Watanzania msilalamike. Shukuruni na tuendelee kuomba Mungu. Nchi hii hatua kwa hatua inatoka mikononi mwa wakoloni weusi CCM...!

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
810
1,652
Hakuna ubishi kuwa, mambo katika nchi yetu hayako shwari. Uamusho na ukombozi huwa hauji katikati ya furaha ya kula na kunywa.

Mambo yalifikia ukomo wa uharibifu mwaka 2015 mara baada ya John P. Magufuli kutawazwa kuwa Rais wa 5 wa Tanzania.

Huyu alianza kwa kuharibu mfumo wa kisiasa na ustaarabu wa Watanzania. Akabomoa ustaarabu wa kupingana kwa hoja ktk majukwaa ya kisiasa bila kupigana ama kuuana.

Hayati John P. Magufuli akaja na utamaduni mpya usio na hofu ya Mungu. Utamaduni wa kuteka, kutesa na kuua wapinzani wake kisiasa waziwazi na mchana kweupe bila woga.

Baadhi walikubaliana na aina ya utawala na uongozi wake uliokuwa na kila elements za kishetani.

Akaharibu na kujiua mwenyewe kwa kupora mchana kweupe pasipo hofu haki za raia wote wa nchi hii kupitia chaguzi za mwaka 2019 na 2020.

Aaah, hii ilikuwa mbaya sana

Hat Mungu hakuweza kulivumilia hilo. Ilibidi aruhusu kifo kimwondoe mtu huyu ili kuikoa nchi yetu.

Hivi ndivyo ambavyo Mungu hufanya kwa wanaotawala watu kwa niaba yake wanapotaka kujiinua juu ya mamlaka yake.

Hebu kila mmoja ajiulize na kujibu swali hili

Kwamba, kwa aina ya uongozi wake John P. Magufuli uliojaa u - mimi na ukatili, kama angeruhusiwa kuwepo ktk nchi hii mpaka leo tunadhani angeshatengeneza himaya (empire) mbaya na ya hatari kiasi gani kwa raia akiwatumia watu hatari kwa sampuli ya Ole Lengai Sabaya, Bashite au Makonda, Jerry Muro, Ally Hapi, Job Ndugai na wengine?

Sikilizeni ndugu zangu wananchi wa Tanzania.

Tanzania inatoka mikononi mwa CCM taratibu na hatua kwa hatua

Nalisema hili kwa mamlaka toka ktk engo nyingine kabisa ambayo wengi hamtanielewa.

Mikakati kwa msaada wa Mungu mwenyewe ipo na inafanyika taratibu maana vita yetu sisi wengine tunaipigania ktk masafa mengine.

Nawaomba wote tuendelee kuchukua hatua. Tekelezeni wajibu wenu kwa hekima na busara. Tusinyamaze kimya.

Pale ambapo ni lazima kusema, kila mtu aseme.

Na pale ambapo ni lazima kutenda, kila mmoja na atende kwa busara akijua kuwa shetani mwizi na muuaji bado yupo ndani yao. Ukienda vibaya, watakuua tu...!!

Kifo rahisi kabisa cha Rais wa nchi aliye madarakani mwaka 2021 ni ishara njema sana kwa wanaotaka na kulilia ukombozi wa mara ya pili wa nchi hii toka kwa wakoloni weusi wenzetu waitwao CCM.

Magufuli na mambo yake akaishia hapo.

====================

March, 2021 kwa binde na msuguano mkali ndani ya CCM na serikali, mwanamama Mzanzibari Samia Suluhu Hassan akatawazwa Rais wa 6 wa Tanzania kuchukua mahali pa hayati John P. Magufuli.

Hili la mtu toka nchi nyingine iitwayo "Zanzibar" tena mwanamke kutawala nchi nyingine likawa kosa kubwa lingine kufanywa na CCM.

Wanaofikiri pafupi, wakadhani Tanzania imekombolewa ghafla. Hapana, mambo hayaendi hivyo...!.

Ukombozi unaenda hatua kwa hatua. Huyu mama amekuja kuusogeza ukombozi hatua inayofuata... Amekuja kuachilia maumivu mengine na kupitia kwake, Tanzania inakombolewa na Tanzania inakwenda ktk majira na msimu mwingine mpya wa kiutawala na kisiasa CCM ikiwa imeshazikwa.

