Watoto 19 wafa kwenye disco la Idi Tabora

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kuna taarifa ya vijana 19 kufa na 17 kujeruhiwa vibaya katika ukumbi flani ambao sijapata jina lake ni katika sherehe za Eid huko Tabora. Kwa kirefu tutawaletea.

Mungu azipumzishe roho za marehemu mahala pema!
 
Mungu apumzishe roho zao mahali pema. Tunawaombea walioumia, wapate nafuu haraka.
 
Mungu, azipokee roho zao na kuzipumzisha kwa amani, milele!

Furaha zinageuka kuwa vilio ... inasikitisha sana!
 
Mungu apumzishe roho zao mahali pema. Tunawaombea walioumia, wapate nafuu haraka.
Inasikitisha sana, imetokea tukiwa katika matengenezo muhimu kwa JF, lakini naamini ujumbe umefika.

Ni katika jengo la NSSF, kwenye ukumbi wa disko. Inadaiwa hewa ilikuwa ndogo sana na walibanana sana ndani ya ukumbi.
 
Mwenyezi Mungu awajaalie walioumia kupona.

Mwenyezi Mungu apokee roho za waliofariki katika makao yake. Amen
 
Huo ukumbi naujua! Mungu awajaalie subira wafiwa na waliojeruhiwa awajaalie kupona, amin, amin, amin.
 
Huo ukumbi naujua! Mungu awajaalie subira wafiwa na waliojeruhiwa awajaalie kupona, amin, amin, amin.

Unaweza kutupa description ya ukumbi huo kwani kuna lawama zinaangukia watu bila taharifa za kutosha.
 
Inasikitisha sana, imetokea tukiwa katika matengenezo muhimu kwa JF, lakini naamini ujumbe umefika.

Ni katika jengo la NSSF, kwenye ukumbi wa disko. Inadaiwa hewa ilikuwa ndogo sana na walibanana sana ndani ya ukumbi.

Siku za sikukuu kubwa Tanzania kama Xmas na Idd haifai kabisa kwenda kujirusha maana hata wasiokuwa na kawaida ya kujirusha nao wanataka kujirusha siku hizo matokeo yake kila sehemu ya starehe inakuwa inafurika mpaka inatapika. Likitokea tatizo kidogo tu la watu kutaka kukimbia basi maafa yatakayotokea ni makubwa mno. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na awape wafiwa subira na faraja katika kipindi hiki kigumu kwao.

Idd: Watoto 14 wafa kwa kukanyagana

na Yusuph Magasha, Tabora
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

ZAIDI ya watoto 14, wamefariki dunia baada ya kukosa hewa na kukanyagana ndani ya ukumbi wa starehe wa Babol's Night Club, wa mjini hapa.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka mjini Tabora, zilisema kuwa vifo hivyo vilitokea jana na vimetokana na watoto wengi kuingia ndani ya ukumbi huo kuliko uwezo wake.

Kiongozi mmoja wa ukumbi huo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kuwa zaidi ya watoto 50 walitolewa ndani ya ukumbi huo na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora wakiwa wamepoteza fahamu na watoto alioshuhudiwa kupoteza maisha, walifikia 14.

Akifafanua jinsi tukio hilo lilivyokuwa, kiongozi huyo alisema jana kulikuwa na watoto wengi walioruhusiwa na wazazi wao kuja kusherehekea sikuku ya Idd el Fitri ambapo kulikuwa na ‘Disco Toto' ndani ya ukumbi huo.

Alisema watoto hao waliwazidi nguvu walinzi waliokuwa wakisimama mlangoni na matokeo yake, walikuwa wengi kuliko uwezo wa ukumbi.

"Inawezekana walinzi waliwaachia au watoto waliwazidi nguvu, hivyo waliingia kwa wingi na kuanza kukanyagana," alisema kiongozi wa ukumbi huo.

Kutokana na idadi yao kuwa kubwa, watoto hao walianza kukosa hewa na hivyo kukanyagana wakihaha kutoka, ndipo baadhi yao walipoteza fahamu na kupoteza maisha.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini (DC), Moshi Mussa, alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo, lakini hakuweza kutaja idadi ya watoto waliokufa, kwani ndiyo kwanza alikuwa anafika hospitalini hapo.

"Tukio ni la kweli, lakini nisubiri nitakupa taarifa kamili baadaye, maana ndiyo nipo hospitalini hapa," alisema DC huyo. Naibu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Daud Siasi, alithibitisha kutokea kwa tuko hilo na kwamba alikukuwa akilifuatilia zaidi ili aweze kutoa taarifa kamili.

Hata hivyo mmiliki wa ukumbi huo ulioko katika jengo la NSSF, Shar Patel, hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.
 
Kuna taarifa ya vijana 19 kufa na 17 kujeruhiwa vibaya katika ukumbi flani ambao sijapata jina lake ni katika sherehe za Eid huko Tabora. Kwa kirefu tutawaletea.

Mungu azipumzishe roho za marehemu mahala pema!

Kama ni kweli zimethibitika basi ninasema Inna Lilah Wa Inna Ilahi Rajwun. Ila ninasubiria habari kwa kirefu
 
Poleni wote ,mlioguswa na misiba hii. Hii haitajawahi kutokea Tz, basi tujifunze kutokana na makosa.
 
That is the most terrible, slow way to die. Suffocation
Poor kids, God rest their souls
Jamani town planners!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom