benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Serikali imesikia kilio cha Wananchi na imetangaza rasmi kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 21 Februari 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho hivyo.​
NIDC-ANNASTASIA-2.jpeg

--

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wamefanya mabadiliko ya kanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 21, 2023 wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho.

Waziri huyo, amesema marekebisho ya kanuni yamekamilika na zimeshaanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la Serikali la Februari 17, 2023.

"Nitoe rai kwa watoa huduma kwa wananchi hasa taasisi za kifedha, benki na kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo uliopita kwa sababu havitakuwa na ukomo tena wa matumizi.

"Marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe," amesema Masauni.

Kwa uamuzi huo wa Serikali, wananchi sasa wataondokana na wasiwasi pamoja na hofu pale vitambulisho vyao vya taifa vitakapokwisha muda wake.

Lakini sasa hakutakuwa na ukomo tena na hawatalazimika kuvihuisha kwa kulipa Sh 20,000.

MWANANCHI

Pia, soma; Kwanini kitambulisho cha taifa kina muda wa kuisha matumizi
 
Hiyo inapendeza, binafsi nilishangaa toka mara ya kwanza nilipoona kitambulisho cha taifa kina expiry date, nikajua tu hilo lilikuwa dili la wapigaji, kwasababu ya awamu ile vilipotolewa kwa mara ya kwanza, watu walikuwa wanajipigia tu.
 
Awamu ipi walikuwa wanajipigia tu mkuu
 
Back
Top Bottom