Haya matatizo muyaonayo sasa ya viongozi kuiba mali na fedhs za umma na kufanya ufisadi uliokithiri, ukame, nchi kukosa umeme, ukosefu wa madawa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu, maji, mikopo ya elimu ya juu na huduma zingine za kijamii yanayofungamanishwa na tatizo la nchi kukosa uongozi bora ni njia tu ya kuwaharibu watawala hawa japo ni kwa maumivu makali ya sisi wananchi.

Tuvumilieni jabo ni kwa kitambo kidogo tu. Nchi nyingine mpya ya Tanzania itazaliwa si kitambo kirefu. Niaminini mimi.

Wanaosema kuwa wananchi wa nchi hii ndiyo wajinga na mbumbumbu na wapole sana kwa kuwa tumeruhusu hali hii, hawajui wasemalo...!

Haya yameruhusiwa na Mungu mwenyewe. Mungu ameruhusu tuwe hivi. Mungu mwenyewe anadhibiti haya...

Nawakikishia jambo moja kuwa, kwa wakati mwafaka, Mungu ataachilia mwamko na ujasiri wa hatari kwa watu wake mpaka watawala watakuja kushangaa na watakimbia wasione hata pa kujificha nyuso zao....

Laiti CCM na serikali wanayoingoza wangekuwa na akili na maarifa, basi wangetengeneza mambo yao haraka, Mungu angeweza kuwasamehe na kuwarehemu...

Lakini kwa kuwa akili na ufahamu wao umefungwa ktk ubinafsi na ulafi, basi kama ni kufa, hakika na wafe tu maana hiyo ndiyo haki astahiliyo mjinga...

MUNGU HAWAHI NA WALA HUWA HACHELEWI

Nimemaliza. Usiku mwema kwa kila mtu.
 
Nonsense, wakati wa Magufuli kulikuwa na maji ya kutosha,umeme ulikuwa haukatiki ovyoovyo,bidhaa hazikuwa na bei kubwa yaani hakukuwa na mfumuko wa bei WA ovyoovyo.watu wa Chini walikuwa wanajaliwa,tuliingia uchumi wa Kati Kwa mujibu wa Benki ya dunia.

Kidogo kwenye democracy aliteleza lakini mambo mengine alijitahidi Sana nchi ilikuwa spidi kwenye maendeleo. Sasa hivi mafisadi yamerudi Kwa Kasi makampuni Yao yanatulipisha bei kubwa kufidia hasara ya wakati uliyopita. So usirudie tena kuoanisha upuuzi unaoendelea Sasa hivi na magufuli. Mtu mwenye upungufu wa akili ndo peke yake anaweza kufanya hivyo.Issue ni kwamba Rais wa Sasa hivi na wasaidizi hawana sifa ya kuwa viongozi wa Tanzania.usirudie huu upuuzi.
 
Asante kwa maoni yako.

Lakini sina hakika kama umeipata mantiki ya hoja yote kwa ujumla.

Mimi natazama mambo ktk jicho jingine na kwa masafa ya juu kuliko unavyoona wewe.

Matatizo ya maji, umeme na mengine yamefungwa ktk mfumo wa kiutawala na kisiasa wa nchi.

Kama wakati wa Magufuli "ilikuwa shwari" kama usemavyo, unadhani ni kitu gani kimetokea na mambo kuwa hovyo?

Sikiliza ndugu, mfumo wa hovyo wa kiutawala na kisiasa ndiyo msingi wa matatizo haya whether unataka kuelewa ama hutaki.

Nakuambia hivi, katikati ya haya ndipo watu watawala sasa watatokomea na kupotea kabisa...!
 
Unawaza siasa tu. Usichojua ni kuwa Magu hakuwa mwanasiasa. Alikuwa mwana maendeleo na mzalendo kwa nchi.

Hakujali rafiki ndugu wala jamaa. Pengine we ulihitaji mahaba na ye hakuwa muumini wa hayo ndio maana katika era yake aliumizwa na alihakikisha hakuna shida ya umeme wala maji wala mfumuko wa vyakula.

Mengineyo kawaachia nyie wapenda siasa.
 
Hapendi siasa wakayi huo akazuia wagombea woote walioteuliwa na wajumbe akaweka wa kwake?

Hapendi siasa lakini akawa anapiga porojo za siasa nchi nzima yeye peke yake?

Sikio la kufa......bado mnatetea ujinga hadi leo?
 
Asante kwa maoni yako...

Lakini sina hakika kama umeipata mantiki ya hoja yote kwa ujumla...

Mimi natazama mambo ktk jicho jingine na kwa masafa ya juu kuliko unavyoona wewe...

Matatizo ya maji, umeme na mengine yamefungwa ktk mfumo wa kiutawala na kisiasa wa nchi...

Kama wakati wa Magufuli "ilikuwa shwari" kama usemavyo, unadhani ni kitu gani kimetokea na mambo kuwa hovyo...?

Sikiliza ndugu, mfumo wa hovyo wa kiutawala na kisiasa ndiyo msingi wa matatizo haya whether unataka kuelewa ama hutaki...!!

Nakuambia hivi, katikati ya haya ndipo watu watawala sasa watatokomea na kupotea kabisa...!
Sio mfumo ni uvivu wa kufikiria wa viongozi wetu.unahitajika mfumo wa Aina gani kujua kuwa nchi inahitaji umeme wa kutosha na Luna vyanzo vingi vya umeme? inahitajika mfumo gani kuhakikisha uwepo wa maji wa uhakika.labda useme mfumo wetu unazalisha viongozi dhaifu wakati.
 
Asante kwa maoni yako...

Lakini sina hakika kama umeipata mantiki ya hoja yote kwa ujumla...

Mimi natazama mambo ktk jicho jingine na kwa masafa ya juu kuliko unavyoona wewe...

Matatizo ya maji, umeme na mengine yamefungwa ktk mfumo wa kiutawala na kisiasa wa nchi...

Kama wakati wa Magufuli "ilikuwa shwari" kama usemavyo, unadhani ni kitu gani kimetokea na mambo kuwa hovyo...?

Sikiliza ndugu, mfumo wa hovyo wa kiutawala na kisiasa ndiyo msingi wa matatizo haya whether unataka kuelewa ama hutaki...!!

Nakuambia hivi, katikati ya haya ndipo watu watawala sasa watatokomea na kupotea kabisa...!
Usimamizi mmbovu katika shirika la umeme na hujuma Ili watu wauze magerenator.
 
Kuna misukule ya mwenda kuzimu Bado inapumua ukiiambia baba yenu alikua muuaji yenyewe inakwambia baba alijenga madalaja hapo ndo tunakwama sasa kumbe kuijenga mabarabara mpaka watu watekwe watu wapigwe ma risasi au mpaka watu wabambikwe makesi ya uhujumu uchumi la mwisho mtujibu Kwa sauti kidogo je mbona wasiojulikana hatuwaoni Toka parapanda ilipolia pale (MZENA)?
 
Hapendi siasa wakayi huo akazuia wagombea woote walioteuliwa na wajumbe akaweka wa kwake?

Hapendi siasa lakini akawa anapiga porojo za siasa nchi nzima yeye peke yake?

Sikio la kufa......bado mnatetea ujinga hadi leo?
Ndio maana nakuambia hakupenda siasa. Aliweka watu ambao aliamini atasaidiana nao.
 
March, 2021 kwa mbinde na msuguano mkali ndani ya CCM na serikali, mwanamama Mzanzibari Samia Suluhu Hassan akatawazwa Rais wa 6 wa Tanzania kuchukua mahali pa hayati John P. Magufuli...[/QUO3TE]
Baada ya msiba, kulitokea mbinde gani na msuguano mkali upi ndani ya CCM na seikali?. Mbona the transition, was a smooth transition?.
Hili la mtu toka nchi nyingine iitwayo "Zanzibar" tena mwanamke kutawala nchi nyingine likawa kosa kubwa lingine kufanywa na CCM... [/QUO3TE]
Uraia wa Tanzania ni uraia mmoja, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, kuna Mtanzania tuu, kila Mtanzania ana haki ya kuwa Rais wa JMT!. Zanzibar sio nchi nyingine!, na urais hauna uhusiano na jinsia, hii inamaana, rais anaweza kuwa mwanaume ama mwanamke.
Wanaofikiri pafupi, wakadhani Tanzania imekombolewa ghafla. Hapana, mambo hayaendi hivyo...!.

Ukombozi unaenda hatua kwa hatua. Huyu mama amekuja kuusogeza ukombozi hatua inayofuata... Amekuja kuachilia maumivu mengine na kupitia kwake, Tanzania inakombolewa na Tanzania inakwenda ktk majira na msimu mwingine mpya wa kiutawala na kisiasa CCM ikiwa imeshazikwa...[/QUO3TE]
Duh...!.
Haya matatizo muyaonayo sasa ya viongozi kuiba mali na fedha za umma na kufanya ufisadi uliokithiri, ukame, nchi kukosa umeme, ukosefu wa madawa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu, maji, mikopo ya elimu ya juu na huduma zingine za kijamii yanayofungamanishwa na tatizo la nchi kukosa uongozi bora ni njia tu ya kuwaharibu watawala hawa japo ni kwa maumivu makali ya sisi wananchi....[/QUO3TE]
Duh....!. Hata ukame, hata kukosa mvua!.
Tuvumilieni jabo ni kwa kitambo kidogo tu. Nchi nyingine mpya ya Tanzania itazaliwa si kitambo kirefu. Niaminini mimi...

Wanaosema kuwa wananchi wa nchi hii ndiyo wajinga na mbumbumbu na wapole sana kwa kuwa tumeruhusu hali hii, hawajui wasemalo...![/QUO3TE]

Duh...!.

Haya yameruhusiwa na Mungu mwenyewe. Mungu ameruhusu tuwe hivi. Mungu mwenyewe anadhibiti haya...[/QUO3TE]
Hapa naunga mkono hoja, Mungu ndie huweka serikali za mataifa, hivyo hata JPM aliletwa na Mungu baada ya Watanzania kumuomba Mungu atuletee kiongozi wa type ile, na ni Mungu amemtwaa na kumuta kwake, na badala yake sasa Mungu ametuletea Samia, hivyo hata Samia ni chaguo la Mungu, chochote kinachofanyika awamu hii ya Samia ni Mungu ameruhusu!, na kukifanyika makosa ni Mungu ataadhibu, kila kitu ni Mungu!.

Nawakikishia jambo moja kuwa, kwa wakati mwafaka, Mungu ataachilia mwamko na ujasiri wa hatari kwa watu wake mpaka watawala watakuja kushangaa na watakimbia wasione hata pa kujificha nyuso zao....[/QUO3TE]

Duh...!, ngoja tuusubirie huo wakati muafaka ufike, maana sisi wengine tunajua kwa hakika CCM is there to stay for a long long time to come!. Infact ni CCM itatawala milele!.

Laiti CCM na serikali wanayoingoza wangekuwa na akili na maarifa, basi wangetengeneza mambo yao haraka, Mungu angeweza kuwasamehe na kuwarehemu... [/QUO3TE]

Hapa unamaanisha nini?, yaani hawana akili na maarifa?, Ni mambo gani hayo ambayo wangeyatengeza haraka, wangesamehewa na Mungu?

Lakini kwa kuwa akili na ufahamu wao umefungwa ktk ubinafsi na ulafi, basi kama ni kufa, hakika na wafe tu maana hiyo ndiyo haki astahiliyo mjinga...

MUNGU HAWAHI NA WALA HUWA HACHELEWI

Nimemaliza. Usiku mwema kwa kila mtu.
[/QUO3TE]
Duh...!. Hivi kuna ubinafsi na ulafi gani kipindi hiki compared na vipindi vingine?. Kwa vile hapa umemhusisha Mungu, na kuna wakati Mungu akitaka kufanya jambo lake huwafanya watu wawe na mioyo migumu, lakini unapohusisha kifo, kifo ni kwa wote, watenda uovu hufa, ila hata watenda haki nao pia hufa, wote tutakufa, hivyo usirishie kifo mtu, wewe pia utakufa, mimi nitakufa, sote tutakufa, wote tutakufa siku yetu ikifika!.
Jina la Bwana Lihimidiwe!.

P
 
Back
Top Bottom