Rayvanny wa jamiiForums
Senior Member
- Apr 7, 2023
- 132
- 347
Ni wazi Watanzania wengi hawana kitambulisho cha taifa yani hili suala la kutoa kitambulisho cha taifa hapa nchini limekuwa kama jambo la hiari kwa mamlaka husika hali inayoweza kuchochea uwepo wa rushwa.
Suala la kupata kitambulisho cha taifa lisiwe biashara wala mizungusho kama vifaa hakuna basi serikali ihakikishe kunakuwa na vifaa vya kutosha, kama kuna uhaba wa wafanyakazi kwenye mamlaka husika basi serikali itoe ajira kuziba hilo pengo ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata vitambulisho vya taifa kwani hili siyo suala la hiari ni la lazima kisheria.
Naomba niweke wazi kwamba Watanzania tumechoka tunataka Kitambulisho cha Taifa kipatikane kwa haraka na uhakika na bila masharti.