'Single Mothers' na Changamoto ya Malezi kwa watoto

Kinyonyoke

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
3,495
13,132
Kama mwalimu ambae ninakutana na watoto wengi kutoka katika 'background' tofauti tofauti, naomba niseme watoto wanaolelewa na mzazi mmoja hususani mama (single mother) ni jipu kubwa ambalo linahitaji kutumbuliwa mapema Sana.

Watoto wanaolelewa na mama pekee bila uwepo wa mzazi wa kiume, Uchunguzi wangu umenibainishia kuwa, asilimia kubwa hawapati malezi na usimamizi stahili hali inayopelekea kuongezeka kwa wimbi la vijana wa hovyo wasio na maadili kwenye Jamii.

Tunapojaribu kufuatilia na kuzungumza na watoto wenye matatizo ya kinidhamu wengi wao unakuta Msingi wa malezi ni lege lege huku ukijengwa na mzazi mmoja (mama). Jambo ambalo lisingekuwepo endapo mtoto huyu angelelewa na wazazi wote wawili.
Japo Sisemi kwamba watoto wanaolelewa na wazazi wote hawana changamoto za kinidhamu. La hasha! ila watoto wanaolelewa na mama pekee wamezidi. Too much!....

My take ni hii, ewe mzazi hususani wa kike, unaweza ukawa 'independent and strong woman', lakini tambua mtoto anahitaji pia malezi ya mzazi wa kiume, hata matatizo ya ushoga kwa kiwango kikubwa yanachangiwa na malezi ya mama pekee.
Watoto wenu wa kiume wana'develop 'feminine traits' mbele ya macho yenu na mnawaangalia tu.

Japo kina mama wachache wanajitahidi katika malezi bila uwepo wa baba lakini asilimia kubwa mnafeli na mnahitaji msaada kuwalea watoto wenu..

Watafutieni watoto wenu Watu ambao wata act Kama fatherly figure, watakaoweza kuwa discipline na kuwa 'good role models' kwao kwa mustakabali mzuri wa maisha yao.
Badilikeni kabla hamjachelewa.

Mjumbe hauwawi.
 
Back
Top Bottom