Mambo 42 kuhusu kabila la Wamatengo

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,529
14,421
_____________________

1.Wamatengo ni kabila la watu wanaoishi na wenye asili ya mji wa Mbinga, katika mkoa wa Ruvuma.

2.Kabila hilo linasifika kwa ukarimu na uhodari wa kazi.

3. Wamatengo wanapenda kuishi sehemu za milimani katika eneo lenye hali ya hewa nzuri na rutuba inayowawezesha kushiriki katika shughuli za kilimo cha mazao kama mahindi, maharage na mihogo, lakini pia ni wakulima mahiri wa mazao ya biashara (kahawa) na shughuli za ufugaji.

4.Pia wanafuga wanyama mbalimbali kwa madhumuni tofauti. Kondoo, Ng’ombe na Sungura wanafuga kwa ajili ya kitoweo, kuku kwa ajili ya tambiko na mahoka.

5.Katika mgawanyo wa kazi, wanawake wanashughulika na kilimo, lakini wanaume na vijana wa kiume kwa asili shughuli yao kubwa ni kuchunga wanyama mchanganyiko,kazi na biashara.

6.Chakula cha asili cha Wamatengo ni ugali wa mahindi na mboga za majani au maharage.

Pia wanakula maboga na viazi vitamu. Mihogo na ulezi wanatumia kutengenezea pombe, hususan wakati wa njaa.

7.Katika mfumo wa maisha ya zamani, Wamatengo hawakupenda vyakula vya ngano na kahawa kwa kuamini kwamba vimeletwa na wakoloni, lakini sasa mfumo wa maisha umebadilika na wanatumia kama wanavyotumia vyakula vingine.

8.Baadhi ya Wamatengo waliishi mapangoni hasa wakati wa vita, lakini sasa wamejenga nyumba za mitindo ya kisasa na ukubwa tofauti sehemu za milimani ambapo Baba, Mama na Watoto huishi nyumba moja na mifugo hujengewa banda lao.

9.Kiasili nyumba za Wamatengo ni za miti ambazo hukandikwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi.

10.Nyumba zao ni maarufu kama mgongo wa tembo na pia hujenga nyumba za msonge.

11.Nguo za asili za Wamatengo huitwa mbinda na zilitengenezwa kwa kutumia miti inayoitwa mitawa.

Miti hiyo ilikatwa kisha kutolewa magamba ambayo yalipondwapondwa kisha yakalowekwa mtoni kwenye maji yenye matope meusi kwa muda wa siku moja hivi.

12.Vazi la asili la wanawake liliitwa mpati. Walilifunga kiunoni kisha wakachukua kipande cha vazi lililotengenezwa kwa magome ya miti na kulipitisha katikati ya miguu ili kufunika makalio na sehemu ya siri.

13.Wanaume pia walivaa vazi hilo kwa kufunika sehemu nyeti pekee.

14. Wamatengo ni wakarimu kwa kupokea na kumpa mgeni malazi na chakula.

Ikiwa mgeni ni ndugu hukalishwa mkekani, huchinjiwa kuku na hupewa nyama yote na ugali kama heshima.

Mgeni akishindwa kumaliza nyama ‘yake’ huzichukua na kupeleka nyumbani kwake.

15.Baadhi ya wageni hasa wakwe (wayemba) walipewa heshima ya kipekee kwani walitengenezewa pombe na kuchinjiwa mbuzi.

16. Wamatengo hawampi mgeni yeyote chakula chochote kabla hawajaonja wenyewe kwanza. Mathalani ugali, mwenyeji humega tonge moja na kula kama ishara ya kumhakikishia mgeni kuwa chakula ni salama kisha humkaribisha na kumwacha aendelee kula peke yake.

17.Pia wana desturi ya kuonja kinywaji kabla ya kumpa mgeni.

18.Ingawa wajibu wa kupika kwa asili ni wanawake, lakini wanaume wa Kimatengo hadi leo hupenda ama tuseme si ajabu kushirikiana na wake zao kupika.

19.Asilimia kubwa ya Wamatengo wa siku hizi wameachana na utamaduni huo ingawa bado upo kwa baadhi ya wanafamilia walioshika mila hasa sehemu za Vijijini.

20. Wamatengo wa kale waliamini kuna Mungu na walitumia njia mbalimbali kuwasiliana naye.

21.Wamatengo pia walitegemea msaada kwa ndugu zao marehemu (mahoka) kwa kuwa waliamini baada ya kuaga dunia wafu walikwenda kukaa karibu na Mungu.

22. Kijana wa kiume anapobalehe wazazi humshawishi atafute mwenza. Kijana huaambiwa kwa Kimatengo “namu henu mpali mwotu gwiono”, wakiwa na maana sasa tafuta jiko lako, wewe sasa ni mkubwa kutosha kuoa.

23. Zama hizo ilikuwa sio rahisi kumpata mchumba kwa sababu wasichana walikuwa hawaruhusiwi kwenda shule wala kukusanyika katika matamasha kama ilivyo sasa.

24.Michezo ya matanga, ngoma maarufu kwa jina la mhambo ni sehemu ambazo vijana walikutana na kuweza kuchumbiana.

25. Kijana wa kiume humpa msichana unyasi, udodi au ushanga kama ishara ya kuomba uchumba, hivyo msichana alikuwa na hiari ya kupokea ama kukataa.

26.Endapo msichana anapokea naye humpa mvulana mojawapo akikubali vitu hivyo kama ishara ya kutokuvunja ahadi ya uchumba huo.

27.Mahari yaliyotolewa kwa familia ya binti ni jembe moja, mbuzi watano na kipande cha nguo cha (mbinda) kwa ajili ya mama mzazi, nguo ambayo hivi sasa inajulikana kama mkaja wa mama.

28.Tofauti na makabila mengine, Wamatengo hawafanyi sherehe yoyote wakati wa kushika uchumba wala siku ya harusi.

29.Baada ya bwana harusi kukamilisha mahari, shangazi wa bibi harusi humpeleka mwali kwa mchumba wake na kumkabidhi bwana harusi na kuwaruhusu kuanza maisha ya ndoa.

30. Mila na desturi za wamatengo zinataka Shangazi kuishi na wanandoa wapya na kuwaelekeza mambo muhimu katika ndoa.

Shangazi alilala chumba kimoja na wanandoa hao na kufuatilia mwenendo wa wanandoa hao wapya ili aweze kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa kama bibi harusi alikutwa na bikira au la (yalifanyika zaidi zamani siyo siku hizi).

31. Mabadiliko ya mfumo wa maisha yameondoa baadhi ya vipengele kwani Wamatengo wanafanya sherehe ya harusi na shangazi wa bibi haruhusiwi kuingia chumbani kwa maharusi.

32. Ikiwa mvulana atamchukua msichana bila kufuata utaratibu kwa Kimatengo (makunja) washenga hupeleka kuku au mbuzi kwa wazazi wa msichana kuwataarifu na baadaye hulipa mahari kwani bila kufanya hivyo mvulana na msichana wanabaki kuwa wachumba na kama mtoto akizaliwa kipindi hicho huwa mali ya wazazi wa msichana.

33.Wanaume wa Kimatengo walioa mke zaidi ya mmoja kwa kuwa wanapenda kuwa na watoto wengi.

34.Katika tamaduni za Wamatengo Mama akiwa mjamzito wa miezi mitatu hutengwa na hukaa nyumba ya peke yake hadi atakapojifungua.

Walifanya hivyo kama ishara ya kuboresha afya ya mama na mtoto kwa kuwa waliamini kuwa mjamzito akijumuika na watu wengine anaweza kupatwa na magonjwa ambukizi, kuangaliwa vibaya na watu au kumkasirisha mama mjamzito.

35.Mara baada ya kujifungua mama mzazi alitunzwa na mkwe mpaka kitovu cha mtoto kipone.

Akishapona hufanyiwa tambiko maalum. Kwanza huogeshwa kwa maji yaliyochanganywa na dawa maarufu kwa jina la mbatabata, kisha hunyolewa na kusubiri taratibu za kutolewa nje.

36.Siku ya mtoto kutolewa nje mama wa baba wa mtoto hulowanisha mbatabata kisha huchukua dawa nyingine iitwayo luhamu na kuichomeka juu ya paa la nyasi sehemu ya mlangoni na kusubiri jua lichomoze.

37.Kipindi za uzazi mke hujitenga na mumewe kitendo kinachojulikana kama 'masegati' kwa lugha ya Kimatengo.

Mtoto anapofikisha miezi sita hupewa uji maarufu kama ukoba ambao hutengenezwa kwa unga wa ulezi na kinywaji kiitwacho nimbi ambacho ni togwa ya watoto wachanga.

38.Wamatengo wanawalea watoto katika maadili na kazi, Mama kumfunza binti kazi mbalimbali za kilimo pamoja na za nyumbani kama kupika, kuokota kuni, kufua na kufinyanga vyungu.

39.Wanaume wanakutana sehemu inayoitwa pasengu kupeana mawaidha na mafunzo kama jinsi kuchunga na kuwinda.

40.Msichana anapofikia umri wa kuvunja ungo anamwambia shangazi yake na shangazi huwafikishia wazazi taarifa na kumweka binti ndani kwa muda wa mwezi hadi miezi sita kabla ya kuchezwa unyago.

41.Wamatengo wanaamini mtu akifa roho yake huchukuliwa ahera kuishi maisha mengine. Roho hizo huitwa mahoka na huwa na uhusiano na watu wanaoishi duniani.

42.Wamatengo kabla ya mauti wanasamehe, kupatana na wagomvi na kulipa madeni.
43….. Ongeza……
__________________
MAREJEO
1.”Historia, mila na desturi za Wamatengo,” (Egino Ndunguru)
2. “The Death of Mganda?: Continuity and Transformation in Matengo Music,” (Stephen Hill), Vol. 48, No. 4, Musical Performance in Africa (Winter, 2001), pp. 27-41(Inidiana University Press)
3.KamusiElezoHuru
 
Yes mkuu naunga mkono hoja yako, na hope's ile kahawa yao itawatoa kwenye umasikini, ni moja ya kahawa bora kabisa hapa duniani, dhahabu hii isiachiwe royal families pekee kunufaika nayo
 
Ni watu ambao wanatabia za kipuuz mfano akimwona mwenzie kavaa nguo, na akamtajia bei ya nguo husika bas nae huenda dukan na kusema nipatie nguo ya bei flani akimaanisha aliyoiona kwa jamaa yake hata kama mwenzake alipigwa yeye hajali Pia nawasifu ni watu wa kuigana sana ukinunua gari na yey mwakan lazima anunue,, kama ulikuwa unasikia maji hayapandi mlima lakin ukienda umatengoni utakuta maji yanatolewa chini na kupitishwa juu ya milima na kwa kas ya ajabu
 
Wanafuga na kuchunga nguruwe zaidi.
 
Back
Top Bottom