Zoezi la majaribio (pilot study) la kuwapatia huduma ya vitambulisho vya taifa diaspora wa Tanzania wenye sifa wanaoishi Nchini Marekani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Wenyeviti, Jumuiya za Watanzania, MAREKANI.

ZOEZI LA MAJARIBIO (PILOT STUDY) LA KUWAPATIA HUDUMA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA DIASPORA WA TANZANIA WENYE SIFA WANAOISHI NCHINI MAREKANI

TAREHE 17 - 24 JANUARI 2023

UBALOZINI WASHINGTON mc.

Tafadhali husika na somo lililopo hapo juu.

2. Ubalozi unapenda kuwafahamisha kuwa Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) watakuwa hapa Ubalozini kuanzia tarehe 17 hadi 24 Januari 2023, kwa ajili ya kutoa huduma ya vitambulisho vya Taifa kwa Diaspora wa Tanzania wenye sifa wanaoishi nchini Marekani. Zoezi hili ni la majaribio (pilot study) wakati Mamlaka hiyo inapojipanga kutoa huduma hiyo kwa Diaspora wa Tanzania wenye sifa wanaoishi nchi


3. Diaspora wenye sifa stahiki wanaohitaji huduma hiyo wanatakiwa kupakua fomu ya maombi kupitia tovuti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (www.nida.qo.tz) na kuijaza kwa herufi kubwa kwa kutumia kalamu ya wino mweusi. Aidha fomu hiyo iliyojazwa inatakiwa kuambatishwa na nyaraka nyingine zikiwemo:

Pasi ya kusafiria ya mwombaji

ii. Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji

iii. Vyeti vya kuzaliwa ama viapo(affidavit) vya wazazi,

iv. Kibali cha ukaazi/kitambulisho au maelezo ya kina juu ya ukaazi wa mwombaji.

Nyaraka hizi zinatakiwa kuwasilishwa wakati wa kupata huduma ya vitambulisho hapa ubalozini.

4. Aidha, ni vyema kufahamu kwamba, zoezi hili litakuwa ni kwa ajili ya kupokea maombi ya vitambulisho hivyo kwa ajili ya kuyafanyia kazi. Vitambulisho vitaletwa Ubalozini baadae baada ya maombi hayo kushughulikiwa na Diaspora wataarifiwa mara vitambulisho vyao vitakapowasilishwa Ubalozini.

5. Mnaombwa kuwafikishia ujumbe huu Wanajumuiya wenu ili waweze kufika hapa Ubalozini kupata huduma hiyo ya vitambulisho vya Taifa. Huduma hiyo itatolewa kuanzja saa 3:00 Asubuhi hadi 11:00 Jioni kwa tarehe zilizotajwa. Kwa maelezo zaidi kuhusu suala hjli mnaweza kuwasiliana na Ubalozi kupitia barua pepe ubalozi@tanzaniaembassy-us.orq au simu namba 202-888-1089/202-884-1083.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu wa siku zote.

Malik S. Hassan Kny: BALOZI
 

Attachments

  • ZOEZI_LA_MAJARIBIO_PILOT_STUDY_LA_KUWAPATIA_HUDUMA_YA_VITAMBULISHO.pdf
    92.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom