Watoto 19 wafa kwenye disco la Idi Tabora

The managers of the hall in central Tanzania where a disco stampede killed at least 19 children aged under 13 have been arrested and questioned by police.

Reports say as many as 400 children were packed into the hall, twice the recommended number.

The event had been organised as part of the Eid al-Fitr festivities to mark the end of the Muslim month of Ramadan.

The regional police commander in Tabora town said the children began fainting because of lack of air.

Seventeen children, aged between five and 12, are still in hospital.

Source: BBC World

The president has extended his condolences to the families, and demanded that those responsible are brought to justice.

Cheap tickets

The stampede took place in the Tabora region, about 750km (470 miles) north-west of the commercial capital, Dar es Salaam.

Witness John Mbele said he was passing in his car when he heard people shouting for help.

"I tried to organise some people to bring some children in the car and send them to hospital," he told the BBC's Focus on Africa programme.

"They were unconscious. The problem was there were not enough cars to take the children to the hospital," he said.

"Nobody was controlling the roads, a few police were there but they could not control the mass.

"The children were just shouting, many of them did not know exactly what was happening."

Tabora regional police commander Daudi Siasi was quoted as saying that the hall had a capacity of 200 but more than double that number were inside at the time of the disaster.

The hall was said to be overcrowded after cheap tickets had gone on sale.

Some of the victims are reported to be as young as five.

Tanzanian newspapers have described the tragedy as "the biggest in Tanzania's history" and "the worst-ever disaster during Eid al-Fitr".
 
Last edited:
Tuendelee kusubiri. Kufunguliwa mashtaka kwa huyo mmliki kunategeme ni mwanachama wa chama gani, kuna uwezekano pia kuwa hizo dola 500(yaani thamani ya waliokufa) ndio imetoka hakuna kitakachoendelea zaidi ya hapo. Uswahili utapigwapigwa tu and life will go on, na tukio kama hilo litatokea tena. It sounds so pesmistic lakini huu ni ukweli.
 
This is a terrible thing.. lakini there is no problem with the president giving 500,000 per family. Huo ni mchango wa msiba and not compensation. JF has lost its objectivity and pipo just politicize kila kitu. that is a shame.. An investigation is necessary and all at fault should be punished so that it serves as a lesson... inasikitisha sana!
 
Nashangazwa habari kutoka Tabora ni ngumu kweli kufika. mablogu, na magazeti (kama ya Global Publishers) ambayo huchapisha habari haraka haraka hadi leo hii hawajaweka habari ya mauti hayo, so hasn't michuzi na wengine. What is going on?

kwani kutoka dar to NEW YORK na DAR to TBR wapi mbali?
mjj hata manzese ni mbali kuliko new york ukitokea magogoni
si unakumbuka mzee mmoja mwaka fulani alimua ni bora kuenda kumuona bongoman kulikowagonjwa muhimbili wakati madaktar wamegoma, kwa hiyo mzee hilo sio jipya kwa wakubwa hawa ingelikuwa mzee kaenda kuangalia mpira taarifa ziko katika vyombovyoote namichuzi nae ndio hivyoo tena
 
i15_taboraNSSF.jpg


Ukumbi ambako tukio la watoto hawa kufariki limetokea. Ukumbi ulikuwa ghorofa hiyo ya juu.
 
This is a terrible thing.. lakini there is no problem with the president giving 500,000 per family. Huo ni mchango wa msiba and not compensation. JF has lost its objectivity and pipo just politicize kila kitu. that is a shame.. An investigation is necessary and all at fault should be punished so that it serves as a lesson... inasikitisha sana!

unfortunately, politics revolve and involve everything we do.
 
Yes nilihahidi kuja na update za msiba za watoto hawa 20 waliopoteza maisha yao jana, hadi mchana huu wazazi na walezi ikiwa ni pamoja na ndugu na jamaa wa watoto hawa wamekubaliana kuchukua maiti za watoto hawa nakwenda kuwazika kila mmjoja kwani kuna matabaka ya udini.

Likin nirudi katika issue yenyewe ingawa jana watoto hawa walifikishwa katika hospital ya mkoa wa Tabora Kitete lakini bado hosp hii haina madakatari wala Nurses wa kutosha, hata hivyo bado vitu kama oxygen concentrator na oxygen sylinder kwa ajili ya emergency preparedness bado ni shida katika taasisi muhimu kama hii amabayo ni lifesaving kuna haja ya kuweka nakufanya jitihada za kutafuta staff wa kutosha hosp hii. najua wana JF hamuwezi kuamini hosp hii inao madaktari qualified kwa maana ya MD sio zaidi ya 2, na sasa inatumia madaktari wa kichini amabao wamekuja kwa muda je hawa mabwana wakiondoka itakuwaje. kwa siku ya jana ilikuwa ni mshikemshike kwani watoto baada ya kufikishwa Kitete tulitegemea wale majeruhi wangewekwa katika oxygen kwani ndo ilikuwa shida kwa watoto hawa lakini ilifanyika huduma kama ile ya huduma ya kwanza kwa kupetapeta watoto hawa kwa nguo, sidhani kuwa hii ni sahihi kwa chombo kama hiki kutumia nguo na kanga kuanza kupungia watoto au mtu aliyekoswa hewa.

Kwa ujumla hosp ya mkoa wa Tabora bado inahitaji mabadiriko mengi kwa nyanja zoote kwani bado huduma pale zinalegalega sana.

Ndugu zangu wana JF najua serikari ya mkoa itaunda tume lakini pia tungeoomba tume hii iwe huru na itoe haki na si kama tume ambazo tumezoea miaka yooote kutoa tahalifa isiyo nzuli.

Nashangazwa habari kutoka Tabora ni ngumu kweli kufika. mablogu, na magazeti (kama ya Global Publishers) ambayo huchapisha habari haraka haraka hadi leo hii hawajaweka habari ya mauti hayo, so hasn't michuzi na wengine. What is going on?

Muvimba na MwanaKijiji,
Kwanza nianze kwa kusema nimeingia kwa Michuzi na kuona kaweka picha za jengo na Marehemu. Pili kwa Muvimba nashukuru kwa habari za huko kwetu. Nilipiga simu leo na kuambiwa juu juu kwani jamaa niliyempigia kwa sasa hayupo Tabora mjini. Inasikitisha na kuuma sana.

Mwanakijiji, sijui kama unakumbuka pana wakati nilikuwa nasikitika na kulaani baadhi ya mikoa kupendelewa sana. Nakumbuka Mushi alinilaani kuwa nina ukabila. Ila muda huo nilikuwa ndiyo kwanza nimetoka huko. Picha halisi ya huko ilinisikitisha sana. Moja ya habari nilizosikia ilikuwa ni huduma za hospitali yetu ya Kitete. Nilivyoambiwa kuwa kuna daktari mmoja kwa kweli sikuamini. Mmoja nilisikia alikuwa kamaliza shule Urusi na kuwekwa hapo, alilala mitini na kwa sasa yuko Mwanza. Na huyu anatokea mita chache kutoka Kitete. Ule mkoa kwa kweli uko nyuma kwa kila kitu. Watu wengi hufikiri Tabora ni ile enzi ya Tabora Jazz na Nyanyembe. Ukwelii ni kuwa tangu miaka hiyo, Tabora imebaki palepale. Sasa hapo ni Tabora, ukienda wilayani sanasana hospitali za Wamisheni kama Nkinga ya Pentecost Swedish, Sikonge ya Moravian nk.

Serikali sanasana husamehe kodi tu. Ukipotea kwa miaka kadhaa na kurudi unakuta watu wengi wamekufa sawa na idadi ya waliozaliwa. Wengi najua itakuwa hata vigonjwa vya kawaida kabisa. Ukiona Mzee kule ujuwe huyo jamaa DONGO lake si la kawaida.

Pana wakati kulikuwa na mjadala kwamba wakati wa uchaguzi Kikwete aliahidi kumsadia mtoto mmoja kupatiwa matibabu. Mtoto huyu alikuwa wa Sikonge. Wengine walisifia na wengine wakilaani kuwa anatoa SAMAKI badala ya NDOANO. Nafikiri hata ikiundwa tume, sidhani kama itasaidia.

Cha muhimu ni kuunda tume kuangalia Mkoa wa Tabora kwa ujumla. Something must be done kuuSUKUMA ule mkoa walau hatua kumi mbele. Ila unapoleta Wakuu wa Mikoa kama Ditopile ambaye alikuwa anakwenda Dar hata mkuu wake wa kazi hajui kwa kweli inakuwa kichekesho. Tena anakwenda kutanua huku akisema au wakisema "Mkoa wa Tabora acha tu wafe". Na kweli Wamekufa, wanakufa na wataendelea kufa.
 
SIkonge, unanikumbusha kwenye janga jingine lililotokea Singida ambapo gari lilipinduka na kuua watu kwa moto mkali. Ilikuwa si umbali sana toka Singida mjini. Tukaja kugundua kuwa Singida mjini (at the time) walikuwa hawana gari la kuzimia moto (fire truck). Wenye kupiga kelele tukapiga kelele.

Suala la Tabora siyo la ajabu kwa maana ya kwamba maendeleo yako DAr, Arusha, na baadhi ya mikoa (Mwanza) ni mmojawapo. Maendeleo ya vitu.

Kama tukio hili lingekuwa limetokea Bilicanas au mojawapo ya vilabu vyetu Dar, na mzazi mmoja ambaye ni Kigogo angekuwa amepoteza watoto wawili au watatu kelele zingepigwa sana. Wamekufa Tabora nani amekasirika? Watu wanaelekeza hasira kwa mtu ambaye amethubutu kumnyoshea mtu kidole. Watu hawa hawataki "mtu wao" anyoshewe kidole. Hawasikii hasira ya tukio hili at least angalau hawaoneshi hasira hiyo kama wanayo.

Kilichotokea Tabora kama kilichotokea MV. Bukoba, kama kilichotokea Dodoma (ajali ya treni), kama kilichotokea Mererani (karibu mara nne ndani ya miaka hii 7), kama kilichotokea Shauritanga, hakitukasirishi. Tuko tayari tumekinga mikono ya "mapenzi ya Mungu".

Hivi kweli hospitali ya Mkoa ina Daktari mmoja/wawili? Je kuna vifaa gani vya kutosha vya hewa pale. Hivi kama Taifa tunashindwa kuwa na minimum requirements za hospitali zetu. Kwamba:

a. Hospitali ya Mkoa lazima iwe na madaktari wasiopungua ishirini, mabingwa wasiopungua wanne (magonjwa ya watoto, kina mama, ya uambukizo na ya ndani);

b. Je tunashindwa kusema kuwa kikosi cha uokoaji cha mkoa lazima kiwe na angalau vifaa hivi na vile ambavyo viko katika standard hii 24 hours?

c. Kwamba mahali popote ambapo kuna mkusanyiko wa watu kila jengo limewekewa wingi wa juu wa watu wake na wakizidi Polisi wananguvu ya kuzuia watu kuingia?

d. Kwamba mahali popote kwenye ukumbi au makusanyiko ya hadhara kila penye watoto 10 lazima kuwe na angalau mtu mzima mmoja kuwaangalia?

Yote haya watu hawayafikirii. Bahati mbaya ni kuwa wengine tulipoandika kuhusu suala hili la kujiandaa kwa majanga tuliambiwa tunajifanya tunajua sana. Nilipoandika Aprili 16 kuhusu "Taifa lisiliojiandaa kwa majanga, limejiandaa kwa maafa" mtu mmoja aliandika na kusema hivi (kitu ambacho naona kinarudiwa humu leo hii):

"Hili jamaa linajifaya linajua kila kitu anafikiri Watanzania wote ******* mwenye akili yeye tu

na peter - 16.04.08 @ 12:40 | #6854"

Nilihitimisha makala hiyo kwa kusema hivi:

Niseme tena kuwa taifa lisilojiandaa kwa majanga, limejiandaa kwa maafa. Kama hatutaamua kubadilika sasa kabla ya majanga makubwa mbeleni, tusianze kulia kilio cha mbwa pale ambapo tutajikuta tunapata majanga mengine ambayo tungeweza kupunguza ukatili wake na watu watakapoanza kutoa udhuru wa kwanini wasibebe lawama.

Nimetoa changamoto, tujiandae!

Lakini unafikiri watasikia? Unafikiri watatilia maanani? Watakuja na kumshambulia Mwanakijiji!! Well, it doesn't solve the problem. Tutaendelea kutoa machozi kutokana na majanga haya ya kizembe hadi pale tutakapokubali kujiangalia na kunyenyekea kuukubali ukweli. Kwamba, Tanzania haijajiandaa kwa majanga hivyo imejiandaa kwa maafa.
 
The managers of the hall in central Tanzania where a disco stampede killed at least 19 children aged under 13 have been arrested and questioned by police.

Reports say as many as 400 children were packed into the hall, twice the recommended number.
...

Uroho wa pesa ndio umesababisha haya maafa. Ukumbi designed for 200 people unaenda kuweka watu 400. Halafu unamlalamikia aliyejenga jengo...

Upupu mwingine unaudhi kupita kiasi...
 
Uroho wa pesa ndio umesababisha haya maafa. Ukumbi designed for 200 people unaenda kuweka watu 400. Halafu unamlalamikia aliyejenga jengo...

Upupu mwingine unaudhi kupita kiasi...

Unaposema ulidizainiwa kwa watu 200 una maana ulidizainiwa kuwa ukumbi wa disko kwa watu mia mbili? na hivyo ulikuwa na vent ya kutosha kwa watu mia mbili wakicheza na kuruka ruka kwenye muziki?
 
taarifa iliyotolewa ni kuwa hiyo siyo fidia is just a condolence
 
I am sory, i wish wangekuwa wameokoka, sasa unajua kwa imani yangu, mtu akifa wakati hajampokea Bwana, ndo moja kwa moja motoni, sasa, sisi tuliobaki, tupate fundisho kuwa, sikikuu za kimungu kama hizi sio sikukuu za kufanya maovu. poleni wafiwa.ila hata tukiomba Mungu azilaze mahali pema roho zao, hatafanya hivyo, ni kujilisha upepo tu.
...Mnh!!! Hata watoto wadogo nao wanaingia motoni kwa dhambi gani? Mnafiki wewe!!!
 
Hivi, wale watoto waliokufa jana Tabora, unajua wengine wadogo sana, hivi walikuwa wanaenda wapi? watoto wadogo kama wale wanaweza wakawa wanaruhusiwa na wazazi wao kwenda disco? nijuavyo, disco ni sehemu za anasa na madhambi, hivi kuvifundisha vitoto vidogo kama vile, visichana vingine vina umri wa miaka kumi na mbili ndo vinaanza kuwa saa sita vituani mwao, wengine wadogo kabisa, mzazi gani mbumbumbu kama huyo anaweza akawaruhusu watoto wake waende kwenye uchafu kama huo? hebu watz tujifunzeni kulea watoto vizuri jamani, unajua unavyo mueksipozi mtoto kwenye mazingira ya kishetani, ndivyo shetani anavyoweza akamchinja na kumuua kama ilivyokuwa kazi yake, hivyo, sisi ambao tumebakiwa na watoto, hebu tuwafundishe watoto maadili mema na tuwe na akili za kuwakuza watoto kuchukia mambo machafu kama ya disco na mengine, ili waishi. ndo maana watoto wadogo siku hizi wanapata ukimwi, kwasababu there is no closer look toka kwa wazazi wao, wanawaacha wanajifanyia mambo kama kuku wa kienyeji unaowaacha waende kula vichakani na jioni warudi home kulala. Je, tunajifunza nini na watoto kwenda madisco? ni uchafu huu, there is no faida yoyote. think about that.
 
Personally nilikuwepo ukumbini, nina watu wangu wanaofanya shughuli zakibiashara hapo, inasikitisha sana, inauma sana, inatisha, miili 16 imezikwa jana wawwili leo na mmoja nasafirishwa leo kwenda Kigoma kwa mazishi
 
hiyo ina hasiria jinsi gani maadili hakuna,mambo ya dico toto tangia zamani yalikuwepo ila je tunajifunza nini kuwepo kwa haya? ni maadili? au ndio wakati wazazi nao kujipatia muda wao nao wafurahi wenyewe kwa kuwapeleka watoto huko? maswali ni mengi tu nafikiri ila hii ni fundisho tayari...
 
Nasikia ivyo vifo vimetokana na bifu za wafanyabiashara wa kumbi za jirani ati kisa jamaa ana make kupita kiasi.
Cha kushangaza under normal circumstance out of suffocation watu 19 hawawezi kufa ghafla vile.
Anyway tusubili tume
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom