Watoto 19 wafa kwenye disco la Idi Tabora

Nasikia ivyo vifo vimetokana na bifu za wafanyabiashara wa kumbi za jirani ati kisa jamaa ana make kupita kiasi.
Cha kushangaza under normal circumstance out of suffocation watu 19 hawawezi kufa ghafla vile.
Anyway tusubili tume

Kesho ukisikia gerezani Keko au Segerea wamekufa kwa suffocation itakuwa BIFU ya serikali na......???
 
Kumbe mauaji ya watoto Tabora yangeweza kuepukwa
Victor Kinambile, Tabora na Kizitto Noya

KAMA mamlaka za mkoa mkongwe wa Tabora zingejua kusoma alama za nyakati, basi maafa ya watoto 19 kwenye ukumbi wa Bubbles Night Club yaliyotokea siku ya Iddi Mosi, yasingetokea.

Ukumbi huo ulishapata hitilafu kwa miaka miwili mfululizo na kusababisha watoto kadhaa kuzirai, lakini wakanusurika kifo, lakini hakukuwepo na hatua zozote thabiti zilizochukuliwa kuepusha uwezekano wa maafa kabla ya msiba huo mkubwa wa kitaifa.

Watoto hao, waliofariki kwa kukosa pumzi na kukanyagana, walizikwa jana mjini Tabora na Kigoma.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, aliwaambia waandishi wa habari njana kuwa ukumbi huo, ulio katika jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ulianza kuwa na hitilafu tangu mwaka 2006 wakati watoto 26 walipopata tatizo kama hilo, lakini wakaokolewa na kukimbizwa hospitalini ambako maisha yao yaliokolewa.

Siku hiyo pia ilikuwa ni siku kuu ya Idd el Fitr.

Mwaka jana, tukio kama hilo lilitokea kwenye ukumbi huo na watoto wapatao 14 walidhurika kutokana na hitilafu kama hizo na wakakimbizwa haraka kwenye Hospitali ya Mkoa ya Kitete, ambako kwa mara nyingine madaktari walifanya kazi ya ziada kuokoa maisha yao.

Miongoni mwa walionusurika alikuwemo mtoto wa mbunge wa viti maalum Tabora, Mwanne Mchemba.

"Mkoa uliunda tume iliyowashirikisha watu muhimu kutoka katika makundi mbalimbali muhimu ya kijamii, lakini mpaka linatokea tukio hili tume ilikuwa haijatoa ripoti," alisema Mwinyimsa.

Mkuu huyo wa mkoa hakutaja watu waliokuwemo kwenye tume hiyo na kama ripoti yake walikuwa wakiitarajia lini.

Mji wa Tabora ulikuwa umekumbwa na simanzi baada ya watoto hao waliokosa hewa baada ya viyoyozi viwili vilivyo kwenye ukumbi huo wa disko, ambao ulijengwa ili utumike kwa mikutano, kuzima ghafla. Inasemekana kutokana na umeme kuzima na viyoyozi kushindwa kufanya kazi, watoto walikosa hewa na baadaye kukanyagana wakati wakijaribu kujiokoa na hivyo kusababisha maafa hayo.

Jengo hilo linamilikiwa na NSSF na awali ukumbi unaotumiwa kwa disko ulikuwa maalum kwa ajili ya mikutano, ambayo huchukua watu wachache, lakini uligeuzwa na kuwa wa burudani na hivyo kufunikwa sehemu za kutolea hewa ili kuzuia sauti kutoka nje.

Shirika hilo la hifadhi ya jamii, lilikuwa la kwanza miongoni mwa watoa ubani baada ya kutoa ubani wa Sh 500,000 kwa kila familia iliyopoteza mtoto na Sh100,000 kwa kila familia ambayo iliathirika, ahadi ambazo pia zilitolewa mapema kabisa na Rais Jakaya Kikwete, ambayo aliahidi viwango hivyo kwa familia zilizoathirika.

Wakati huohuo, Mwinyimsa alisema Jeshi la Polisi mkoani Tabora, linawashikilia wakurugenzi wawili na mameneja waliokuwa wakiendesha disko toto katika siku hiyo ya Idd.

Aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wakurugenzi hao na mameneja wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa na polisi kuhusu chanzo cha tatizo lililosababisha watoto hao kupoteza maisha.

Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni mkurugenzi wa disko hilo, Oneten Teck, Projestus Fidelis na meneja wake Jaffar Rashid. Wengine ni mkurugenzi wa Bubbles Night Club, Shashikant Manji Patel na meneja wake Vituko Salala.

Alisema jeshi hilo limempa taarifa rasmi ya kushikiliwa kwa watu hao, huku likimuarifu kwamba walinzi wa milangoni katika madisko hayo mawili "mabaunsa", nao wanasakwa ili waweze kuhojiwa kuhusu sakata hilo.

Alisema wakurugenzi hao watahojiwa pia na tume huru iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mkasa huo, ambayo alisema imeanza kazi jana na kuwataka wananchi watoe ushirikiano kwa tume hiyo ili iweze kupata taarifa za ukweli zitakazofanyiwa kazi na serikali.

Akizungumzia watoto waliokuwa bado wamezirai hospitalini, alisema wamepatiwa huduma nzuri za afya na kwamba wote wamelazwa wodi za daraja la kwanza.

Alisema vijana wanne waliruhusiwa mara baada ya maendeleo ya afya zao kuwa nzuri na kuwataja vijana hao kuwa ni Msimu Rehani, Sakina Alli, Kulwa Idd na Tatu Hamad, huku akibainisha kuwa vijana wawili bado wako hospitalini ambao ni Jumanne Mashaka na Naomi

Joseph.

Naye Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Prof. Juma Kapuya

alisema kuwa serikali itachukua hatua madhubuti dhidi ya wote

watakaobainika kuhusika katika kadhia hiyo, na kueleza kuwa nia ya

serikali ni kuona tukio hilo lililotekea Tabora, halijirudii tena wala

kutokeza katika sehemu nyingine hapa nchini.

Hadi kufikia jana, idadi kamili ya watoto waliokuwa kwenye kumbi hizo mbili za disko haijajulikana na imebainishwa kuwa idadi hiyo itajulikana baada ya tume iliyoundwa kukamilisha kazi yake.

Wakati huohuo, mazishi ya watoto waliokufa kwenye ukumbi huo yalianza juzi jioni na baadhi kuzikwa jana mjini hapa, huku miili

ya watoto wawili ikisafirishwa kuelekea Kigoma na Goweko.

Mazishi ya watoto hao yamevuta umati wa wakazi wa Tabora.

Mkazi mmoja, Sheikh Ali Kondollah, akizungumza mara baada ya maziko ya ndugu wawili - Mwanahamis Waziri na Hadija Waziri- yaliyofanyika Rufita, aliitaka serikali iharakishe kutoa ripoti ya uchunguzi wa tume na kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika kwani wananchi wanahitaji kuona hatua zikichuliwa badala ya kuwepo kwa mlolongo wa tume zisizokuwa na majibu.

Nacho Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kulisema maafa hayo ni matokeo ya ufisadi unaotokana na uporaji wa viwanja vya wazi.

Mkurugenzi mtendaji wa Tamwa, Ananilea Nkya alisema jana kuwa watoto wamekosa maeneo ya wazi ya kucheza kutokana na viwanja vingi kuporwa na mafisadi na kubadilishwa matumizi.

Alisema Tamwa inaamini kwamba watoto wa Tabora waliokufa ama kuumia kwa kukosa hewa hawakupaswa kucheza disko ndani ya kumbi za starehe na badala yake wangeweza kucheza kwenye eneo la wazi lililoandaliwa kwa shughuli hiyo.

"Tamwa tunaamini kuwa kuvamiwa kwa maeneo ya wazi na hasa mijini kunatokana na kushamiri kwa vitendo vya ufisadi hasa rushwa na uroho wa watu wachache waliopewa mamlaka katika ngazi za serikali za mitaa, kata, halmashauri na wizara inayohusika na ardhi," alisema.

Kwa mujibu wa Nkya, katika miaka ya hivi karibuni rushwa na ufisadi vimechangia maeneo mengi yaliyotengwa kwa ajili ya viwanja vya michezo na burudani hasa mijini, kugeuzwa viwanda vidogo, gereji, mabaa, migahawa, maduka, hoteli na vituo vya mafuta.

Alisema kutokana na hali hiyo watoto mijini wamekuwa hawana mahala pa kucheza badala yake wanalazimika kutumia haki yao ya msingi kucheza katika maeneo hatari ikiwamo barabarani na kwenye kumbi za starehe.

"Tunawaomba Watanzania wote tutafakari ni watoto wangapi wamepoteza maisha yao kwa kugongwa na magari wanapokuwa wakicheza barabarani? Watoto wangapi wanafanyiwa vitendo vya kikatili kama vile kubakwa kutokana na kucheza kwenye baa ambazo nyingi ziko katikati ya maeneo ya makazi ya watu," alihoji.

"Sisi Tamwa tunaamini serikali ikitaka kuhakikisha janga kama hili la Tabora halitokei tena nchini kwetu, basi ihakikishe kuwa viwanja vyote vilivyotengwa kwa ajili ya shughuli za umma mijini na vijijini, vinarejeshwa hata kama waliopora watakuwa wamejenga vitega uchumi vyenye thamani kubwa ya fedha."

Source : Mwananchi

Kumbe tatizo lilikuwa linajulikana siku nyingi, ila inawezekana watu kwa kutokujali au kupenyezea kitu kidogo ripoti ya tukio la kwanza mpaka leo haijatoka....na sasa wameunda tume nyingine kufanya kitu kile kile ambacho kwa sasa kilitakiwa kiwe kimerekebishwa.
 
Siri zaidi za maafa Tabora zaanikwa

BAADHI ya watoto walionusurika kifo katika ukumbi wa Bubbles Night Club siku ya Idd mosi ambako wenzao 19 walipoteza maisha, wamesema wanaamini ulevi wa baadhi yao ulisababisha janga hilo.

Watoto hao walisema pia kwamba tathmini yao inaonyesha kwamba waliokuwamo ndani ya ukumbi siku hiyo walikuwa kati ya 1,000 hadi hata 1,500.

Uwezo wa ukumbi huo ambao ulijengwa kwa ajili ya mikutano ni kuhudumia watu wazima 150.

Mmoja wa watoto hao akizungumza na waandishi wa habari kwenye maziko ya rafiki yake ambaye walikuwa naye disko siku hiyo, Said Sudy (12) alisema kutokana na wingi wao siku hiyo walishindwa hata kucheza muziki kikamilifu.

Said alisema siku hiyo ya tukio, mabaunsa wa ukumbi huo walikuwa wakimlazimisha kila mtoto aliyekuwa anaingia ukumbini kununua pombe kali aina ya Simba Gin.

Mtoto huyo alieleza kuwa kutokana na baadhi yao kulewa pombe hiyo, kabla ya tafrani walionekana kutapika ovyo na kusababisha harufu kali na joto kuongezeka maradufu ukumbini.

Alisema inawezekana baadhi ya watoto hao waliokuwa wamelewa walishindwa kujiokoa wakati hali ilipozidi kuwa mbaya.

Polisi inaendelea kuwatafuta mabaunsa hao ambao walikimbia baada ya tukio hilo na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humu, Daud Siasi, amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwanasa.

Wakati huo huo, Tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha tukio hilo ilianza kazi jana kwa kuwahoji watu wanne wanaoshikiliwa na Polisi kuhusu tukio hilo. Leo tume hiyo itakutana na watoto waliokuwa eneo la tukio.

Taarifa zinasema tume hiyo itakutana na watoto hao kuanzia saa nane mchana katika eneo la Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini hapa.

Mwito umetolewa kwa wazazi au walezi wa watoto hao kuwaruhusu kufika katika eneo hilo kwa lengo la kuisaidia ikamilishe uchunguzi huo ilioagizwa iumalize katika wiki moja.

Mapema jana miili ya watoto wawili wa familia moja, Donald Kasele (12) aliyekuwa akisoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Milambo Barracks na Jacob Gerad (12) ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Tambukareli imesafirishwa kwenda Tarime mkoani Mara kwa maziko.

Bado tukio hilo limekuwa gumzo mjini hapa.

Source: Habari leo
 
Unaposema ulidizainiwa kwa watu 200 una maana ulidizainiwa kuwa ukumbi wa disko kwa watu mia mbili? na hivyo ulikuwa na vent ya kutosha kwa watu mia mbili wakicheza na kuruka ruka kwenye muziki?

Kwanza pongezi kwa MODS kwa kubadilisha kichwa cha thread na kufunga multiple threads ulizozitengeneza kwa kitu kilekile (sikutegemea utoto ule!).

MMkijiji, sioni sababu ya wewe kung'ang'ania ubishi ambao hauna msingi. TOYOTA wakupe gari la kubeba tani 2, wewe ubebe tani 4 halafu uwashtaki? Utakuwa ujuha. The same applies to Ukumbi.

Tunajua kuna residential na commercial premises. Mpangaji wa commercial property anaweza kuamua kufanya partitions kwa ajili ya ofisi nk kutegemea na mahitaji yake...na kuna vyombo(manispaa?) ambao hupitisha jengo hilo kutumika kwa biashara husika na kutoa leseni ya biashara.

Huo ukumbi unaokuwa designed kama DISCO unafuata building codes gani za Tanzania? Nasikitika kwamba unabishana ubishi usiokuwa wa msingi bali wa ILI MRADI mtu uliyemtarget awe victim.

Mbowe amechukua commercial block pale mjini na yeye kama tenant (sio NHC mind you) ndio anayefanya interior decorations and planning ya disco NA ni manispaa ndio watampa leseni kutegemea na vigezo watavyovihitaji katika ukumbi huo. Sio NHC watakaompa leseni...

Kwa kumalizia tu...hata kama manispaa watampa leseni ya kuingiza watu 500 at a time. Yeye akiingiza watu 1000, huwezi tena kurudi na kusema kwa nini walimpa leseni. Watakuwa wamempa leseni lakini yeye ameivunja kwa kujaza zaidi ya leseni.

MMkijiji, hapa tunabishana kwa hoja na hakuna ugomvi. Wewe ulikuwa wrong kumtarget mtu asiyehusika, simply coz you wanted to settle a score.
 
That is the most ridiculous analogy ever; "wakupe" for free? Ukininunua kuna vitu vinaitwa warranty; na kama wakikupa kitu ambacho ni kibovu na wewe ukatumia na janga likakukuta wao watawajibika. HUjawahi kusikia makampuni ya magari yanapofanya recalls?

True, lakini mpangaji hawezi kufanya chochote kile nje ya mkataba na akifanya hivyo na mmiliki hakupinga au kutoa his consent in writing basi kuna kuwajibika endapo jambo litatokea hasa ikithibitika kuwa mmiliki alikuwa na taarifa za mabadiliko hayo.

Huo ukumbi unaokuwa designed kama DISCO unafuata building codes gani za Tanzania? Nasikitika kwamba unabishana ubishi usiokuwa wa msingi bali wa ILI MRADI mtu uliyemtarget awe victim.

Yaani kwako wewe victim ni "mtu" niliyemtageti na watoto waliokufa kule unawaita nani? Au hata hufikirii in terms of this "victimhood"?

Mbowe amechukua commercial block pale mjini na yeye kama tenant (sio NHC mind you) ndio anayefanya interior decorations and planning ya disco NA ni manispaa ndio watampa leseni kutegemea na vigezo watavyovihitaji katika ukumbi huo. Sio NHC watakaompa leseni...

Akifanya mabadiliko nje ya kile anachoweza kufanyia mabadiliko na janga likatokea tutamwajibisha yeye, na ikijulikana NHC waliacha mtu afanye mabadiliko kwenye majengo yao nje ya mkataba na kufanya shughuli ambazo hazikuwa zimekubaliwa, basi na wao watakuwa liable.

Kwa kumalizia tu...hata kama manispaa watampa leseni ya kuingiza watu 500 at a time. Yeye akiingiza watu 1000, huwezi tena kurudi na kusema kwa nini walimpa leseni. Watakuwa wamempa leseni lakini yeye ameivunja kwa kujaza zaidi ya leseni.

Kama walimpa leseni na yeye akafanya hivyo na wao wanajua kuwa aliingiza watu zaidi ya leseni yake inavyoruhusu, na hawakuingilia kati kusitisha leseni hiyo na watu wakadhuruka basi watoa leseni nao wanawajibika; na hilo haliondoi kuwajibika kwa waliochezesha disko hilo. Huwezi kuona hilo?

MMkijiji, hapa tunabishana kwa hoja na hakuna ugomvi. Wewe ulikuwa wrong kumtarget mtu asiyehusika, simply coz you wanted to settle a score.

Kwanini unafikiri Dr. Dau ni mtu "asiyehusika"? Sina scores kusettle kwani kwenye both counts ya THI the Appellate Court sided with my position so baada ya kupoteza hoja ile labda mtu mwingine anamtetea Dr. Dau to settle scores siyo mimi.

Na hakuna mahali popote ambapo nimesema lolote dhidi ya Dr. Dau character, education, personhood, or kumuita jina lolote ambalo si lake. Ni kuwalaghai watu kuwa hoja zangu zimemtegeti "mtu". Hoja zangu zimemmlenga Mkurugenzi wa NSSF who happened to be Dr. Ramadhani Dau. Na hazikuishia hapo.
 
Kwanza pongezi kwa MODS kwa kubadilisha kichwa cha thread na kufunga multiple threads ulizozitengeneza kwa kitu kilekile (sikutegemea utoto ule!).

MMkijiji, sioni sababu ya wewe kung'ang'ania ubishi ambao hauna msingi. TOYOTA wakupe gari la kubeba tani 2, wewe ubebe tani 4 halafu uwashtaki? Utakuwa ujuha. The same applies to Ukumbi.
That is the most ridiculous analogy ever; "wakupe" for free? Ukininunua kuna vitu vinaitwa warranty; na kama wakikupa kitu ambacho ni kibovu na wewe ukatumia na janga likakukuta wao watawajibika. HUjawahi kusikia makampuni ya magari yanapofanya recalls?

That is the stupidiest argument ever, we are arguing on "wakupe" au ununue?! The issue is you rented something that was designed for 200 and you put 400 and go back and complain to those who designed it for 200. Unarukia kwenye warranty?! You are all over the place...blind man fleeing :)

True, lakini(?) mpangaji hawezi kufanya chochote kile nje ya mkataba na akifanya hivyo na mmiliki hakupinga au kutoa his consent in writing basi kuna kuwajibika endapo jambo litatokea hasa ikithibitika kuwa mmiliki alikuwa na taarifa za mabadiliko hayo.

Again you are given something for 200 and you put 400. Who has breached contract? The one who gave you something for 200 or YOU who decided to put 400?!

Yaani kwako wewe victim ni "mtu" niliyemtageti na watoto waliokufa kule unawaita nani? Au hata hufikirii in terms of this "victimhood"?

Victim ni yule anayebeba lawama ambazo sio zake. The kids are victims, YES! But not victim coz of DAU! You are purposely steering away from the issue at hand.

Akifanya mabadiliko nje ya kile anachoweza kufanyia mabadiliko na janga likatokea tutamwajibisha yeye, na ikijulikana NHC waliacha mtu afanye mabadiliko kwenye majengo yao nje ya mkataba na kufanya shughuli ambazo hazikuwa zimekubaliwa, basi na wao watakuwa liable.

shughuli ni commercial purpose. Sasa iko nje ya mkataba?

Kama walimpa leseni na yeye akafanya hivyo na wao wanajua kuwa aliingiza watu zaidi ya leseni yake inavyoruhusu, na hawakuingilia kati kusitisha leseni hiyo na watu wakadhuruka basi watoa leseni nao wanawajibika; na hilo haliondoi kuwajibika kwa waliochezesha disko hilo. Huwezi kuona hilo?

Nani anawajibika, manispaa aliyetoa leseni ya watu 200? Au mchezesha disko aliyevunja leseni na kuingiza watu 400? You can do better than this...

Kwanini unafikiri Dr. Dau ni mtu "asiyehusika"? Sina scores kusettle kwani kwenye both counts ya THI the Appellate Court sided with my position so baada ya kupoteza hoja ile labda mtu mwingine anamtetea Dr. Dau to settle scores siyo mimi.

Read again...

Na hakuna mahali popote ambapo nimesema lolote dhidi ya Dr. Dau character, education, personhood, or kumuita jina lolote ambalo si lake. Ni kuwalaghai watu kuwa hoja zangu zimemtegeti "mtu". Hoja zangu zimemmlenga Mkurugenzi wa NSSF who happened to be Dr. Ramadhani Dau. Na hazikuishia hapo.

HOJA zako zimelenga kuspin blame kwa Dr Dau. Period!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom