tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 22,153
- 18,813
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, imezoeleka kwamba kila mtawala aingiaye madarakani huongoza kwa vipindi viwili vya miaka 5, yaani jumla ya miaka 10 ijapokuwa hakuna uhalali wowote wa kisheria kufanya hivyo zaidi ya mazoea tu. Waswahili walinena: “kimya kingi kina mshindo mkuu”. Kufuatia kimya cha watanzania kwa takribani miaka 3, sio jambo la kushangaza kimya hiki kikaja kusababisha mshindo mkuu mwaka 2020.
Hapa ndipo watanzania wengi watakuja washikwe na butwaa wasifahamu ni nini kilichotokea. Ukiondoa kikundi cha “mashabiki” wachache wasiopungua 100 ambao kazi yao kubwa ni kumpigia mfalme vigelegele kwa kila anenalo, liwe kandamizi au la kuwaumiza wanyonge. Watanzania walio wengi nyoyo zao zimevunjika kwa kiwango kikubwa sana.
Ndani ya chama kuna makundi kinzani ambayo yameanza kuchomoza kuelekea 2020 na yana nguvu za kutosha kufanya “mapinduzi” yasiyotarajiwa kwa manufaa mapana ya watanzania wanyonge wanaioishi kama yatima tangu mwaka 2016. Kada maarufu wa CCM, Mheshimiwa Cyprian Musiba watu wengi wanamdharau lakini alishawahi kugusia jambo hili hapo kabla. Kwa kuwa Musiba ni mmojawapo wa kikundi cha watu 100 wanaoshangilia kila jambo, ipo haja ya kuamini kwamba mwaka 2020 litakoea tukio ambalo halijawahi kuzoeleka miongoni mwa watanzania.
Hivyo basi, wanyonge wa nchi hii msilie sana kwani Mungu ameishasikia kilio chenu. Futeni machozi ya damu yachuruzikayo chini ya mashavu yenu. Mwaka 2020 Mungu atawatendea muujiza wa ajabu.