Ubinaadamu kazi nyie! Mtu akiwa CCM kwanza anabadilika anakuwa kama mnyama kwanza: ona hili zee linawakana watoto wake: angeulizwa kama anaweza KUWAJUA muone angesemaje:
Mkuu ni kweli hujui kwanii amekimbilia kwenye media?
Nitakuelewa ikiwa pia ungehoji kwanini CDM kukimbilia media kupoke wanachama hawa wawili tu tena na vigogo wakati kilasiku watu wanajiunga kimya kimya cdm
Watu mnakuza mambo yasiyo na tija. Wakiwa watoto wake au wasiwe watoto wake, amewakana au hajawakana, na wamejiunga na cdm, tatizo ninini? Usiku mwema.Kwa iyo hata kama ni watoto wa kaka ake hawapaswi kumuita baba????
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Watu mnakuza mambo yasiyo na tija. Wakiwa watoto wake au wasiwe watoto wake, amewakana au hajawakana, na wamejiunga na cdm, tatizo ninini? Usiku mwema.
What goes around comes around.Hii ndio balaa ya kuhusudisha watoto wa vigogo.Slaa anatakiwa kubadilika sasa na aache umbeya, inanishangaza sana Rais mtarajiwa anashindwa kupata taarifa za uhakika na kuona kama kuna haja ya kuita media ama lah.
Na sisi watoto tuwe na tabia ya kuwataja Wazazi wetu halisi hata kama ni ''wauza kuku'' ama mafundi ''viatu'' hii habari ya kutumia majina,bila kutofautisha ama kufafanua hasa pale inapobidi ni ''kaugonjwa'' kengine hapa Bongo.
Kinachoendelea hapa ni michezo ya kisiasa tu....
Jana hapa kila mtu alimtolea maneno ya kashfa Wasira kwakuwa tu watoto wake wamejiunga CDM, media zikapamba na vigogo wakawapokea kwa mbwembwe nia ni kummaliza wasira kisiasa
Lakini leo kajibu si watoto wake wa kuzaa kama inavyoripotiwa na kupambwa tunaanza kumuita mjinga
Tatizo ni CDM wenyewe kuupamba sana ujio wa hao mabinti as if wamemkomoa Wasira na kwakuwa wasira nae kichwa maji katumia njia ile ile kujibu
Ebu tusiwe double standard, Dr. Slaa kuna mawili aidha kapotoshwa ama kaamua kupotosha kwa makusudi.Nilichokitambua mimi jana hasa baada ya kupewa kadi kwa mbwembwe ni kuwa Watoto wale ni wa Wasira wa kuzaa.Niliamini hasa baada ya Slaa kumu-attack huyu mzee moja kwa moja na ndicho Watanzania wengi walikitambua jana.
Tuache tabia ya kuelezea matokeo na kusahau chanzo.Hapa chanzo ni Slaa na Wasira ni matokeo tu.Inashangaza Pro CDM kugeuza Wasira kama ajenda.Tuache ushabiki na isiwe ''kajamba kuku pafyumu,bata aaaagh''.Hiki kizazi cha ajabu kabisa.