Siku 14 Kutumika Kugawa Vitambulisho vya Taifa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Unahitaji kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na una namba pekee? basi mamlaka hiyo imeanza kugawa vitambulisho milioni 18.6 kwa Watanzania wenye namba, kazi itakayofanyika kwa siku 14.

Ugawaji wa vitambulisho hivyo, utahusisha wananchi katika mikoa saba ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Ruvuma.

Vitambulisho hivyo vinapatikana katika ofisi za vijiji na Serikali za mitaa na vitagawanywa kwa siku 14.

Chanzo Mwananchi
 
Nafahamu kuna vijana waliojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria baada ya kumaliza form six na kuhitimu mafunzo hayo September, 2023. Wakiwa huko huko kwenye makambi ya JKT walilazimika kujiandikisha ili kupata vitambulisho vya NIDA lakini hadi wanaondoka makambini hawakuwa wamepata vitambulisho isipokuwa waliishia tu kupata namba za vitambulisho ambazo walizitumia kwenye kuombea mikopo ya HESLB kwa waliobahatika kujiunga na vyuo n.k. Sasa kwa vijana kama hawa ambao watakuwa masomoni itawabidi kukatisha masomo yao kwa siku kadhaa na kusafiri hadi huko mikoani walikojiandikisha kipindi wakiwa JKT ili kupata hivyo vitambulisho?
 
Ka ilivyo kwa matokeo ya mitihani na mambo mengineyo, ingependeza kutoa majina tu ya watu ambao vitambulisho vyao vimekamilika.
 
Yes, NIDA walipaswa kuweka Majina yote ya watu ambao vitambulisho vyao viko tayari. Tangazo hilo lilipaswa kuwekwa kwenye tovuti yao ili kuwarahisishia kazi Wananchi.
Ka ilivyo kwa matokeo ya mitihani na mambo mengineyo, ingependeza kutoa majina tu ya watu ambao vitambulisho vyao vimekamilika.
 
Back
Top Bottom