtake ahamie kwa baba akifikisha 7 years?
 
Is it a crime if I were to ask you what those rs stood for? just out of curiosity...

Save the asking.....
The first r is what they call me...the second one is what they used to call my old man...
 
Si wote wana matatizo ni imani zao tu. Nilikuwa na marafiki zangu jirani zetu; nilikuwa sijuhi kama wana dada yao mkubwa wa kwanza. Yule dada alikuja town toka kwao mbeya kwa bibi yake baada ya kupata mimba huko kijijini. Na hakukaa sana hapa dar alikunywa sumu eti kisa wazazi wamemkaripia. Sasa familia kama hiyo ina excuse??? Mbona watoto wengine walikuwa wanawalea wenyewe? Ukiuliza why wanasema bibi ameng'ang'ania nimwachie mtoto kwani yuko peke yake. Well kama kuna sababu za msingi Ok. Lakini kama ni kujiaminisha kuwa kijijini ni best, jua mmekula wa chuya. Huo ni unyanyasaji wa watoto. Watoto wanatakiwa walelewe na wazazi at least mmoja kama si wote. Hata wale wanaopeleka watoto boarding wakiwa wadogo am telling you itawa cost.

Nina best yangu mamake alimzaa na mume wa mtu kwa kuwa mama yake alikuwa bado analipa na macho juu akaamua kumsomesha boarding ili aendelee kula raha. Huyo dada kwa sasa ana maisha yake bomba lakini alinambia NK sina mapenzi hata chembe na mama yangu. Aliamua kum dump boarding school ya masista ambako walikuwa wananyanyaswa kishenzi wanateka maji mtoni ili yeye ale raha toka chekechea mpaka high school amesoma boarding.

Kibaya sasa na yeye amepata ujauzito mimba ilitoka lakini ila sijuhi ilikuwa ya nani nadhani pia ni mume wa mtu! But its her mum anayemfanya asiolewe kwani huwa anamwambia daily kuolewa siyo deal soma tu mwanangu uwe na maisha yako. Na kila mchumba anayempeleka kwa mama yake mama anabonda kishenzi mpaka mtoto anabwaga manyanga. Na sasa she is approaching 35 years!

Mkuu is it a Choice ambayo mtu anachukua..???, nadhani hapa tunafanya kosa la kuweka mambo kwa ujumla Mzazi kama mzazi anaona ni wapi mwanae huenda akapata malezi bora; kwahiyo mzazi anaona ni wapi mwanae atapata malezi bora kulingana na yeye alipo na circumstances (tusiseme kwamba ni sababu ya uzembe au kuepuka responsibilities)

Si kweli kwamba wote waliolelewa na bibi zao wanadeka..., mlezi ni mlezi na pale mzazi anapoomba msaada ni kwamba amezidiwa... (Sidhani kama kuna mama ambae hapendi kukaa na mwanae.., unless ana matatizo)
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...kulikuwa na article hii nzuri sana, hebu muipitie kidogo
source; TAWLA na mkakati wa kupinga ukatili wa kijinsia

Mapendekezo ya Tawla ni kwamba utunzaji wa familia lisiwe suala la kijinsia; kila mzazi awe na wajibu sawa wa kuitunza familia.
Mandari anasema sheria za sasa zinamuweka mwanamke kama mnyonge na mtu asiye na uwezo wa kumtunza mumewe hata kama ana mali na afya njema.

"Kuwe na sheria kamili inayomuamuru mwanamke, ili mradi akiwa na mali, kumtunza mumewe au mtalaka wake. Pia ibara ya 116 ya Sheria ya Ndoa inasema gharama za matunzo na huduma baada ya ndoa kuvunjika itatokana na uwezo wa mwanamume na mahitaji ya mwanamke aliyetalikiwa na kwamba ni wajibu wa mahakama kugawa mali ya waliotalikiana kama inavyoona sahihi kwa mujibu wa sheria.

"Ibara hii inatambua pia sheria za kimila kuhusishwa katika jambo hili; lakini Tawla inapendekeza kuwa sheria za kimila hazifai kwa kuwa zinaongoza kwa kumkandamiza mwanamke," anasema.
Pia anasema Tawla inaona kwamba sheria za kimila hazina maana katika mazingira ya sasa ya Tanzania ambayo mtu anaweza kuoana na mtu wa kabila jingine.

Itakuwa bora kama Ibara ya 125 (2) ya Sheria ya Ndoa itafutwa kwani inaitaka mahakama izingatie masuala ya kimila isikilizapo kesi za kugawana mali na watoto, jambo ambalo limepitwa na wakati na ni sheria ya kibaguzi.
Mwenyekiti huyo anashauri kuwa inapaswa Ibara ya 125 (3) ikarekebishwa, kwani inaonekana kama ni haki ya baba kumtunza mtoto akishapita miaka saba kama ambavyo mahakama imekuwa ikitafsiri; kwani hali hiyo imekuwa ikimnyima mama haki ya kumtunza mtoto hata kama mama huyo yuko katika mazingira bora ya kumtunza mtoto.

Anashauri ibara hii itamke kwamba hali bora ya mtoto iwe ni kigezo muhimu cha kuamua nani akae na mtoto kati ya baba na mama.
Aidha, anasema ibara ya 5 ya Sheria ya Ushirikishaji inapaswa kurekebishwa kwa kuondoa kiasi cha fedha cha kulipwa kwa mwezi.
Kiasi cha sh 100 hakitoshi kwa mahitaji ya mtoto na kushauri jambo la busara kama kiasi cha fedha za matunzo ya mtoto kingetolewa kama asilimia fulani ya mapato ya baba.

"Baba kuacha kutoa matunzo kwa mtoto baada ya mama yake kuolewa na mwanamume mwingine kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 54A ya Sheria ya Ushirikishaji si kwamba kuna madhara kwa mama, lakini pia kunahatarisha ndoa yake mpya.
"Hii ni kama kumuambia mama asiolewe tena, vinginevyo atakosa matunzo ya watoto; sheria hii haina budi kurekebishwa," anasema.

Anasema sheria ya sasa inataja kikomo cha umri ambacho mtoto anapaswa kutunzwa na baba yake kama ilivyo katika ibara ya 6 ya sheria ya Ushirikishaji; sheria kama hii haifai na hasa kwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa.
Sheria haina budi kusema kwamba baba atakoma kutoa matunzo kwa mtoto baada ya kumaliza masomo ya sekondari.
Ibara ya 71A ya Sheria ya Kimila ya 1963 inasema kwamba baada ya kutalikiwa mke wa mkulima ana haki ya kupata asilimia 25 ya mazao yaliyopatikana katika mwaka aliotalikiwa.

Sheria hii inamaanisha kwamba mwanamke huyo ataolewa mara moja baada ya kutalikiwa au kwamba atatunzwa vema na familia baada ya kurudi kwa wazazi wake.
Anasema sheria ilipaswa kuangalia mchango halisi wa mwanamke ikizingatiwa kwamba ni mwanamke anayefanya kazi zaidi ya mwanamume vijijini. Amali hazina budi kugawanywa kwa usawa.

"Kwa kuwa ibara hiyo imepitwa na wakati, badala yake kuna Ibara ya 114, Sheria ya Ndoa ya 1971 ambayo inaelezea namna ya kugawana mali zilizochumwa kwa pamoja kati ya mume na mke.
"Ibara ya 74 ya Sheria ya Kimila ya 1963, inasema mume atamtunza mke baada ya kutalikiana, pale kama makosa yalikuwa ya mume. Kifungu hiki hakimpi mke haki ya kugawana kwa usawa mali iliyochumwa pamoja kati ya mke na mume; kuna haja ya kifungu hiki kurekebishwa.
"Ibara ya 11 ya Sheria ya Uraia ya Tanzania, 1995, inasema mwanamke wa nje aliyeolewa na Mtanzania muda wowote katika uhai wa mume wake ana haki ya kuomba uraia kuwa raia wa Tanzania.
"Ibara hiyo haimzungumzii mwanamume mgeni aliyemuoa mwanamke wa Kitanzania ana haki gani. Marekebisho yanahitajika ili mwanamume huyo mgeni aweze kuomba uraia wa Tanzania.

"Ibara ya 166, 167 na 266 ya Sheria ya Adhabu ( Penal Code) inatoa wajibu wa matunzo kwa mtoto na inatoa adhabu kama matunzo hayo hayatolewi. Adhabu zitolewazo ni ndogo mno. Kutokana na hali hiyo, mtu aliyemtelekeza mtoto bila matunzo akipatikana na hatia hulipa faini, lakini anaendelea na ujeuri wake wa kumtelekeza mtoto. "Lakini pia sheria hiyo haisemi mtoto aliyetelekezwa atafidiwaje. Pia umri wa miaka 14 hauna budi kuongezwa hadi 18 au mtoto awe amemaliza shule ya sekondari, kwani mtoto wa miaka 14 bado ni mdogo na hana uwezo wa kujitunza," anasema.
 
Well since uko tayari tayari sana kumtetea rafikiyo unajua sababu ya mama kumweka mbali na mtoto?!Unajua ni katika harakati gani mtoto alitungwa na hata kuzaliwa?!

Kama majibu ya mwaswali yangu unayo na ndio ukweli wa mambo (hujafichwa wala kudanganywa) basi tumia hayo kupima maamuzi ya mama na kuamua kama kuna usahihi au la.Maana sio rahisi mtu akamnyima mwenzake kumuona tu mtoto (achilia mbali kumchukua) bila sababu ya msingi.Na amini usiamini zipo sababu zinazoweza kumfanya baba au hata mama anyimwe kabisa kua karibu/kumwona mwanae ndio maana hata mahakama hua zinatoa hukumu za aina hiyo sometimes.

Ninakuelewa BabyGal ni kweli pengine kuna lililojiri kati ya wazazi hawa; na ni wajibu wa mzazi kuhakikisha usalama wa mwanae. Najiuliza tu iweje mama huyu atake kuhakikisha usalama wa mwanae kwa kwendampeleka kijijini? Ofcoz si vibaya iwapo anampatia/hakikisha kuwa anapata mahitaji yote muhimu but ni nini hicho aichokifanya baba huyu hadi mama kumdenaia kabisa mwanae haki ya kuonana na babake!! kuna kitu ambacho nina uhakika kimejiri na kimempelekea mama kuamua hivi lakini nitamuelewa amam huyu kama 'strategy' hii anaitumia kwa muda flani tu na kisha atalegeza masharti lakini akiifanya ya kudumu kuwa hata iweje haitokuwa; atakuwa anakosea sana. Kama anamprotect from whatever danger, ni vema ikifika wakati ambao anahisi danger inapungua akalegea na kuhakikisha kuwa uhusiano wa baba na mwana unarudi (japo kwa mbali) asimkatalie kabisa..........Inauma sana aisee
 
  • Thanks
Reactions: RR
MJ1 bila hata ya kuangalia sheria....mtoto mdogo (sijui udogo unaishia wapi tho) kukaa na mama yake mzazi ni the best option ya malezi....
Naposema muhimu sio content za sheria namaanisha wazazi wawili wakubaliane kuhusu njia bora zaidi ya kumlea mtoto/watoto wao...

...................Nakubaliana na wewe RR lakini kama ni situation ambayo hakuna maelewano kiasi cha kuwa hata hao wazazi wawili kukubaliana haiwezekani ndipo sheria inapotumika!! So I still think contents za sheria pia ni muhimu!
Kumbuka mara nyingi kwenye ishu za separation na kutalikiani ni nadra sana kuwe na makubaliano na mawasiliano mazuri baina ya wazazi. Mara nyingi huwa ni chuki, visasi na kukomoana......
 
...................Nakubaliana na wewe RR lakini kama ni situation ambayo hakuna maelewano kiasi cha kuwa hata hao wazazi wawili kukubaliana haiwezekani ndipo sheria inapotumika!! So I still think contents za sheria pia ni muhimu!
Kumbuka mara nyingi kwenye ishu za separation na kutalikiani ni nadra sana kuwe na makubaliano na mawasiliano mazuri baina ya wazazi. Mara nyingi huwa ni chuki, visasi na kukomoana......

Bado sitaki kuelewa mantiki ya kumkomoa mzazi wa mwanao!
 
Ninakuelewa BabyGal ni kweli pengine kuna lililojiri kati ya wazazi hawa; na ni wajibu wa mzazi kuhakikisha usalama wa mwanae. Najiuliza tu iweje mama huyu atake kuhakikisha usalama wa mwanae kwa kwendampeleka kijijini? Ofcoz si vibaya iwapo anampatia/hakikisha kuwa anapata mahitaji yote muhimu but ni nini hicho aichokifanya baba huyu hadi mama kumdenaia kabisa mwanae haki ya kuonana na babake!! kuna kitu ambacho nina uhakika kimejiri na kimempelekea mama kuamua hivi lakini nitamuelewa amam huyu kama 'strategy' hii anaitumia kwa muda flani tu na kisha atalegeza masharti lakini akiifanya ya kudumu kuwa hata iweje haitokuwa; atakuwa anakosea sana. Kama anamprotect from whatever danger, ni vema ikifika wakati ambao anahisi danger inapungua akalegea na kuhakikisha kuwa uhusiano wa baba na mwana unarudi (japo kwa mbali) asimkatalie kabisa..........Inauma sana aisee

Mwj1, kwa mara nyingine tena ninakurudisha kwenye mfano wa Aspirin.
Mama mtu akiamua kumchapia mzazi mwenziwe kwa kumtumia mtoto,
miaka ikishapita asiitumie bakora hiyo hiyo kuwaadhibu wengine,...sio busara!
msome Aspirin.


Mheshimiwa moskwito..... kibaya zaidi baba naye alikuwa anajua kuwa yule ni binti yake.... aliuziwa mimba!...... Hili liliibuka baada ya baba kukorofishana na mama na bahati mbaya binti akawa upande wa baba yake.......... akashangazwa kuambiwa baadae kuwa yule anayemtetea wala si baba yake, na kama vipi wajipange ampeleke kwa baba yake halisi ili ahuhudie alivyo "gentleman" kuliko huyo aliyefikiri ndo baba yake...............kilichotokea, naogopa kukiweka hadharani hapa... waweza kulia aisee!

Hakuna sababu iwe ndogo kama mdudu chungu, au kubwa kama mlima kilimanjaro ambayo
Mama inakubalika amnyime baba mtu haki ya kumuona mwanawe, na mtoto kunyimwa haki ya
kumjua babake tangu angali mdogo.

Aspirin weka yaliyojiri, nishaandaa tissues hapa...
 
...................Nakubaliana na wewe RR lakini kama ni situation ambayo hakuna maelewano kiasi cha kuwa hata hao wazazi wawili kukubaliana haiwezekani ndipo sheria inapotumika!! So I still think contents za sheria pia ni muhimu!
Kumbuka mara nyingi kwenye ishu za separation na kutalikiani ni nadra sana kuwe na makubaliano na mawasiliano mazuri baina ya wazazi. Mara nyingi huwa ni chuki, visasi na kukomoana......

hapo kwenye kukomoana hapo,...mnh...Mwj1 pamoja na mapenzi yangu kwako, kina mama wengi wamejaaliwa hilo.
Kuna kina mama wachache waliojaaliwa mioyo ya huruma, mfanoi weye Mwj1 wangu, ...lol...(ulishaanza kununa ee?)
 
  • Thanks
Reactions: RR

...Oooppss, nilidhani umeiona,...wataalamu wa sheria watakuja kuiweka sawa.
Niliandika Haki ya mtoto ni kupata malezi ya wazazi wake wote wawili (kama wapo hai)
na ni Wajibu wa wazazi kuhakikisha hilo linatekelezeka.

Kwa mama hapo anafungwa na wajibu wake kama mzazi kuhakikisha mtoto anapewa Haki yake kuonana na baba yake.


Kwahiyo saikolojia hiyo ndo inaifanya sheria imtake ahamie kwa baba akifikisha 7 years?

Najua wengi wetu mmeshawahi kushuhudia au kuishi ndani ya ‘single parenting'……ama maisha ya magomvi muda wote….namaanisha kuwa mzazi kati ya migongano ya kimahusiano….
Mimi (ex. st) RR nawashauri ‘single parents' (wale walio kwenye magomvi)

  • waache kutumia watoto kama zana ya kupigania uhusiano wao….. au kama kifaa cha kumwadhibu mzazi mwenzake….(hapa wengine hata hupandikiza chuki kwa watoto dhidi ya uapande wa pili).
  • waache ubinafsi katika kufanya maamuzi yahusuyo watoto….sio vizuri mzazi akaruhusu mtoto akakaa na mzazi mwengine, hata kama kisheria mzazi huyu ana uwezo wa kung'ang'ania …as long as it is of best interest to the kid….mfano sioni ulazima wa baba kumchukua mtoto kwa kisingizio cha mtoto kutimiza miaka saba ya kisheria au mama kukataa mtoto asikae na baba kwa akisingizia mtoto hajatimiza miaka saba!
Kumbukeni....mzazi wa mwanao akipata maumivu….basi hayo maumivi yanamfikia mtoto…in some ways!
Ni ushauri tu!


Naomba nami niweke senti yangu moja kama itakuwa na maana hasa wakati mjadala ushafika mbali na mengi mazuri yamezungumzwa.

Kwanza kabisa watoto ni viumbe wanaotokana na kitendo cha watu wawili ( wanaweza wakawa wamekubaliana kuleta kiumbe hiki duniani au kwa kutokukubaliana pale ambapo interest yao ni starehe tu; au labda kwa nguvu /ubakaji).Vyovyote iwavyo sheria na hata mila na desturi zinao utaratibu kulinda maslahi ya kiumbe huyu asiyejiweza hadi atakapokuwa na uwezo kujimudu.Baada ya kusema hayo, nitasema yafuatayo:
1. Wazazi wa mtoto wote wana haki kwa mtoto na pia wajibu.Hata hivyo kibaiolojia, kuna haki nyingine za mtoto zimefungwa ndani ya mama zaidi kuliko baba hasa pale mtoto ni mchanga. Mahitaji haya ni ya kimwili na hata kisaikolojia. Kwa msingi huu, sheria za nchi na hata mikataba na itifaki za kimataifa kwa kutambua hayo yote zimeweka bayana dhana ya " best interest of the child" ili kuhakikisha mtoto hakosewi haki zake kwa sababu kuna interests tofauti ikiwemo ubinafsi wa wazazi au hata walezi ambazo hazimsaidii mtoto kimalezi. Fikiria makabila mengi husema " mtoto ni mali ya baba".Kwa mantiki hii kuna akina baba hufukuza mke au hata mke hutaka kuondoka lakini hushinikiza mtoto abaki. Hata wapo wazazi hudai watoto wa watoto wao wa kiume kwa kisingizio kuwa ni damu yao.Je damu pekee ndio tiketi ya kudai watoto hata wachanga? Hilo swali nkuachia msomaji.

2.Kuna wazazi hutumia watoto kama silaha kali katika magomvi yao.Hili jambo liko sana na hutumiwa na wote - mama na baba.Kitu kinachosahaulika ni athari kubwa kwa mtoto ( huenda mtoto anawapenda wazazi wote) kuona analazimishwa kumchukia mpendwa wake!Iweje mama unayegombana na mzazi mwenzio, utumie mtoto asiyejua chanzo cha ugomvi wenu kukuunga mkono na kumpiga vita baba yake mzazi?
Kuna watoto wengine wanakuwa wameona na kushuhudia ubaya wa mzazi mmojawapo kutokana na ama tabia mbaya za mzazi au kutokana na ukatili unaoonyeshwa na mzazi mmojawapo.Hapo ni kazi ya yule mzazi mwingine kujitahidi asimchonganishe mtoto na mzazi mwenzie.
3. Kisheria, miaka saba siyo kibali cha kuruhusu/kulazimisha mtoto kwenda kwa baba kama wengi wanavyodhania. Kigezo ni " maslahi ya mtoto" na siyo umri au mila zinavyodai.Nimeona nisisitize hili ili tujitahidi kuelimisha jamii kwenye hili.

Katika kuamua hizo "best interests" au maslahi ya mtoto, mahakama ndio wataamua ( kama wazazi wenyewe watashindwa ktumia busara zao na kuacha mtoto akae pale atakapostawi zaidi),na watatafuta ushahidi ikibidi hata kuwaita watoto mahakamani na kuwauliza.Siyo lazima mzazi mwenye uwezo kifedha ndio apewe kukaa na mtoto.Mahakama inaweza kumweka mtoto chini ya mzazi aliyedhaifu kifedha na kuamuru mwenye uwezo kifedha atoe matunzo.Mara nyingi wakina mama ndio hupewa watoto unless ithibitike kuwa huyo mama hana uwezo pengine kutokana na tabia zake.
 
Nilikuwa na marafiki zangu jirani zetu!

Well..... Well..... Unajua kila case inabidi itazamwe kwa undani and the bottom line ni "what are the best interest for the kid" na si vinginevyo, kwahiyo action anayofanya A inaweza kuwa sawa kutokana na motives zake mfano:-
  • Je ni bora kila mtoto akae na Baba yake hata kama ni abuser?
  • Je ni bora kila mtoto akae na mama yake hata kama ni druggie?
  • Je ni bora mzazi unganganie kukaa na mtoto wako hata kama environment ya hapo ni detriment kwa mtoto, au labda kuna company anazokaa nazo zinampotosha...
  • Je kuna ulazima wa kumwambia mtoto mdogo biological father wake ni nani hata kama huyo baba he wants nothing to do with the Kid (kumwambia huko kutamuongezea mzigo au kumpunguzia mzigo)
Kwahiyo tutaona kwamba the bottom line what matters ni (betterment ) ya mtoto and it does not matter anayapata wapi hayo... (kuna watoto yatima wanapata malezi bora kuliko familia za baba na mama)

Takes more to be a father and that action even a fool can perform lakini only a father takes decent care..., and sometimes a single parent can do a better job alone kuliko angekuwa na mwenzake
 

Mwj1, kwa mara nyingine tena ninakurudisha kwenye mfano wa Aspirin.
Mama mtu akiamua kumchapia mzazi mwenziwe kwa kumtumia mtoto,
miaka ikishapita asiitumie bakora hiyo hiyo kuwaadhibu wengine,...sio busara!
msome Aspirin.




Hakuna sababu iwe ndogo kama mdudu chungu, au kubwa kama mlima kilimanjaro ambayo
Mama inakubalika amnyime baba mtu haki ya kumuona mwanawe, na mtoto kunyimwa haki ya
kumjua babake tangu angali mdogo.

Aspirin weka yaliyojiri, nishaandaa tissues hapa...

Hapo nimekuelewa vema Mbu na Asprin nimemwelewa nilipokuwa naijibu post ya BabyGal nilikuwa najaribu kufikiria ni tatizo gani lililojiri hata BabyGal afikirie kuwa huyu Mama alikuwa na haki ya kumnyima baba mtoto kwa hiyo tusimlaumu..ndio kichwani mwangu nikasema labda kama Baba alikuwa anamabuse mtoto wake sexually au kwa namna yoyote ile ambayo Mama huyu ilimfanya aone kuwa huyu Baba adhabu yake ni kumweka mbali na mwanae (Mbali ambako hatowezafika, mbali ambako hata yeye mama mtu hakai huko, mbali kijijini kwa wazee wake) Yaani kilichomfanya hata huyu mama akaona kuwa mwanae atakuwa 'safe' kama atakaa mbali na babake ...na mbali na YEYE MAMA MZAZI hata kama uwezo wa kumtunza anao. Hilo tu ndo lililopelekea mie kusuggest 'adhabu ya muda' kwa maana ya kuwa kama ilikuwa ni abuse then mtoto akishapata sense yake (kiasi cha kuweza kuresist hiyo abuse) basi apewe haki yake! Sasa ni 'danger' gani ambayo hadi mtoto afike chuo ashindwe kujihami?

Huyu mmama wa kwenye ishu ya Asprin na wale wote ambao wanashindwa kuwaonyesha watoto wao wazazi wao ..........huwa siwaafiki na ninacheea kusema kuwa ninawalaani kwani maneno huumba (sijui kama maandishi nayo huumba) but nachelea isije backfire kwangu!!

MUNGU na awape ufahamu wale wazazi wote waliozibeba siri za aina hii mioyoni mwao, wawezizifunua na kutua mizigo ya dhamirani)
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

hapo kwenye kukomoana hapo,...mnh...Mwj1 pamoja na mapenzi yangu kwako, kina mama wengi wamejaaliwa hilo.
Kuna kina mama wachache waliojaaliwa mioyo ya huruma, mfanoi weye Mwj1 wangu, ...lol...(ulishaanza kununa ee?)

Ni kweli mydia usemayo kina mama wengi tumejaaliwa hilo, I used to have the same view kama wanawake wengi, ..ule wa watu mmeachana kwa makasheshe mpaka kushikiana visu....baba/mama akaondoka ..unaanzia wapi kumruhusu aje awaone watoto? Au mtu kaikataa mimba, nikalee mwenyewe na matuc juu, nipate shida halafu mtoto ana miaka saba site ndo anakuja kujidai ni wangu...Nilikuwa sitaki kabisa kusikia mjadala huu.......zilikuwa ni akili za kitoto nakiri. Kuna a very good friend of Mine, alinifungua macho na kunitoa utoto.... aliniuliza kwani unafikiri Baba wa mtoto anawezakumdhuru mwanae?...nilikosa jibu na tangu siku hiyo nilibadili mtazamo wangu juu ya mambo ya custodian ya watoto.

N.B: Nimenuna umenisema hadharani badala ya chumbani- umenipiga kibao, badala ya kutumia upande wa khanga! LOL
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Haya mambo magumu sana kubalance..Uhusiano unaoshikiliwa na 'eti kwa kuwa tumezaa' hua hauna tija, kwani watoto hawatapata wanachotarajia kutoka kwenu na nyie pia mtakuwa mna-share just one roof lakini kila mmoja anachapa mwendo (responsibly lakini) kivyake....ugomvi wa partners tutake tusitake hua una athari sana kwa mtoto, sana tu.
 
Back
Top Bottom